Brother Michuzi habari gani?
Noamba kuleta ujumbe wangu huu na kukuomba uniwekee katika blog yako.. Natanguliza shukrani. Kwa jina naitwa Taymour nina umri wa miaka 43 ninaishi neasden london uk.
Ni mtanzania, sijajiripuwa, sijaukataa uraia wangu, sijadanganya kwa namna yeyote au kuoa ili tu kupata karatasi za kuishi.Nimebahatika kupata karatasi za kuishi na kufanya kazi kihalali kabisa na kwa "pure luck" kutokana na wakati pamoja na aina ya kazi ninayofanya.
kwa ufupi nilikuwa ni miongoni mwa wale walionufaika na demand ya IT in "millenium boom" 1999/2000. kampuni yangu iliniombea extention ya working visa na passport yangu iliporudi nilipewa ruhusa ya kufanya kazi kwa muda wa miaka mitano.
Baada ya miaka mitano kwisha niliweza kuomba ruhusa ya kuishi indefinitely kwa kutumia sheria na kanuni za nchi na ndio ikawa hadi sasa niko na ninaishi katika nchi hii.Nadhani kwa ufupi nimejieleza kwa kiufupi, madhumini ya kuanza kwa kujieleza ni kujarbu kupunguza makali ya waosha vinywa watakaojibu post yangu hii.
OK, Kwa ufupi ningelipenda kutafuta mchumba - sio girlfriend - maana ninawajuwa wnegi wanaoita girlfriend/boyfriends zao mchumba. Natafuta mwanamke nitakaeweza kwenda kwao kuomba kufunga doa nae.
Awe anaishi popote pale nchini tanzania au nje ya tanzania but akiwa tayari yupo uk ni advantage zaidi. Ni muhimu awe yuko tayari kuja kuishi uk, hata hivyo kutokana na ukubwa wa kampuni ninayofanya kazi awe yuko tayari kuhamia nchi nyengine (dubai, holland, finland au canada) endapo nikihamishwa kikazi.
Sifa nyengine nitazieleza kwa yule atakaeonyesha interest juu yangu.
Nitajibu kila email nitakayopata na nitajieleza zaidi katika email. Hakuna haja ya kutumiana picha wa wakati huu. wakati ukifika sote tutajuwana tu.
Sikusudiii kuchukuwa nafasi kubwa katika blog ya jamii, ila nakuahidi nikifanikiwa kupata mchumba kupiti glob yako basi exclusive picha za mwanzo ni zako. email yangu ni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 58 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 04, 2009

    kaka michuzi za leo hongera kwa kuliendeleza libeneke !

    napenda kuwatahadharisha watz wenzangu siku hizi kuna gonjwa hatari la ukimwi. jamaa kajieleza vizuri lakini bado hajajieleza kikamilifu sina lengo la kukashifiana ila ni kutahadharishana.

    mwenye macho haambiwi tazama watu wengi hapa uk wamepata makaratasi kwa status za afya zao.

    kwanini asirudi nyumbani akajichagulia badala yake asumbuke kwenye internt ???????????????????

    broo michuzi kama itakua inachafua hali ya hewa basi japo ku edit unaweza lakini ujumbe ufike
    mdau kenton uk

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 04, 2009

    we bwana unaboa sasa unajitamba kwani mtu aliejilipua lakini likizo anaenda bongo ,maendeleo kila kitu anafanya na kuwasaidia ndugu na jamaa ana kosa lipi?kumbuka kwamba watu wanajilipua ili kufanikiwa tu kufanya mambo yao hapo uk kiufupi na sio eti hawautaki utz,mimi tena wewe ndio naona mtumwa wa wazungu kwani unawaogopa kiasi hata mtu kujilipua unaona soo.na uzee huo ujaoa ngoma yako ngumu utampata nani si ajabu umeachika kwa nyodo zako,pia nahisi sura yako mbaya sana ndio maana hutaki mambo ya kutumiana picha

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 04, 2009

    haki ya nani vile!!

    kwishnei

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 04, 2009

    makubwa

    yan kabisaaa domo zege???

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 04, 2009

    Sema shida yako badala ya kuweka mbwembwe nyingi kujieleza huku na huku. Kwani nani alikuuliza uanze kujibaraguza kwamba oh hujajilipua oh wewe umebahatika kukaa majuu sijui nini na nini. Kwani ulifikiri hiyo ni fasheni ndugu?

