Home
Unlabelled
dk. liky abdallah aongelea soka la bongo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Mimi naomba niulize kitu kimoja tu. Licha ya kunyoa nywele na kupendeza kama kijana wa miaka 30, Dr. ametumia mbinu gani kupoteza ule unga kichwani? Yaani kapendeza sana,,,,,ametoka chicha... Hongera.
ReplyDeleteDr. Liky Naona Mswaki umekubali.
ReplyDeleteKichwa kimependeza watakoma.
Wenu Mzee wa Ununio
Yote Tisa. Kumi hiyo mechi yetu ya kirafiki na watoto wa Sadaam Mjini Iraq, ndio nahutaji habari zake. Je, tuna bullet proof vest za kutosha? Ama tutawapeleka vijana wa JKT?
ReplyDeletenaona michu kama uatuzingunguwa na vidio zako ambazo hazifiki mwisho wa maongezi- DR KIVUITU
ReplyDeleteDk licky naona leo haukwenda kazini kubeba magunia ya unga. Au mkuu wa naniii kakupa kazi ya kupiga picha? maana naona pembeni kuna PC na feni. hhahahah ongera DK lakini soka la kulipwa linaendana na maendeleo ya nchi . Bongo bado sana tusiwalaumu wadau wa soka. Hivi sasa Simba kila mfadhili ana mchezaji wake wa kumlipa mshahara biashara ikienda kombo mwezi huo mshahara hautoki je kama ndio watatakiwa kuwalipa washezaji kwa wiki si itakuwa balaaa.Yanga nao wanamtegemea Manji siku akiondoka ni balaaa tupu kama lililowakuta Moro united.
ReplyDeleteDuuh Dr.Licky unatuaangusha sasa sisi,hiyo lugha ya ughaibuni waachie wenyewe.Nimekusikia ukipata taabu sana kulitamka neno deliver.Ingekuwa vyema unge tafuta neno lake la kiswahili kuepuka hiyo fedheha ya kujiuma umaa.Ubwabwa na lugha hiyo haviendani kabisa.Ila tuache mzaha leo umetoka chicha ile mbaya!!
ReplyDeleteSamahani mdau hapo juu.Hiyo mechi na ndugu zetui wa Iraq itakuwa tarehe ngapi na mwezi gani?Sijamsikia Dr,kompyuta yangui siyo nzuri.Watachezea Baghdad au Tikrit?Ni hayo tu
ReplyDeleteDr nakubaliana na wewe lakini naona bado unaogopa au unawaogopa hao wafadhili in a fact that wao ndo wanazozihujumu hizi club mbili kubwa na kung'ang'ania mfumo wa enzi hizo za kizamani. Nakuomba Dr kama mdau mwenye mtazamo wa maendeleo ya soka bongo Vision ya kwako na G. Mpodela hazina tofauti kwani huyu jamaa halishawahi kusema Club ya yanga iwe kampuni, hii ndo proffesial mi nafikiri unachotaka kutuambia. Tuachana na mambo ya 'komando yosso' ndo wanatupotezea muda kwani wao ndo kula yao, hao ndo wananawaweka hao wafadhili na mambo kama ya channel ya mapato ya club inaishia mifukoni mwa watu, tuachane na Kudanganyikwa wadau wezangu, club hizi mbili zina fans wengi wa kutosha ku-runs kama proffesional, kweli penye miti mingi hapana wajenzi.
ReplyDeleteDr nakuomba uonane na watu ambao wanaijua vizuri 'Project Management' wakufahamishe vizuri kwani takubaliana na wewe uliposema mpira ni science. Tuachane na mfumo wa mwenyekiti, mwenyekiti wa shina sijui mwenyekiti wa tawi la yanga and so so many things which i dare even not to say.
Hivi kweli hatulioni hilo watu wamekalia kupiga domo tu kuhusu hizi club na wengi wao ndo wanafanya kama source of income kutunza familia zao, badala kuendeleza ku fainanse club
Nitakuwa wa kwanza kununua share ktk hizi club mbili kama zitaingizwa ktk soko la hisa.
Michuzi,hoja yako ya Katiba kusema michezo ni ya Ridhaa katika Tanzania ina maana sana, maana kimsingi serikali inaiweka michezo yote katika kundi moja, hivyo endapo utaruhusu(kikatiba)kuwa michezo iwe ya kulipwa, je netiboli, wavu,judo,kikapu na michezo mingine watamudu kweli?.
ReplyDeleteKumbuka kauli mbiu ya michezo Tanzania ni "Michezo ni furaha".
Dr Rikky,TFF inatakiwa ijikite zaidi katika utafiti wa kitaalam, juu ya ukuzaji wa hii bidhaa iitwayo soka,utafiti unaonyesha chochote kinachohusishwa na soka, kinauzika kwa haraka.TFF inapata udhamini mnono kuliko chama chochote cha soka katika afrika mashariki na kati,pia kusini mwa jangwa la sahara, na hii inaashiria wadhamini wengi wanapata matokeo mazuri kwa kujishirikisha na TFF.Kinachotakiwa ni kuishawishi serikali ibadili usimamizi na uendeshaji wa soka, ili muundo wake uwe wa kibiashara zaidi,huku michezo mingine ibaki kuwa ya ridhaa.Hii italeta ushindani wa kuanzishwa vilabu vingi,na wawekezaji watajitokeza kwa wingi, na hivyo serikali kupata kodi, huku maendeleo ya soka yakienda mbele. Wadhamini tofauti, na kwa kufanya hivi, soka la Tanzania litakuwa na hatimaye kila timu kuwa na uwanja wake, na maduka ya bidhaa zao, pia wanachama wanaolipa ada, viingilio, magazeti ya timu, tovuti za timu, viongozi kuwa na anuani za barua pepe, zinazoishia...michuzi@simbasports.com, au rikky@youngafricans.com badala ya yahoo...hotmail,gmail....
