mrisho ngasa akiwanyanyasa mabeki wa new zealand kabla ya kutoa krosi iliyomkuta henry joseph aliyemdondoshea jerry tegete ambaye alisawazisha kwa kichwa
kipa wa new zealand haamini kwamba JERRY tegete (namba 10, nyuma ya goli) kamtoboa
mabeki wa taifa stars wakiondosha hatari langoni pao
new zealand wakishangikia goli lao la tuta
ilikuwa gado-kwa-gado dakika zote tisini
nyanda shabani dihile alikuwa imara langoni

mdau mbaga wa TBC akiwajibika wakati kituo hicho cha taifa kikirusha laivu gemu hili
manahodha na waamuzi kabla gemu kuanza
neshno ilivyokuwa usiku huu. kama nou camp unaambiwa....

mashabiki toka kila kona ya jiji walikuwapo kuburudika
wana red cross walikuwepo tayari kwa huduma ya kwanza
kikosi cha huduma ya dharura cha ultimate security kilikuwapo pia

benchi la wageni
benchi la wenyeji
New Zealand kabla ya gemu
Taifa Stars

TAIFA STARS USIKU HUU IMEONDOKA KIFUA MBELE BAADA YA KUIBAMIZA TIMU YA TAIFA YA NEW ZEALAND BAO 2-1 KATIKA MCHEZO MARIDADI WA KIRAFIKI ULIOFANYIKA KWENYE NESHNO JIPYA NA KUHUDHURIWA NA UMATI MKUBWA WA WADAU.
WAGENI WALIKUWA WA KWANZA KUPATA BAO KWA NJIA YA TUTA MNAMO DAKIKA YA 10, BAADA YA BEKI WA TAIFA STARS KUUNAWA MPIRA NDANI YA 18.
STARS WALISAWAZISHA KWA BAO SAFI LA KICHWA LILILOFUNGWA NA MSHAMBULIAJI CHIPUKIZI JERRY TEGETE, ALIYEUNGANISHA MAJALO SAFI YA NAHODHA HENRY JOSEPH ALIYEWEZA KUVUKA MSITU WA MABEKI WA NEW ZEALAND.
BAO LA PILI NA LA USHINDI LILIFUNGWA NA MSHAMBULIAJI MWINGINE DOGO, MWINYI KAZIMOTO, KWA KIKI KALI ALIYOITWANGA BAADA YA KUTULIZA GAMBANI, KISHA PAJANI, PASI TOKA KWA MUSSA HASSAN MGOSI DAKIKA ZA MWISHONI MWA MCHEZO WAKATI WADAU WALIISHAANZA KUONDOKA WAKIJUA NGOMA LEO NI DROO.
KUNRADHI KWA KUCHELEWESHA MATOKEO KWANI MTANDAO ULIPATA KWIKWI KWA JAMU...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 03, 2009

    thanks usihofu michizu sometimes.. kidogo, ila tu libekene linaendelea tunakubali hilo.
    ila Stars hongera kwa hushindi dhidi kws Newzland.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 03, 2009

    Hongera starz toka kwa shabiki no 1
    mdau stellenbosch

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 03, 2009

    Safi sana, hongera sana Staaz.
    Wadau wa zomeazomea mpo? Tumwachie Maximo apunguze bangi kambini. Tegete na Kazimoto walioleta raha leo wote ni chipukizi wa Maximo. Wazee wa zomea zomea walitaka awaite Chuji na Boban.
    Huu ushindi utatupandisha kutoka nafasi ya 109 kwa mujibu wa FIFA hadi kwenye themanini na kitu. Tukipata mechi moja zaidi na timu iliyo juu itatufikisha ndani ya sabini na kutoa nafasi kwa wachezaji wa bongo kusajiliwa moja kwa moja England kwa kuwa nchi itakuwa inatimiza sharti la kuwa ndani ya 70 bora za dunia. Tuchangamke tuwape dili kina Mrisho Ngassa na Nizar Khalfan. Tukipata wachezaji wawili watatu ndani ya Premier timu yetu itatisha.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 03, 2009

    HEKO! TFF, wapi tunaweza kupata jezi za uzalendo? Mmeingia ubia na jamaa hawa au? http://www.worldsoccergifts.com/store/cpshop.cgi/soccer.2010southafrica.3495709+tanzania-taifa-stars.html

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 04, 2009

    wazee wa wivu mpo? Maximo #1

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 04, 2009

    Nafikir sasa Maximo atatembea kwa amani maana alikuwa analalamika sana walipochapwa na DRC wmashabiki mitaani walikuwa wanamuharass sana

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 04, 2009

    Huyo Mama wa huduma ya kwanza aliyevua viatu anatakiwa aonekane yuko gado kwa lolote kutokea muda wowote. Na asivae viatu vya dating, ndio maana hayuko comfortable, ana vivua. Vaa raba Mama.

