Takribani wanachama 500 wa CCM Nchini Uingereza wahudhuria Mkutano Mkuu wa Tawi jijini Reading UK uliofunguliwa na mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Mhazini Mkuu wa CCM Taifa Mhe.Amos G. Makalla.
Pamoja naye toka Tanzania ni Mshauri Mkuu wa Siasa wa Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe.Rajabu Luhwavi. Katibu wa Tawi Bi Susan Mzee aliwakilisha Taarifa ya maendeleo ya CCM UK na Mwenyekiti wa CCM UK Nd. Maina Owino alimkaribisha Mhe. Amos Makalla kufungua rasmi Mkutano huo Mkuu.
Mhe. Makalla alisema kazi ya ujenzi wa Chama na Taifa la Tanzania ni letu wote na lazima wote kwa usawa bila ubaguzi tuvune matunda ya Uhuru wetu Viongozi hao wa kitaifa waliwataka Watanzania kuongeza juhudi za makusudi kuitangaza Tanzania kwa mema na pia Kutosita kutoa ushauri juu ya mambo mbalimbali ili kuboresha utawala bora na maadili mema ya uwajibikaji.
Aidha wote wamewataka Watanzania wanaoishi Ughaibuni wasikae kimya na watoe taarifa katika vyombo husika pale wanapo ona hawajatendewa haki kwa mujibu wa sheria za Tanzania mara warudipo nyumbani. Watanzania wengi walihamasika na kuendelea kujiunga na CCM siku hiyo ya Jumapili 26/07/2009.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 29, 2009

    kama watazania baada ya kuona na kuonja maendeleo, na kama baada ya miaka 48 ya uhuru tanzania bado ni maskini wak utupwa kwa sababu ya ccm, na kama richa ya kwamba muishio mbali nje ya tanzania mnayafahamu haya na bado mnaendekeza ubinafisi na kuisaport ccm, je hamuoni kuwa mmnaokosea mwenyezi mungu na watanzania kwa ujumla.
    MICHUZI, kwa kuwa wewe pia ni mfia nchi, na kwa sababu watoto wako tuponao tz na tunateseka nao, je unasababu ya kutotoa post hii.
    ni kwa sababu hiyo ya watanzania kutojali wenzao ,na kuwa wabinafsi na wapenda sifa kwa kuunga hata ujinga nimeamua kutotoa huduma kwa watanzania ninao wapenda sana.
    SAMAHANI KWA MSIMAMO WANGU.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 29, 2009

    Jamani nyie watu hamna kazi za kufanya?eti wana ccm?nyie mko nje ua nchi hapo mnatakiwa mshirikiane na watanzanua wenzenu bila kujali itikadi za kisiasa kujadili pamoja na kutafuta mbinu za kunyanyua hali ya maisha ya watanzania kwa ujumla sio kujadili mambo ya chama hapo ugenini mtajikuta ipo siku mnaanza kubaguana kwa itikadi za chama tu.acheni hizo watanzania wenzangu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 29, 2009

    Aaagh! Nimeamini 2010 kazi ipooo.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 29, 2009

    Mbona uvundo wa pale JK eapoti hawakuusemea,wamekalia ujanja ujanja tu. "Twajua wanachotafuta jamani tuwe macho"

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 29, 2009

    Mi sisemi kitu mmm

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 29, 2009

    Kweli sisiemu inanguvu, nawaomba watanzania wenzangu wa usa tujiweke tayari kuuzulia mkutano kama huu pindi mabo yakikamilika

    CCM juu!!!!!!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 29, 2009

    Mbona vyama vya upinzani havifungui matawi?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 29, 2009

    Swali: Nini mantiki na madhumuni ya hili wimbi la uanachama wa CCM katika nchi za nje? Naombeni uelimisho ndugu. Ahsanteni.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 29, 2009

    kweli majuu hamnazo!hii ni ishara ya upungufu wa matukio huko majuu,poleni njie!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 29, 2009

    Sio dhambi kuwa mwana CCM. Kuhudhuria mikutano ya siasa ni utashi wa mtu binafsi. Hakuna aliyeshikiwa bunduki ili aende kwenye mikutano.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 29, 2009

