MDAU ANAYEKWENDA KWA JINA LA BUNURI SHEFA, AMA FATUMA KAMA ALIVYOELEZA KWENYE INGIZO LAKE, NDIYE MDAU WETU WA MILIONI 6 NA MSHINDI WA KITITA CHA DOLA 1000.
HONGERA SANA MDAU BUNURI SHERFA AMA FATUMA KWA USHINDI HUO. GLOBU YA JAMII INAKUOMBA UWASILIANE NAYO KWA KUPITIA ANUANI ILE ILE YA EMAIL ULIYOTUMIA UKURASA WA GLOBU YA JAMII YENYE TARAKIMU ZA 6,000,000 ILI MIPANGO YA KUKUPATIA CHAKO IKAMILISHWE.
HAPA CHINI NI UKURASA WA EMAIL YA issamichuzi@gmail.com IKIWEKA BAYANA INGIZO LA MSHINDI NA BILA SHAKA NA MAINGIZO MENGINE KAMA INAVYOONEKANA KATIKA UKURASA HUU CHINI AMBAPO INGIZO LA MSHINDI LIMEWEKEWA MRABA WA RANGI YA CHUNGWA.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 35 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 03, 2009

    kaka michuzi nimekutumia mail nikionyesha kuwa mie ni mshindi wa milioni sita na ukurasa wake pia. Sasa sielewi tofauti na vigezo vya namba unatumia nini? Naomba ufafanuzi katika hili

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 03, 2009

    dah, ebwana kweli sasa mimi na hii pae yangu ya milioni sita nimepoteza muda tu, duh ebwana kweli sijui tatizo ni nini lakini hii sio issue

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 03, 2009

    Inamaanisha counter yako kaka michuzi inamatatizo. Inamaana unahits zaidi ya hizo ulizozionyesha. Kwa mtindo huu kama hutaiaddress ishu hii nadhani watu hawatapenda kushiriki tena maana inapoteza muda wao finally vigezo vinakuwa tata. Ukitumia time ya kwenye email kama kigezo, unaignore factor nyingine km server nk. I suppose the issue should be addressed.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 03, 2009

    kaka michuzi, twaomba vigezo!! umetumia nini kuamua kwamba mshindi ni yupi?? maake hata mie nimetuma 6,000,000, sasa ntuambie mbinu iliyotumia.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 03, 2009

    Mbona inbox yako inaonyesha kuna washindi zaidi ya mmoja? Umetumia vigezo gani kujua kwamba huyo uliyemchagua ndio real? Mi nimeuliza tu wala sijatukana, manake unaweza ukaminya hii comment!

    ReplyDelete
  6. Conradus-UkereweJuly 03, 2009

    Pole kwa kazi bro.Umesema uamuzi wa jopo ndo wa mwisho, lakini mimiSitofautiani na hao watoa maoni wa juu,binafsi ningependa kufahamu huo ukurasa wa 6000000 unaweza kufunguliwa na mtu zaidi ya mmoja? kwani mimi nami nimekutumia Scrin Print 3 zinazoonesha kua mimi ni mdau wa 6000000,lakini sio niliyetangazwa mshindi.

    Najua kua u muungwana, naomba utoe maelezo mazuri tusijue kama kuna ufisadi unafanyika

    Nijuavyo mimi (kwa elimuyangu ndogo) ni kua ukurasa huo hauwezi kufunguliwa na zaidi ya mtu mmoja.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 03, 2009

    Inawezekana hii bahatisha haina standards kwani nilipo-hit button 2.42am sawa na 10.42 nilipata 6,000,000 within a minute nikaprint screen 2.43am sawa na 10.43 lakini cha ajabu nimekuja kusomeshwa kama 2.48 sawa na 10.48.
    Sasa ninaelewa ni kwanini mchezo huu hakuna ku-appeal.
    Kunauwezekano mkubwa mdau aliyeshinda ali-refresh screen na kuwahi kutuma, kwahiyo labda ili ushinde ni kuwahi kutuma na si kuwahi kuhit the number.
    I got a lesson sidhani kamanitarudia kucheza hii kitu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 03, 2009

