msanii anayetamba kwa sana hapa bongo kwa sasa, marlaw, anatupeleka kwa 'rita' katika kuthibitisha kwamba yeye ni moto wa kuotea mbali katika bongo fleva. hii ni kabla ya blockbuster yake ya 'pii pii' ambayo leo hii imekuwa kama wimbo wa taifa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 04, 2009

    kaka michuzi najuwa suali langu halihusiani na maoni ya hapo lkn niambie mbona najaribu sana kukutumia ujumbe au kuweka taaswira lkn huwa hazikufiki

    ReplyDelete
  2. Kibao kizuri sana hiki na msanii nyimbo zake zote poa keep it up.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 04, 2009

    Mashairi Unayajua dogo. Nimekuaminia

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 04, 2009

    Huyu Marlaw anapatikana vipi? Nitakuwa Dar hivi karibuni nataka kuwasiliana naye.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 04, 2009

    Kwa kukusaidia ndugu wa kwanza hapo juu ni kuwa Michuzi huwa ana roho mbaya mpaka uwe somebody fulani Mafuru, Liongo au uwe mdau kutoka uaghibuni ndio atatoa comment yako au picha yako . nashangaa halafu anaiita blog ya jamii. jamii ni sisi sote sio watu fulani fulani. najua pengine Michuzi comment hii hutoitoa lakini msg deliver. mimi ni ndugu yako kabisa tumecheza wote utotoni(aggrey) chandimu Amtulabhai. lakini kuna wakati huwa unabore . halafu samahani Issa anayekuambia ukweli ndie anayekupenda, una tabia moja inakuwa kama unajidharaulisha kwa watu utaona kijana mdogo kiumri zaidi yako,lakini kutokana na kiuwezo fulani cha pesa au kikazi unaanza kumuita Brother mara uncle acha hizo unajidharaulisha Issa .kama utajiri wakuwaita brother ni kina Bakhresa unaowajua vizuri na wanaokujua vizuri toka wanashona viatu livingstone . utadhani sio mtoto wa mjini Michu?. ni hayo tu plz usimind . mdau mliokuwa pamoja aggrey Zee la bandari Leicester-UK.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 04, 2009

    Naona hii si sehemu ya malumbano ni kutoa comments kuhusu huyu mwanamashahiri mahiri Marlaw, kama mtu unamalalamiko please mwandikie Michuzi barua pepe na umpigie simu muongee, hii ni sehemu ya comments siio malalamiko.

    Huyu kijana Marlaw sauti yake imetulia na kama nilivyoahidi mwanzo nitashuka kumchukua huyu bwan'dogo na kumleta ughaibuni na kutengeneza album za nguvu. Marlaw kama unasoma comments hizi kaa mkao wa kula uimbaji wako na sauti yako! "GOLDEN VOICE" I can see a lot of potentials in you and you need big support in making really business! I will look for you soon!
    Mdau USA

    ReplyDelete
  7. Vijana wetu ndio hao, wana vipaji sana, na kazi ngumu wanafanya. Tatizo moja na jinsi jamii inavyoshindwa kuheshimu haki zao, na hapa namaanisha haki miliki ya kazi zao. Utakuta ufisadi wa ajabu wanafanyiwa wa kuwapotezea kipato halali cha kazi yao. Jamii yetu inatisha.

    Nilipokuwa nafundisha pale Chuo Kikuu Dar, miaka ya sabini na kitu, niliwahi kutembelewa mara kadhaa na marehemu Patrick Balisidya, mwanamuzi wa kiwango cha juu, akinieleza matatizo aliyokuwa anapata kutokana na ufisadi huu. ufisadi. Inasikitisha.

    ReplyDelete
  8. NautiakasiJuly 05, 2009

    Nawaunga mkono wote wanaompa live bila chenga MICHUZI. Ni ukweli usiopingika (kwa walofanya utafiti) kwamba michuzi ana "bias" au sijui niseme (inferiority complex)kwenye kupachika ujumbe au taswira, kama haijatoka ughaibuni au kwa demu (mwanamke) uwezekano wa kuiona hapa taswira au ujumbe wako sahau, au rabda uwe mnakula makange pamoja..!
    Kama haitoshi ukiandika maoni hapa kama hayamfurahishi yeye au swahiba wake (hayaendani na mtazamo wake) basi kama mwenyewe anavyosema "hayatoliona juwa", hutumia kivuli cha kuchafuwa hali ya hewa kutimiza dhamira yake mbaya..! Ana itakadi kama za chama chake unoko unoko, udikteta , kutokubali kubadilika!!! Ilimradi tafrani tu!
    Najuwa maoni haya hutoyatoa sababu hayakufurahishi Au utayatoa kwa ajili ya kutafuta huruma za wadau wa ughaibuni (si ndo unaowabeba!)

    Ushauri: Hii blog bora uiite blog ya watu wa ughaibuni...teh teh teh

    Hilo nalo nenooooooooooooo...!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 05, 2009

    Michuzi mbona umemwondoa Lovenes Love wa Radio, au ndo katika kumprotect na mashambulizi kuhusu website yake? we kiboko kwa kweli hii blog ni yako na wala siyo ya jamii kama unavyotuongopea.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 05, 2009

    Wooow!! This is a lovely number...I have been playing for a while now while working as well...

    Keep it up young man, i hope I will be able to find and buy your album online.

    J.
    Toronto

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 05, 2009

    Wow! I have just searched this young man on YouTube and didn't know he is the one who played 'Bembeleza' as well which i have been loving it!!!
    Kwa kweli una kipaji kikubwa sana and I love your style.
    Sasa hivi nafurahia kipao hiki kwenye YouTube kwani naweza kuweka 'full screen'

    Asante sana Michuzi kwa kutuletea starehe.
    Nakuja nyumbani soon na nitapenda kununua album yako kwani kusikiliza miziki bure kama ninavyofanya sasa hivi najisikia vibaya sana. I want to help in someway.
    J.
    Toronto

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...