Kaka, hii imetokea leo alfajiri pale Tabata (Madonna Hospital), na kusababisha bonge la foleni kubwa. Hata sijui pailoti alikuwa anataka kutua wapi. Nasikia wiki iliyopita mambo yalikuwa hivi barabara ya kawawa rodi
Kazi njema kaka
Mdau Tabata


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2009

    jamani hili tatizo la Makontena kuanguka hapo hapo si mara moja ni kila baada ya miezi miwili mitatu huwa yanadondoka, labda serikali itusaidie kutatua hili tatizo manake siku litakapodondokea daladala likiwa na abiria ndo serikali itaamka, na tumshukukuru Mungu kwa kuwa haijawahi kutokea mtu kuumia au kudhurika. ila ikitokea hivyo itakuwa ni madhara makubwa sana. tunaomba serikali itusaidie sisi tunaotumia hiyo barabara hata kuweka sign kuwa kuna kona mbaya au mteremko mbaya.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 22, 2009

    kaka michuzi sio wiki iliyopita tui tabata kwa kweli karibia kila mara utakuta foleni kubwa ukiuliza kontena limedondoka ni zaidi ya mara 2 sasa tunapata kesi hiyo kwakweli wakazi wa tabata tunapata shida sana ukifikiria barabara yenyewe nii ndogo magari mengi sasa makontena makubwa yanapopita kule matokeo yake hudondoka pale ni shida sana,tunaonomba wahusika wafanyie utatuzi suala hili kwani linatukera sana wakazi wa tabata.mtu unatoka kazini saa kumi na moja unafika nyumbani saa tano usiku kweli jamani.tina

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 22, 2009

    Mbona mahali hapo ni kawaida malori makubwa kupata ajali na kusababisha foleni za ajabu ajabu kila kukicha. Foleni za hapo tumezizoea iwe tunakwenda au tunatoka makazini.

    Pia barabara hiyo hadi Segerea kwa bibi kwa kutengenezwa kila siku ni kawaida. yaani wataweka leo lami na baada ya miezi kama mitatu mbele lami iliyowekwa inakuwa imeshachakaa na kukwanguliwa kuwekwa lami nyingine. Na muda huu wanaume wako kazini kukwangua kipande cha barabara. Miezi mitatu au minne mbele watakwangua na kuweka lami mpya kutengeneza noti! Kama siyo kitega uchumi cha wakubwa tuelewe nini basi? Hii ndiyo Bongo bwana.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 22, 2009

    Hii Ngoma ilimshinda jamaa then ikapiga "Rivesi" fasta hapo mlimani..

    Style hizi huwa ni kawaida sana hasa Utingo anapopewa Funguo ili alitoe CCM (parking) na alisogeze karibu na Gest alipolala Dereva.

    Hayo Madude yanataka uzoefu, siyo tu kulenga barabara kama
    vi-corolla waendeshavyo Dada zetu.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 22, 2009

    Hii ndio hali halisi ya Kitanzania sheria hamna mtu anaweza kufanya analotaka kwakuwa ana uwezo wa kipesa au anajuaana mkubwa fulani. Hii barabara ninavyoijua mlori mkubwa kama huo ulienda kufanya nini huko? Alama zipo lakini watu vichwa ngumu. Viboko ingekuwa dawa murua kwa watu kama hawa.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 23, 2009

    Wewe anon wa 3.30 badala ya kuchangia kuhusu tatizo la hatari la makontena kuanguka barabarani unaleta dharau kwa wanawake. Hivi watu wengine huwa hambadiliki na wakati mkaanza kuonyesha japo chembe ya heshima kwa mama na dada zenu? Kama una mke kweli unamheshimu wewe kama unaweza kuandika sentensi kama hio hapa? Naomba Mungu akupe hekima kwa kweli.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 23, 2009

    Jamani bongo si ni tambarare? sikujua tambarare mambo kama haya yanatokea, foleni masaa 4 nakuendelea? tambarare ni kupaa hamna dk mbili zakupoteza ovyo. goodluck na tambarare yenu!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 23, 2009

    naungana nawe 12:36am

    uyo annon 03:30pm...sijui kabanwa na ngiri,sijamuelewa anaposema vi-corolla-----

    sio kosa lako nafikiri ngiri tu km sio bu..s..ha linaanza kukubana

    uo ni wivu baada ya kuona kinamama wanabanana kwa kwenda mbele

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 24, 2009

    haya sasa juzi kontena jana tena narudi nyumbani foleni tena tabata mgari mkubwa umeharibika sijui umeshingwa kupiga rivasi pale pale tabata relini jamani.natamani niwe kiongozi mkubwaaaa niamue mwenyewe,wee anonmy wa 3:30 eti vikolola una hasiraaaa kwasababu haunaaa eeeeeeee na madada ndio wanaoongoza kwa magari hapa mjini,shauri yako njoo tukutunze wewe angalia kijana.Tina

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...