    Amini usiamini nimepata tarakimu hizo za mshindi na nimetuma kwa michuzi on the spot, nashangaa mshindi sio mimi na ukurasa bado upo open na picha nimepiga, huyo mshindi ni batili kwani tupo wengi na wadhamini wako voda waangalie hii kitu haiwezekani hii siyo haki hata kidogo

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 03, 2009

    Michuzi Madame Rita hakukosea Alikuambia ukweli hapo nyuma mie naona Ungewapa hao wa 10:43 wagawane pesa Umeona Umeandikiwa " MAMBO MICHUZI FATUMA" kusikia Fatuma akaona yeeeeeeeees Picha ya mikonozzz inakuja hahaha! Michuzi kuwa Fair na Wanaume pia LOl! Jumbe.

    Michuzi hii Page kidogo ungeweka Siri sababu wengi wasije kuchukuwa Number za watu wakaanza kupiga. Inshallah tunampongeza Bunuri Shefa kwa ushindi na wengine mungu akiwajalia watashinda siku nyengine. Jumbe.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 03, 2009

    Kumbe mkuu nawe ni msanii kihivo? Mbona washindi mwenye namba 6,000,000 ni wengi sana? nikicheki hiyo attachment hapo juu, wengi wamedai kuwa wao ndo washindi na wamekutumia hiyo page! Anyway ulisema uamuzi wa majaji ndo wa mwisho, haya bwana! Sifatilii tena hii kitu, ntakuwa nasoma makala tu!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 03, 2009

    Michuzi, kwa kweli nilikuwa na shaka kama hiyo 'counter' ya website yako ni ya kweli, na nilipoona umeweka tangazo hilo nikafuatilia kwa makini. NAMIMI kama wanavyodai wengine nime-log in kwenye Blog yako, nikawa wa 6M. Nimetuma email pamoja na attachment kwako (cha kustaajabisha hata kwenye list ya waliokutumia email sioni email yangu kwako ingawa kwangu imeonyesha 'delivered'.

    Naomba utujulishe kwani hii iatashusha TRUST na INTEGRITY ya Blog yako kama hakuna UWAZI. Tafadhali toa evidence zaidi ya mshidi huyo, sio list ya email tu.

    ReplyDelete
  12. Mdau UKEREWEJuly 03, 2009

    kaka mithubu naweza ukakuza huo mtundiko kwa hapo chini ili niweze kuona muda ilipochukuliwa hiyo screen print kwani ninahisi ni ya kwangu ila jina langu limeweka kapuni

    ReplyDelete
  13. Kaka tunaangalia muda uliotuma yule wa kwanza ndoo mshindi anayefutia ni standbay kwahi hiyo kaka au dada click hapo kwenye majina utaona mda na saa na dakika pamoja na majiana yenu yote mliotuma pole na ahsante kwa kujaribu karibu tena

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 03, 2009

    kaka siamini huu ni uzushi nimekutumia email mbili na nina evidence za waraka nilioupiga picha wa mdau wa milioni sita nashangaa jina na mshindi ni mwingine ebu hakiki aisee na ushahidi ninao nipe namba yako ya simu nitakuonyesha.

    ReplyDelete
  15. Conrad UKEREWEJuly 03, 2009

    We mkuu wa nanihii,naomba unielekeze labda elimu yangu ni ndogo.Hivi inawezekana hou ukurasa wa 6000000 ukafunguliwa na mtu zaidi mmoja? Mimi nimekutumia screen print za huo ukurasa wa 6000000 niliyoipata saa 8:44am(za huku UKEREWE/sawa na 10:44am za huko nyumbani)ila aliyetangazwa mshindi ni mtu mwingine.Naomba nifafanuliwe MKUU WA NANIHHII.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 03, 2009

    Michuzi,

    Technically it seems this COUNTER SYSTEM IS FLAWED,

    looking at your mails, it seems genuinely you have decided to go for the first received mail, that is of FATUMA, but in matter of facts, Aboud Karama, Deo Mawenga, and few others have also hit 6M on their counter.

