Tafadhali mdau wa Afghanistan na yeyote yule anayepatwa na mkasa kama huu, aende kumwona mkurugenzi wa Uwanja wa ndege wa Julius Nyerere au atoe taarifa kwa Mkurugenzi mkuu wa mamalaka ya viwanja vya ndege kwa kupitia anuwani wya barua pepe
aeleze tarehe ya tukio na Flight Number ya ndege aliyojia.

Kama uhalifu ulitokea hapa Julius Nyerere, unaweza kubainika na
kujulikana aliyehusika kwa kupitia na kuangalia rekodi za zamani za
CCTV za maeneo yote ya mizigo.

A Mbamba

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 55 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 25, 2009

    Je CCTV camera inaanza kuchukua image tokea buti ya ndege inapoanza kufunguliwa na mtu anaposhusha mizigo ndani ya buti? Hapo dawa yake sio hizo images bali ni kuwa na wafanyakazi ambao ni waaminifu. Mwanadamu huwezi kumchunga kwa CCTV tu. Je ikibainika waliiba, je wanapitaje magetini kwenda nyumbani? Nchi za wenzetu mizigo inashushwa mbali pasipo hata na CCTV lakini mtu hana tamaa ya kupekuwa begi au sanduku la mtu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 25, 2009

    Acha visingizio vya CCTV, mbona hata bandarini mambo ni hayo hayo tu. Na wakati majirani zetu kenya, bandari yao haina wizi kama Dar.Suala hapo ni kuwa wakweli kwamba maisha ya ujanja ujanja hayakubaliki hata kidogo katika karne hii

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 25, 2009

    Asante kwa taarifa. Tafadhali tambua kwamba aliyeibiwa au wengi waliobiwa vitu vyao hawako ndani ya nchi, na hata kama wangekuwepo huo muda wa kuja kutazama CCTV ili kumtambua wahusika haupo, na hata huo muda ungekuwepo, vitu hivyo tayari vimetoa na wahusika wameingia hasara kifedha na kisaikolojia.

    Mkurugenzi ni vizuri atambue kuwa kama anashindwa 'kusafisha hiyo nyumba yake' kwa kuhakikisha wizi unakwisha basi sisi tutaanza na kibarua chake.

    Lazima tuwe wawajibikaji, tuache longo longo.

    ReplyDelete
  4. Tatizo la eapoti lipo katika idara zote. Mi naona hayo ni maneno ya kujiosha tu lakini ukweli ni wezi na hao wezi wanajua kama kuna kamera uwanjani hivyo wanaiba wakijua kabisa kamera haziwachukui sio watoto hati. kinachotakiwa Uongozi ufanye uchunguzi wa siri ili kuwabaini wezi na kuiondolea taifa aibu. kama kweli wana nia ya kuliondoa tatizo hilo na sio kuangalia CCTV hawataona kitu huko.Tunatia aibu jamani kila siku nikisafiri napata matatizo uwanja wa dar tu. Ukiingia mbinde ukitoka mbinde.

    ReplyDelete
  5. ni mazingaumbwe tuu ya bongo kama kawaida

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 25, 2009

    Hamna lolote, usanii mtupuuuu!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 25, 2009

    Mh A Mbamba,ulikuwa hufahamu kuwa
    mizigo yetu inafanyawa ufisadi hapo
    airport?Kama ulifahamu iweje imechukua muda mrefu kutoa hilo suluhisho?Ninawasiwasi kuwa na wewe unahisika na wizi ama umewapanga vijana wako wakufanyie
    kazi hiyo,kama sivyo tunaomba tupewe taarifa za watuhumiwa kukamatwa.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 25, 2009

    Hii msg mimi bado sioni kama inasaidia hata kidogo. Ninachokiona hapa vile vile vitendo vya viongozi kukana kuwa kuna uhalifu mpaka uwapatie ushahidi. Hivi unapotoa e-mail badala ya kufunga free telephone uwanjani za mtu yeyote aliyeibiwa kupiga simu moja kwa moja kwenye mkurugenzi at the time of tukio unatarajia nini?.

    Au ndiyo kwa kuwa sasa MKONGO wa SEACOM umetua Dar basi tunataka kujifanya kila kitu mtandao?.

    Hivi mtu akikuandikia email halafu ukaitrash si ndiyo yale yale ya kulindana?. Wewe kama una CCTV kweli kwa nini wafanyakazi hauwa-fuatilii hatua kwa hatua, maana mwizi ataonekana tu wakati anaiba na siyo kutafuta kuwa nani alikuwa kazini siku hiyo umtoe kafara kwa ili kuongeza public trust ya uwanja uliyojaa ma-vulture wa mizigo ya watu.