    Pili hiyo wala sio sababu ya kuwafanya mabinti wakunganganie kiuchumba kwani hawajali umejilipua ama vipi. Be yourself, talk about yourself na sio umbeya. Wachumba hawapo interested na kwamba umejilipu ama la. Tena mbona waliojilipua kwa usemi wako wamepata wachumba na maisha yao ni safi? Sasa wewe unachoshindwa kujiamini ni nini? Unaonekana mtu wa makeke sana wewe. Wasichana watafuta wachumba mjipigize kwenye huuu mwamba walah mtakiona. mbwembwe zenyewe hizi? Mh!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 04, 2009

    Mh balozi wa naniii, sina kipingamizi ila post nyingine naona zinalenga kupima upepo. Ushauri wangu, uko UK pita kila kona tafuta mcumba, vinginevyo kwani huna ndugu au jamaa nyumbani, washirikishe wakusaidie na wewe funga safari uende na acha uzushi, sasa wangapi wanasoma blogs?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 04, 2009

    unatafuta mchumba humu?kweli wewe kipofu ! wachaa usanii

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 04, 2009

    DU!DU! DU! YEYEEEEEE YEYEEEE AH AAAAA YEYEEEEEE EEE YAP YAP YAP YAP E BWANA EEEE ....... EXPRESS YOUSELF

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 04, 2009

    mbona ujaeleza mchumba uyo awe na sifa zipi?wasifu upi?umejielezea wewe mwenyewe na kazi yako tu

    ReplyDelete
  10. UMEFULIA MSHKAJI

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 04, 2009

    kwanza sina ni mbaya na ushauri kwako. ukweli kwanza kitu kimoja uwe tayari kupima kabla ya kila kitu, kitu cha pili ndio kitafuata kujitambulisha kwa wazazi kama ulivyoelezea, ula mchumba utapata hiyo nakupa 100%, kitu cha mwisho ni kwamba watu wengi watasema sana, ila wewe ndio uwe mtu wa kumchunguza tabia, bila kuonekana wazi wazi au ukaonekana na wivu kwake. asante ni hayo tu.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 04, 2009

    43 years ol-unmarried!! kazi kwelikweli

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 04, 2009

    Historia yako inajielezea yenyewe ndio maana una miaka 43 bila mchumba. Sasa kama unajifanya una bahati sana mbona hukubahatika sana kupata mchumba basi? Well this is your time kujilipua now kutafuta mchumba. Tatizo lako ni mbwembwe zako zisizokuwa na maana yoyote. Please utakapopata mke this time time utuandikie jinsi ambavyo ilibidi kujitundika kwenye blogs kutafuta wife kwani wendio kwenye hilo tulibahatika.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 04, 2009

    PIGA UWA HUYU KIMEO NA NYINYUI MNAOTAKA KUJA UGHAIBUNI KWA TIKETI YA HUYU JAMAA POLENI SANA NA MUWE WACHUNGUZI YAKNIFU
    PIA KWANINI USIENDE UKO NA UKACHAGUA HAKUFAAEE AU AFYA MGOGOLO

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 04, 2009

    Mtu miaka 43 mpaka sasa hujaona mchumba kiasi kwamba imebidi utafute kwenye blog. Kama unataka mchumba wa Kibongo uje bongo uchangue mwenyewe acha usanii. Wewe unafikiri kuishi kwako UK ndio wanawake watatuma application kwa wengi. Uchumba si kazi mzee mpaka useme utapata applications halafu hufanye review na kuchugua iliyo bora.

    Mke wa kuoa unafikiri anapatikana tu kirahisi kirahisi, utakula wa chua kwa uvivu wa kuchambua.

    Bongo wanawake wapo wazuri lakini inabidi uchangue mwenyewe physically sio kuomba application through the Internet.

    Kazi kwako.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 04, 2009

    hongera waosha vinywa! hii ndio sababu kubwa ninayohakikisha napitia blog hii kila siku mchana.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 04, 2009

