JK akiwa na Rais wa Zimbabwe Mh. Robert Mugabe pamoja na mwenyeji wao ambaye ni mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na Kiongozi wa Libya Kanali Muamar Ghadaffi mjini Sirte wakati wa hafla ya chakula cha usiku kwa viongozi waliohudhuria mkutano wa AU huko Libya usiku wa kuamkia leo ambapo mkutano huo wa siku tatu umefikia kilele

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 04, 2009

    Hahaha Tizama Mugabe anavyomtizama Kikwete huyu Kijana mdogo sijui nikimtuma aniwekee maji atakubali au lah?.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 04, 2009

    Damn, them sofas looks so comfy!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 04, 2009

    msaada tutani: kazi kuu ya AU ni nini haswa? ninafikiri kila taifa linachangia kutoka pesa za walipa kodi wake sijui ni kwa nini tuwe na hiki kitu kinaitwa AU. wenye kujua tafadhali nisaidieni. kila nikisikia AU ninahisi kichefuchefu

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 04, 2009

    mdau wa Sat Jul 04, 02:27:00 AM yaani unataka kujuwa zaidi ya viongozi wa kiafrika kunufaika na malipo ya bonus za wao na waliofuatana nao, kuenjoy maakuli mazito mazito wakati wananchi wao wanakufa na njaa, kulala kwenye mahoteli makubwa makubwa wakati wananchi wao hawana hata kibanda, wake zao kutembezwa na magari ya fahari na kufanya shopping za kila aina wakati wananchi wao hawajui hata watachokula asubuhi hii, kwa mwenyeji kujionyesha kugharimu kila kitu kwa mapesa tele mpaka unadhani kuwa nchi haina matatizo au madeni kibao,kubadilishana mawazo na mbinu za kuzidi kubaki madarakani na ku-play mind game na wananchi wao? jawabu ni kuwa AU lengo lao kubwa ni kukutana na kujidanganya kama afrika inaongozwa na waafrika, haisikilizi amri za mataifa makubwa, halafu wakiondoka hapo tu wanafanya kinyume na kila mmoja anakimbilia kwa mataifa makubwa kuwasikiliza wanachotaka, kuomba misaada na kunyeyekea.

    Ukipata jawabu nzuri zaidi ya hii nijulishe.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 04, 2009

    Anonymous wa Sat Jul 04, 10:54:00 AM

    nakupa 5. Ulichosema ni mwisho, sina cha kuongeza.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 04, 2009

    No matter what people say, Ghadafi has good intention to Africans, we should listen to him

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 04, 2009

    Anonymous wa Sat Jul 04, 10:54:00 AM umenimaliza kabisa, yaani nakubaliana nawe 110%

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 04, 2009

    body language ya JK na mugabe inaonyesha dhahiri kuwa wana bifu, tena mugabe anaonyesha anafikiri ni namna gani huyu kijana aniletee tafshani hapa?

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 04, 2009

    muone huyo brazamen anavyouza sura hahaha kakunja 4 shaka hana,watoto wake shule safi,msosi mboga7,shopping havi,na nadhani hapo wamekwenda kutumia tu na kuenjoy pesa zawalipakodi,hebu hona hio mikochi sidhani kwastyle hio kama hutasinzia,hebu cheki mikutano ya wezetu walioendelea europe na us wanakaa ktk mabench na wamebanana kinoma na watu wanawajibika kisawasawa cheki hao walivyoanika mivitambi yao.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 04, 2009

    Anonymous wa Sat Jul 04, 10:54:00 AM umesema kweli kabisa, ndo maana sipendi siasa wakati mwingine. juzi tu raisi wa zimbwabwe nusu awauwe raia wake wote, leo na hao viongozi wa africa wako meza mmoja!!! siasa bwana, ovyo.

    kokoliko

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 04, 2009

    Uzuri wa hiyo picha ni kwamba Gaddafi na Mugabe wanaangalia upande mmoja na Kikwete anaangalia upande mwingine. Baada ya kuangalia picha unabaki kujiuliza maswali kwamba maana yake ni nini.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 04, 2009

    Hivi jamani mimi nawashangaa, sasa mnataka Raisi atembee na mkokoteni, avae kandamili, pensi na T-shirt, asiende kwenye mikutano, akae kwenye benchi kama watu wengine, asifanye shopping akae na nyinyi vijiweni apige domo kutwa nzima.Mimi ninachosema, msingojee serikali yetu ifanye kitu, tuingieni mtaani tufanye mambo sisi wenyewe. Watu wanataka kulishwa, JK akienda nje basi matatizo, tubadilisheni mkanda tafuteni mambo mengine ya kuongelea ambayo yataweleteeni maendeleo! kazi kweli kweli!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 05, 2009

    jongwe anammaind jk, cheki jicho, kama anasema, bwana wewe siku hizi hatuombani chumnvi?

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 05, 2009

    mdau wa Sat Jul 04, 11:38:00 PM hatupingi JK kuvaa vizuri, tunalopinga ni kutumia pesa za wavuja jasho kwenda katika mambo ambayo hatuoni manufaa yeyote.

    By the way, si rais wetu anatakiwa kutuwakilisha sisi? yeye ndio anaeonyesha picha ya mtanzania, kwa hivyo kuna kosa gani kuvaa kandambili? kwa nini avae nguo za bei kali sana? kuna kosa gani kupanda gari ya kawaida tu? kwani si uongo kuwa watanzania hatumiliki ayafanyayo? jee JK anaona aibu kuonyesha dunia namna watanzania tulivyo? au JK anadanganya dunia kusema kuwa hivi ndvyo watanzania tulivyo ilhali sio kweli?

    Ni mwakilishi wetu na aonyeshe basi walala hoi tunavyoishi.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 06, 2009

    Waosha vinywa bwana, very narrow minded. Huyo anon wa 10.54 akiukwaa urais nae ndio wale wale. wangapi hapa Afrika tumewaona? Walijidai kutetea mashlahi ya wanyonge weee, walivyoingia tu madarakani, wako wapi? Kaeni kimya mfanye kazi mlete mabadiliko!

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 06, 2009

    mdau wa Mon Jul 06, 07:42:00 AM, aidha hujui maana ya narrow minded au umejikwaa dole, maana uliyasema yanaonyesha ni namna gani wewe mwenyewe ni narrow minded. sasa ulitaka watu wabaki kimya kila anaeingia madarakani ale awezavyo? amka unuse vumbi la bongo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...