msanii anayetamba kwa sana hapa bongo kwa sasa, marlaw, anatupeleka kwa 'rita' katika kuthibitisha kwamba yeye ni moto wa kuotea mbali katika bongo fleva. hii ni kabla ya blockbuster yake ya 'pii pii' ambayo leo hii imekuwa kama wimbo wa taifa
Home
Unlabelled
marlaw akikupa 'rita'
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


kaka michuzi najuwa suali langu halihusiani na maoni ya hapo lkn niambie mbona najaribu sana kukutumia ujumbe au kuweka taaswira lkn huwa hazikufiki
ReplyDeleteKibao kizuri sana hiki na msanii nyimbo zake zote poa keep it up.
ReplyDeleteMashairi Unayajua dogo. Nimekuaminia
ReplyDeleteHuyu Marlaw anapatikana vipi? Nitakuwa Dar hivi karibuni nataka kuwasiliana naye.
ReplyDeleteKwa kukusaidia ndugu wa kwanza hapo juu ni kuwa Michuzi huwa ana roho mbaya mpaka uwe somebody fulani Mafuru, Liongo au uwe mdau kutoka uaghibuni ndio atatoa comment yako au picha yako . nashangaa halafu anaiita blog ya jamii. jamii ni sisi sote sio watu fulani fulani. najua pengine Michuzi comment hii hutoitoa lakini msg deliver. mimi ni ndugu yako kabisa tumecheza wote utotoni(aggrey) chandimu Amtulabhai. lakini kuna wakati huwa unabore . halafu samahani Issa anayekuambia ukweli ndie anayekupenda, una tabia moja inakuwa kama unajidharaulisha kwa watu utaona kijana mdogo kiumri zaidi yako,lakini kutokana na kiuwezo fulani cha pesa au kikazi unaanza kumuita Brother mara uncle acha hizo unajidharaulisha Issa .kama utajiri wakuwaita brother ni kina Bakhresa unaowajua vizuri na wanaokujua vizuri toka wanashona viatu livingstone . utadhani sio mtoto wa mjini Michu?. ni hayo tu plz usimind . mdau mliokuwa pamoja aggrey Zee la bandari Leicester-UK.
ReplyDeleteNaona hii si sehemu ya malumbano ni kutoa comments kuhusu huyu mwanamashahiri mahiri Marlaw, kama mtu unamalalamiko please mwandikie Michuzi barua pepe na umpigie simu muongee, hii ni sehemu ya comments siio malalamiko.
ReplyDeleteHuyu kijana Marlaw sauti yake imetulia na kama nilivyoahidi mwanzo nitashuka kumchukua huyu bwan'dogo na kumleta ughaibuni na kutengeneza album za nguvu. Marlaw kama unasoma comments hizi kaa mkao wa kula uimbaji wako na sauti yako! "GOLDEN VOICE" I can see a lot of potentials in you and you need big support in making really business! I will look for you soon!
Mdau USA
Vijana wetu ndio hao, wana vipaji sana, na kazi ngumu wanafanya. Tatizo moja na jinsi jamii inavyoshindwa kuheshimu haki zao, na hapa namaanisha haki miliki ya kazi zao. Utakuta ufisadi wa ajabu wanafanyiwa wa kuwapotezea kipato halali cha kazi yao. Jamii yetu inatisha.
ReplyDeleteNilipokuwa nafundisha pale Chuo Kikuu Dar, miaka ya sabini na kitu, niliwahi kutembelewa mara kadhaa na marehemu Patrick Balisidya, mwanamuzi wa kiwango cha juu, akinieleza matatizo aliyokuwa anapata kutokana na ufisadi huu. ufisadi. Inasikitisha.
Nawaunga mkono wote wanaompa live bila chenga MICHUZI. Ni ukweli usiopingika (kwa walofanya utafiti) kwamba michuzi ana "bias" au sijui niseme (inferiority complex)kwenye kupachika ujumbe au taswira, kama haijatoka ughaibuni au kwa demu (mwanamke) uwezekano wa kuiona hapa taswira au ujumbe wako sahau, au rabda uwe mnakula makange pamoja..!
ReplyDeleteKama haitoshi ukiandika maoni hapa kama hayamfurahishi yeye au swahiba wake (hayaendani na mtazamo wake) basi kama mwenyewe anavyosema "hayatoliona juwa", hutumia kivuli cha kuchafuwa hali ya hewa kutimiza dhamira yake mbaya..! Ana itakadi kama za chama chake unoko unoko, udikteta , kutokubali kubadilika!!! Ilimradi tafrani tu!
Najuwa maoni haya hutoyatoa sababu hayakufurahishi Au utayatoa kwa ajili ya kutafuta huruma za wadau wa ughaibuni (si ndo unaowabeba!)
Ushauri: Hii blog bora uiite blog ya watu wa ughaibuni...teh teh teh
Hilo nalo nenooooooooooooo...!
Michuzi mbona umemwondoa Lovenes Love wa Radio, au ndo katika kumprotect na mashambulizi kuhusu website yake? we kiboko kwa kweli hii blog ni yako na wala siyo ya jamii kama unavyotuongopea.
ReplyDeleteWooow!! This is a lovely number...I have been playing for a while now while working as well...
ReplyDeleteKeep it up young man, i hope I will be able to find and buy your album online.
J.
Toronto
Wow! I have just searched this young man on YouTube and didn't know he is the one who played 'Bembeleza' as well which i have been loving it!!!
ReplyDeleteKwa kweli una kipaji kikubwa sana and I love your style.
Sasa hivi nafurahia kipao hiki kwenye YouTube kwani naweza kuweka 'full screen'
Asante sana Michuzi kwa kutuletea starehe.
Nakuja nyumbani soon na nitapenda kununua album yako kwani kusikiliza miziki bure kama ninavyofanya sasa hivi najisikia vibaya sana. I want to help in someway.
J.
Toronto