NDUGU,JAMAA, MARAFIKI NA WADAU WA BLOG HII YA JAMII NINGEPENDA KUWATAARIFU YA KUWA NIMEPATWA NA MSIBA WA MAMA YETU MPENDWA BI KHADIJA( NADIA) OMARY ARUBATI AMBAYE AMEFARIKI DUNIA SIKU YA IJUMAA MCHANA TAREHE 24.07.09. (sio 24.08.09, kunradhi)
MSIBA HUPO KINONDONI NYUMBANI KWA MSTAHIKI MEYA WA KINONDONI MHESHIMIWA BWANA SALUM LONDA NA MAZISHI YANATARAJIWA KUFANYIKA LEO SIKU YA JUMAMOSI SAA SABA MCHANA KATIKA MAKABURI YA KISUTU.

MWENYEZI MUNGU AIWEKA ROHO YA MPENDWA MAMA YETU MAHALA PEMA.

AMIN

Allah says in the Qur'an (2:152-156):

“Fadhkurunii adhkurukum, washkuru lii walaa takfuruwn* Yaa ayyuhal-ladhiina aamanuu! sta’inu bi swabiri was-swalaah, innallaha ma’aswaabiryn* Walaa taquuluw liman yuqtalu fiy sabilillah amwaatum bal ahyaau, walaqil-laa tash’uruun* Wa lanabluwannakum bishay-in minal khaufi waljuu’i, wa naqswim-minal amwaali wal amfusi wa-th-thamaraat, wabash-shiris-swabiriyn* Alladhyna idhaa aswaabat hum muswyba, qaalu innalillahi wa inna ilaihi raaji’uun”

Therefore remember Me, I will remember you; and be thankful to Me and do not be ungrateful to Me. O ye who believe! seek help with patient perseverance and prayer; for Allah is with those who patiently persevere. And say not of those who are slain in the way of Allah: "They are dead." Nay, they are living, though ye perceive (it) not. And We will most certainly try you with somewhat of fear and hunger and loss of property and lives and fruits; and give good news to those who are patient. Who, when a misfortune befalls them, say: Surely we are Allah's and to Him we shall surely return.

Malumbo S.Malumbo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 25, 2009

    AMEFARIKI DUNIA SIKU YA IJUMAA MCHANA TAREHE 24.08.09? NADHANI UMEKOSEA TAREHE.......... POLENI SANA KWA KIPINDI HIKI KIGUMU WAKATI WA MSIBA

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 25, 2009

    Na kwake Mola tutarejea sote, poleni sana wafiwa kwa msiba. Allah awape subra na nguvu katika kipindi hiki kizito.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 25, 2009

    Pole sana ndugu. Mungu amulaze mahali pema.Asante

    Sahihisho kidogo: Jana ilikuwa tarehe 24 Julai 2009. na sio Mwezi wa Nane.


    Pole, pole sana ndugu.

    P.E.D

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 25, 2009

    Asalaam aleykum warahmatullah
    Nawaomba mtukaribishe kushiriki katika kuwaombeeni nyote na marehemu
    Mwenyezi Mungu kwa rehma zake hutuweka hapa kwa muda ambao Yeye tu ndo anaoutia kadiri yake na ni Yeye tu ndiye anayeamua kila linalomfikia binAdam
    Allahu Akbar
    Death is not the end of ones life. it is the opening of another door to the other greater and more fulfilling life...creating you again in forms that ye know not..56:60
    Life to come is better,Wal akhiratul khairun wa aabka 87:17
    Mungu awapendi nguvu na awazidishie iman
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  5. Inalillah wainah lilahi raajauun, may allah gives you and your family subirah and eeman inshaal.

    ReplyDelete
  6. Poleni sana na msiba uliowapata ndugu zangu.Apumzike kwa amani
    Pia-Ahsante kwa kututafsiria uliyoyasema(kiarabu) wengine kiarabu hakipandi.Ni vizuri kwa ndugu zangu kuandika ujumbe ktk lugha mbili,ili tuliokimbia umande tujue mnachomaanisha.

    ReplyDelete
  7. Inna Lillahi wa Inna Ilaihi Raajiun.

    May Allah forgive her shortcomings and grant her Janna Firdaus.

    Wafiwa, Inshallah Mwenyezi Mungu atawajaalia subra. Ina Laaha maa Swabirin (Mungu yupo na wenye kusubiri)

    Amin

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 25, 2009

    Mwaandike lugha fasi inayoeleweka siyo english wala kiaarabu please ninafikiri ueropean people does not even speak fluent english at all they do speak broken englishdo not be follower my tanzanian people

    ReplyDelete
  9. Germany/FrankfurtJuly 26, 2009

    Pole sana malumbo kwa kufiwa na mama yako mpendwa bi-Nadia!yaani nimesikitika namkumbuka bi-Nadia enzi zake Iringa"Mama alikuwa anajulikana mji mzima" Mnyalukolo usijari sisi wote njia yetu ni hiyo hiyo Mungu amuweke mahari pema peponi.AMEN

    ReplyDelete
  10. Poleni wafiwa. Nisameheni nilitaka kujua huu msiba uko kwa Mstahiki Londa huyu mama wakoje? Swali langu lina nia nzuri tu kama siwaudhi. Mstahiki mimi ni mpiga kura wake. Hivi sasa niko nje ya nchi. Ni hilo tu ndugu zangu. Poleni sana

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 26, 2009

    INNA LILLAHI WA INNA ILAIHI RAJI'UN.POLENI SANA WAFIWA.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 27, 2009

    Wewe annonymous wa 7/25/ 9;42PM Kafiri nini? Una maana gani kusema kuhusu lugha? Qur'an imeandikwa kwa kiarabu na kutafsiriwa kwa lugha nyingi. Please be clear on your comment, hakuna anayefata mkumbo BUT THAT IS THE LANGUAGE USED IN QUR'AN! Usiandike pumba kama hujui historia ya dini za watu!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 27, 2009

    Bashir kukujibu ni kwamba huyu bibi marehemu anakuwa ni Mkwe wake mstahiki Londa. Ni mama wa mke wa Londa, bi Halima. Poleni wafiwa kwa hakika sisi sote ni waja wa mwenyezi Mungu na Kwake tutarejea.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 28, 2009

    wafiwa wote poleni sana mungu atawajanza nguvu na baraka tele mtasipokea kutoka kwa baba wa mbinguni,misiba mingine ya K'zoo na indiana ninani kafiwa baba na ,ninani kafiwa bibi mamdogo mi ninafikiri msiba wa mzazi ndiyo una matter hii mingine is just a family member I do not know with this recession and economy teh!teh!teh!watu mnahitaji fedha kwa mabavu loh?loh?loh?The Dallas Community, Angelina Magessa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...