Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 28, 2009

    Haya haya, leteni hoja za muungano waosha vinywa, manake wakubwa wanaanza kutoa vitisho `ole wenu nyie mtakaovunjamuungano?' Ni akina nani hao wanaoweza kuvunja muungano, hii sioo rahisi nahisi ni kichefuchefu cha siasa na kutafuta umaarufu. Watu wanachotaka ni kuuboresha muungano bwana!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 28, 2009

    MIMI NAPENDA KUENDELEA KUITWA MTANZANIA KATIKA UHAI WANGU WOTE,LAKINI KITU KIBAYA KINACHONIUMIZA MOYO WANGU NI HUU MUUNGANO,NAFIKIRI NI MUHIMU SANA KUUVUNJA HAUNA FAIDA YOYOTE,ZAIDI YA MANENO YASIYO ISHA ,SISI TUNANYANYASWA ,SISI TUNATAWALIWA NK WAKATI UMEFIKA WA KUUVUNJA LIMEVUNJIKA TAIFA KUBWA KAMA RUSSIA ITAKUWA SISI.WAACHE ZANZIBAR WAISHI KIVYAO,TUONE NANI ATAUMIA BARA TUENDELEE KUITWA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA WAO HIVYO HIVYO.TUSIPOANGALIA TUTAENDELEA KUZALISHA CHUKI NA KUTOAMINIANA ZAIDI NINA ASILIMIA MIA MOJA ZANZIBAR NA BARA KURA ZIKIPIGWA ASILIMIA 90% PANDE ZOTE HAWAUTAKI HUU MUUNGANO

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 28, 2009

    Haya mimi nashauri kila mmoja achukue chake.namsapoti huyo wa pili.kwa kuwa imefika sasa hata huo mkataba wa muungano watu hatuonyeshwi,kwa maana hata ndoa ina hati.na watu wa leo sio wa mwaka 1947 tuambiane ukweli vunjilia mbali.tayari mnagombania mafuta ambayo bado yanatafutwa je yakipatikana si itakuwa balaa.nasisitiza vunja vunjilia mbali kabisa kabisatumechoka sasa

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 28, 2009

    Masoud kipanya kavamiwa kule kwenye jamiiforums.com eneo la habari mchanganyiko juu ya katuni yake.twendeni tukamtetee mdau wetu.jamaa wa jamii forums wana bifu nae.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 28, 2009

    anon wa 2 umenena, tena sisi tuitwe tanganyika haswa!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 29, 2009

    ukiona jambo linafichwa na wanaosema kutishiwa amani ujue kuna mambo hapo... kama wazanzibari wameona muungano hauwafai tena nyie mnaoosha vinywa mnapata kiherehere cha nini? potelea bondeni na uvunjike....

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 29, 2009

    CHEMSHENI UBONGO ENYI WABONGO. ACHENI KUFUGA GONJWA HILO JAMANI. WAAMBIENI VIONGOZI WALIWEKE BAYANA HILO SUALA LA MUUNGANO ILI WANANCHI WALIJADILI.
    MFICHA MARADHI, KIFO HUMUUMBUA. KADRI TUNAVYOENDELA KUPUUZA HII CANCER, NDIVYO INAVYOENDELEA KUJIZATITI MWILINI. 45 YEARS YA MUUNGANO INATOSHA KUANZISHA MJADALA WA MUSTAKABALI WA MUUNGANO.
    KUNA MIFANO MIINGI DUNIANI INAYOONYESHA MADHARA YA MASUALA KAMA HAYA ENDAPO YASIPITATULIWA MAPEMA.

    ReplyDelete
  8. mzanzibariJuly 29, 2009

    Suala zima la muungano linaendeshwa kimabavu.kichuki na kiufisadi.
    Nikiwa kama Mzanzibar nina uhakika kuwa Zaidi ya Asilimia 95% ya Wazanzibar,wake kwa waume hawautaki kabisa huu muungano.
    Kuogopa na uchu wa madaraka ni sababu pekee inayowafanya hao wachache kuendelea kuutetea muungano.
    Muungano tuliokuwa nao sasa ni muungano uliandaliwa kwa makusudi ya kuidhoofisha Zanzibar,kisiasa,kiuchumi na kijamii.na ni muungano ulioekwa kuhakikisha Daima Zanzibar itaendelea kupiga magoti mbele ya Tanganyika.(fact)
    Katika Miaka michache ,tumekuwa tukishuhudia kutolewa shutuma kadhaa ambazo zinaonyesha wazi kutokuwepo na usawa ndani ya mfumo mzima wa Muungano tuliokuwa nao,Aidha pia jamii imekuwa ikishuhudia harakati za Wazanzibar wanaoipenda nchi yao kutaka kujikwamua kutokana na makucha ya udhalimu,unyanyasaji na uonevu wanaofanyiwa na ndugu zao wa Tanganyika kwa kisingizio cha muungano.
    Napenda ifahamike kwamba Wazanzibari wamekubaliana kuikomboa nchi yao sasa. pia Wazanzibari wanaamini kuwa Hakuna hujuma,nguvu wala ujanja wowote wanaoweza kufanyiwa ili kuzuiya kugomboka kwa nchi yao.
    Vitisho vinavyotolewa na kina Pinda na wenzake ni vitisho vilivyopitiwa na muda.na ambavyo havina nafasi katika karne hii tuliyonayo.
    Wazanzibar tunaamini kuwa Kuna Idadi kubwa sana ya Watanganyika wasioutaka Muungano huu.na pia tunafahamu kuwa watanganyika hao wanazo sabau nyingi na za maana zinazopelekea kutotaka kuwepo muungano huu.
    Kwa Watanganyika wasioutaka muungano tunawaeleza kuwa sisi Vijana wa Kizanzibari tunakubaliana na sabau zenu za msingi na pia tunaheshimu uamuzi wenu wa kuupinga huu muungano.
    Muda umefika sasa Kila mmoja achukuwe serikali yake na afanye mambo yake apendavyo yeye na wananchi wake.
    Bila ya muungano huu tulionao sasa Tunaamini kuwa Tanganyika na Zanzibar tutaishi kwa amani na upendo tofauti na tunavyoishi sasa kama nchi moja ambapo kila upande wa muungano umejaa malalamiko kwa mwenzake wa upande wa pili.
    Muda umefika kwa viongozi wa Tanzania kuheshimu mawazo na maamuzi ya kila upande wa raia zake na kuruhusu kuwepo na nchi mbili zitakazoheshima ulimwenguni kote nazo ni TANGANYIKA na ZANZIBAR.
    Iwapo matakwa ya watanganyika walio wengi pamoja na WAzanzibari takriban wote ya kutokuutaka huu muungano yatadharauliwa basi Tanzania isubiri kuingia katika hatari ya kukosekana amani kutoka pande zote zamuungano.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...