Brother Michuzi,

Mheshimiwa mkuu wa wilaya, balozi wa nanii, mzee wa libeneke; natanguliza shukrani kwa kuweka uchungu wangu kwenye mtandao wetu wa jamii kuhusu wizi wa mizigo eapoti yetu ya uwanja wa ndege

Kwa kuwa wadau wengi wamelalamika sana kuhusu hii kitu, leo nimeamua kuwasiliana na watu wa Swissport ili kupata picha kamili.

Kwa ufupi nimeongea na maofisa wawili, mmoja ni bwana Daniel ambaye ni ofisa wa cargo. Yeye alisema hausiki sana na mizigo midogo, nikamuuliza kama kuna utaratibu unafanyika kupunguza wizi akasema kuna hatua kadhaa zinachukuliwa ikiwa ni pamoja na Airlines kushusha mizigo yao wenyewe (kukodisha watu wao wa kuhandle mizigo).

Bwana Daniel alini-direct kwa bwana Michael ambaye ni mkuu wa usalama wa eapoti ya uwanja wa ndege wa Dar. Michael yeye akasema wao hawawezi kubeba lawama kwasababu wakati mwingine mizigo inaibiwa njiani kabla ya kufika Dar. Akatoa mfano wa Ethiopian Airline ambapo mizigo ilikuwa inaibiwa kabla ya kufika Dar. Na akasema unapokuwa na transit, or stop nyingi then risk ya kuibiwa inaongezeka.

Mimi nikamwambia kwamba watu wengi wanalalamika kwamba mizigo inaibiwa pale inapopakuliwa kwenye ndege kabla ya kuwekwa kwenye konveya beliti; akasema kwamba inawezekana ila wanafuatilia ili kukomesha.
Anyway hayo ni majibu ambayo kila mtu aliyategemea, sasa mimi nilimuuliza nifanye nini ili next time nikija nilete hata sabuni ya kuogea. Akasema kabla ya kupanda ndege wapigie simu swissport Dar, ulizia kitengo cha security wambie utafika na ndege gani; basi watafuatilia mzigo wako kuanzia Kilimanjaro mpaka Dar. Najua ni usumbufu ila ndo hivyo ni bora usumbuke na simu kuliko kuibiwa vitu vyako.

Vile akasema hakikisha kabla ya kusafiri pima mzigo wako, andika exact weight na ukifika Dar pima tena kabla ya kuondoka Eapoti ili kuhakikisha kila kitu kiko salama.
Hii hapa ndo website ya swissport Bongo
http://www.swissport.com/network/company.php?id=321

Hicho ndo kidogo ninachoweza kufanya, kama kuna mtu atapata njia nyingine tafadhali tusaidiane kwani hii ni haibu kwa nchi na inakatisha sana tamaa.
Brother Michuzi influence yako Bongo ni kubwa kichizi, ukitusaidia kama hivi kila mara tutashukuru sana. Maana toka uitundike ile part I eapoti palikuwa hapakaliki na mizigo ya abiria inapewa ulinzi utazani JK!

Mdau mwenye usongo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 25, 2009

    Hapo Airport hata utume kin..si, wataiba. Hivyo vitu hatuokoti jamani!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 25, 2009

    wizi mtupuu, hao jamaa wa air port wanacheza dili na vijana wa mtaa wa samora, kwa kuzidiza kelele hizi za vilio itasaidia kupunguza aibu hii ila wizi hautakwisha.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 25, 2009