Kutokuendelea kwetu hakupo katika mambo ya mpira tu bali kila idara katika Nchi .Licky kuna mambo anayona kwa upe mzuri.
ReplyDeleteHuyu jamaa ni mtu aliyebobea katika field yake ya mpira. Na kweli anastahili kuitwa dokta. Watu waliochangia kusema kuwa nchi imedumaa idara zote na sio mpira tu, sawa. Lakini haina maana watu wenye upenzi na mpira waache kuweka target zao za kuendeleza mpira. Badala ya kuweka mandulele kwenye wizara, wawekwe watu wenye ujuzi wa ndani. Hatuwezi kukaa na kusema nchi haijaendelea na hivyo tusiongelee na kujaribu kuendeleza mpira. Wacha waliobobea kwenye mpira wafanye shughuli yao kuleta maendeleo huko. Mnataka wote tushike jembe tukalime? Pia sio lazima wachezaji walipwe kwa wiki kama Uingereza. Hii ni system yao ya ulipaji, yani haiko kwenye mpira tu. Sisi system yetu ni kwa mwezi, na hivyo mchezaji naye awe analipwa kwa mwezi.
ReplyDeletemtoto
Ni kweli Dr Licky anatoka mkoa wa Kigoma???
ReplyDeleteWadau tutaongea mambo mengi sana lakini kimsingi kama alivyoonea Dr ni kuwa mchazaji hachezi mpira akiwa na amani kama mshahara wake ni unpredictable.Yaani hakuna uhakika kuwa malipo yapo ama hayapo.Timu zina wanachama,wazee wa timu na mlolongo wa uongozi.TFF kutegemea viingilio.Kama huo ndio utaratibu,mpira hatuwezi.Wenzetu timu zao hazina mlolongo huo.Lazima tukubali umiliki binafsi wa timu.Mchezaji kupitia agent wake atasaini mkataba na mmiliki wa timu kutegemea kiwango chake ki-mpira.Mkataba huo unatekelezwa na pande zote mbili.Tusipobadilika tutaongea,tutasema, tutazungumza,tutabishana,tutatofautina na tutalaumiana ukweli ni kuwa hutaendelea.Bila soccer overhaul wadau tukubali kuwa mpira umetushinda.Wenzangu wenye mawazo mazuri zaidi kuhusu mabadiliko,mawazo yanakaribishwa kwa faida ya Taifa.
ReplyDeleteHiyo Katiba inayoongelea mpira ni katiba ya Chama cha Mpira au Katiba ya nchi?
ReplyDeleteBy the way Michuzi, ile timu ya kampuni ya bia haiitwi PLISNER, sema PILSNER, sawa Mkuu?
na hapa unajitokeza tena ule mgogoro unaonikereketa sana kwa miaka mingi sana: wanahabari wetu SI weledi wa lugha!
ReplyDeletehii kauli ya MICHEZO NI RIDHAA kamwe mheshimiwa mkuu wa wilaya hukuielewa vilivyo. neno RIDHAA lina maana mbili: moja ni HIYARI na nyingine ni BURE. mimi nashawishika sana kuwa maana iliyotumika katika katiba ni hii ya kwanza, yaani HIYARI. na nadhani kwa kuwa katiba yenyewe iko tangu zama za MWALIMU (wakati wa siasa ya UJAMAA) wakati ambao KULAZIMISHANA ilikuwa sehemu muhimu zaidi ya maisha ya mtanzania, na kwa kuwa yeye mwenyewe MWALIMU alichukia michezo (ukiacha riadha jeshini), ndipo akatunga hii sheria ya kuwa MICHEZO NI HIYARI YA MTU. hakuwa na maana kuwa wanamichezo wasilipwe, bali mtu asilazimishwe kushiriki michezo. na alikwenda kombo ile mbaya, sababu katika nchi ambayo kadirio la umri wa kuishi ni dogo mno, ama alitakiwa asilitie azimio hilo katika katiba, au aligeuze liwe MICHEZO SI RIDHAA, na raia washurutishwe kufanya michezo ili kuboresha afya zao na kujiongezea umri!!
na kama katiba ingemaanisha kuwa MICHEZO NI BILA MALIPO, mbona basi wachezaji wa timu ya taifa hupewa posho? vipi basi nchi isingeingilia kati Mohammed Salim alipouzwa abudhabi, Kassim Manara alipouzwa Austria?
MICHEZO NI RIDHAA maana yake MICHEZO NI HIYARI, ni ridhaa ya mtu mwenyewe.
au vipi wadau?
ahsante
Mndengereko, Ukerewe