    Jamani kujilipua ndio nini? I have no idea... Msaada kwenye tuta

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 04, 2009

    hivi mashetani nyinyi ni wapi aliposema kuwa hakuwahi kuoa? hivi miaka 43 ndio uzee, mbona ni juzi tu hapa tumepewa taarifa ya mneguaji alieposwa na mtasa mwneye umri kupita wa baba yake, au tu kw avile ni mtasha basi ni ok? kwa nini wengine mnalazimisha akapime. pia ni wapi aliposema kwa hajawahi kurudi nyumbani? Kajieleza uzuri ili asije dhaniwa vibaya lakini bado mashetani wa hapa hawakuridhika wameona eti anajidai. Watanzania tuna matatizo mtu akiowa mzungu mnamsema anatafuta wa nyumbani mnamkejeli sasa mntaka afanye nini? Akina dada kama unataka kujuana nae you better take your chance what have you got to loose? mkibadilishana email utajuwa tu kama yuko ok au ni feki. ukiridhika mta expand contact zeni labda via sms kabla ya kuonana live uso kwa uso.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 04, 2009

    Jamani watu wengine ni wapuuzi kwelikweli, mke anatafutwa kwenye internet tangu lini? labda kama unatafuta porno stars useme. Kwa umri wa 43 bila mke,mmh sikuelewi.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 04, 2009

    43 YEARS OLD UNMARRIED..ULIKUWA WAPI WEWE?MMMHHH NI KIMEO HICHI HAKIANANI..MABINTI TUWE MAKINI JAMANI KUOLEWA TUNAPENDA LKN HUYU HATA TUKIZAA MTOTO EG. BABY AKIFIKA 15YRS BABA ANAELEKEA 60 KESHAZEEKA DUH. HUKO KUNAKOMTOA NYOKA PANGONI TENA KUTAKUWA KWISHNEY KUTIANA MAJARIBUNI TU HUKU. AKA

    ReplyDelete
  21. Kibakuli Ngongoseko Jr. SwedenJune 04, 2009

    Haya wenye vinyweleonyweleo( virusi) wasilianeni na jamaa huyu maana amechoka kuishi kwa amani hadi anakutafuteni kwenye internate.
    Miaka 43 unataka kupata watoto au wajukuu??
    Je, huna walakini au kasoro yoyote ya kimwili au kimaisha?
    Vipi hujawahi kupata mtoto hata wa kusingiziwa hadi umri huo??
    Kuna jamaa mwenye jina kama lako na anapenda sana kukiuka taratibu za kiungwana wakati wa nanihii, je sio wewe kweli.
    Mh.Balozi unaweza ku-edit kama hali ya hewa imeharibika lakini ujumbe ufike kwa muhusika.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 04, 2009

    YALEYALE KAISHOZI KAGERA.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 04, 2009

    Mind your bloody business cuz.... maisha ya wenzako yanakuhusu nini?? kujilipua, kukataa uraia sijui bla blaah, ndio maana mpaka leo hujaoa na hakuna anayekutaka.. wanawake wote hawa duniana na miaka yako 43 hujaona mpaka leo, na mwenyewe ushakaa chini na kutafakari utapata wapi mke, ukaamua kuja kwa muthupu..?! mwe inabidi mzee ujiassess vizuri....do u even know who u r??
    What a looser.
    NB: ni minekana uraia wangu long time, na nina mke mzuriiiii, kazi nzuriiii, maisha mazuriiiii.. haya wewe na uzalendo wako mpaka leo hujaona ndani...!

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 04, 2009

    Mimi nakushauri uende tanzania ukatafute mwenyewe mchumba.fanya old school, waulize wazazi wako,ndugu zako,waambie wakutafutie mchumba. ofcourse unaweza kupata mchumba on internet,but pia unaonyesha uko full of yourself. ungesema tu, wewe ni mtanzania,unaeishi uingereza na unataka mchumba kuanzia miaka fulani hadi fulani.etc etc! umechemka kidogo.
    Nenda bongo likizo, wanawake kibaoooooooooo,chaguo lako tu.au waambie wazazi wako wakutafutie,mtoto wa fulani bin fulani,like old ways.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 04, 2009

    Akina dada kueni macho na hawa viruka njia wanaojifanya wanatafuta wachumba kwenye internet wamebega "Miwaya." Wewe mtu kama amekamilika kwa nini usinde kwende kwenu kutafuta mchumba. Umri sio tatizo, hata mimi mwenyewe ni msichana wa nina umri 37. Lakini huyu mtu anaonekana kuwa na matatizo fulani hivi. Na hapo unapoishi kuna wasichana kibao na wewe tu. Kama ni MAZABE umeisha pata unawezo wa kutoka nje ya nchi na kuingia. Kafe mbele na virusi vyako.

