Ndugu michuzi,
naomba tu uwajulishe ndugu zangu watanzania kwamba kuni hii DV Lottery unapocheza na kushinda waweza kuja kuishi na kufanya kazi Marekani.
Watanzania wengi tuwe tunaijaribu maana kwa sasa tunapigwa bao kwa sana na watani wa jadi. kucheza kwake ni free na link ni hii hapa http://travel.state.gov/visa/immigrants/types/types_1318.html

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 05, 2009

    Wazo ni zuri na mie pia naunga mkono kuwa Wa TZ nao wacheze kwa wingi hiyo lottery. The only thing: DV - 2009 na DV 2010 zilishapita na sasa wale waliocheza DV - 2010 wanaweza kuangalia matokeo ktk http://www.dvlottery.state.gov.
    Iwapo hakutakuwa na mabadiliko, basi tuchezeni DV-2011 ambayo, most probablly, itachezwa from Oct 2 to Dec 01 this year.
    Blackmpingo

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 05, 2009

    Kaka thanks for the information nilikuwa nataka sana kujua hilo lakini nilikuwa nashindwa nianzie wapi! Ni vizuri kwamba umetuonyesha njia na kututaarifu kuwa dv 2011 itachezwa october - december 2009. Sasa swali langu ni kwamba hivi zile passport size digital photos huwa zinapatikana wapi? please kwa wale mliowah kucheza mara kwa mara mtuelekeze.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 05, 2009

    Hivi nani kawaambia kuwa watanzania wanataka kuja kuishi Marekani?! Nendeni nyie mnaotaka. Sisi wengine humu humu na tutahakikisha hatukoki, labda kwa majukumu ya kitaifa.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 05, 2009

    Asante saana uliotoa link hii. Naona wabongo wengi hawastukia hii deal, Wakenya waijua ile mbaya na wanaichangamkia ile wacha, na sasa wapo wengi saana wanaokuja kwa green kadi. Jamani hasa vijana waliomaliza form 4 au form six na collage changamkiieni hii kitu bila kukata tama jaribu tena na tena mungu siku atakusaidia. Hata kama hutaki kuja kuishi huku njoo na mikakati maana ukipata unahesabika kama raia wa huku, kwa hiyo itakuwezesha kwenda college na kulipa local tution na unaruhusiwa kufanya kazi at the same time. Ukipata unachotaka na unaona uko sawa wazeza kurudi kwenu hakuna atayekuzuia. Hivyo ndivyo walivyofanya vijana wengi kutoka Asia hasa Malyasia ndio maana wapo waliopo.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 05, 2009

    we kama hutaki kuishi na kufanya kazi marekani ni poa, lakini usilazimishe kila mtu akusikilize wewe. huyo aliyetoa hizo information amefanya vizuri kwani kunawatu wana hobby ya kutoka bongo. otherwise nashukuru kwa mdau uliyetoa hizo info ni kweli kabisa, hiyo lottery ni free. isipokuwa kinachowashinda wengi ni requirements otherwise Watz wanaotaka kucheza nyie endeeni na muda ni huo mdau alosema. thanks mdau

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 05, 2009

    UNAWEZA UKASHINDA AND STILL UKABAKI HOME. kUWA NA GREENCARD SI JAMBO BAYA.
    WEWE NDIO WALE WANAOPINGA URAIA WA NCHI MBILI BILA KUTOA SABABU ZA MSINGI NINI?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 06, 2009

    Ati unatoka kwa majukumu ya ktaifa tu. kwa vile kuna marupurupu sio. Wee unaogopa kukchacharika ili upate ticket na nauli ya kuja huku sio, Tuulize tulioipata hiyo visa ni $ tulilipa...hiyo green card bure kucheza lakini fees, doctor, nauli ya kusafirisha familia yangu etc etc inacost so much....Lakini sasa hivi hela yangu imesharudi yote mara kumi na maisha yangu ni 10 times better kuliko nilivyokua bongo.

    Acheni uvivu wabongo wa kungojea kusafirishwa na serikali...kam awewewni fisadi huna haja ya kucheza hii kitu lakini kama wewe ni mlala hoi na unaelimu ya form four ...msikatishane tamaa jaribu bahati yako.....

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 06, 2009

    mimi nina swali,mbona nasikia maisha bongo ni poa sana, tena kuna watu kazaa wametoka UK wamekuja kutembea huko wananiambia nisiogope kurudi kimoja na mimi nimeshahishi huku miaka 10,nimemaliza bachelor of science sasa kazi ni vipi sababu mimi mshiko wangu huko poa kazi zipo je bongo?na hiyo lottery ni vipi kama kazi zipo na maisha ni mazuri?