    Red Cross America huwezi kuona emergency responder kaweka viatu pembeni yuko comfortable anaangalia mpira.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 04, 2009

    ongera stars kwa ushindi mzuri pia pongezi kwa kocha macio maximo kwa kazi yako nzuri!

    mdau canada.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 04, 2009

    MAFİSADİ WA ZOMEA ZOMEA MPOOOOO , NAJUA LEO MLİKUWA MOJA YA WATU MLİOSHANGİLİA , HONGERA STAZZZ KWA USHİNDİ

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 04, 2009

    IMEKAA POWA SANA JAPO KUWA HABARI ZA MPIRA NINZURI ZIKIJA NA PICHA SASA HAYA NI MAZUNGUMZO BAADA YAMPIRA,mAMBO YANAENDELEA HERI YA KIDOGO KULIKO KUKOSA KABISA.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 04, 2009

    Utasikiatu kiwango kimepanda kwa kipimo cha mechi moja.Tunavyo wai kusaau

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 04, 2009

    mara tunacheza na vankuwa whaitikapu mara nyuzilendi mara huyo mara yule...je lini tutacheza na wabrazili au waajentina ili kweli tujipime nguvu!!!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 04, 2009

    New Zealand ina nafasi gani kwenye rank ya FIFA?
    mdau kisiju.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 04, 2009

    Ngoma imeshaweka Fifa
    http://www.fifa.com/associations/association=nzl/fixturesresults/gender=m/index.html

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 04, 2009

    Madu June 04, 2009 12:46 AM, wewe kiwango unapimia nini? Kijiko?

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 04, 2009

    Mwinyi Kazimoto, japokuwa sijaona gemu hilo bao linaonekana kali, nilikuwapo uwanjani siku anapata cap yake ya kwanza mechi ya kirafiki na Zimbabwe, of course ni mara ya mwanzo anachezea timu ya taifa kwa hiyo alikuwa hajatulia sana, wadau wakaanza kuzomea atolewe, naona mambo yake yanajieleza sasa, tuwe na subira jamani,
    mdau Canada.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 04, 2009

    KUNA MDAU MMOJA ANAITWA KISIJU ANAROHO YA NYOKA..YEYE ANAANGALIA MABAYA TU..HATA WACHAWI NA WASHIRIKINA WOOTE WALIANZA NA TABIA KAMA YA KWAKE...NEW ZEALAND INAKWENDA KUCHEZA NA MABINGWA WA MABARA..INAKWENDA KUPAMBANA NA AKINA ITALY, SPAIN , BRAZIL SOUTH AFRICA KWA HIYO ILE SIO TIMU YA KIWANGO CHETU, TUNASTAHILI KUJIPONGEZA SANA TU...WATANZANIA TUNA TATIZO LAUJUAJI..TUNAJIONA SISI NI BORA KULIKO UWEZO WETU HALISI..HILO NDILO LINALOMSUMBUA SANA KISIJU NA WATU WA AINA YAKE..HATUJIWEKI KWENYE LEVEL YA KWETU TUNAISHIA KUJIFANANISHA NA WALE WALIOTUZIDI

    NDIO MAANA KUNA WATU WANAAMINIK KABISA ETI AINA HII YA WACHEZAJI TULIONAO WANASTAHILI KUFUNDISHWA NA MAKOCHA KAMA MOURINHO, FERGUSON, VAN GAAL NA HIDDINK..AINA HII YA MASHABIKI WANAJIONGOPEA NA HAWAUJUI MPIRA KWA MAANA HALISI..WANAISHI WAKIWA WAMEZUNGUKWA NA MAJUNGU NA USWAHILI NA HAWA NDI WALIOJAA KWENYE SIMBA NA YANGA.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 04, 2009

    Ahsante sana kwa mapicha yako mkuu

    KILI
    BG

    ReplyDelete
  19. kiwango cha soka angalau sasa kinakua bongo

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 04, 2009

    Bahati ya mtende ila timu bado sana bado kabisa kushinda dhidi ya new zealand sio kipimo sahií kama mnabisha mtaona kwenye mabara. Maana ukizungumzia oceanic basi Australia hua inazitungua timu za huko goli 10 hadi 30 bila sasa kuna soka huko? Poleni mnaofurahia ushindi huo maana hamna chochote cha kujivunia hapo unless si mfuatiliaji wa world football

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 04, 2009

    Hongera tena kwa ushindi Taifa Stars, mmetupa raha watanzania. at least naweza kusema, ah,tumewafunga New Zealand. Ila nina maoni kuhusu Jezi.Wahusika wa timu ya taifa inabidi waangalie jezi ya timu ya taifa upya.kusema kweli ni very ugly.Rangi mbaya,design mbaya.ya goalkeeper ndo kabisa,so ugly.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 04, 2009

    Taifa Stars hongera lakini sio saaana kwani bado mnatakiwa mkaze buti zaidi.