    Inaonyesha ni kiasi gani watu mambo yamewaendea vibaya. Ila si mbaya kuwekeza upande mwingine wa dunia kwani, mgaa gaa na upwa hula wali na mboga. Samahani kama huo usemi nimeukosea.
    Mdau

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 29, 2009

    kwakweli!!!!!!!!!!watanzania tumefundishwa kupenda chama zaid kuliko nchi.ni vp bendera ya tanzania ingepeperushwa kama kinavyo peperushwa kigwanda cha kijani?tofaut na nchi nyingine zilizo endelea na zinazoendelea.ila ndo ivyo tena tutafanyajee

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 29, 2009

    Michuzi umenibania mchango wangu. CCM ni fisadi. Na narudia hawa wote wanaoshabikia hiki chama ni watoto wa mafisadi. Kwa nini ulitupilia mbali maoni yangu?

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 29, 2009

    Kwa nini chama cha watanzania UK hakina nguvu kama CCM Uk
    Watanzania tuipende nchi yetu kwanza

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 29, 2009

    Leo kweli michuzi nimeamini wewe una ubaguzi. inamaana maoni yamtu tofati na mwana CCM huwezi kuya bandika??ah,,bwana michuzi blog yako naona nikama unataka kuiwekea doa mbaya...hakuna kitu kisicho na upinzani.mimi nimeshaandika maoni mala tatu lakini unanibania tu.mimi sio mwana CCM,haimanishi unifukuze kwenye blog yako bwana!! ah nimekushangaa kweli.Ushauli wa bure acha kutundika mikutano ya vyama hapa,blog siyo ya CCM nadhani, utagombanisha watu ,

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 30, 2009

    Hata mimi ameshanibania mara kibao kisa tu nimeikosoa CCM, hivi wewe Michuzi pamoja na kutoka kwenye familia ya kilalahoi na huku ndugu zako kibao wakiwa bado wanateseka kimaisha kutokana na Ufisadi wa CCM lakini wewe ndio unajiona mjanja kisa tu Mafisadi wanajifanya marafiki zako, utakuja kujuta siku moja ndugu yangu kwa sababu Mafisadi hawana urafiki wa kweli na wanachokithamini ni Pesa na Power ili wazidi kuiibia nchi na wananchi wote, badilika Michuzi. Hata usipolitoa hili bandiko lakini Message Sent.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 30, 2009

    utaitangaza vipi nchi yako kupitia chama cha siasa? huoni hapo ushaweka matabaka? chama kina mantiki gani unapozungumzia utaifa ambao kwa ughaibuni ndio haswa unatakiwa udumishwe. tuonyeshe uzalendo kwa kupepelusha bendera za taifa nasio hivyo vihengachifu.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 30, 2009

    MIJAMBAZI TU HIYO!!!
    NAONA KICHEFUCHEFU. WENGI WA HAWA JAMAA WENYE AKILI MBOVU WANA MALENGO BINAFSI TU KUANZISHA HIYO MIJITWAI YAO HUKU ULAYA, HAWANA LENGO KUISAIDIA JAMII NA WALA HATA HAWAJUI WATANZANIA MASIKINI WANAMATATIZO GANI. ADHAMU YAO INAKUJA,SUBIRI!

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 30, 2009

    Hivi CCM wamekuwa kama wanapigania Uhuru? shame on you, hayo yalikuwa yanafanya na vyama vya kupigania uhuru kama ANC.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 30, 2009

    jamani na wapinzani si mfungue matawi yenu nje ya nchi mmekatazwa na nani?kazi kusema tu ccm mafisadi..hv leo hii tukabidhi nchi kwa chama kingine..haaaa..si bora tubaki hapo hapo.
    narudia tena
    KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI..
    KIDUMU CHAMA TAWALA....

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 30, 2009

    yeah we are Tanzanian (bongo)!!!!i wonder why for 45 years we didnt learn any thing...from our independence....
    Mdau wa Kamachumu..

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 31, 2009

    nyie thutheni,.....kathirikeni.....wendhenu ndio hivyo tena ha ha habari ndiyo hiyo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...