Meneja Uhusiano wa Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule (kushoto) akikabidhi mabati kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia, Lewis Kalinjuna kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa shule ya sekondari Kitomondo, wilayani humo.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule (kushoto) akikabidhi mifuko ya saruji kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia, Lewis Kalinjuna kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa maabara ya shule ya Kitomondo.

Meneja Uhusiano wa Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule (kulia) akikabidhi kemikali kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kitomondo, kwa ajili ya kusaidia mafunzo kwa njia ya vitendo katika maabara ya shule hiyo, wilayani Mafia.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hamisi, North Caroline, USAJune 13, 2009

    Asanteni Voda kwa msaada wenu katika kuinua kiwango cha elimu huko Mafia. Wananchi angalieni msaada huo usiingie kwenye midomo ya mafisadi viwembe.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 14, 2009

    mabinti wamependeza na hijab zao.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 14, 2009

    E bwana huyo MKURUGENZI siyo ULIMWENGU MANZI huyu jamani!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 14, 2009

    Rostam kuingia biashara ya TV?

    Habari ambazo zinaingia taratibu na kuthibitisha kile ambacho kimetarajiwa kwa muda mfanyabiashara maarufu toka Igunga na Mbunge wa Jimbo la Igunga Mhe. Rostam Aziz inadaiwa yuko mbioni kuingia katika umiliki wa kampuni ya ya utangazaji wa Televisheni. Habari hizo zinatudokeza (exclusively) kuwa baada ya matukio ya wiki iliyopita ambapo mmiliki wa makampuni ya IPP Bw. Reginald Mengi aliwataja wale aliowaita "mapapa wa ufisadi" akiwemo Bw. Rostam sasa na yeye ameamuka kujibu mapigo.
    Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na malalamiko kuwa Bw. Mengi anatumia vyombo vyake vya habari katika kuendeleza kile anachokiita mapambano ya ufisadi na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakitajwa kuwa ni mafisadi wakijikuta hawana ubavu wa kushinda naye. Licha ya kuanzisha vyomo mbadala vya habari kama magazeti na ushirika wa radio bado kundi la watu hao wanaona kuwa matangazo ya televisheni hayajawapa nafasi ya kutosha na hivyo bado imebakia kuwa ni himaya ya Bw. Mengi.

    Katika kutekeleza mpango huo, inadaiwa na chanzo chetu kuwa Bw. Rostam ambaye anahisa katika kampuni ya Vodacom na ushirika wa karibu na wadau wengine wa kampuni hiyo anataka kuunganisha biashara hiyo ya televisheni na mambo ya simu ambapo minara mikubwa ya kurushia matangazo ya simu inaweza pia kutumika kurushia matangazo ya televisheni.

    "anataka kutumia mtandao mkubwa wa Vodacom kwa ajili ya mambo ya televisheni" amesema mtoa taarifa wetu. "Kwa vile kampuni yake ndiyo yenye mtandao mkubwa hapa nchini basi itakuwa ni rahisi kwake kusikika nchi nzima kuzidi vyombo vyote vya habari.Iwapo mpango huo utatekelezwa basi mfanyabiashara huyo atakuwa anaongoza kusikika eneo kubwa nchini."ga alisema.

    Huko nyuma Bw. Rostam aliingia katika umiliki wa gazeti maarufu la Rai ambalo katika enzi zake lilivuma kwa hoja mahiri, habari za kina na taarifa zisizokuwa na mfano. Hata hivyo, baadaye gazeti hilo lilionekana kuwa na mrengo fulani wa kisiasa na matokeo yake waanzilishi wake wakajikuta wanaliacha na kwenda kuanzisha magazeti mengine.

    Mtindo huu ndio unatarajiwa kufanywa ambapo Bw. Rostam (yawezekana na wahusika wengine) wataamua kununua hisa kwenye mojawapo ya makampuni ya televisheni ambayo ni marafiki kwao na kutoka hapo kuanza kuleta upinzani wa kibiashara na bila ya shaka wa kisiasa dhidi ya Bw. Mengi.

    KLHN Inaendelea kufuatilia habari hii.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 16, 2009

    Wewe unaongelea biashara za Rostam una lako jambo, kama una mtaka mengi sisi tunataka ukweli kalagabaho na uchochezi wenu.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 17, 2009

    MISADA TULEETEENI WAKAZI WA MAFIA LAKINI KAMA MNAVYOONA JINSI TUNAVYOLEA WATOTO WETU KIHESHMA NAKIADABU, KWANZA ANGALIA WALIVYOPENDEZA, ISIJE LEO AU KESHO MNATULETEA HABARI ZA UMODO MASHULENI TUTAWACHINJA!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...