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 06, 2009

    anony wa kwanza lottery ya 2009 ishapita, tusubiri ya 2010 na sio 2011 kama ulivosema. Bongo tambarare kwa wachache ila wengi maisha bado ni duni, msitudanganye bwana, nilikuwepo huko juzi, hata apo Dar wanayoifaidi ni akina EPA tu, wananchi wa kawaida bado maisha magumu! waulizeni watz wangapi wana afford kwenda shopping mlimani city kila wiki? wachache, maana bei zao kama au zaidi ya ulaya. expensive bila sababu. ivo watu wanaoshop apo wengine ubishoo tu, same product waweza ipata kwingine kwa bei nzuri, ila wengine tunaenda mlimani city ili tuweze simulia mashoga zetu after weekend! shoga ulifanya nini weekend, nilienda gym then mlimani city bla blaaa!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 06, 2009

    Anony wa 6:55 am, nimecheka sana na maoni yako. Lakini acha utani, kuna wachache tu wanaoishi vizuri Bongo, tunachuzana tu. Kila nikija Bongo, sioni hali inabadilika kabisa. Kijijini kwangu mpaka leo hatuna maji wala umeme na watoto wanafuga nbuzi badala ya kusoma.

    Hio Green card sio mchezo hata ukishinda. Kama wadau wanavyosema hapo juu, lazima uwe na pesa ya kutosha ili ujigharamie ticket na check up. Pia, marekani kama huna elimu, ni vigumu sana kupata kazi za maana. Kuna wanafunzi chungumzima wa Kibongo wanateseka hapa kwa kuwa wanashindwa kulipa gharama za maisha. Ukienda kwenye mikutano ya kibongo, ni kupofolewa macho tu. Kama ukishinda, hongera sana lakini kumbuka kuna gharama nyingi mbele ya safari.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 06, 2009

    Nani aliyewambia kuwa maisha ughaibuni ni rahisi kama wanavyosema wengi hapa?!. Mimi nakutana na watanzania wanahangaika kama wehu. tatizo kubwa la watanzani wengi ni kutazama maendeleo ya nchi kama ndiyo fedha mfukoni. Si kweli. hapa bongo ukichakarika vizuri unaweza kuwa na maisha mazuri sana kuliko hata huko ughaibuni. La msingi tunasema-play your part.

    Hii tabia ya huku majuu kubanana kwenye chumba watu kumiau zaidi ati mna-save mimi siikubali hata. Kama kweli mngekuwa mna-save na maisha yenu mazuri, basi tungeona wazazi wenu TZ wakifurahia. Tofauti na hivyo wazazi wengi wenye watoto huko nje ndiyo wana hali mbaya sana kuliko walionao hapahapa! Wachache sana wanaweza kutamba mbele za watu kuwa nina mtoto majuu anafanya kazi.

    Kwa hiyo msidanganye wenzenu ambao wana brains nzuri za kuhangaika wakaja huko na kupotelea bila sababu. Waambie ukweli hali halisi wa maisha ya huku tafadhali.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 06, 2009

    HIYO NI BAHATI NASIBU UNAWEZA KUCHEZA USIPATE, MIMI NAISHIHUKU USA, NIMECHEZA MIAKA 15 SASA KILA MWAKA SIJAPATA HIYO NI BAHATI TU SI YA KUTEGEMEA SANA

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 07, 2009

    Kuishi nje sio kwa kila mtu. Lazima uwe na elimu ya maana ili uweze kupata bahati ya kazi nzuri. Nasema bahati kwa kuwa kila kazi inafuatiliwa na watu 200 au zaidi. Elimu yako na experience lazima iwe inatafutwa na mwajiri sio tu elimu. Uchumi wa Marekani sasa umeharibika sana, wengi wao wanaondoka kutafuta maisha nchi nyingine kama Korea, Japan, Canada na Snandinavia. Kwa sasa bora utuliye nyumbani, kwani hakuna kazi hapa. Bora jiendeleze kielimu badala ya kuvamia nchi za watu bila ya kuwa na bajeti ya kula nchi za watu. Kuishi Bongo au nje ni juu yako. Mimi binafsi naudhika sana na matatizo ya umeme, maji na elimu,na nimeweza kuishi nje kwa kutumia elimu yangu na bahati ya kazi. Nategemea kuishi nje maisha yangu yote. Lakini wenzangu wamerudi bongo na wanaendelea vizuri tu.

    Pia kama una uwezo na muda, serikali za Kanada, Australia na New Zealand wanatafuta wasomi kila siku. Kama sikosei, kama una dola 15,000 na elimu ya chuo kikuu na experience ya kazi ya miaka mitatu au mitano, utapewa viza hapo hapo Bongo ya kuishi kwao (resident/permanent visa)kama unataka kwenda kubahatisha maisha nje.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 07, 2009

    huko marekani wanatoa pipi za bure nini? au hela zinaokotwa chooni?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...