hapa ni maeneo ya magomeni mapipa jijini dar milango
ya saa moja kasorobo za jioni na kajua kaleeeee kanateremka mama...
raha yake ni kwamba taa za barabarani sio kwamba hazijawashwa bali haziwaki kimoja kwa sababu isiyojulikana. na kama zikiwaka mwanga wake ni hafifu kwa kuwa wanatumia balbu za watts 15 na kuufanya mji uwe kiza totoro hata kama taa za barabarani zikiwaka.
redio mbao zinadatisha kwamba wanahofia kwamba balbu zenye watts kubwa zaidi zibnakula sana umeme. Bongo tambararezzzzzzzzz....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 27, 2009

    MIMI NAKUBALI KABISA KUWA BONGO TAMBARARE ILA NINACHOSHANGAA MIMI NI KUWA KAMA TAMBARARE MBONA AIRPORT WANATUIBIA TUMIZIGO TWETU?

    AU TAMBARARE KWA KINYUME?
    ILA VIBAKA WA AIRPORT TUNAWAOMBEA NJAA YAO IPUNGUWE WAACHE WIZI KWANI INATIA AIBU TAIFA

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 27, 2009

    What!!! 15 watts?
    Hivi bulbs za taa za nyumbani si watts 40 au 60??

    Michuzi bwana hiyo sio kweli...sijawahi hata kuona bulbs zenye power ndogo kama 15W.

    Nchi hiyo wahusika wa kila sector wako likizo.....hakuna anayejali kazi anayotakiwa kufanya (over 95%).
    Wanaofanya kazi zao inavyotakiwa ni chini ya hiyo 5% I can bet my ....

    J.

    Toronto.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 27, 2009

    Mhe. Mkuu wa Wilaya na nanihii..hakika umekumbusha mbali na enzi za mchaka mchaka palue Muhimbili kwa Mwl. Ndosi...ukiingia darasani chepe chepe baada ya raundi kadha pale kidongo chekundu..

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 27, 2009

    MITHUPU NAONA ULIKUWA KOKUP JKT, NA ULIKUWA KIDOLE TUMBO!!
    DISCO HALIKUIMBWA HIVYO....LILIENDA HIVI..
    kiongozi:JUA LILE LITELEMWIKE MAMA
    kuruta: JUA LILEE LITELEMWIKE MAMA
    kiongozi:KURUTA NAOO WATELEMWIKE MAMA
    kuruta:KURUTA NAO WATELEMWIKE MAMA
    kiongozi:AI YA IYAA HUYO NAMPENDA!
    kuruta: AI YA IYAA HUYOO NAMPENDA

    mengine utajaza
    hiyo ni 1977 kabla tu ya nduli kutuchokoza.
    Na jamaa tulivyokuwa fiti mpaka leo nashamgaa!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 28, 2009

    Issa, hako ka "heading" ka "jua lile litelemke mama" wengi umetukumbusha mbali! Kulikuwa na afande mmoja (Makutupora) enzi hizo za JKT kwa mujibu wa sheria akiitwa "green kwanja", alikuwa hasikii cha mtu. Saa 10 za alfajiri anatuamsha kwenda mchakamchaka, anatuhenyesha mpaka kurudi kwenye uji saa 2 asubuhi!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 28, 2009

    Ila nikirudi kwenye mada ya taa za barabarani "Jiji la Dar" ni aibu tupu. Milingoti ipo ila taa haziwaki, na hii inasababisha usalama wa watu kuwa mdogo kwani kukiwa na mwangaza inasaidia kupunguza wizi. Yaani ukizimikiwa na gari ghafla ni heri ukimbie uiache kutokana na giza lililopo. Na ukikuta taa zinazowaka basi ni barabara mpya ambayo bado globu hazijaanza kuungua au taa kuharibika. Sijui ni kitengo gani kinachohusika, ila kama ni gharama kulipia umeme si waweke zinazotumia mwanga wa jua? Mbona Tanzania imebarikiwa kuwa na wanasanyansi na wabunifu ila vipaji vya hawa watu havitumiwi hadi wanaamua kwenda ugenini ambako wanatambulika na kuthaminiwa. Hii ni aibu kwa Jiji na nchi kwa ujumla. Inatia uchungu!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 28, 2009

    Michuzi naomba sana usiwasemee hao wanaohusika kuwasha taa za barabarani kwani JIJI sasa hivi linatisha hata ukienda pembezoni mwa mji ni giza totoro. Taa zimewekwa karibuni kwa sehemu zingine lakini ghafla haziwaki kabisa hebu fanya uchunguzi utujuze.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 28, 2009

    Ancle Michu una mambo!
    Ako kajikorasi kananikumbusha pale Rubungo P.School wilaya ya Muleba Nyuma ya Mahakama ya Mwanzo,asubuhi saa 12 kwata sana afu mnapita kwenye nyasi za kuchipua zile,kipindi icho "no shoes" ole wao wale wenzangu mimi wenye wadudu miguuni!

    Anyway tuendelee na TOPIC.
    "Sikwamba balbu zinakula umeme,ila wao ndo wamekwisha zila zile za kulipia umeme na kununua balbu"
    By Mdau Mbeki 4rm St.Joseph College of Engineering(Brigita Campus)-DSM

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...