Naibu Waziri wa Habari Michezo na Utamaduni Joel Bendela akifungua rasmi mashindano ya Vodacom Dares Salaam Marathon,yaliyo anzia uwanja wa uhuru kupitia Ikulu na kumalizikia katika uwanja huo leo.
Mamia ya wanariadha wakijiandaa kuanza mashindano ya riadha ya Vodacom Dares Salaam Marathon.

Mshindi wa Mashindano ya Vodacom Dares Salaam Marathon katika mbio za kilometa 21 kwa wanaume Fabian Joseph akishangilia baada ya kumaliza mbio hizo na kuibuka kuwa mshindi wa kwanza na kujinyakulia kitita cha shilingi Milioni 1.
Mshindi wa Mashindano ya Vodacom Dares Salaam Marathon katika mbio za kilometa 21 kwa wanawake Sara Ramadhani akishangilia baada ya kumaliza mbio hizo na kuibuka kuwa mshindi wa kwanza na kujinyakulia kitita cha shilingi Milioni 1.
Naibu Waziri wa Habari Michezo na Utamaduni Joel Bendela wa pili kutoka kushoto akishiriki katika mbio za kujifurahisha za Vodacom zijulikanazo kama Vodacom 5 KM Fun run,(kushoto)Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru,watatu Mbunge wa zamani wa jimbo la kilolo Venas Mwamoto,mmoja wa watoto walio shiriki mbio hizo na Mkurugenzi wa Bodi ya Kampuni ya Vodacom Tanzania Peter Kisumo.




Afisa Habari wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu akipeana mikakati namna ya kupata habari na Mwandishi mwandamizi wa shirika la utangazaji la kimataifa BBC Abdalah Majura,kabla ya kuanza mashindano ya Vodacom Dares Salaam Marathon.

Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru akimpongeza mshindi wa pili katika mbio za kilometa 21 Martin sule,(kushoto)Naibu waziri wa Habari Utamaduni na michezo Joel Bendera.
Mshindi wa Mashindano ya Vodacom Dares Salaam Marathon katika mbio za kilometa 21 kwa wanawake Sara Ramadhani akipokea zawadi ya kuwa mshindi wa kwanza toka kwa Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Joel Bendera,(kushoto)Mkurugenzi wa Bodi ya wakurugenzi wa Vodacom Peter Kisumo.
Mmoja wa watoto alieshiriki mbio za Vodacom Dar Marathon kilometa 5,Zijulikanazo kama Vodacom Fun run akikabidhiwa zawadi baada ya kuibuka mshindi mdogo kuliko wote.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 22, 2009

    Mashindano kama haya yangesaidia kupata wakimbiaji wa timu yetu ya Taifa,bila kumuajiri maximo wa mbio.
    I `m just think.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 22, 2009

    safi sana safi sana

    jamen tutoe mafuta kwa mazoezi

    mwanza mbona hamji?kila siku arusha,kili na dar

    khaaaaaaaa

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 22, 2009

    Kwa kweli inapendeza na kutia moyo kuona vitu kama hivi vinafanyika hapa nyumbani,Si kwa kweli si mchezo Martina Nkurlu nimekuona bana hahahaahh long time sana mazeiya inapendeza sana piga kazi ili tuendeleze hili libeneke!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...