    Mdau
    UK

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 04, 2009

    anonymous wa June 04, 2009 3:59 PM,hivi uko nchi gani? utaulizaje kama mke anatafutwa netini? hujawahi kusika online dating? watu wanakutana online na wanaowana na kuishi kwa furaha na amani.

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 04, 2009

    Hapo hujajilipua, 43, 44, 45 lazima ulipuke. Kwa ufupi wewe ni wale wanaume wasiokuwa na umakini sijui hata hiyo kazi unafanje, nadhani wewe ni mbeba box, au Bwana afya! Mchumba anapatikana kwenye jamii unayoishi mahali unapofanyia kazi, kanisani, n.k. Sasa wewe unataka kufumba na kufumbua umepata mke! Practically 0.000009 probabity ya kupata mwanamke wa interest yako!

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 04, 2009

    MSANIII TU ETI SIJAUKANA UTANZANIA WALA SIJAONGOPA WALA SIJAOWA ILI NIPATE KARATASI OK YOTE UMEWEZA.

    MBONA HURUDI KWENUUUUUUUUUUUUUU TANZANIA KAMA KWELI UNAUPENDA UTANZANIA RUDI KWENU ISHI TANZANIA HUNA LOLOTE. KUDADADEKI ULAYA MCHEZO RUDI HUKU UONE VIBOMU. JAMES WAKUFUJA.

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 04, 2009

    Bro sishtuki maelezo yako ya kalala mbwembwez ila nakuonea huruma sana kama uko serious kwa hili.
    psychologically u will be pleased wanawake watakavyojigonga ku-reply ila tegemea kupata KIFAFA ya nguvu/demu mwenye mitabia mibaya kwakuwa lengo lilikuwa kukutana na selebriti na kuishi mamtoni.
    Jifunze toka kwa Eddy Murphy bro alipojishusha kutafuta mchumba. U ar doing veri opositi na tegemea kufurahia replies na picha na talks tamu ila wengi wa namna yako wamewahi kuumia sana kupata dem aliyetimiza lengo la kutana na staa wewe ila atashindwa kukupenda kwakuwa she will feel being a slave wa mambwembwe yako.
    Wengi wameumizwa-Sijui wewe sir
    Goodluck

    ReplyDelete
  30. Mtu kuwa na miaka 43 bila kuoa sicha ajabu duniana. huwezi jua kwanini kafika hiyo miaka bila bibi. Toeni maoni endelevu sio kuponda hali aliyonayo sasa hivi.

    "There is no greater evidence of superior intelligence than to be surprised at nothing"

    ReplyDelete
  31. AnonymousJune 04, 2009

    mdau wa Tarehe June 04, 2009 4:07 PM kinachokushangaza ni nini hasa? kuna watu tele wameshapitiza miaka 45 na bado wako single. sijui uko wapi duniani lakini naweza kukupa majina ya watu maarfu tele ambao wameshapitiza 45 na bado wanapiga kazi na kuzalisha girlfriends/wake zao.

    nawe mdau wa Tarehe June 04, 2009 3:59 PM yes watu duniani kote wanatumia internet kutafuta wachumba, uko wapi wewe, watu wamejitajirisha kwa kuanzisha online dating agency wewe umebaki unauliza kama mke anatafutwa netini, au mwenzangu netini kwa ufahamu wako ni blogu ya michuzi tu?

    ReplyDelete
  32. Anon wa 3:52 pm

    Napenda sana akili yako!, na asante kwa kutukumbusha kuwa yule dada mchezaji kapata mchumba mwenye umri mkubwa lakini nobody questioned why he wasn't married at his age. Lakini watu wanamuona mswahili mwenzetu noma hajaoa mpaka sasa. Mbona kuna watu wengi tu 40+ hawajaoa? cha ajabu nini? it's someone's decision kuoa au kutooa mapema. After all life expectancy yetu ingekuwa kubwa, basi tu kwa sababu ya magonjwa and for that case it's perfect fine kwa yeye kuoa sasa. Wenzetu life expectancy yao can go up to 100yrs., mtu wa 40yrs is pretty young to them, lakini sisi kwa nini tunakuwa na mawazo ya kiumaskini? huyu kaka akijitunza vizuri who knows, anaweza afike hata 100+ yrs!, not only him, but anybody. So mdau wa 3:52 pm I concur your point, we shouldn't exploit other people's interests or choices for our own personal, unjustified reasons. Let's be positive minded at least once, it won't hurt!

    Kaka, I wish you all the best!

