Marekani Barack Obama mwezi Mei mwaka huu
Rais Barack Obama wa Marekani amemsifia Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania, akimwelezea kama kiongozi wa mfano ambaye amefanya kazi nzuri ya kupeleka huduma za waziwazi kwa wananchi wake.
Rais Obama amesema kuwa Rais Kikwete ni mmoja wa viongozi wa Afrika walioonyesha uongozi thabiti ambao uko tayari kusonga mbele katika kuwaletea maendeleo wananchi wao.
Rais Obama amemwaga sifa hizo kwa Rais Kikwete katika mahojiano na taasisi ya mawasiliano kwa njia ya inteneti ya AllAfrica.Com wakati akijiandaa kufanya ziara yake ya kwanza katika eneo la Afrika Kusini mwa Sahara, kwa kutembelea Ghana.
Rais Obama aliwasili Ghana usiku wa kuamkia leo (Ijumaa, Julai 10, 2009) kuanza ziara ya siku mbili ya kwanza katika eneo la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Rais Obama anatarajiwa kuondoka Ghana leo kurejea kwao Marekani.
Kabla ya kutembelea Ghana, Rais Obama tayari alikwishakutembelea Bara la Afrika kwa kuzuru nchi ya Misri, iliyoko Afrika Kaskazini katika wiki za karibuni.
Rais Obama ambaye aliwasili Ghana akitokea katika Mkutano wa Nchi Zenye Viwanda Vingi Zaidi Duniani wa G8 nchini Italia, aliiambia taasisi ya AllAfrica.Com katika mahojiano yaliyofanyika Ikulu ya Marekani kabla ya kuondoka kuelekea Russia, Italia na Ghana:
“Lazima kukumbuka kuwa pamoja na kwamba nitaitembelea Ghana kwa ziara hii, tayari nimemkaribisha Tsvangirai wa Zimbabwe katika Ofisi ya Rais wa Marekani. Tulikuwa na Rais Kikwete wa Tanzania kabla ya hapo katika Ofisi hii hii, na katika kila mkutano najaribu kuelezea ujumbe huo huo.”
Aliongeza Rais Obama: “Tumeona kazi nzuri sana inayofanywa na uongozi katika Tanzania ukielekeza nguvu zake katika kutoa huduma za wazi wazi na dhahiri kwa wananchi wake, na kila mahali ambako watu wanataka kujisaidia, na sisi tunataka kuwapo kama washirika wa uongozi.”
Rais Obama alimwalika Rais Kikwete kuwa kiongozi wa kwanza kabisa wa Bara la Afrika kukutana naye katika Ofisi ya Rais wa Marekani tokea kuapishwa kuwa kiongozi wa Marekani Januari 20, mwaka huu.
Rais Kikwete alikutana na kufanya mazungumzo na Rais Obama katika Ikulu ya Marekani mwezi Mei mwaka huu, 2009.
Akisisitiza kuhusu umuhimu wa Bara la Afrika na uongozi wa Rais Kikwete na Afrika kwa jumla, Rais Obama alisema: “Nadhani Bara lote ni muhimu. Na nadhani kuwa tunao uongozi imara katika Bara la Afrika ambao uko tayari kusonga mbele na tunataka kusonga mbele nao.”
Rais Obama pia alisisitiza kuwa Afrika inahitaji kuendelea na juhudi zake za kuimarisha utawala bora, ili kuzidi kuvutia uwekezaji kutoka Marekani.
“Jambo la kwanza ni kwamba itakuwa vigumu kuvutia uwekezaji kutoka nje bila kuwako na utawala bora. Uwekezaji wa namna inayoboresha maisha ya kila siku ya wananchi wa Afrika. Kama maofisa wa Serikali wanataka binafsi kulipwa asilimia 10, ama 15, ama 25 juu ya kiasi cha uwekezaji, hakuna mwekezaji ambaye atakwenda kuwekeza kule. Hilo ni jambo la kwanza.”
Aliongeza kiongozi huyo: “Jambo la pili, nadhani wakati baba yangu aliposafiri kutoka Kenya kuja Marekani na akarudi nyumbani kwenye miaka ya 1960, pato la taifa la Kenya na Korea Kusini lilikuwa sawa...kwa hakika la Kenya lilikuwa kubwa zaidi. Nini sasa kimetokea katika miaka 50 tokea wakati huo hadi sasa?”
Alisisitiza: “Tulichoshuhudia ni Korea kuchanganya uwekezaji kutoka nje, kujishikamanisha na uchumi wa dunia pamoja na mkakati mkali wa aina ya viwanda ambavyo vililenga katika kuzalisha kwa ajili ya kuuza nje, msisitiko mkubwa kwenye elimu ya nguvukazi yenye ujuzi, ikisisitiza kuwa uwekezaji wa nje unakwenda sambamba na upatikanaji wa teknolojia, ili kuweza kuvijenga na kuviendeleza viwanda vya ndani.”
