
Hi wadau
Hili kundi la watoto wa mitaani hapa kwenye taa za movenpick jijini Dar linazidi kuwa kubwa wahusika waamke na kufanya kitu maana in any day wataanza kuiba kwenye magari
Naomba kuwasilisha
Mdau Edwin Mac Temba
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom
Hili kundi la watoto wa mitaani hapa kwenye taa za movenpick jijini Dar linazidi kuwa kubwa wahusika waamke na kufanya kitu maana in any day wataanza kuiba kwenye magari
Naomba kuwasilisha
Mdau Edwin Mac Temba
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom
----------------------------
Asante mdau kwa kuendeleza libeneke na
pia hongera kwa kutumia vyema BlackBerry yako.
Wadau wenye nyenzo kama hiyo mnakaribishwa katika libeneke.
Leteni taswira na hata video kupitia
-Michuzi
Ndugu yangu hao si "Watoto wa Mitaani" ni "Watoto wasio na Makazi Maalum" . Kwanza hata wangekuwa watoto wa Mitaani basi Jiji lingekuwa na wajibu wa kuona wanapata huduma muhimu za Kijamii, alkini unavyojua Jiji letu hapo Dar wanashinda hata kutunza mazingira na Bustani ndogo. Wewe, Mimi, na Taifa kwa ujumla kukweba wajibu huu wakusadidia Jamii hii ya watoto tunabeza "UTU" wao na kuwaita watoto wa Mitaani. Basi ndugu yangu Mtafute sister Mmoja hapo Dar Es Salaam anaitwa Sista Jean Pruett, MM kwenye nyumaba ya sanaa au dogodogo center yoyote Dar, au Bokao au Kigogo yeye atakupatia Elimu ya kuondoa ujinga na woga wa kusaidia watoto hawa. Ubarikiwe katika kulea watoto wa familia yako, na pia jiupushe Kabisa na kuajili au kunyonya watoto.
ReplyDeleteKwanini usimshukuru Mungu baba wa mbinguni, kununua ghari isiwe tija ya watoto wa mitaani kukuibia wewe why do'nt you take them kuleena na Mhidini Issa mICHUZI NINAOMBA USINIBANIE MAONI YANGU UBAKI KUWEKA YA WATOTO WA VIGOGO KILA KITU WATOTO WA MITAANI INCLUDING YOUR NIECES,COUSINS,AND YOUR NEPHEWS
ReplyDeleteHata wewe mtoa mada ni mhusika...hao watoto wa mitaani ni sehemu ya jamii yetu. Cha msingi si kujivua majukumu ya kusaidia watoto kwa kisingizio eti kuna 'wahusika'. Wewe na mimi tujaribu kuchangia kwa hali na mali kujaribu kulipunguza tatizo hili au ikiwezekana kuliondoa kabisa.
ReplyDeleteAliyewanyima wao ndiye aliyekupa wewe
ReplyDeleteumenichefuwa kweli badala uje na aidia ya kuwasaidia unaleta utumbo wako hapa kama huna msaada si ukae kimya, au hiyo kutu unayoendesha inadhamani kuzidi binadamu wenzako??
michuzi nakuheshimu naomba usinibanie
Wadau wametoa pointi tatu muhimu, kwanza kwamba hao sio "watoto wa mitaani", pili "wahusika" ni sisi Watanzania na tatu tunapaswa kutengeneza mikakati ya kuwawezesha kuwa na uhakika zaidi na maisha yao ili wasiishie pabaya.
ReplyDeleteHakuna mdau aliyechokoza lakini kwamba ni nini hasa tukifanye ili Watanzania wenzetu hawa wapate nafuu. Kuna mwenye mawazo kwa hilo? Sina wazo kwa haraka haraka lakini litaponijia nitawapa wadau.
Kingine mdau uliyetuma taswira hii zingatia usalama barabarani. Usiendeshe gari na kupiga picha. Picha inaashiria kwamba mpiga picha alikuwa yuko upande wa kulia wa gari maana kipande cha mbele ya gari kilichoonyeshwa ni kipande cha kulia. Huo ni upande wa dereva. Pia Land Cruiser nyekundu inaonyesha kukata kona na foleni sio kubwa kwa hiyo huenda magari ya upande alipokuwepo mpiga picha yalikuwa yameruhusiwa kwenda barabara ya Bagamoyo/Ali Hassan Mwinyi. Ukichanganya hilo na uwepo wa waenda kwa miguu waliokuwa karibu kabisa na barabara kama sio barabarani kulikuwa na kila sababu kwa dereva kuongeza umakini. Tena basi kuna eneo la kujidai kwa waenda kwa miguu yaani kivuko cha pundamilia, sehemu ambayo dereva anapaswa kuongeza umakini maradufu ili kuwapa haki waenda kwa miguu.
angalia wasije wakakibia ur blackbery? or black ferry? whatever? my blackberry!
ReplyDeleteDu hii kali? this is what they call, MALAISE OF MEDERNITY, where individualism is a factor no.1 Aliyetuma ujumbe kajitoa kabisa kwenye hili tatizo kana kwamba halimuhusu.
ReplyDeleteWHY? labda kwa sababu anendesha gari na anatumia BLACK BERRY. I wonder where we are going? I don't blame him, but it shows how TANZANIANS have become so insensitive to these social calamities.
