Habari za kazi mzee wa libeneke!

Kwanza nikupongeze kwa kazi nzuri unayofanya kuelimisha na kusheherehesha jamii. Mungu ninayemuamini mimi (naamini na wewe ni huyo huyo) na akujaalie afya bora uzidi kuwepo tuone kazi zako.

Nimelazimika kuandika baada ya kuona malalamiko ya wizi kwenye kiwanja cha ndege cha "kimataifa" cha Mwalimu Nyerere...Da es Salaam. Wengi wameoa maoni yao kumponda mdau, lakini mimi naungana naye kutaka malalamiko yetu yafikishe kunakohusika.
Kaka Michuzi, mimi ninaishi na kufanya kazi katika mojawapo ya nchi zenye hali mbaya ya usalama na vita, mabomu kila siku, tena ya kikweli kweli yaliyodhamiriwa kuua watu (si yale ya Mbagala). Nipo Afghanistan!!
Sasa nafanya kazi ninayojua mwenyewe, kwa kuwa nyumbani kazi kwa anuani, na mimi sina c/o, nikaamua kuja huku. Nimesota miezi kadhaa, vekesheni yangu ya kwanza 2007 nikapitia UAE, nikapiga shopping la uwezo wangu, Simu mbili (kali za wakati huo), Camera ya kueleweka na vitu vingine.
Kwa kuwa Afghanistan na UAE wizi haupo nikajua mambo mswano hadi home kwa hiyo sikujali sana mambo ya kuweka loki ya kufuli kubwa kwenye begi langu..Du yuu noo wati?...Napokea begi langu hadi home uswazi, nimealika familia kugawa zawadi kulingana na ahadi...aibu tupu!! Kaka nimeambulia kufungua mabokisi bila zawadi!! Keni yuu imajini? Kamera na simu umbili kwa mpigo?? Halafu tunaita ni uwanja wa ndege wa kimataifa? Ina maana wakati wale jamaa wanaobeba mizigo wakiiweka kwenye mkanda huwa hawana msimamizi? Maana hadi unafungua sanduku/begi la mtu na kutoa simu toka kwenye mabokisi yake watu hawakuoni??
Kwa kweli hii ni aibu sana kwa nchi yetu, maafisa wa pale uwanjani wanauhusika na usalama waache kukazania kukagua pasi zetu za kusafiria mara kumi kumi kumbe wanatoa nafasi kwa jamaa kufanya mambozzzz.....!!
wajaribu kuwa makini, inauma sana kuona unasota ughaibuni lakini jitu moja lisilojua ubinadamu linafanya upuuzi huu. Wanaohusika hebu wawe macho..tunakerwa sana na tabia za wafanyakazi wa pale, wizi na kutokuelewa wajibu wao!!

Kaka Michuzi hebu wakilisha hii tafadhali
Semesozi
Mdau wa Afghanistan

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 25, 2009

    WAGENI PIA WANAIBIWA, NI AIBU KUBWA KWA NCHI, NAKUUNGA MKONO, LAZIMA HILI SUALA LIFUATILIWE KWA KINA.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 25, 2009

    eeebwanaee hawa jamaa kama hawakukuibia basi wanadai ulipe kodi za ajabu ajabu la sivyo utoe rushwa. duuuhh huu uwanja wa ndege airport unanuka sana.

    ReplyDelete
  3. Tafadhali mdau wa Afghanistan na yeyote yule anayepatwa na mkasa kama huu, aende kumwona mkurugenzi wa Uwanja wa ndege wa Julius Nyerere au atowe taarifa kwa Mkurugenzi mkuu wa mamalaka ya viwanja vya ndege kwa kupitia anuwani wya baruwapepe info@airports.go.tz.Aeleze tarehe ya tukio na Flight Number ya ndege aliyojia.

    Kama uhalifu ulitokea hapa Julius Nyerere, unaweza kubainika na kujulikana aliyehusika kwa kupitia na kuangalia rekodi za zamani za CCTV za maeneo yote ya mizigo.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 25, 2009

    kwanza mimi nilishawahi kubomolewa sanduku langu ila walilamba viatu hawakukuta kitu cha thamani.
    sasa Jamani kwa nini tusimwandikie barua waziri mkuu apangue safu za uongozi hapo uwanjani ili uongozi mpya uondoe wezi, kwani kelele za internet hazimfikii mapema waziri mkuu au Rais.
    Mimi binafsi nitawasiliana na wote hao mara nitakapofika Bongo kwa Barua au simu hata kama kuna urasimu.mara baada ya miezi mitatu.
    ila tatizo sio kama tunawachukia wafanyakazi wa uwanja wa ndege ila tatizo ni wizi tunaouchukia jamani.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 25, 2009

