Pamoja naye toka Tanzania ni Mshauri Mkuu wa Siasa wa Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe.Rajabu Luhwavi. Katibu wa Tawi Bi Susan Mzee aliwakilisha Taarifa ya maendeleo ya CCM UK na Mwenyekiti wa CCM UK Nd. Maina Owino alimkaribisha Mhe. Amos Makalla kufungua rasmi Mkutano huo Mkuu.
Mhe. Makalla alisema kazi ya ujenzi wa Chama na Taifa la Tanzania ni letu wote na lazima wote kwa usawa bila ubaguzi tuvune matunda ya Uhuru wetu Viongozi hao wa kitaifa waliwataka Watanzania kuongeza juhudi za makusudi kuitangaza Tanzania kwa mema na pia Kutosita kutoa ushauri juu ya mambo mbalimbali ili kuboresha utawala bora na maadili mema ya uwajibikaji.
Aidha wote wamewataka Watanzania wanaoishi Ughaibuni wasikae kimya na watoe taarifa katika vyombo husika pale wanapo ona hawajatendewa haki kwa mujibu wa sheria za Tanzania mara warudipo nyumbani. Watanzania wengi walihamasika na kuendelea kujiunga na CCM siku hiyo ya Jumapili 26/07/2009.
kama watazania baada ya kuona na kuonja maendeleo, na kama baada ya miaka 48 ya uhuru tanzania bado ni maskini wak utupwa kwa sababu ya ccm, na kama richa ya kwamba muishio mbali nje ya tanzania mnayafahamu haya na bado mnaendekeza ubinafisi na kuisaport ccm, je hamuoni kuwa mmnaokosea mwenyezi mungu na watanzania kwa ujumla.
ReplyDeleteMICHUZI, kwa kuwa wewe pia ni mfia nchi, na kwa sababu watoto wako tuponao tz na tunateseka nao, je unasababu ya kutotoa post hii.
ni kwa sababu hiyo ya watanzania kutojali wenzao ,na kuwa wabinafsi na wapenda sifa kwa kuunga hata ujinga nimeamua kutotoa huduma kwa watanzania ninao wapenda sana.
SAMAHANI KWA MSIMAMO WANGU.
Jamani nyie watu hamna kazi za kufanya?eti wana ccm?nyie mko nje ua nchi hapo mnatakiwa mshirikiane na watanzanua wenzenu bila kujali itikadi za kisiasa kujadili pamoja na kutafuta mbinu za kunyanyua hali ya maisha ya watanzania kwa ujumla sio kujadili mambo ya chama hapo ugenini mtajikuta ipo siku mnaanza kubaguana kwa itikadi za chama tu.acheni hizo watanzania wenzangu.
ReplyDeleteAaagh! Nimeamini 2010 kazi ipooo.
ReplyDeleteMbona uvundo wa pale JK eapoti hawakuusemea,wamekalia ujanja ujanja tu. "Twajua wanachotafuta jamani tuwe macho"
ReplyDeleteMi sisemi kitu mmm
ReplyDeleteKweli sisiemu inanguvu, nawaomba watanzania wenzangu wa usa tujiweke tayari kuuzulia mkutano kama huu pindi mabo yakikamilika
ReplyDeleteCCM juu!!!!!!!
Mbona vyama vya upinzani havifungui matawi?
ReplyDeleteSwali: Nini mantiki na madhumuni ya hili wimbi la uanachama wa CCM katika nchi za nje? Naombeni uelimisho ndugu. Ahsanteni.
ReplyDeletekweli majuu hamnazo!hii ni ishara ya upungufu wa matukio huko majuu,poleni njie!
ReplyDeleteSio dhambi kuwa mwana CCM. Kuhudhuria mikutano ya siasa ni utashi wa mtu binafsi. Hakuna aliyeshikiwa bunduki ili aende kwenye mikutano.
