Xabi Alonso wa Liverpool akiongea na akina Dada hawa wakati wa mazoezi na vijana kwenye moja ya shule huko Singapore, Liverpool wanacheza na Kombaini ya Singapore kwenye mchezo wa Kirafiki hapo jumapili.
Mashabiki kibao wa Bwawa la maini hapa Malaysia wamekodisha mabasi ambayo yanaondoka jumamosi usiku kwa ajili ya kwenda Singapore kuona Mechi hiyo, Malaysia – Singapore ni mwendo wa masaa 5 kwa basi, (ila kama Buffalo ni masaa 3 tuu... kudadadeki). Spoti na starehe kama kawa ndani ya nyumba.
Wiki iliyopita (17th July) Manchester walikuwa hapa ambapo walicheza mechi ya kirafiki mechi iliyokuwa ya kwanza kumtambulisha mchezaji Michael Owen ambaye aliingia dakika ya 60 na kupachika bao.

Timu za Uingereza zimekuwa na ushabiki mkubwa katika Asia na zinafanya vizuri kwenye upande wa masoko ya bidhaa zao na mashirika mbali mbali ya Asia yamekuwa ni mmoja wa wadhamini wa timu hizi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 25, 2009

    Eti owen kafanya nini?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 25, 2009

    wewe anon hapo juu sat jul 11:23:00am,

    hana maana hiyo unayofikiria, mii nadhani unafikiria dakika 69 au sio!

    P.E.D

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...