




Mto Akagera, Nile
Kaka Michuzi hivi karibuni nilitembelea kwa Mkulu Kagame, nilipitia njia ya Kahama na nikaweza kuona mambo mengi sana ikiwemo sehemu ambayo wanasema kuna majambazi kupita kiasi katika njia ya kutokea Kahama kuelekea Rusumo, (border ya Tz na Rwanda)…
Hapo kati kuna msitu mkubwa ambao unatunza majambazi pamoja na sokwe kwahivyo basi kuna sehemu tulifika tukapewa escort, Askari kanzu ambao walikuwa na AK47 mikononi wakatuvusha kupita msitu huo na tukawaacha njia panda kwenda Ngara(border ya TZ na Burundi) tukasonga.
Tulipofika Rusumo(Border ya Tz na Rwanda) tuligongewa pass zetu upande wa Tz na ukikaribia Immigration upande wa Rwanda kuna Daraja hapo kuna mto unapita ambapo katika kuulizia nikaambiwa unaitwa mto Akagera ambao ndio huohuo unaokwenda hadi Tanzania na kuitwa Mto Kagera na unapita kwenye mwambao chini ya Ziwa Victoria ambao pia huchepukia Uganda kule Jinja na kuitwa Mto Nile( River Nile).
Mto huu Akagera(Rwanda) unaanzia kwenye milima (kwa kuwa giza lilitanda sikuweza kunyakua milima ile) ilikuwa kwa mbali ila kwa macho nilikuwa naona maji yanapotokea kwa mtiririko, naahidi December nitakuja na picha za chanzo cha mto huo wenye majina mawili (Kagera, Nile).
Mdau Leonard Saveri
----------------------------------
GLOBU YA JAMII INAMPONGEZA MDAU LEONARD SAVERI KWA KUENDELEZA LIBENEKE BILA KINYONGO, YOTE IKIWA NI KATIKA KUWEKA MAMBO SAWA BIN SAWIA.
TASWIRA NA HABARI ZA KUELIMISHA, KUBURUDISHA NA KADHALIKA ZINAPOKEWA KWA MIKONNO MIWILI NA GLOBU HII YA JAMII AMBAYO ANKO NANIHII ANA FURAHA NA FAHARI KUONA KWAMBA MWENENDO WAKE NI WA KIJAMII HASA KWA JINSI MICHANGO TOKA KILA PEMBE YA DUNIA INAVYOMIMINIKA.
KWA WARAKA HUU GLOBU YA JAMII INAKARIBISHA MICHANGO YA AINA YOYOTE KATIKA KUENDELEZA LIBENEKE. NDOTO YA ANKO NANIHII NI KUONA SIKU ZIJAZO KILA POSTI INAKUWA INATOKA KWA WADAU NA SIO KUTOKA KWAKE, KWANI GLOBU HII SI YAKE TENA!
-MICHUZI
buurraza misupu a.k.a balozi a.k.amkuu wa kaya ya nanihii unajua sana kutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa, mara gulobu siyo mali yangu ni yenu wanajamii,sasa mbona watu hawaishi kulalamika umewabania post zao? mmoja wao mimi ua kwa vile sijalalamika?
ReplyDeletehata haya si malalamiko (ili na hii isibanwe) msisitizo tu. uskonde mazee,ila maadili muhimu kwa maendeleo ya golobu,umesikia balozi?
Jamani hata mimi nayejua english ya kuombea maji tu nahisi hayo maneno "WELCOME TO TANZANIA AGAIN" kwenye bango la TANROADS hayajakaa sawa ni swahenglish. Nimechemsha?
ReplyDeleteAnko Heshima yako ilindwe! Kwanza Samahani naomba uniweke kapuni maana wabongo awachelewi kuponda si unajua tena. Mimi napenda sana kuendeleza libeneke ila Camera zangu zishakuwa kimeo 1 ni FUJI FINEPIX 4 Hiyo imeingiwa na Virus basi hakuna cha picha tena wala nini, naomba ushauri wako wapi naweza kupata fundi mzuri wa kunirekebishia, harafu ya pili ni SONY MEGAPIXEL 7.2 Hii imekufa Betri sijui Duka lipi naweza kupata Betri bei nafuu, maana sehemu kama mbili nilizopenya penya nimeambiwa Betri Tsh.90,000/=. Usawa wenye mgumu huu si unajua mambo ya "GLOBAL FINANCIAL CRISIS" Anko naomba msaada wako wa ushauri nirudi kwenye libeneke.
ReplyDelete(NASISITIZA ANKO HAPA NIWEKE KAPUNI)
Mdau,
J.Big (Cameraman EATV),
Email yangu ni:
jmbwile@yahoo.com
MDAU TUNASHUKURU KWA PICHA, MIMI KAMA MDAU NILIYEKULIA KATIKA MJI WA RUSUMO JINA LA MTO SIO AKAGERA NI RUVUBU.
ReplyDeleteTopic imeshapita lakini hilo bango inglishi ya wapi hiyo wametafsiri wakaacha maneno mengine...mtu anayejifunza kiswahili hapo ameliwa .....Safari njema mbona hawajaisema kwa kidhungu..... Have a nice trip, journey or whatever and then blah blah blahh tanzania kwa kulipua lipua najua hapo tenda iliuzwa na mtu alilipwa vizuri tu
ReplyDeleteMdau 10:33:00am, kama unavyojua tena sisi twazidi jifunza, asante sana kwa maelezo na tumepata jina lingine lao huo mto mmoja...aisee!
ReplyDeletehapa na warundi nao lazima waje na jina lao kwa mto huu.
ze mdau.