Mmoja wa washiriki ma maonyesho ya mitindo ya mavazi , Amina Omary (19) ambaye ni mlemavu wa ngozi ( Albino) akifanya mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya kushiriki shindano la mitindo ya ubunifu wa mavazi lijulikanalo ' Nane Nane Fashion Designing Award) linalotaraajiwa kufanyika hivi karibuni mjini hapa.
Baadhi ya washiriki ma maonyesho ya mitindo ya mavazi , Amina Omary (19) ( mbele ) na Tabia Omari ( 24) ambao ni watu wenye ulemavu wa ngozi ( Albino) wakiwa katika mazoezi kwa ajili ya shindano ya mitindo ya ubunifu wa mavazi ijulikanayo ' Nane Nane Fashion Designing Award) linalotarajiwa kufanyika hivi karibuni mjini hapa. Picha na mdau wa mji kasoro bahari John Nditi


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 21, 2009

    Jamani hivi albino ni "ulemavu"? Huo si ulemavu bali ni ukosefu wa melanine pigments ambazo kazi yake nikuipa rangi ngozi! Lakini tusiwaite walemavu kwani ulemavu ni "kilema" cha viungo vya mwili. Ambavyo havifanyi kazi kabisa, nadhani tuwatafutie jina ambalo ni la heshima kidogo.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 21, 2009

    albino ni walemavu pia sababu ya ngozi yao , ni rahisi sana kupata magonjwa kama cancer. na nani kakuambia kuwaita walemavu ni kuwa kusea heshima. labda ukiwaita zeruzeru ndio utakua umechemsha.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 22, 2009

    we anonymous said umedhihirisha ulivyo mvivu wa kufikiri! yaani kwa upeo wakojina mlemavu halina heshima sio? tafakari kwanza kabla ya kutenda

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 22, 2009

    Bora katika fani ya Mavazi itawatoa endapo akiwa na shepu nzuri sababu Mavazi haviingiliani na ngozi saana. Kwa kweli hapo naunga mkono sana tena sana kwa kuwawezesha wenzetu hawa ila sikuunga mkono kwa wenzetu hawa kushiriki mashindano yale ya umiss kutokana na kigezo cha kuwa mzuri kwani uzuri hauhitaji kasoro kabisa.

    Big up dada jitahidi utafanikiwa.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 22, 2009

    KUNA KASORO GANI KUMTAJA KAMA NI MSHIRIKI BILA YA KUTAJA HITILAFU ZA MAUMBILE YAKE? MIMI NINAMUONA KUWA NI MSHIRIKI KAMA WALIVYO WENGINE, KWA HILO HUENDA MIMI NINAMAKENGEZA. ENDELEENI KUMBAGUA KWA KUWEKA MBELE HITILAFU ZA MAUMBILE YAKE KWANI HUO NI UTASHI WENU.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 22, 2009

    Yaani anony.wa kwanza hiyo comment yako ya kwanza sio kweli kabisa. Kuwa kilema haimaaninishi ni kwa viungo vya mwili tu, hata akili, hata ngozi (kwa mwili kutoweza kutengeneza melanine pigment kwa ajili ya rangi ya ngozi) is still a disability/ulemavu. -mbuta

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 22, 2009

    weye michuzi vipi yakhee?? kwani lazima utwambie kama hao ni walemavu wa ngozi? sisi wenyewe twawaonaaaa. maana ukiwataja hivyo haipendezi hata kidogo? mie ningekushauri uwataje kwa hiyo sifa yao ya urembo na uache hiyo hitilafu yao ya ngozi

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 23, 2009

    Michuzi sidhani kama unahitaji kutaja kwamba walemavu wa ngozi wewe weka picha na maudhui wadau tutaona wenyewe, mi nadhani nyinyi waandishi wa habari ndo mnaongeza kasi ya watu kuwafikiria vibaya hawa wenzetu.Nakubaliana na mawazo ya Omar Said.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...