    Jamani tunaomba wazee wa usalama watuimarishie usalama nje ya uwanja sio tuu wakti wa takika 90 za mchezo na hata baada ya mchezo hata angalao nusu saa hivi. Wengi wetu tunahofia kuja kushangilia wachezaji wetu tukihofia wakati wa kurudi majumban kwetu kukabwa.

    Nje ya uwanja kunakuwa na vibaka wengi kwani wakati wa mechi naona wazee hawa wa kukaba ndio wanakuwa wanahamia huko. Watanzania tunakabwa na hata wageni wanakabwa. Hii inatia aibu kwa Taifa letu kwani jana mzungu alikabwa akitoka uwanjani akiwa anakwenda kutafuta taxi ya kurudi hotel alipofikia.

    Tunaomba kilio hiki kifikishwe tunatumai kaka Michuzi utatusaidia pia.

    Ahsante

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 04, 2009

    Watu huwa hawaizomei timu ya taifa au wachezaji. anayezomewa ni MAXIMO kwa kuvuruga timu na kuipangua mara kwa mara. Mechi ya jana kama wangekuwepo Athumani Iddi, Haruna Moshi na Kaseja tungewafunga hawa New Zealand Magoli hata 4-0. Ile penalt kama angekuwa Kaseja angeidaka, yule Kipa Dihile alikuwa anarukaruka tu kabla haijapigwa hatimaye akaruka baada ya mpira kuingia golini hakujipanga vizuri aliruka tu kama ushahidi, penalt kwa Kaseja ni mchezo tu ana timing nzuri sana. Ukiangalia mpira wa jana utaona mpengo ya Athumani Iddi na Haruna Moshi, maana Ngassa alikuwa anachachalika na hakuna mmaliziaji. Sijui kwanini huyu kocha anamchezesha Mgosi mwishoni, ukweli ni kwamba alipoingia mgosi aliongeza nguvu na kubadilisha mchezo. Maximo hajajua kusoma mchezo haraka.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 04, 2009

    ivi why uwa tunazomea wazalendo wetu tena timu ya Taifa??fala sana nyie watu alaaa,nchi zoote na vitimu vyao huwa wanashangilia saaana tu ata km mepigwa bao,km hamumpendi kocha mumtoe yeye na kamati lake sio kuvunja vijana tamaa...nyambafu

    aisee hongeren saaana vijana kututoa.

    km kawa viti vya ofisini

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 04, 2009

    ni kweli JEZI HAZIJATULIA
    so much crazy color yan mmebeba au meshona bendera ya Taifa??

    khaaaa ebu vumbueni rangi makini

    watu wenyewe weusi afu mirangi mweusiii tu

    ni hayo tu

    tuko pamoja vijana Taifa starz

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 04, 2009

    CAMP NOU la Tz oyeeeeeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 04, 2009

    naomba siku jamen tucheze izi mechi na england,brazil au basi netherlands

    afu siku iyo tunashangilia tu Taifa stazz ata km tutafungwa goli 50

    japo tuone tunakuwaje na tufurahi tu

    cha ndimu

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 04, 2009

    aliyekabwa pole

    wee wafikili nini uwanja tu uko uswazi TMK

    hahahahaaaaa

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 04, 2009

    Ndugu wadau, mimi niko concerned sana na kiwango cha Henry Joseph.Najua wengi huwa hatumfuatilii sana kama ilivyokuwa kwangu mwanzoni, nahisi ni kwa sababu ya jina lake, timu anayochezea na ni captain wa National team..Lakini mkimfuatilia kwa makini na kuangalia pasi ngapi anafikisha na mipira mingapi anapoteza mtakubaliana na mimi kuwa huyu mchezaji anahitaji kujua kwamba tuna expectation kubwa sana kwake..Henry kama huwa unasoma blog ya jamii naomba ujue hili kwamba pamoja na mchango ulionao, unahitaji kuimprove sana gemu yako.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...