baadhi ya wasanii wataoshiriki kwenye tamasha hilo
viongozi wa simba, african lyon, pamoja foundation na tigo wakiongea na waandishi

TIGO, SIMBA SPORT CLUB, AND AFRICAN LION WAUNGANA KUFANYA TAMASHA LA
“TUSIMAME PAMOJA KWA AJILI MBAGALA"

Dar es Salaam 04 Juni 2009 kampuni ya simu za mkononi Tigo imeamua kuungana na Pamoja Foundation, Simba Sports Club, African Lion club ya Mbagala na wasanii mbalimbali wa hapa nchini kufanya tamasha la pamoja jijini Dar jumamosi juni 6,2009 ili kukusanya pesa kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mlipuko ya mabomu uliotokea mwezi ulipita huko Mbagala.

Akiongea na waandishi wa habari Afisa Uhusiano wa Tigo Jackson Mmbando alisema tamasha litajulikana kwa jina la “Tusimame pamoja” na litafanyika jumamosi katika viwanja vya Uhuru yaani uwanja wa zamani wa Taifa. Lengo la kusimama pamoja ni kutaka kukusanja pesa ili kusaidia familia zetu zilizoathiriwa na athari ya mlipuko ya mabomu Mbagala.

Tamasha linakutanisha wasanii kibao wakali wa muziki nchini Tanzania kila mmoja amejitolea kushiriki kwenye jukwaa siku hiyo bure ili tu kuonyesha kuguswa na tatizo walilo nalo wenzetu.

Kwa ujumla hii itakuwa ni nafasi ya kipekee kwa wasanii wetu kujenga umoja na kushawishi watanzania kuunga mkono jitiada zao na kusaidia wenzetu wenye mahitaji.

MKOLONI G SOLO artist: “Pamoja Foundation na wasanii wote tumeamua kujiingiza kikamilifu katika harakati za serikali yetu kusaidia wenzetu wa mbagala kwakuwa upendo na umoja ni nguzo ya Tanzania yetu leo wasanii tutatumia sauti na vipaji vyetu kusimama pamoja na Mbagala kwa kipindi hiki.

Tunatarajia kusimama pamoja na kukutanisha mashabiki wetu wengi pamoja kutoka ndani na nje ya jiji la Dar es salaam kwaajili ya wenzetu wa Mbagala ambao bado wako kwenye shida.

Wasanii mbali mbali wanatarajiwa kutumbuiza siku hiyo wakiwemo wa nyimbo za injili, bongo Flava, Hip Hop, Taarab na vikundi vya kuchekesha vitakuwepo.

Mapato ya kiingilio kinachotarajiwa kukusanywa ndicho kitakachokabidhiwa kwa waathirika wa mabumu wa mbagala kupitia ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar.

Pia kutakuwa na t-shirt zitakazouzwa ndani ya uwanja na mapato pia yataunganishwa na kukabidhiwa kwa wahusika.

Pia kutakuwa na mpambano wa mpira wa miguu kutoka kwa timu kubwa za hapa nchini Simba Sport Club na African Lion ambazo pia zitapambana siku hiyo. Hivyo kwa wale wapenda soka wanayo nafasi ya kusimama pamoja na wasanii kuchangia kwa kuunga mkono timu hizi zilizoonyesha uzalendo kwa Taifa bila kujali tofauti za ushabiki na kuonyesha umoja.
Mgeni Rasmi siku hiyo ni Mkuu wa Mkoa wa dare s salaam Mh. William Lukuvi
Wasanii wafuatao watakuwepo siku hiyo

Muziki wa injili
Sifa, Joseph Nyuki.

Muziki wa dansi
Fm Academia, Akudo

Bongo Flava
Prof Jay, AY, Ngwair, Nakaaya, Maunda Zoro, Wanaume halisi, anaume TMK Family, Dogo Mfaume, omary Omary, MB Doggy, Mapacha, Wagosi wa Kaya, Dani Msimamo, Hussein Machozi, Dknob, Zola D, Mbishi Real, TMK majita, TMK Unit, Ali Kiba, Kikosi cha Mizinga, Bushoke, Dully sykes, Kala Jeremiah, LWP…

Taarab
Mzee Yusuph, Omary Tego

KIINGILIO KATIKA TAMASHA viti maalum itakuwa shilingi 5000 kawaida 3000 na kiingilo kwa watoto ni shilingi 1000 tu. Pia tumeandaa tiketi maalum kwaajili ya watu mbalimabli kuchangia kwa hiari za shilingi elfu 50,000/- kila moja.

Tigo Tanzania, Simba Sport Club, African Lion sports Club, Pamoja foundation na wasanii wote tunatoa shukrani zetu za dhati ka wadau wote waliojitolea kufanikisha tamasha hili bila kusahau vyombo vya habari vyote hapa nchini.
Tunaamini kuwa Pamoja Tutasimama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2009

    BRAVO...ALUTA CONTINUA. AFADHALI JAMANI MUWASAIDIE WAHANGA HII SERIKALI HATARI IMEKATAA RIPOTI YA KAMATI YA KUTATHMINI WAATHIRIKA NA KUDAI ETI FEKI. BONGO BWANA HATUAMINIANI ASLANI.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 05, 2009

    CCM WAPENI HELA YAO WATU WA DECI

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 05, 2009

    Safi sana. Ila msisahau Jumamosi yanalipuliwa mabomu mengine 11! Kwa hiyo waathirika wanaweza wakaongezeka.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 05, 2009

    wabongo nao,watu wameshapata dili hapo.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 05, 2009

    kinachoelekea sasa ni WIZI MTUPU,hii mchango kila siku na wahanga bado wanalalamika.Hivi nyie TIGO mnajipatia zaidi ya TZS 300,000,000 kwa dakika mnavyotunyonya kwenye gharama zenu kubwa, hamuwezi kutoa msaada hadi nanyi mchangishe? hiyo CSR ni kwenye madawati matano na computer zenu used tu.?tatizo letu mtachangisha na haziwafikii walengwa.na huu mfuko wa waziri mkuu wa maafa hivi huwa uanapatiwa bajeti kwa maafa gani? mbona majanga yakitokea tu haohao ndio wa kwanza kuwaomba wafadhili na wananchi wachangiane, basi tupunguziwe kodi jamani kwani kodi yote ni mashangingi na ufisadi,yakitokea majanga tuchangishane tena.umasikini hautokwidha nchini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...