Rais Obama amesema kuwa kwa maana hiyo Afrika inayo mifano ya kuiga. “Hivyo, tunayo mifano. Tunajua kiasi cha kazi na nguvu na juhudi kinachotakiwa. Jambo ambalo hatujaliona ni matumizi endelevu, yasiyoyumba ya mifano hiyo katika Afrika kwa miaka yote hii, na nadhani wakati sasa umefika wa kuanza.”
Ziara ya Rais Obama inafuatia ile nyingine ya kiongozi aliyemtagulia wa Marekani, Rais George W Bush iliyofanyika mwanzoni mwa mwaka jana, akitembelea nchi nne za Afrika, na kukaa muda mrefu zaidi, siku nne, katika Tanzania akiwa mgeni wa Rais Kikwete.

Kwani Obama alishawahi kufika Tanzania?
ReplyDeleteBw.Michuzi,badilisha hiyo tarehe aliyopokelewa JK na Obama navyojuwa mimi ni kuwa tar 20 january ndipo alipoapishwa Obama na JK alikuwa Marekani mda siyo mrefu uliopita.
ReplyDeleteJaribu kuwa makini unapobandika habari.
wewe mdau ndo hujaelewa hayo maelezo,jaribu kusoma kwa makini sio unakosoa tu.shame on youuuu
ReplyDeleteWee anonymous hapo juu Sat Jul 11, 12:43:00 PM...usikurupuke kabla hujasoma vizuri..tatizo wabongo wako negative siku zote wanatafuta makosa kabla ya kusoma kwa hiyo hata kama kosa halipo atalazimisha hadi alione...ni kama UDSM tangazo limewekwa tuu mtu kaliona tangazo analifata akalisome keshatayarisha kalamu ili alikosoe na kulichafua..Tubadilike..Michuzi kasema..kikwete kakaribishwa white house hakutaja hata tarehe ila tarehe aliyotaja michuzi ambayo ni 20jan ni ya kuapishwa obama...tuition ya kiswahili muhimu mtu wangu ntakulipia
ReplyDeleteMdau ughaibuni
Sasa bro michu hii post yako ni counter punch kwa Atta Mills nini?. Maana kama wao ni first African country Obama kutembelea sisi tunakuwa ni first African country kwa rais wetu kwenda WH ya Obama.
ReplyDeleteIla Ghana hatuwafikii hata kwa chembe kwenye Democracy jamaa system yao ipo fair sana, tena sana. Sisi kwetu viuchaguzi vidogo tu kama Busanda na Biharamuro viongozi woote wanatoa macho na kuhakikisha liwalo na liwe lazima washinde badala ya kuwasikiliza wananchi wamemchagua nani?. Na hiki ndicho Obama atakachokuwa anatupondea na kuipa shavu Ghana.
KUANZIA LEO TAREHE JULY 11, 2009. NAMUOMBA RAISI WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA VIONGOZI WAKE WOTE WABADILIKE, WAKOMESHE RUSHWA NA WAIPIGE VITA RUSHWA NA HONGO KWA VITENDENDO NA SIYO KWA MANENO. TUNAWAOMBA SANA TUKIWA KAMA VIJANA WA TAIFA LENYE AMANI AFRIKA NZIMA TUINUKE NA TUSIMAME KIDETE ILI MIAKA KUMI KUANZNIA SASA NA SISI TUJE TUIONE TANZANIA IKIINUKA KWA UCHUMI KAMA GHANA, RAISI WETU KILA KUKICHA YUPO MAREKANI MBONA HATUJAMSIKIA RAISI OBAMA AKIITAJA HATA KWA DAKIKA MOJA TANZANIA, KWELI IT IS A SHAME, MIKOPO NA MAPESA YOTE UNAYOKUJA KUOMBA KILA SIKU UNAPELEKA WAPI NDUGU RAIS,HUTUBA YA RAISI OBAMA IMENIGUSA SANA NATAMANI KAMA SIFA WALIZOMWAGIWA GANA NCHI NDOGO NA YENYE WATU WACHACHE KULIKO YETU, HIZO SIFA ZINGEMWAGWA KWET TANZANIA AMBAKO RAISI WETU YUKO MAREKANI MOST OF THE TIME AKIOMBA NA KUOMBA NA KUOMABA.TUKOMESHE KUJILIMBIKIZIA NA VIJANA TUAMKE NA KUWAUMBUA HATA KAMA NI BABA YAKO MWAMBIE PESA ZA WANANCHI ZITUMIKE KWA MANUFAA YA WANAMCHI NA NCHI KWA UJUMLA NA SIYO KUJIWEKEZEA WAO WENYENYEWE.NCHI IJENGWE, RUSHA IKOMESHWE, KAZI ZITOLEWE KUTOKANA NA ELIMU NA KISOMO CHA MTU NA SIYO MIMI NI MTOTO WA FULANI AU HUYU KIAJANA BABA YAKE NI RAFIKI YANGU WA KARIBU, TANZANIA ITASONGA MBELE NINA IMANI KABISA WASOME TUNAO WA KUTOSHA NA WENYE NGUVU NA AFYA NJEMA KABISA, CCM ACHIA MADARAKA NA WAPE WASOMI WATAWALE NA BADO WAN NGUVU NA UCHUNGU NA NCHI YAO.
