
Ndugu Wanajumuiya,
Kwa niaba ya uongozi wa Tanzania Houston Community(THC), napenda kuwataharifu kwamba tutakuwa na kikao cha jumuiya siku ya Jumamosi (07/25/2009) saa kumi na moja jioni (5:00pm),
katika ukumbi wa Safari Hall
9651 Bissonnet,
Houston,
TX 77036.
Moja ya ajenda ya kikako hicho ni zoezi la uchukuaji wa sensa kwa wanajumuiya wote. Hivyo basi uongozi unaotao tamko kwamba siku hiyo ya mkutano mkuu kutakuwa na mchakato wa kukusanya takwimu za wanajumuiya, ili tuweze kufahamu katika jumuiya yetu tuna wananchi wangapi.
Uongozi unaomba wanajumuiya tujitokeze kwa wingi kwani mafanikio ya zoezi hilo ni mafanikio ya jumuiya yetu Tafadhali uonapo tangazo hili mfahamishe na mwenzio.
Asanteni
Katibu,
Iddi Rashid Mwanyoka
iddyrashy@yahoo.com
Iddi, naomba uwaambie wanajumuiya wezangu sitoweza kufika kesho ila naomba mnihesabu kwani nitakuwa nafungua BOX samahani kwa kutofika kwangu kwani huu ujumbe mmetushitukiza yaani mmetoa siku moja notisi mmhh mimi naenda kufungua BOX ila watanzania wenzangu nawapenda na bills ziko due.
ReplyDeleteMukumbuke kusachi visu yasitokee maafa.
ReplyDeleteeehe, unaona hii? hii ndio sawa - sio ule ushabiki wa kukutana kuwa ni wanachama wa CCM kwenye Ughaibuni. Hawa ndungu wanakutana kuwa ni WaTanzania wanaoishi hapo Houston - Marikani. Na hii iko sehemu nyingi za miji wa Marikani kama Atlanta, Boston n.k ambao waBongo wana vyama vya wa Tanzania na sio chini ya CCM.
ReplyDelete