ReplyDeleteInaonyesha ni kiasi gani watu mambo yamewaendea vibaya. Ila si mbaya kuwekeza upande mwingine wa dunia kwani, mgaa gaa na upwa hula wali na mboga. Samahani kama huo usemi nimeukosea.
ReplyDeleteMdau
kwakweli!!!!!!!!!!watanzania tumefundishwa kupenda chama zaid kuliko nchi.ni vp bendera ya tanzania ingepeperushwa kama kinavyo peperushwa kigwanda cha kijani?tofaut na nchi nyingine zilizo endelea na zinazoendelea.ila ndo ivyo tena tutafanyajee
ReplyDeleteMichuzi umenibania mchango wangu. CCM ni fisadi. Na narudia hawa wote wanaoshabikia hiki chama ni watoto wa mafisadi. Kwa nini ulitupilia mbali maoni yangu?
ReplyDeleteKwa nini chama cha watanzania UK hakina nguvu kama CCM Uk
ReplyDeleteWatanzania tuipende nchi yetu kwanza
Leo kweli michuzi nimeamini wewe una ubaguzi. inamaana maoni yamtu tofati na mwana CCM huwezi kuya bandika??ah,,bwana michuzi blog yako naona nikama unataka kuiwekea doa mbaya...hakuna kitu kisicho na upinzani.mimi nimeshaandika maoni mala tatu lakini unanibania tu.mimi sio mwana CCM,haimanishi unifukuze kwenye blog yako bwana!! ah nimekushangaa kweli.Ushauli wa bure acha kutundika mikutano ya vyama hapa,blog siyo ya CCM nadhani, utagombanisha watu ,
ReplyDeleteHata mimi ameshanibania mara kibao kisa tu nimeikosoa CCM, hivi wewe Michuzi pamoja na kutoka kwenye familia ya kilalahoi na huku ndugu zako kibao wakiwa bado wanateseka kimaisha kutokana na Ufisadi wa CCM lakini wewe ndio unajiona mjanja kisa tu Mafisadi wanajifanya marafiki zako, utakuja kujuta siku moja ndugu yangu kwa sababu Mafisadi hawana urafiki wa kweli na wanachokithamini ni Pesa na Power ili wazidi kuiibia nchi na wananchi wote, badilika Michuzi. Hata usipolitoa hili bandiko lakini Message Sent.
ReplyDeleteutaitangaza vipi nchi yako kupitia chama cha siasa? huoni hapo ushaweka matabaka? chama kina mantiki gani unapozungumzia utaifa ambao kwa ughaibuni ndio haswa unatakiwa udumishwe. tuonyeshe uzalendo kwa kupepelusha bendera za taifa nasio hivyo vihengachifu.
ReplyDeleteMIJAMBAZI TU HIYO!!!
ReplyDeleteNAONA KICHEFUCHEFU. WENGI WA HAWA JAMAA WENYE AKILI MBOVU WANA MALENGO BINAFSI TU KUANZISHA HIYO MIJITWAI YAO HUKU ULAYA, HAWANA LENGO KUISAIDIA JAMII NA WALA HATA HAWAJUI WATANZANIA MASIKINI WANAMATATIZO GANI. ADHAMU YAO INAKUJA,SUBIRI!
Hivi CCM wamekuwa kama wanapigania Uhuru? shame on you, hayo yalikuwa yanafanya na vyama vya kupigania uhuru kama ANC.
ReplyDeletejamani na wapinzani si mfungue matawi yenu nje ya nchi mmekatazwa na nani?kazi kusema tu ccm mafisadi..hv leo hii tukabidhi nchi kwa chama kingine..haaaa..si bora tubaki hapo hapo.
ReplyDeletenarudia tena
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI..
KIDUMU CHAMA TAWALA....
yeah we are Tanzanian (bongo)!!!!i wonder why for 45 years we didnt learn any thing...from our independence....
ReplyDeleteMdau wa Kamachumu..
nyie thutheni,.....kathirikeni.....wendhenu ndio hivyo tena ha ha habari ndiyo hiyo.
ReplyDelete