ReplyDeleteTOGETHER WE CAN, VIJANA OYEEEE, HARAMBEEEEEE KWA SANA.
Namimi naunga mkono tabia ya kuwa na mtizamo hasi kabla hata hujasoma kitu haipendezi. Utakuta mtu hata akisoma/au akisikiliza badala ya kuzingatia ujumbe unaotolewa yeye lengo ni kutafuta dosari hata kama haibadilishi maana ya ule ujumbe wote.
ReplyDeleteJK asimwagiwe sifa asizozistahili. Lazima damu imwagiki kwanza ndipo tupige hatua na kufikia demokrasia ya kweli.
ReplyDeleteKatika nchi nyingi za afrika ambazo zimetingwa na wimbi la ufisadi,ukiritimba,urasimu, ukabila nk. usidhani demokrasia itakuwa rahisi kupatikana. Jerry Rawlings ndiye aliyeipika Ghana kwa kuwamaliza mafisadi na wala rushwa wote.Leo hii tunaiona Ghana inafanya vizuri lakini kumbe ni kwa sababu ya mtu mmoja aliyetoa sadaka.
JK ameshindwa kabisa kulishughulikia suala ufisadi, ameshikwa na kigugumizi kupita kiasi kuchuwachukulia hatua za kisheria watuhumiwa wote waliobainika kujihusisha na uhalifu na uhujumu uchumi. Hivyo hastahili hizo sifa kwa mtizamo wangu duni.
So what?
ReplyDeleteinanisikitisha kwamba eti raisi ni wa nchi ya Tanzania lakini sifa anazojivunia ni watu wa nje! hii imekaa kushoto sana kwangu binafsi.Eti leo tunaona ni fahari kwa raisi wetu kusifiwa na raisi wa marekani!,kweli?, kam yeye ni kiongozi mzuri basi asisubiri kusifiwa na watu wa nje ,whatever happens to his own people? kwa nini wewe michuzi na raisi wako msijivunie kwa kusifiwa na wananchi waliomchagua ,kwanza ina manufaa gani kwa wananchi wa tanzania eti raisi wao kasifiwa na Obama! Yeye kama kweli ni kiongozi mzuri na ni raisi wa nchi ya tanzania kwa nini asubiri kusifiwa na obama? kimantik,i kama anafanya kazi yake vema approval yake should come from his voters whom,in my opinion have by far been dillusioned and robbed continually by his team.
ReplyDeleteMza-choshwa
MICHUZI WEKA MAONI YA WATU USIYABANIE, SI WEWE UNAYEANDIKA NI SISI USIOGOPE KUNYIMWA VAKESHENI, HIYO NDO DEMOKRASIA, NA PENGINE ITASAIDIA VIONGOZI WETU KUJIREKEBISHA AU KUJIFUNZA KITU, LEO NIMETUMA MAONI YANGU UMEYATIA KAPUNI, UJUWE NA WEWE UNAKUWA MMOJA WA WATU UNAWOWAKANDAMIZI WANANCHI KWA VILE UNAFADIKA NA VEKESHENI ZAKO NDO UTAKI SISI TUSEMA TUYOWAZA. NCHI NI YETU SOTE SI YENU PEKE YENU, MTUMWA HAUWAWI, UKIULIWA UTAKUWA WAMEKUONEA.
ReplyDeletePela Kikwete ananyoosha suti, eti amepongezwa na Obama!kwa lipi? mbona rushwa,ufisadi, hongo bado Tanzania na Kenya zinaongoza? wewe tulia tu hapo TZ..anayesifiwa anaonekana nihuyo mzee na inchi yake ya Ghana.watanzania tusiwe tunajisifu kwa vitu visivyokuwepo!!
ReplyDeletekero ya zenji kila siku wanaibuka na jipya awa jamaa wanataka NCHI YAO...
ReplyDeleteuko tarime/rorya ndo balaa lingine yan uongozi umeshindwa kutatua hilo?...
mahakama ya kadhi ndo balaa lingine linalotaka gawa waumini wa dini izi za KIGENI...
MIGODI ya majiwe yetu ya dhamani ndo kasheshe aswaaa...
bandari ya Darisalama kituko kingine...
albino kuuwawa,no ufumbuzi...
EPA,RICHMOND,TICTS,BoT minara,mh...
sasa ishu ni kusimama apo na urefu wao na weupe au???