    Kitu kinachonikasirisha kwenye uwanja ule siyo kupotea kwa mizigo hata tabia ya wafanya kazi ya kuombaomba umwachie dollar, euro au pound zimekithiri sana. Hasa sehemu za check up, pia wanalazimisha mtu uache mzigo kwa kisingizio umezidi ili wao wachukue na hata kama unajamaa yako unataka kumpatia wanakwambia hairuhusiwi kweli!, jamaa hawana aibu kabisa wanaomba hata matonya ana nafuu maana yeye anakinga bakuli tu hakubughuzi kama hawa wafanya wa DIA.

    Kuanzia huyo mlinzi anaye monitor hizo CCTV mpaka anayekuwa monitored wote ni wezi kwa sababu wanashirikiana na pengine hata kuharibu evidence ya CCTV.

    Ili kusafisha uwanja, ajiri watu waaminifu na usiwe na mercy kwa lalamiko lolote.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 25, 2009

    Hapo ndo umeongea! Watafuteni hao wezi wawajibishwe kwa mjibu wa sheria! Camera zile zinaona kila mahali, tangu boot inafunguliwa mpaka abiria anachukua mzigo wake. Jamaa hapo juu wanazungumzia uaminifu! Let me tell you something! Mtu huwa anapractice uaminifu mahali palipo na law and order. Wazungu kwao ni wanaheshimu sana sheria na wanautiifu wa hali ya juu! Lakini wakija Afrika kusiko kuwa na sheria kamilifu utasikia mambo ya blood diamond, Mara wamekwepa kodi etc. Usimamizi kwanza, sheria zifanye kazi, wahusika wawajibishwe, utaona mtu kama atadokoa tena!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 25, 2009

    sina hata hamu na hapo airport bongo,niliibiwa vitu vya karibu euro 10000,perfums,piece moja ya mziki wangu,saa...inamaana huyo mkurugenzi ndio anajua leo...

    CCtv hskuns chochote,namuunga mkono mdau aliyesema,kwamba tunahitaji wafanyakazi waaminifu.
    Sasa,mfano wakisema,umeme ulikatika na cctv zilikuwa hazifanyi kazi,ntafanya nini...
    kama zinafanya kazi inakuwaje watu hao wana jeuri ya kuiba,hali wakijua wanaonwa?
    wote wanashirikiana.
    This makes me 2 hate home,
    Im living here,I have peace of mind and everything.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 25, 2009

    jamani nimevumilia nimeshindwa kuhusiana na huu wizi wa air port,kwanza huyu jamaa anaesema eti apigiwe simu kutaarifiwa aina ya ndege na mizigo mtu ulliyonayo hana akili hata moja maana kama abiria wote watampigia simu si inamaana bado anajukumu la kusimamia mizigo yao yote yaani abiria wote? kitu ambacho ndicho sisi tunataka akifanye.haya hata kama atapigiwa simu na abiria mmoja au wawili inamaana mizigo ya hao waliopiga simu tu ndio italindwa then mingine aiache iibiwe kwakuwa hawakumpigia simu hivi hiyo ni akili au tope?tunaomba sana uongozi mzima hapo uwanja wa ndege uwajibike katika kutatua tatizo hili na si kutuambia tupige simu.na hao wachangiaji wanaodai watu washukie kenya sielewi wanafikiria nini yaani mtu unaishi mbea alafua ukashukie kenya uanzane tena na mamizigo kwenye mabasi hadi mbea na hata hivyo kama kila abiria ataamua kufanya hivyo basi ndio mtakuwa mnarisk maisha yenu wenyewe kwani wezi wakishajua mchezo wenu ni huo eleweni kuna siku buss hilo litatekwa na mtachijwa then muwe mmepoteza roho zenu na mizigo yenu pia.yaani nchi inatia aibu hadi mtu ukifikiria kurudi nyumbani unakata tamaa ubebe kitu gani.naomba mkuu wa nanihii ujitahidi raisi apate haya malalamiko yetu maana tumechoka.
    mdau scandinavia....

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 25, 2009

    WATANZANIA WANA TABIA MBAYA INATAKIWA KUKOMESHWA, KWA NINI UIBE KUTOKA KATIKA MIZIGO YA WATU! DAWA NI KUFUKUZA KAZI TU, HUWEZU TUMA KITU TANZANIA BILA YA KUCHOKONOLEWA, KUANZIA POSTA, BANDARINI NA AIRPORT, NIMETUMA MAGARI MARA KIBAO NA YOTE YAMEIBIWA VITU, HALI NI MBAYA NA WAKUBWA WA SEHEMU HIZO ZA KAZI WANAKUMBATIA NAO NI WEZI PIA, HIVI SERIKALI INAJUWA HILI AMA NAO WANAFAIDIKA KWA NAMNA MOJA HADI NYINGINE EBU WACHUKUWE HATUA.