    This is my suggestion to you, based on those facts, try to do the lottery instead of just picking a first come first saved basis, in which I am sure you based you final decision PRIMARILY on this scenario.

    yangu maoni tu.

    Aliyewahi kuwa mshindi!
    Shukran

    ReplyDelete
  17. mdau -uturukiJuly 03, 2009

    Umeanza uhuni lini, mbona namba ya kuonesha idadi ya maoni inaonesha ZERO COMMENTS wakati kina maoni kibao.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 03, 2009

    Leo wengi tumefulia, unajua unashinda halafu unaanza kutamba badala ya kutuma email chap chap kwa michuzi.

    Lakini next time Michuzi inabidi mshindi awe moja tu, badilisha widget ya kusoma hit/count ili tupate mshindi moja tu. Hongera mshindi wetu

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 03, 2009

    email zetu wengine hata hazijasomwa!! nimekoma!! sirudii tena!! mbona email haionyeshi tarehe ya kupokelewa?

    ReplyDelete
  20. baba AishaJuly 03, 2009

    Bahati ya mwenzako usiilalie mlango wazi. Hongera saaaana shem.
    Mdau Stockholm

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 03, 2009

    mimi bwana nashukuru nimekuwa wa milioni sita na moja mdau jina kapuni tmk.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 03, 2009

    NAMBA INAONYESHA UKISHAFUNGA BLOG KUWA WEWE ULIKUWA WA NGAPI KATIKA KUFUNGUWA HIYO BLOG SI WAKATI UNAFUNGUWA, UNAPOFUNGUWA ILE NAMBA UNAYOIONA NI MTU ALIYEPITA SI WEWE, KWA MAANA HIYO UNAPOONA NAMBA KWENYE SCREEN WEWE BADO HUJAHESABIWA UTAHESABIWA BAADA YA KUTOKA KWENYE BLOG, KWA MANTIKI HII MTU ALIYESHINDA NI YULE ALIYEFUNGUA BLOG NA KUONA NAMBA 5999999 KWENYE SCREEN YAKE AKITOKA NDIPO MWNINGE AKIFUNGUWA ATAONA 6000000 YA YULE ALIYEPITA. AS SIMPLE AS THAT, KAMA VILE A. B, C. OR 1, 2, 3 NO MIUJIZA

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 03, 2009

    Hii kweli ni bahati nasibu. Maana counter emeenda, mimi nikapata 599,999 nikiwa kwenye compyuta yangu, na mkewangu pia akiwa kwenye compyuta yake akapata naye 599,999. Tukashangaa hapo tukasema, lazima kutatokea watu wa milioni6 zaidi ya mmoja kutokana na tulichokiona. Sasa tusubiri kusikia watakaudhulimiwa.Maana kutakuwa na wa halali na ofcourse kuna wale wajanja pia. Hakuna uhallali ila ni bahati ya mtu TU!asante lakini kwa moyo huu unatia changamoto.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 03, 2009

    Watu wazima mnahangaika na kadola ka elfu moja. Hamna aibu. Kweli umasikini ni mmbaya. Halafu mnasema sijui Bongo tambarare, Bongo inalipa, mnatuchuza. Inaonyesha njaa iliopo Bongo.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 03, 2009

    watu wengine bwana utafikiri hawajaenda hata darasa moja.michuzi ameshawapa inbox yake kuwathibitishia mshindi lakini bado tu mnalalama kama hamna kazi za kufanya mkalale tu. michuzi hana ubaguzi na ameshazoea maoni yenu ya kipuuzi.kubali matokeo sio kulazimisha matokeo.mdau wa milioni sita ametulia tuli nyie kazi kusemasema.

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 03, 2009

    Duh muache mwenye bahati abahatike!!! Yani nimeikalia compyuta kila wakati narefresh lakini wapi. Wakati wa bahati blog imekuwa slow kufunguka ilipofunguka nikakuta zimeshapita number mbili....Kweli bahati nasibu hii...Haya bwana mdau kazinyake hizo sijui ulikesha ukiomba??!!!
    Maskini sina bahati mie H ndoto zangu zimeshahama...