    KUSEMA UKWELI MIMI NAKUPA UKWELI KABISA, KWAMBA WIZI UPO TENA WA KUTISHA KAMA MAALAKA SINAZO USIKA HAZIJACHUKUA HATUA HARAKA, NA NINA USHAIDI KABISA KWANI NILISHA FANYA KAZI BALE MIAKA MITATU NAPAJUA VIZURI SANA, MIZIGO INAIBIWA NDANI YA NDEGE PALE WALE WAFANYAKAZI WA SWISSPORT WANAPOSHUSHA MIZIGO KAMA IKISHINDIKANA NDANI YA NDEGE WANAIBA KWENYE MAGARI YAO WANAYO PAKIA MIZIGO, PIA WALINZI NAO WANAUSIKA KWA KIASI KIKUBWA HASA WALINZI WANAO KAA KWENYE MTAMBO WA KUSCAN MIZIGO, WAKIONA NDANI KUNA COMPUTER(LAPTOP), CAMERA, SIMU NA VIDEO CAMERA WANAWASILIANA NA WAPAKIA MIZIGO KWENYE NDEGE ANAMWAMBIA KWENYE BEGI FULANI KUNA HIKI NA HIKI NA WALE WANDANI ATAFANYA JUU CHINI WATALIFUNGUA NA KUIBA. HIVI NDIVYO WIZI UNAVYOFANYIKA NA UTAWALA WA SWISSPORT UNALIJUA HILI KUNA WAFANYAKAZI WENGI TU WAMEFUKUZWA KAZI KWA TUUMA ZA WEZI. DANNY

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 25, 2009

    pole sana kaka kwa kazi unayoifanya alafu mtu anakuibia zawadi zako kweli inauma sana lakini mimi kuna siku nilishuka na begi bila kufuri sikuibiwa kitu ila marafiki zangu wengi yashawakuta na kuna usumbufu usio na sababu unaweza kushuka na passport ya bongo lakini wanakuuliza unafikia wapi yaani uwape adreess yako,,, hii kweli ni vicheleo na sio kichekesho

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 25, 2009

    Mdau wa Afghanstan pole sana, na pole pia kwa kuishi huko. Ukiona vipi rudi home ndugu yangu. Afadhali ukaishi Mbagala kuliko huko. Bali kama una dili endelea.

    Wizi wa JK Nyerere airport ni aibu kubwa. Aibu kubwa zaidi ni pale unapokutana na wahudumu ombaomba wanaokuomba uwaachie sarafu zilizobaki wakidai kwamba huzihitaji kwani wapaa nje ya nchi. Kuomba ni haki ya mtu, lakini ukiwa wa-control passport halafu waomba chenchi, message unayotuma ni kwamba unadai hongo ili Mtz atoke nje ya nchi.Tusiishie kuandika kwenye Blog, jambo hili tujaribu lifike kwa wizara husika na bungeni pia. FirePower UK

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 25, 2009

    Watanzania wenzangu msishangae kabisa mimi nilipokuja kutembea Tz nikagongewa katika pasi yangu ya TZ unaruhusiwa kukaa TZ siku 90 na hurusiwi kufanya kazi au biashara nilishangaa saana baada ya kuona muhuri huo nilipofika nyumbani.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 25, 2009

    Hebu fikiri! Umemwahidi mke wako zawadi nzuri, au mtoto wako! Halafu ufike nyumabni ukutane na sanduku tupu!!!!!! Im telling you vacation yako it will never be the same again! Wizi pale Airport ni fedheha kwa taifa, shame on us! Aibuuu! Kazi za ukuli kwetu tunaziona kama ni za watu wasio na shule! Ndio maana wanaiba wameokotwaokotwa tu!
    Kazi hizi jamani ni professional! watu lazima wafundishwe darasani miiko na maadili ya kazi. Sio kuokota mtu tu kisa anaweza kunyanyua mzigo. Shule inaweza transform mtu the way anavyo fikiri, mtazamo na kufanya maamuzi, Pia inamfanya mtu alinde hadhi yake na aheshimu kazi yake! sehemu zingine tunapita hakuna vitu hivi kabisa! Weka hata kipande cha sabuni au hata jiwe kwenye bagi lako uone watakavyo funufunua! A delibarate search! wanasaka! CCTV camera zipo! Ukiriport utapigwa tarehe mpaka uta givup! Manake wanalindana! Rais Ingilia kati! Najua suala hili litapungua kwa mtu baada ya kelele za watu lakini hili sio suluhisho!
    Waajiliwe professionals waliokalishwa darasani wakafunzwa namna ya ku handle mzigo wa abiria kwa uaminifu mkubwa!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 25, 2009

    Nimefanya kazi Airpot Dar! Suala hili lipo sana! Abiria kila siku wanalalamika kuibiwa laptop, simu camera etc. Huwezi ambia watu waweke vitu hivyo kwenye hand laggage maana kwao hakuna wizi kama huu! Labda! Tutume matangazo huko kwenye viwanja mablimbali kwamba "ABIRIA WANAOSAFIRI KUELEKEA DAR TUNAOMBA MHAMISHE ELECRTONICS ZENU KWENYE HAND LAGGAGE MANAKE KUNA UDOKOZI WA VITU HIVI PALE JNIA"
    Hivi ndivo tuanvojitangaza! aibu kubwa sana! Unasafiri kwenye ndege halafu unawaza sijui mzigo wangu utafika salama! Jamani