    michuzi naomba nipachike hili japo litawauzi wengi lakini huu ndio ukweli wenyewe na hii ni salama kwa watu wote pamoja na wewe michuzi hasa hiyo Kamera yako.Mimi nina rafiki yangu anafanya kazi kitengo cha RAMP'Na hawa ndio wahusika wakubwa wa kupakia na kupakua mizigo,ushirikano wao unaanzia kwa Askari Polisi aliyeko nje ya ndege,security wa swissport,supervisor anayesimamia ndege pamoja na Bosi mkubwa wa shift,Sasa wizi unakuwaje?wale jamaa wa ndani ya ndege(hold)ambao wanapakua mizigo mle ndani wana funguo za kila aina ya begi na wale wa nje kama nilivyosema kazi yao kubwa ni kutoa ulinzi kwa wale jamaa walioko ndani ya ndege,sasa mle wanafungua mabegi yote ambayo wanahisi kuna chochote chenye Thamani kuanzia camera,pesa,cheni na chochote kile.Baada ya hapo mali inauzwa njia panda Aerport au kama ni thamani kubwa mali inakwenda mitaa ya Kariakoo au Samora Avenue.Ni history kubwa lakini kamera kama yako kaka michuzi ikiibiwa inaweza kuuzwa kama 1,50000/= hadi 200000/=.Hivyo wale wote wanaoibiwa jaribu kutembelea maeneo hayo jifanye kama vile unatafuta kununua kati ya hivyo ulivyoibiwa,Baada ya hapo mgao unatembea kwa wale wote niliorodhesha,hivyo ni channel kubwa na meneja mkubwa naye huwa anapewa manukato'colone'

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 25, 2009

    Kuna watu wengi wanaishi kwa kudalalia mizigo inayoibiwa hapo Airport kuna mtu anauza laptops na Camera tuu zinazoibiwa Airport na jamaa alikuwa Polisi zamani anakaa Chang'ombe.
    Sasa hebu niambie huyo Mkuu wa usalama ana share yake kwa jamaa na kila wakiuza analipwa. Ushahidi upo

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 25, 2009

    huyo jamaa anayesema mizigo inaibiwa kwenye ndege au Ethiopia ni mwongo. mimi nimesafiri mara nyingi wakati mwingine huwa nashukia Nairobi na huwa natumia ethiopia au Egypt au KLM. mara zote nikishukia nairobi huwa siibiwi lakini niliposhukia dar mabegi yakatoka matupu.

    ni hapo hapo uwanja wa ndege. hao usalama waache kuwa ongo.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 25, 2009

    Mbona mimi sijaelewa anaposema inabidi upige simu kabla hujaondoka ili wajue utasafiri na ndege gani ina maana kila mtu akipiga simu si itakuwa vurugu. Kwanini wasifikirie njia ya kulinda mizigo yote tu?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 25, 2009

    hii ya uzito nilikutana nayo INDIA madrass, ambapo waliopotelewa mizigo au kupungukiwa uzito tofauti na ujazo wao wa awali,kulikuwa na kitengo cha malalamiko ya mizigo, na kama umepotelewa mzigo kabisa, walitoa pesa fulani ya kuanzia kama laki mbili bila kujari mzigo wako unanini, na walifuatilia mzigo umepotea wapi. hii inawezakuwa nzuri nafikir, lakini tupige kelele hadi kieleweke.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 25, 2009

    MAJIZI MATUPU. Ni aibu kwa Temu na Kampuni nzima!! Wawajibishwe!! Serikali iko likizo nini?

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 25, 2009

    Jamani kutokana na hali kuwa mbaya inatubidi tuwe tunashukia uwanja wa Jommo Kenyatta jijini Nairobi kwani huko kuna usalama zaidi. Halafu unachukua basi mpaka Bongo maana haina jinsi sasa. Cheni ya wizi huo ni kubwa mno wapo vigogo wakubwa huwezi kuamini. Kaka yangu anafanya kazi huko, vitu alivyokuwa ankujanavyo home ni balaa, niliwahi kumchoma, lakini bosi wake aliniambia najifanya najua sana enhee, nikatimuliwa home. mara nyingi huwa naenda Japan na Ufilipino na wakati wa kurudi napitia Nairobi au Malawi, then nakuja na basi. Hilo suala haliwezi kuisha na wabongo hawatakaa waendelee ng'o.Inauma sana wajameni.

    Mdau namba mbili.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 25, 2009

    Point zangu ni mbili tu mdau alieleta post hii azisikie na kuzifikisha tena kwa hao waliotowa majibu.

    1. Suali la Airlines kushusha mizigo yao wenyewe (kukodisha watu wao wa kuhandle mizigo). hili litatatuaje tatizo la kuibiwa ikiwa waajiriwa wenyewe ni wabongo? au wanakusudia kuwa kila shirika lilete wafanyakazi kutoka nchi zao? as long as wapakuze wa mizigo ni wabongo basi hakikisha wizi utabaki, hii sio solution.