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 03, 2009

    Nilisahau kukuambia Hongera, hongera sana...Yani unabahati wengi tulikuwa tunaziwania, mamia ya watu.

    Mshukuru Muumba wako kwa kukupa nyota hiyo.

    Rgds h

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 03, 2009

    Kanuni ya tatu ya kumpata mshindi inasema "uamuzi wa majaji ni wa mwisho" kwa hiyo maswali yanayoulizwa yangekubalika kabla mshindi hajatangazwa. Ni sawa na soccer kuwa uamuzi wa refa ni wa mwisho hata kama baada ya mechi ameona wazi kuwa kafanya makosa hawezi kurudi nyuma. Mshindi uliyetangazwa hongera.

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 03, 2009

    kwa kweli mimi nimejaribu kufungua page mbili kwa wakati mmoja zote zikawa na namba moja ,kwa hiyo uwezokano wa kupata washindi wengi ni mkubwa.kwa maoni yangu anatakiwa kwa watu wote walioshinda pachezeshwe bahati nasibu nadhani hiyo ndio itakuwa suluhisho la swala hilo.kila la kheri kwa washindi wote amboa hamjachaguliwa

    ReplyDelete
  30. AnonymousJuly 03, 2009

    Hiyo inayohesabu maoni ni aina ya Widget, ambazo ziko nyingi sana. Sasa inawezakana widget aliyoweka inasoma kila baada ya seconds kadhaa watu wakiingia mara moja kwa muda moja inashindwa kutofautisha na inatoa namba moja.

    Kinatotakiwa atafute widget inayoweza soma in millseconds, may itasaidia kidogo lakini still kuna minor chance ya watu kuwa zaidi ya moja pia.

    Mie mwenyewe nimefulia, lakini ndiyo maisha hayo wandugu. Next time , naona mdau wa 7000000 anakaribia. LOOOL

    ReplyDelete
  31. AnonymousJuly 03, 2009

    wewe unaesema watu wazima wahangaikia kidollar elfu, wewe pia waihangaikia hivyo hivyo usingekuwa hapa. sababu hujaipata ndio wajidai, ukipewa waipokea na mikono miwili na miguu miwili pia. sore loser!!

    ReplyDelete
  32. AnonymousJuly 04, 2009

    Kwa mdau 09:00 PM July 03,

    Sio wote tunaokuja hapa tuna shida. Wengine tunapenda kucheka na picha za Balozi tu. Maoni ya watu wanavyosumbuka na hio counter ya milioni sita ndio iliyonichekesha sana.

    Hiko ka elfu kamoja dola naipata katika siku MOJA hapa hapa Bongo, sina haja ya kusubiri siku nzima katika internet cafe za wahindi.

    Wabongo wabishi hata kama ni walala hoi.

    ReplyDelete
  33. AnonymousJuly 04, 2009

    Poleni wadau asiyekubari kushindwa sio mshindani wahenga wamelonga. Tunatakiwa kumpa ongera mshindi na si kumlaumu balozi wa naniii. Mimi mwenyewe nilitamani nishinde ili pesa nikawape yatima maana wao ndio wanazihitaji zaidi yangu. Nitajaribu tena siku za mbele.

    ReplyDelete
  34. AnonymousJuly 04, 2009

    dah burudan kweli kweli,siku ya siku nimeamka zangu nikaona namba ina karibia 6000000,nikaacha shuhuri zote fungua browser kibao za michuzi,kama 30 ivi,afu nikaanza kuzicheki vzr nikakuta the closest was 6000001,i was kind pissed at my self for sometime but now after reading these posts it kind funny how mad people can get for 900$ bucks

    ReplyDelete
  35. AnonymousJuly 06, 2009

    he teh teh wabongo acheni wivu na roho mbaya kwa misupu asiyekubali kushindwa si mshindani na bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi.Baada ya kumpa hongera mshindi mnaanza kumkandia michuzi wa watu.Ndio maana ikaitwa bahati na sibu mnaniboa.Namuaminia kaka michuzi tuendelezee libeneke.I miss tz

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...