KUTOKANA NA KWIKWI KATIKA UONGOZI WA JUMUIYA YA WABONGO HUKO WASHINGTON DC , AMBAKO GLOBU YA JAMII IMETHIBITISHA KWAMBA KUNA MAKUNDI MAWILI YANAYOTOFAUTIANA NA KESI IPO UBALOZINI KUPATA UFUMBUZI WA NI UPANDE UPI HASA UNAOSHIKA UONGOZI HALALI WA JUMUIYA, NA KWA MASIKITIKO MAKUBWA NAOMBA MSAADA TUTANI TOKA KWA WAHUSIKA KWA NIA NJEMA TU.
MSAADA NINAOOMBA NI KUKUBALIWA KUSITISHA TANGAZO AINA LOLOTE KUTOKA WASHINGTON DC HADI HAPO UTAPOPATIKANA UTHIBITISHO KUTOKA CHANZO HURU (MFANO UBALOZINI) KWAMBA UPANDE FULANI NDIO ULIO HALALI KUENDESHA SHUGHULI ZA WADAU WANAJUMUIYA YA WABONGO WASHINGTON DC.
GLOBU YA JAMII, AMBAYO NI KWA WADAU WOTE ULIMWENGUNI, ISINGEPENDA KUJIINGIZA KATIKA LIBENEKE LA UPANDE WOWOTE, HIVYO PANDE HUSIKA ZINAOMBWA KUKAA CHINI NA KUFIKIA MUAFAKA AMBAO KWA JINSI NIJUAVYO KILA UPANDE UNA WADAU WENYE BUSARA, SIDHANI KAMA ITASHINDIKANA KWANI WOTE NIA YAO NI MOJA - KUWAUNGANISHA WADAU.
HIVYO SHIME NA TUJITAHIDI TUFIKIE PAZURI LIBENEKE LIENDELEE KAMA KAWA. GLOBU YA JAMII INAZITAKA RADHI PANDE ZOTE MBILI KWA UAMUZI HUU WA KUSITISHA MATANGAZO TOKA WASHINGTON DC AMBAO NIA YAKE NI KUJENGA NA SI VINGINEVYO.
-MICHUZI
Inaelekea kwenye hizo jumuiya kuna maslahi flani hadi kufikia hatua ya kuwa na migogoro ya uongozi kama ya Simba na Yanga.
ReplyDeleteMichango ya mwezi iyo.UFISADI popote mladi wawepo Wataanzania.
ReplyDeleteHAYA NDIO MATATIZO YA KUKOSA LA KUFANYA.NA KUOTA CK MOJA MTAONGOZA NCHI
ReplyDeletematawi ya vyama yamegongana nini? tuliwambia matawi hayo yana mambo.
ReplyDeletekwani mnahitaji viongozi wa vikundi vya nini? kuweni huru mtese US, kwani raisi si OBAMA hatoshi?
michuzi acha uandishi uchwala hayo makundi yanakuhusu nini?wewe unachotakiwa ni kutoa habari tu hapa hatupigani wala hatusemeani ovyo juzi wote tulikula nyama greencastle hakukuwa za zengwe wala nini huo ubalozi unatuhusu nini?usituletee mifarakano isiyokuwepo wabongo hapa dc tunamepeana tafu kila likitokea noma huo ubalozi hatujauona hata siku moja,jumuiya hii ina katiba yake inayofuatwa siku zote utoe habari za dc utoe usitoe mpango wako sisi jumamosi tupo meadowbrooke tunajinoma,mipigo ya dc huiwezi hii tuachie wenyewe.
ReplyDeletehere we go!! hii ndio kazi ya watanzania kila walipo. kugombana wenyewe kwa wenyewe au kugombani vyeo. Hebu tuambieni ndugu zenu ni nini chanzo cha ugomci wenu? i bet ni sura ya $. Na kwa nini mnahushisha ubalozi? hamjui kama hakuna sheria yeyote ile inayosema kuwa watanzania waishio nje ya nchi wawe na jumuia yao tena iwe moja kwa kila nchi? sasa tatizo ni nini kila kundi na lianzishe jumuia yao who cares kuwa na jumuia kila mtaa.
ReplyDeleteMpasuko wa kisiasa uko Zenji wala si DC. Watu hawana time na hayo mambo. Jumuiya inayotakiwa ni ya watanzania na sio CCM. Hao watu wa CCM ndio wanaotaka kujifanya ndio jumuiya ya watanzania DC.
ReplyDeletebadala ya kupiga box mnaanzisha migogoro, inaonekana mna damu ya kifisadi.
ReplyDeleteMimi ni Mtanzania naishi Nebraska. Nasikia eti Washington D.C kuna makundi mawili [MOJA NI LA WATU WANAOJIWEZA NA JINGINE LA WASIOJIWEZA.] Sijui ni kweli ama ni maneno. Lakini kama ipo hii ni hatari kwa Watanzania. Msianzishe ukabila kama jirani zetu Wakenya kuweni kitu kimoja katika jamii husika.
ReplyDeleteMdau USA
Hii migongano ni ya kikabila au? kwani nafahamu watanzania tuna UMOJA popote ulimwenguni. Kwani huko Washington, DC kuna tatizo la nini? or just a TITLE?
ReplyDeletekama kawaida ya wananchi wa nchi za africa. kugombania madaraka,popote pale wapatapo mwanya.
ReplyDeleteanony wa june 4, 2:38 nakuunga mkono hawa jamaa wanadamu ya kifisadi. Waswahili wanasema jivi linamfanana mnyaji. Pesa za ufisadi ndizo zilizo wafikisha huko kwa hiyo wananaendeleza tu tabia ya wazazi wao ya kung'ng;ania madaraka.
ReplyDeleteMichu,
ReplyDeletePlease tunakuomba pia kusitisha matangazo ya CCM-UK.