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 25, 2009

    Hii Bongo mzee, unashangaa wanakuuliza unafikia wapi na una paspoti ya Bongo? Si wanataka wajue wapi utakuwa usiku wakutumie vibaka.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 25, 2009

    kaka michuzi hongera kwa kazi nzuri !

    haya mambo ni ya kusikitisha na ni aibu kwa kweli . ni mwezi mmoja tu ilikua tarehe 21 jun nilitoka zangu birmingham uk kupitia dubai na kutua dar 22 jun nimetoka air port hadi nyumabni nashkuru sikusumbuliwa pale mlango wa kutokea nje kumbe nilishalizwa kule ndani nafika nyumbani jezi mbili za arsenal na moja ya man u brand new na sim moja ya sonyericcson c902 brand new zimeyeyuka ndani ya begi nilisikia uchungu na kulaani wafakanyakazi na ongozi wote wa pale ukweli hapafai kuna wezi wa kutisha. WAFANYAKAZI WASAFISHWE HARAKA IWEZEKANAVYO !

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 25, 2009

    Wizi upo sana. Mimi waliniibia tochi na rangi ya viatu na brush za viatu!! Can you imagine hiyo njaa kali sana! Hata hivyo sio sababu ya kufungua mizigo ya watu, siku nyingine watapambana na cobra ndio watakiona cha mtema kuni! Anony Tarehe Sat Jul 25, 12:25:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous, safi sana, maana maswali mengine bwana yanakatisha tamaa. Mimi nimerudi nyumbani halafu unaniuliza nakaa wapi na naenda wapi? Huko ng'ambo tunyanyaswe, na nyumbani tena? Makubwa!!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 25, 2009

    MICHUZI WEWE MTU WA SERIKALI UPO KARIBU SANA NA AKINA KIKWETE NA WATU WAKE TUFIKISHIE HIZI HABARI, SI WATAFUTE UMAARU TU BILA YA KUJALI MAMBO YETU, NIMESHAONA MAMBO YA SERIKALI YANAANDIKWA KWENYE BLOG YETU HII NA WAKUBWA WA SERIKALI NA HIZI HABARI WAZIPATE, PIA HASA HAO WAKUU WA IKULU, HUWAGA WANATUPA HABARI ZAO HUMU NASI TUNAWAPA HIYO, WATUSAFISHIE BANDARINI, POSTA NA UWANJA WA NDEGE.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 26, 2009

    Tanzania!!! we acha tu! Kuanzia mawaziri mpaka wabeba maboksi wa uwanja wa ndege na bandarini ni matatizo matupu!
    Lakini hii yote ni hurka tu! na niushenzi na ni upumbavu.
    Nilishaweka suti case kwenya container na ilikuwa na DVD player 3 na accessories nyingine....kwanza wakadai ile suit case haikuwa declared...na baada ya kufunguliwa wakasema hizo dvd player, zilipiwe ushuru...jamaa alokuwa akishughurikia akalipia...lakini baada ya kufika nyumbani DVD player mbili alizolipia ushuru hazimo na wamechukua na remote control zote hivyo hata hiyo iliyobakia...ikawa haina remote control.
    I was really disgusted and ashamed...is this where s'one can call home???
    Hii siyo njaa, tusidanganyane...ni hurka tu! tumeona kuanzia kwa viongozi wa kitaifa mpaka wafagiaji.
    Nchi inatakiwa kubadilika, la sivyo!! tutaonana wabaya.
    Nakupa pole ndugu yangu na naomba nikueleze kuwa...siyo wewe peke yako.
    Ndiyo maana nashauri, mtu yeyote anayepeleka container Tanzania..kubali gharama zote, pitisha Mombasa......Naipenda sana nchi yangu Tanzania, lakini utamaduni wa wizi ulokuwepo Tanzania...unakera.
    Mdau London

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 26, 2009

    bongo tambarare nyie hamjui!!!????ebo!!!!

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 26, 2009

    Aibu na uduni itawale maishani mwenu wezi muibao majasho ya watu,mmediriki na kuchagua kutamani yasiyochumwa na mikono yenu,jasho,huzuni na vilio vya mnawowazulumu yanagubika nyoyo zenu!Hakika mnafanya mambo yaliyo mabaya na yasiyopendeza mbele ya MUNGU.MSIFANYE HIVO.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 27, 2009

    Nina mpango wa kutengeneza pipi za kinyesi nitaziweka nje nje ili jamaa wakafaidi.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 28, 2009

    Heri umetuambia pipi na chocolate hazina dili tena.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...