    Suali la pili: sio kweli kuwa wezi hutokea zaidi kama una transit nyingi. nimeibiwa mara mbili kwa kuvunjiwa kufuli za begi zangu na niliingia na direct flights.

    Nakumbuka ni muda mfupi tu kuna muimbaji mmoja alifika bongo na baada tu ya kupita immigration akajikuta mobile yake ishatekwa ilhali alikuwa nayo muda wote alipokuwa ndani ya ndege. sasa hapo u-transit ulikuwepo wapi?

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 25, 2009

    ili tatizo inabidi lipelekwe kwa raisi JK lishugulikiwe, kidogo itasaidia kama alivyosaidia mengineyo. tukibaki tunablogi mda wote ni kazi tupu.

    Pia swala hili ni sawa na swala la wizi wa parcels POSTA. barua za maana (documents).

    kAMA KAKA MICHUZI INAWEZA KUFIKISHA MALAMIKO YETU MAFUPI HUKO NYUMBANI TUTASHUKURU SANA.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 25, 2009

    huyo afisa aliyekwambia uwapigie simu swissport Dar kila unaposafirisha mzigo, anakichaa. Kwani wangapi watakuwa wanapiga simu....
    sampuli ya maongezi itakuwa kama hivi

    Wewe: ati jamani....
    swissport: eeeeeh.....
    Wewe: nakuja na begi lenye laptop, saa za bei, camera, navitu wa thamani kubwa...
    swissport: ndio bwana... rangi gani begi lako...
    Wewe: rangi ya zambarau...
    swissport: oki basi likifika tutaling'ang'ania hili.


    unafika bongo usije ukaona begi lenyewe halijafika kabisa!!!


    P.E.D

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 25, 2009

    Samahani wakuu huu wizi mnauzungumzia umerudi tena? Sababu mwaka 2006 kule Swiss Port waliweka kamera (cctv) kwenye warehouse kote na tv yenyewe ilikuwa ofisini kwa meneja wao. Wizi ulipungua au kwisha sababu niligundua hata wakina dada walikuwa waaancha pochi zao bila wasiwasi wowote..!! Imenisikitisha sana kuona sasa wamerudi tena; pengine zile kamera ziliharibika na kama kawaida yetu Tz mafindi uchara wakashindwa kuzitengeneza.


    All in all, Tanzania inakatisha tamaa in so many levels. Yaani hata mtu ujitahidi vipi; Tanzania ni sawa na kulea mtoto mtukutu ambaye huna cha kumfanya zaidi ya kumvumilia na kuendelea kumlea taratibu.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 25, 2009

    mmh, hii kali, huyu afisa anayeitwa michael anachemka. ivi kazi yao ninini???. yaani kila ninaposafiri nipige simu niwaambie kuwa nasafiri???. kwanini mizigo haiibiwi tunaposafiri toka dar kwenda ulaya na amerika???. juzi kapuya amesema bungeni,watanzania wengi siyo waaminifu, wezi, wavivu, walalamishi. hii ni laana.marangapi shirika la posta limepoteza mizigo ya watu???, kwanini mizigo inapotea inapofika tanzania na si inapotoka tanzania??? aibu sana

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 25, 2009

    HAO MAOFISA PIA NI WEZI, CHA MSINGI WATANZANIA TULIOKO HUKU NJE KAMA TUNAENDA NYUMBANI NA TUMEBEBA VITU VYA DHAMANI NI BORA TUSHUKIE KENYA NAIROBI NA TUCHUKUWE BASI KWENDA TANZANIA, NI BORA ADHA KULIKO KUIBIWA. MPAKA HAPO MAMBO YATAKAPO REKEBISHIKA, NA PIA TUWAAMBIE WATALII WASISHUKIE TANZANIA WASHUKIE KENYA NAIROBI, WE CAN DO IT BY INFORMING THEM VIA VARIUOS WEBSITES AND TELEVISIONS CHANNELS HERE ABROAD, MPAKA SERIKALI ITAPOONA INAKOSA KIPATO TOKA KWA WATALII, OR EVEN WE CAN ADVICE THE TO AVOID TANZANIA IN TOTAL AND GO TO OTHER COUNTRIES (ELSEWHERE).

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...