Ukiwaangalia vizuri utagundua kama hawana tofauti na wanao, wadogo zako, au wapwa zako. They only lack one thing; a family to take care of them. Kwa mazingira ya zamani, endapo moja au wazazi wote wamefariki, au wameshindwa jukumu lao, basi mjomba, shangazi, babu na bibi wanastep up kuchukua jukumu. LEO HII TUMETAWALIWA NA UBINAFSI. KILA MTU ANAJIJALI MWENYEWE.
DON'T EXPECT THEM TO BECOME RESPONSIBLE CITIZENs IF "WE" DON'T DO SOMETHING NOW.
Nilikuwa nimezoea kuona hali kama hii mjini NAIROBI, sikutegemea kwamba na sisi tutafanya the same mistake.
Mac Temba, fanyan utafiti kidogo juu ya familia yako kwa kutumia "Family Tree theory", inawezekana ukakuta nyumani kwenu kuna Ugonjwa wa akili, hivyo ni vyema kabla ya kuambukiza ugonjwa hu kwa watoto wako na wajukuu nenda hapo Muhimbili kitengo cha walemavu wa akili usaidiwe.
ReplyDeleteOnce again!
ReplyDeleteMambo vp wadau? Poleni sana na mjadala japo nami nataka nchangie kidogo.
Pamoja nakwamba ni jukumu letu ila yawezekana hata hao watoto wenyewe wakawa na matatizo pia au kama sio wao basi ni sisi walezi!
Mfano kama kuna mdau aliyewahi kufika Mwanza yaweza kunsaidia kuhusu hili.
Nakumbuka katika jiji la Mwanza pale barabara ya Balewa karibu na Shule ya msingi NYANZA nyuma ya MSD opposite Hindu Hospital kama sikosei ndipo kituo cha kulelea watoto wetu hawa kiitwacho KULEANA kinapopatikana ,mwaka 1998 watoto wote wa Mwanza walikusanywa na mzungu na kupelekwa katika kituo hicho lakini hadi kufikia mwaka ya elfu 2006 watoto wote walikuwa tayari wamerudi tena mitaani wakaendelea kuwakaba tena baba na mama zao,hasa mitaa ya Nyerere,Maeneo ya U-Turn na Nkurumah road,Makoroboi,Mwanza Hotel karibu na Kuleana Cafeteria,Nyuma ya uwanja wa Nyamagana,n.k.
Nlipouliza kwanini watoto wamerudi tena mtaani wadau wakituo kile walisema eti watoto ni wakorofi hawataki kukaa ndani na skul hawapendi kwenda ukitaka waende hadi uwape pocket money ya kutosha,so wanarudi mtaa eti kutafuta pesa kwasababu kule kituoni hawapewi pesa na kweli nlivofika kwenye kile kituo nlicheki mazingira nkaona sio mazuri tena maana hata fence ya kituo imetobolewa na hii ni kuonyesha kuwa watoto hutoroka kwa kukata fence iyo.So tuachane kuilaumu serikali maana serikali ndo sisi badala yake kupange mipango madhubuti ikiwezekana wapangiwe bajeti maalum bungeni,na elimu kuhusu uzazi wa mpango na ukimwi vihimizwe ipasavyo,sio tunawaachia hili jukumu wageni(wazungu) then wakishaondoka kurudi kwao tatizo linarudi palepale kama hilo la kuleana Mwanza.
Ni mimi mdau Mbeki 4rm St JOSEPH College of Engineering & Technology(Coet)-Brigita Campus-DSM
Kwaida Matatizo ya watoto katika Malezi yanapojitokeza kwaida wao huwa wanaashiria tatizo kwenye familia au jamii nzima- wao katika family system (Macro-approach) mtoto anajulikana kama Identified patient (IP), lakini ukweli ugonjwa unakuwa kwenye system nzima, yaani familia au jamii, kama mchangiaji mmoja alivyosema kuwa hapo mwanza "Walikusanywa na Mzungu" , tayari lugha ya kuwa watu wemekusanywa kama Mbuzi tayari ni ishara wazi kuwa taifa tayari limezama kwenye matatizo makubwa; zaidi mgeni kama mtu toka ulya au Ameirca kuja kulea watoto wa hapa Tanzania ni vigumu mno, kwani tamaduni zinakuwa tofauti, kwani malezi si vitu mbali ni utu amabao uejengeka katika tamaduni, familia na jamaa mahalia. HIVYO WATOTO WAKIONYESHA UKOROFI PINDUKIA TUJUE KUWA SISI TUNALO TATITZO KUBWA; ANGALIA WATOTO WENYE MATATIZO SHULENI-FUATILIA FAMILIA ZAO PENGINE UTAKUTA KUNA UPENDELEO KATIKA MALEZI, AUA BABA NA MAMA HAWANAISHI MAISHA YA KUTOAMINIANA, AU PENGINE MAMA UA BABA NI MLEVI PINDUKIA; AU KATIKA FAMILIA WANAISHI KWA MAJUNGU NA KUBEZA WATU WENGINE; KUNA MENGI UNAWEZA KUPAMBANUA. HUU NI WAKTI WA KUAMUKA NA KUJITAFITI SISI WENYEWE WATANZANIA AMBAO NDIO WALEZI NA WAZAZI WA WATOTO HAWA UNAO WAONA KWENYE MITAAKWA KUKOSA KMAKAZI MAALUM: SERIKLAI, VYOMBO VYA DINI NA NA JAMII NZIMA TUNAPASWA KUFANYA KAZI KWA PAMOJA KUWASAIDIA WATANZANIA WENZETU.
ReplyDelete