    ReplyDelete
  33. AnonymousJune 04, 2009

    wengine mna wivu tu, wivu unawasumbua waachieni watu wengine bwana.

    ReplyDelete
  34. AnonymousJune 04, 2009

    Jamani kujilipua si kuvaa mkanda wa baruti na kuitegua....booom!! Waulize watoto wa kipalestina na watamil wanavaaje hiyo mikanda. We mtafuta mchumba kwenye blog kazi unayo, maana mwenzio mimi nilianza kuwa na mchumba nursery school, primary,secondary na kuchapa nimechapa, du chuo ndo usisikie huku uraiani ndiyo usiseme.Span ya 43 yrs unatakiwa uwe ulishapitia weeengi kiasi cha kuchagua yupi kati ya hao uishi naye.Pole sana.

    ReplyDelete
  35. AnonymousJune 04, 2009

    Babu mambo ya kujilipua yanahusu nini? kama ndio unajipa ujiko basi umechemsha big time, anyway mimi nafikiri tatizo lako kubwa huna SOCIALIZING skills, hata ukipata huyo mke atakushinda mazee, atakukimbia!! unahitajika ujifunze jinsi ya kujichanganya na watu, uanze kwenda kwenye maghafla na sherehe mbali mbali, dansini, pub,concert, football game nk na ukianza kujichanganya na watu, huyo mke utampata easily kama unasukuma mlevi sio CUPID.

    ReplyDelete
  36. AnonymousJune 04, 2009

    jamaa atakuwa Muhaya huyu, aende tu bukoba atapata.

    ReplyDelete
  37. AnonymousJune 04, 2009

    kKAKA MITHUPU NA HII NDIO ADHA YA WENZETU KUKIMBILIA MAJUU NA KISHIA KUWA WATUMWA!
    MIAKA 43 NA JAMAA HAJAOA .ANATAFUTA MCHUMBA KWA INTERNET!!LAHAULA!
    HAPO SOCIAL LIFE NI SIFURI KABISA, HATA UKIPATA MCHUMBA TOKA TZ UTAKAA NAYE KWA MIEZI 3 HALAFU ATATAMANI KURUDI KWAO.
    HUO HUKO NI UTUMWA PERIOD

    ReplyDelete
  38. AnonymousJune 04, 2009

    Panda ngege uende Tanzania upate mchumba au nenda kokote duniani. Huitaji visa kurudi UK

    ReplyDelete
  39. AnonymousJune 04, 2009

    Dear mtafutaji! unaelekea you have a lot of potentials katika maisha yako, nafikiri kuna tatizo kwani mpaka kujianika kutafuta mchumba natafuta kuingia kwenye majaribu makubwa sana. Nafikiri huu sio utaratibu mzuri wa kutafuta mchumba katika blog ya jamii. Cha kufanya nenda kwenye singles.com, harmony.com na site nyingine nyingi weka profile yako kisha utaanza kupata mawasiliano ya kila aina ya wachumba. Lakini inakubidi uwe makini sana kwani watakuja mbwa mwitu wakali wenye kuvaa ngozi ya kondoo na kukurarua vipande vipande na kupoteza mwelekeo wa maisha yako.
    Kama una makaratasi nenda nyumbani kuna mabinti wazuri waliotulia na wapo tayari kuanza maisha.
    Mdau USA

    ReplyDelete
  40. AnonymousJune 04, 2009

    Jamani mtu usilinganishe tabia yako ukafikiri watu wote wako hivyo "eti 43 yrs ulisha pitia wengi" hio maana yake nini? Mtu kama wewe hujitunzi usifikiri watu wote wako hivyo, kuna watu wanatulia na kutunza maisha yao. Miaka 43 kwa mtu anaejitunza mbona kidogo sana hio. Watu wanafika 80+ sasa utasema 43 ni mzee? Kuishi kwa mtu anaechunga afya ni mpango wa Mungu lakini 43 bado young sana huyo.

    Mungu akujalie ndugu lakini sidhani kama njia unayoitumia kupata mke ni sahihi (ni ushauri tu).

    ReplyDelete
  41. AnonymousJune 04, 2009

    kazi kweli kweli ..nani anasema miaka 43 ni pretty young....jamani tusifananishe life letu wabongo na hao mabosi wetu wazungu....wenzetu unaweza kuta na 40 lakini tiyari ana watoto ila hajaoa...kwa kweli ni kazi kweli kwelli..someone with 43 years in UK anatafuta mchumba online from Tanzania..man..you have a right to enter and be away from Uk any time..why dont u go back home and search for a woman...maaana kule utakutana na wazee wenzako wa miaka 43 mtaoana...hahaha kwa nini unaogopa kurudi bongo au ndo wale mkiwa ulaya mnasahau home....Usiache mbachao kwa msala upitao..Sasa nini faida ya kukaa miaka kibao ulaya afu huna raha katika maisha...