    ReplyDelete
  13. SIO AIR PORT TU,KWANI HATA POLISI GARI LIKIKAMATWA JEKI NA SAITI MIRA HUWA VINAPOTEA.
    HAKUNA SUALA LA UAMINIFU WA MTU KATIKA SUALA LA MALI AU PESA.HAPA KINACHOTAKIWA NI PROPER ADMINISTRATION.WENZETU ULAYA MTU HAAMINIWI ILA NI ADMINISTRATION SYSTEM NDIO INAMBANA MTU.KAMA NI KU SCAN MIZIGO NA INAKWENDA KWA DEPARTMENTS.KIKIPOTEA KITU ITAJULIKANA KIMEPOTEA WAPI NA MIKONONI MWA NANI.HAPO NDIO CCTV HUFANYA KAZI KTK HATUA YA MWISHO HASA KWA UPANDE WA POLISI.
    TATIZO LETU HAPA BONGO NIKWAMBA HAKUNA KITU KINAITWA ADMINISTRATION KABISA KILA UNAPOENDA KUNA MIANYA YA WIZI(LOOPLES).HATA KUPOTEA KWA MAPESA YA TAIFA AU UKWEPAJI WA KODI.MTU HATAKIWI KUAMINIWA HATA SIKU MOJA ILA ABANWE NA SYSTEM KAMA WENZETU.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 25, 2009

    Tanzania Wenzangu:

    Dawa ya hawa watu, TRA na DAR airport ni kutumia Nairobi na Bandari ya mombasa, Tumechoshwa na ufisadi na Wizi

    Waziri wa FeDHA pitisha Fimbo TRA, Jumanne Kawambwa Fumua Viwanja vya Ndege, majambazi na yanatia aibu

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 25, 2009

    Mjumbe hauawi, vipi mdau anashambuliwa kwa kutoa maoni ya kujaribu kusaidia wadau wasiendelee kutaabika?
    Wadau tushirikiane kuvalia njuga tatizo hili tulimalize. Sema noma hukawii kuambiwa kwamba system ya CCTV ilikuwa dauni kwa sababu umeme ulikuwa umekatika na jenereta imeishiwa mafuta.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 25, 2009

    Huyu mkurugenzi anataka kuleta siasa sasa
    Watu tumepoteza na wanpoteza vitu muhimu sana
    Mimi tangu walponiibia Laptop yangu ambayo ilikuwa nifanye presentation after six hours from my Arrival
    Yaani alivyonipa wakati mgumu nadiriki kusema huyu mkurugenzi kazi imemshinda
    Sasa tukuletee malalamiko wewe kivipi waka sheria inasema wazi uripoti polisi na hao polisi ukienda karatasi hawana.
    Bora atuahidi kuzuia huo ubaladhuri na sio kumpelekea malalamiko asituletee mambo ya kina Zombe
    Kama wtu wako wa chini wanaiba you are responsible kwa huo udhalimu
    USHAURI WA BURE BORA AACHIE NGAZI WANAOWEZA KUDHIBITI HUO WIZI.

    Mdau mlalamika nambali one
    Yaani tukikutana popote uji introduce kama wewe ni mkurugenzi mkuu wa pale itabidi nikudai wewe tuu

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 25, 2009

    Inasikitisha sana hali ya hapo airport ni mbaya sana.dawa ni kuwapunguza wafanyakazi wote na kuweka wapya waaminifu.matukio mbalimbali yako kwenye CCTV lakini hakuna hatua zinazochukuliwa.Na kama mzigo wako umekuja unaccompanied ndipo utaelewa usumbufu ni nini

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 25, 2009

    Mbamba, acha Siasa Bwana!....Eti Tutaangalia kupitia record za zamani za CCTV!..Uaminifu kwanza halafu CCTV ndo zinafuata.

