Mkurugenzi Mtendaji wa NMB Ben Christiaanse akizindua NMB Mobile
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano Imani Kajula akiwa na maafisa wengine wa NMB. Mkuu wa wateja binafsi Abdulmajid Nsekela, Mkuu wa Idara ya Uhusiano Shyrose Bhanji na Mkuu wa Fedha Waziri Barnabas.


NMB YAZINDUA HUDUMA ZA KIBENKI KUTUMIA SIMU ZA MIKONONI-NMB mobile.

Banki ya NMB imeweka historia nchini Tanzania kwa kuzindua huduma ya NMB mobile inayomuwezesha mteja kupata huduma za kuangalia salio, kutuma fedha, kuangalia statimenti fupi, kununua luku, na muda wa maongezi wa Vodacom au Zain.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa NMB mobile, Mkurugenzi Mtendaji wa NMB Ben Christiaanse alisema ‘’ Hii ni hatua kubwa kwa NMB na wateja wake kwani sasa wateja wana wigo mpana wa kupata huduma na pia kuokoa muda, fedha na adha ya foleni’’. Mwaka 2006, NMB iliandaa mkakati wa miaka mitano wa kuboresha huduma. Hadi sasa NMB ina matawi zaidi ya 130, ATM zaidi ya 210 Nchi nzima. NMB inatazamia kuwa na ATM zaidi ya 270 ifikapo mwisho wa mwaka 2009.

Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa NMB Imani Kajula akielezea faida za NMB mobile alisema ‘’ NMB mobile inawezesha wateja wa NMB Personal Account, NMB Student Account na NMB Wisdom Account kupata huduma za NMB popote walipo wakati wowote na kwa gharama nafuu. ‘’
Kujiunga na huduma ya NMB mobile ni rahisi na haihitaji mteja kwenda kwenye tawi la NMB, unachotakiwa kufanya ni kupiga namba *155*66*123# kisha fuata maelekezo”.
Huduma ya NMB mobile inapatikana kwa wateja wa NMB wenye mitandao ya ZAIN na Vodacom. NMB inategemea kuwezesha huduma hii kupatikana kwa kutumia mitandao mingine pia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 25, 2009

    hii hata ulaya haipo. safi sana, lakini sasa tutakufa masikini, kwani najua ijumaa na jumamosi baa zitauza sana, kwani pesa sizipo katika simu. cha muhimu simu kuwa na charge tu. kama ATM tu zimetufilisi, hii si ndo itakuwa kiboko kabisa.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 25, 2009

    Hongera sana Kisura..naona sasa jasho lote limelipa.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 25, 2009

    Michuzi hii si huduma ya kihistoria Tanzania. CRDB bank PLC wana huduma hii ya SMS yapata miaka minne sasa, tena imeboreshwa zaidi na unaweza hata kuhamisha pesa kwa SMS kwa kipindi hiki.
    Upo mzee wa bwawa la maini?

    Baba D

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 25, 2009

    Baba D umechapia, inatakiwa uweze kutofautisha SMS alerts na Mobile phone banking. NMB pia wana SMS salary alert kwa ajili ya kuwajulisha wafanyakazi punde pesa zinapoingia. NMB mobile inakuwezesha kuingia kwenye account yako popote ulipo, tena hii inatumia USSD technology na ni real time. Unaponunua Luku hapo hapo unapata huduma na TANESCO wamepata mshiko wao, voucher za simu ni real time pia, kutuma fedha au kuangalia balance haya yote ni realy time. Mobile phone banking ni huduma mpya sana ndiyo maana M-PESA ya Safaricom ni huduma dunia nzima inaipigia mfano. Jamani penye ukweli tuseme, benki za bongo zimeanza kuamka. Nafanya kwenye mobile company, hivyo nanusa, CRDB nao wanataka kuanzisha mobile banking kutumia JAVA technology. Baba D upo au haupo? uliza staff wa CRDB watakwambia wanafanya pilot ya mobile banking kabla ya kuzindua pia hivyo NMB imeipiga bao CRDB!!!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 26, 2009

    Hongereni sana NMB,Imani kajula naona juhudi zako zinazaa matunda.Nimesikia kuwa ni mchapa kazi sana.
    Hongereni management yote kwakweli.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...