    RUDINI HOME TUJENGE NCHI

    ReplyDelete
  42. AnonymousJune 04, 2009

    Kutafuta mchumba online ni kitu cha kawaida. Mimi mme wangu nimempata online dating. Tunaishi kwenye ndoa yenye upendo na amani. Sasa nawashangaa sana wanaosema eti utapaje mke au mme kwenye internet. Sasa nyie mnaouliza haya maswali sijui mko pande gani mwa dunia.

    Kuna we site nyingi sana, make mimi kabla sijapata nilicharibu nyingi tu hadi nikafanikiwa. Kaka jaribu hizi ama wengine. Mme wangu tulikutana kwenye hii web
    www.catholicsingle.com

    www.eharmony.co, www.justsayhi.com,
    www.true.com,
    www.datehookup.com, www.match.com, www.plentyoffish.com, www.okcupid.com, www.chemistry.com, www.perfectmatch.com, www.loveaccess.com,
    www.5stardating.com, www.lavaplace.com, www.maturesingle.com,
    www.matchmaker.com
    www.christianet.com
    www.dreamdates.com
    www.justaperfect.com
    www.affairmatch.com
    www.love.org
    www.arcentral.com
    WWW.LOVEBYNET.COM
    www.pickupdate.com
    www.answers.com
    www.facethejury.com
    www.marriednet.com
    www.oneplusyou.com
    www.4ppl.com
    www.exceldating.com
    www.omnidate.com

    Zipo nyingi tu na wengine mnaweza kujaribu.


    Hao wanaojifanya eti huwezi kutafuta mme kwenye net kihama chao.

    Mdau
    Agatha-Nebraska-USA

    ReplyDelete
  43. AnonymousJune 04, 2009

    wewe unayesema huyu jamaa ni MUHAYA ukome kama ulivyokoma ---- la ---- ----'hili li jitu lazima litakuwa haya makabila ya ajabuajabu kama wasukuma au michaga.IQ ya muhaya ni more then kutafuta mke kwenye internet,iwapo jamaa angekuwa anauliza labda formulae ya kutengeneza atomic bomb hapo ningekubali huyu muhaya

    ReplyDelete
  44. AnonymousJune 04, 2009

    Wacha kudharau wenzio, eti sijajiripua sijakana uraiya na nimepata uraiya kibahati whaaaat!!!kwani bongo inaruhusu uraiya wa nchi mbili,kama umechukuwa uraiya huko wewe sio mbongo tena full stop.

    ReplyDelete
  45. AnonymousJune 04, 2009

    wakina dada msiwasikilize watu wengi wana chuki humu ndani
    wengi wameolewa hawako happy na hawana ujanja wa kukimbilia nafasi kamaa hii imetokea wanataka kuwazibia wengine
    kwa sisi tunaokaa ulaya ni kitu cha kawaida mtu kutafuta mchumba online ni kitu cha kawaida, kuna wakazi wengi sana wanakaa ngambo kwenye blogu ya jamii lakini kutokana na chuki yao wanajidai kwamba ni jambo jipya...
    wakina dada changamkieni nafasi..

    ReplyDelete
  46. AnonymousJune 05, 2009

    mambo ya kujiripua ayajakuhusu kusema ulikuwa useme shida yako nyambafu wee...mbona ujasema km ulishawai kuambiwa km ww ni gay?hii sio blog ya kijinga uwe na adabu next tm...

    ReplyDelete
  47. AnonymousJune 05, 2009

    MJOMBA ENDELEA KUPIGA NGUNGU BAFUNI MIAKA 43 BADO VIRGIN KAMA SUSAN BOYLE, NENDA KWENYE NYUMBA ZA WAZEE UKATAFUTE WAJANE. UKIKOSA KABISA INGIA HOMELESSES UKABEBE WABWIA UNGA. MI NIMEJILIPUA NA NINAKULA NGOZI YA PAPAI KAMA KAWA NA MITOTO MIX N' MACH. KALAGHABAHO UTADUMAA MPAKA NYUZI YA MWISHO YA UBONGO NYAMAFU WEYE. MIAKA 43 HUJUI KITUMBUA KAMA KINA CHUMVI AU SUKARI AU SUKARI GURU, NDIMU YA UNGA.

