Makamu wa Rais Dk. Mohamed Ali Shein akimshika mkono Abdallah Hassan Mitawi katika kumuozesha bintiye, Mwsanaharusi Mohamed Shein, kwenye msikiti wa Al-Ibrahim Mombasa huko Zenj mwishoni mwa wiki. Kulia kwa Dk Shein ni JK na Rais wa Zanzibar Mh. Amani Abeid Karume na mbele kulia ni Sheikh Thabit Noman Jongo aliyesimamia shughuli hiyo. Hassan anafanya kazi TVZ wakati mai waifu wake ni afisa mawasiliano Benki ya Watu wa Zanzibar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 27, 2009

    Hongereni bwana na bibi Mitawi, Mungu aibarik ndoa yenu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 27, 2009

    Huyu chalii aliye ozeshwa na hivi vichwa vyote lazima na yeye ni kichwa siku akimletea huyo manzi noma ishu anaisolve Karume.Ila hawa viongozi wanapo kwenda kuozesha kazi tulizo watuma inakuaje?na kwenda kwenye dili kama hii najua msafara lazima na watu kama walinzi na wanaitifaki kulipwa,kweli tuko freshi kipesa

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 27, 2009

    hongera ndugu yangu inshallah iwe ndoa ya kheri na mola awajaalie vizazi vya kheri.
    mdau coventry university.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 28, 2009

    Huyu wa kulia mwa Shein mbona anafanana na JK Kikwete?

    ReplyDelete
  5. Al MusomaJuly 28, 2009

    Wao wanakuwa hawameremeti?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 28, 2009

    Anon wa 07.53 ina maana mtu akiwa kiongozi asishughulikie swala binafsi kama harusi ya mtoto wake? Mbona wananchi wengine wanahudhuria shughuli zao kama hizo. Kila mtu pale alipo anafanya kazi ya kuendeleza nchi na wananchi kwa ujumla. Viongozi hawawezi kufanya kazi peke yao, tunatakiwa kushirikiana pamoja.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 28, 2009

    Mbona hatumwoni mwali? au mwali kazindwa sehemu sehemu??? Tuelemishane!!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 28, 2009

    ukurugenzi tvz uleeee...

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 28, 2009

    MUHISHIMIWA SANA MTUKUFU RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO NDUGU MRISHO JAKAYA KIKWETE NAPENDA KUKUPA TAARIFA YA MIMI KUFUNGA NDOA MWEZI UJAO PALE ST JOSEPH NINAOMBA SANA TENA SANA MUHISHIMIWA NAMI UHUDHURIE SHUGHURI YANGU.
    AHSANTE
    JOSEPH MTEMA
    MABIBO, DAR.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 28, 2009

    We Anonymous wa 12:37:00 AM hujui kusoma nini?? soma maelezo tena ya Bro Mithupu!!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 28, 2009

    Huyu anony wa Tue Jul 28, 12:37:00 AM, vipi hajasoma maelezo ya picha!! Soma kwanza maelezo ya picha ndiyo utoe maoni, usikurupuke tu!!!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 28, 2009

    hongera mwanaharusi,mungu awape amani na mapenzi katika ndoa,nimmefurahi sana kusikia harusi yako.

    ni mimi mwenzio wa kwerekwe tulosota pamoja mabanda.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 28, 2009

    Hongereni sana wazazi na vijana mliofunga ndoa. mungu awape kheri nyingi, napi pia anibariki niweze kumpata kwe mwema. inshallah, amin.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 28, 2009

    Rais mstaafu mkapa, alipokuwa katika harakati binafsi ya harusi ya mwanae na kwa kutambua kuwa hiyo ilikuwa ni shughuli binafsi alitumia basi dogo kwenda kwenye shughuli hiyo. sijui hawa wakuu wote watatu, katika harusi hii walifanyaje!!!! wadau tupeni data.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 28, 2009

    Anon wa Julai 27 07:53 usiwe na hofu kuhusu suala la watu wa itifaki na wengineo kulipwa kwa kufanya kazi. Ninapenda kukuelimisha kuwa chimbuko mojawapo la itifaki ni sherehe, dhifa na mengineyo yanayofanana na hayo, na siyo maswala ya kiofisi kama ulivyohofu. Visingekuwa vitu hivyo itifaki pia isingekuwapo. Hivyo usiwe na hofu, watu wapo kazini pia kwa maswala hayo.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 28, 2009

    Hongereni maharusi, Mungu awajalie kheri na salama ktk ndo yenu.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 28, 2009

    hivi jamani nijulisheni kama kuna kati ya hao wazee wazito wa nchi ana binti kati ya miaka 23-25 nimtilie timu kikieleweka naweka ndani na mimi!maana napenda sana miguu ya kuku iwe imezunguka harusi yangu ikiwalinda hao watuwazima!
    mzushi-UDSM

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 29, 2009

    Mbona hatuwoni maharusi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...