    ReplyDelete
  48. AnonymousJune 05, 2009

    hii ndo blog ya jamii kama wengine hamkujua. na hata kama ni mhaya so wat?? HAPA WATU WANAPONDA, VIKITOKA HAPA VINAMUANDIKIA NYO, NA HAPO MUORODHESHAJI UMESAHAU http://www.afrointroductions.com/ ambao hamjui kuwa watu wanatafutia wachumba mitandaoni ingia hapo kama hamjakuta madada zenu wakitafuta lol.

    Endelea kutafuta kaka, ´na miaka hiyo umejichunga, kwani wengine wana haraka za kuoa mwishowe wanakufa na ukimwi wakiwa vijana.


    Kila la heri kaka, hope utampata umpendaye.


    MHAYA HALISI, KOKUSIMA

    ReplyDelete
  49. AnonymousJune 05, 2009

    Hapa sioni sababu la kulumbana. Kutafuta mchumba online ni kitu cha kawaida. Nyie wachangia maada vipi? Muacheni kaka wa watu. Na wengine muache madharau. Kama huwezi kuchangia mawazo mazuri kaa kimya. Mara "Muhaya." Tena wewe uliyesema hivyo ninakukemea katika Jina la Yesu ushindwe kabisa. Kama usife moyo ni majungu ya watu ni wabaya wengine na wivu kwa ujumla. Watu muache wivu. Mijibu mengine ina wivu kama Beberu. Mtu kauliza vizuri oho kabebe mabox hii inahusiana nini na mabox ama kubeba wazee. Jibu swali uliloulizwa. Kama huna usiandike uchafu wako hapa. Kwa naana hajatukana mtu yeyote. Kueni watu waelevu na wakufikirika. Watanzania mnapenda sana majumba, na ndo maana atuendelei. Huu umri hajachelewa kuoa na kuzaa watoto. Mijibu mengi imezaa watoto mapema bila kujianda na maisha yenyewe yakubabaisha matatizo kibao kila siku iendayo kwa Mungu. Lakini kaka wa watu pengine kajipanga kiaina fulani mijibu mengine inajifanya inaanza kumuhadama kama mwezi wa Ramadhani.
    Wangapi hapa mna watoto na maisha yenyewe kama sio ya kubabaisha? Watu wanazaa hati ukiwa na miaka 80 Kama yangu ujachelewa hata sekunde moja. Wengine mnaachiwa watoto na wake zenu ama waumme kutwa nzima. Ama unategeshia jirani yako ndo akuangalizie mtoto ndo huende kufanya kazi, sasa mko kwenye net eti ulichelewa wapi kuoa!!!!!!! Cha ajabu nini hapa? Mbona sioni tatizo. Kaka yangu usisikilize viruka njia. Wote tunaongia kwenye blog ni matatizo matupu.

    Tuone mawazo ya kimsingi katika jamii husika.

    MDAU-UKONGA/UWANJA WA NDEGE.

    ReplyDelete
  50. AnonymousJune 05, 2009

    Mie Ninaushauri Kwa MTAFUTAJI... Umewahi Rudi Tanzania toka ulivyotoka Miaka Hiyoooo.... Kama Haujawahi Rudi... Usiiwazie Tanzania ya 1990's... watu wake wamebadilika saana... message(Chat) haitaweza kukupa Habari kamili ya huyo unayemtaka... umekaa miaka yote hiyo... usipoangallia unaweza pata BOOM... USHAURI WANGU... UNA DOC zote za UK... Na unataka Kuoa Nyumbani Tanzania... Nakushauri Cha kufanya Njoo Mwenyewe... Ujichangulie Mwenyewe.... Nakutakia Kila la Kheri.

    ReplyDelete
  51. AnonymousJune 05, 2009

    Wadau jaribuni kutoa maoni positively sio negatively kila mara. Huwezi jua maswaiba aliyopitia kwenye maisha mpk 43 hayapata rightperson. Unaweza kuta amekutana na wanawake pretenders, ambayo sio wife materials au waliompotezea mda kwa kupindi cha ujana wake. Unajua kuwa kwenye relationship miaka mingi sio kigezo cha kusema unaright person. watu siku hizi wanaume kwa wanawake wamekuwa waongo sana mioyoni kwao. kujua undani wa mtu sio kazi raisi hata kama unaspend naye. hivyo basi Wasichana mnaweza kujitokeza kwake na kumdadisi undani na nia yake kwa kumsoma mda fulani then ukiushirikisha ubongo wako unamjua tu. ACTION SPEAK MORE THAN WORDS

    ReplyDelete
  52. AnonymousJune 05, 2009

    Mr Taymour
    pole sana,miaka 43 hujafanikiwa kupata mke anayekufaa.
    Je una mtoto au watoto wangapi?
    nimeishi uk miaka kadhaa now niko bongo,na nimewahi kununua kila kitu ktk internet,chakula,tv,kochi,nguo etc,
    Lakini Swala la MKE,rudi nyumbani utafute mke,wapo wengi sana tanzania,na kwa kuwa unaupenda utanzania,wewe rudi,chukua likizo ya mwezi mmoja or miwili.
    USIFANYE MBWEMBWE ZA UK,jifanye kuwa upo tz na wala ulaya hupajui,ndo utapata mke sahahi,kwani wakijua tu upo uk utazongwa na wanawake matapeli,
    -pia taja sifa za mke umtakaye na kabila lipi tanzania,

    ReplyDelete
  53. AnonymousJune 05, 2009

    mdau wa June 05, 2009 12:42 AM, hivi ndio kwanza uone tv toka ulipotoka kwenu shamba? ni wapi katika post ya mtafutaji amesema kuwa yeye ni virgin? mbona mnazulia mtu mambo yasio ya kweli? au unamjuwa huyu jamaa?

    ReplyDelete
  54. AnonymousJune 05, 2009

    JAMANI MBONA MMEMJIA JUU KAKA WA WATU NAMNA HII? YEYE AMEANDIKA OMBI LAKE KWA MABINTI WALIO INTERESTED WAMJIBU. SASA NYIE MNAODAKIA NA KUMHOJI KWA NINI HAJAOA AT 43, NYIE INAWAHUSU NINI? KAMA MNATAKA AWAOE SEMENI. NADHANI HUYU KAKA AMEONELEA BORA AWASHIRIKISHE WATANZANIA WENZIE KATIKA SWALA LA KUTAFUTA MKE, NA BADALA YA KUMSAIDIA MNAANZA KUMKASHIFU. KAMA ANGEKUWA NA SHIDA YA KWENDA NYUMBANI I'M SURE ANGEENDA KUMTAFUTA HUKO LABDA KWA SABABU ANAZOJUA MWENYEWE HAWEZI KWENDA NDIO MAANA AMEOMBA KUWEKWA KWENYE MTANDAO HUU AMBAO UNASOMWA NA WENGI NDANI NA NJE YA NCHI ILI ANGALAU MWENYE NIA AJITOKEZE.

    MIMI KWA KWELI NIKO INTERESTED KAMA YUKO SERIOUS, NINA MIAKA 33 NA SIJAOLEWA, WALA SIJAWAHI KUOLEWA NA SINA MTOTO. KABLA HAMJAKIMBILIA KUNIITA NINGAYEMBE FIKIRIENI KWANZA. KAKA KAMA UNA INTEREST NIANDIKIE PISCESFISH@MAIL.COM

    ReplyDelete
  55. AnonymousJune 06, 2009

    mimi mwenyewe niko interested na huyu kama, sijaolewa sina mtoto wala sijawahi kuolewa na ni bado niko bikira kabisaa, nina umri wa 32 yrs old. kaka kaka uko interested waweza kunitumia email fame77@hotmail.com

    ReplyDelete
  56. AnonymousJune 08, 2009

    heeeeeeeeeeee jamani?hahahahahaaa

    sasa ya virginity yametokea wapi?

    susan boyle virgin??makubwa

    ReplyDelete
  57. AnonymousJune 08, 2009

    usiwajali wanakuonea wivu, kazi nzuri, elimu imepanda, na kinachowauma zaidi hujajiripua mchumba utapata kutoka hapa tz nakutumia msg kujua interest zingine.

    dada yako.

    ReplyDelete
  58. DDUUUUHH!! HUYO NAYE ANA MIAKA 32 LAKINI BADO BIKIRA!! HIYO KALI SANA, HAJAWAHI HATA KUJITIA VIDOLE! JAMANI BLOGU ZINA RAHA YAKE ....!! HUYO WALA SIMTAKI BURE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...