    Mdau Zanzibar

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 25, 2009

    HIKI NI KITENDO KIBAYA KWELI UNAVYOSEMA ALETE FLIGHT NO JE ALISHAITUPA HIVI VISINGIZIO NA KUANZA KUJITETEA NI JAMBO BAYA SANA HAKUNA MTU MWENYE AKILI TIMAMU TENA WENGI KIASI HICHO KLALAMIKA KWA KITU HICHO TU LAZIMA KUTAKUWA NA TATIZO TENA SI DOGO NI KUBWA CHA MUHIMU NI KUCHUKUA HATUA JE MFANYAJE ILI KUWEZA KUKOMESHA HIYO TABIA

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 25, 2009

    Ah! WIZI MTUPU..hata kwa huyo meneja mwenyewe..ina maana hakuna aliyewahi kumlalamikia kuibiwa miaka yote hii? ameshafanya nini so far na CCTV zake? mana wizi ungekuwa unapungua na sio kuongezeka kama kweli hizo CCTV alizoweka anajua umuhimu wake na anafuatilia zinaonesha nini. Mi naona ni ubabaishaji tu, hamna lolote wanalofanya, wanajuana wote na wanashirikiana, haiwezekani kila siku mizigo iibiwe mtu hadi anafungua begi na kulifunga ina maana hakuna anayeona?

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 25, 2009

    Wadau kuweni reasonable kidogo.

    Munaambiwa musaidie utawala wa uwanja wa ndege kuwatambua wahalifu kwa kutoa ushirikiano kwa njia ya kutoa maelezo amabayo ni very basic sasa badala ya kushirikiana munataka kuendeleza lawama.

    Kama hamutaki kutekeleza sehemu yenu vipi tutaweza kumaliza haya matatizo.

    Hili obmli kutoka uwanja wa ndege ni mfano mzuri wa kuigwa, tuache tabia ya kupoknda kila kitu hata pale amabapo uongozi umeonesha nia ya kushirikiani kutatua matatizo.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 25, 2009

    KUNA NJAA KALI SANA HAPO KUNASIKU WAFANYAKAZI WAWILI KATIKA KUPEKUAPEKUA ZAO SIJUI HATA HUWA WANAPEKUA NINI MAANA MARA WANACHAMBUA NGUO MBILI TATU HALAFU WANAKWAMBIA HAYA ONDOKA BASI KWENYE POCHI YANGU WAKAONA SHILINGI ELFU TANO MBILI NILIKUWA NAKUJA UK BASI WAKANISHAMBULIA ETI HAYO MADAFU UNAPELEKA WAPI MI HELA ZANGU ZINAWAHUSU NINI YAANI BASI TU KARAHA ZA HAPA NA PALE AU MISHAHARA LABDA MIDOGO PIA NIGEWASHAURI MABOSS WA HAPO ANGALAU WAWAPELEKE WAFANYAKAZI WAO NJE YA NCHI WAONE WEZAO WANAVYOFANYA KAZI KWA UFANISI WA HALI YA JUU SI KWA MATAKWA YAO BINAFSI TANZANIA TUACHE TABIA HIZI JAMANI

    ReplyDelete
  23. Issa tunafurahi kuona kuwa ujumbe wetu umewafikia.

    Lakini hii ya kusema watu wapeleke ripoti ya siku waliyosafiri tunadanganya, sie tunachotaka kusikia ni mabadiliko! tusisikie mtu analalamika kuwa kaibiwa. Mwizi anaeijua kazi yake hawezi kufanya mamabo yake Camera ikiwa inamwangalia labda awe kibaka.

    Narudia tena..WE WANT CHANGES SWISSPORT and JNIA. Hii aibu ya sisi kuonekana wezi tunapoongea na raia wa nchi nyingine hadi tunashindwa hata kuwashawishi waje kututembelea imetuchosha..enough is enough.

    Ni matumaini yangu mtabadilika.

    Jasmin

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 25, 2009

    Mi napendekeza tubadilishe jina la Eapoti yetu, napendekeza tuiite FISADI INTERNATIONAL AIRPORT!! Ili popote ulipo ukiwa unafanya booking yako ya ndege unajua mara moja kwamba destination yako ya mwisho unakumbana na Ufisadi. Ni udhalilishaji wa hali ya juu kuendelea kutumia jina la NYERERE wakati maskini Baba yetu alipinga ufisadi kwa nguvu zake zote mpaka siku ya mwisho. Kwa hiyo jamani, kuanzia leo Eapoti yetu ya Dar inaitwa FISADI INTERNATIONAL AIRPORT!!!!

    ReplyDelete
  25. AnonymousJuly 25, 2009

    Aisee hebu acheni kutuyeyusha!! mnatakiwa kutueleza ni kivipi mnakuwa na wafanyakazi wezi wa kupindukia kiasi hicho. Mizigo kupekuliwa na kuibiwa vitu haijaanza leo na watu wote wanaoibiwa huwa wanareport kwenu, sasa tunataka mtuambie kwa kesi ambazo zilishakuwa reported kwenu mlichukua hatua gani. hizo cctv si mnazo tayari, sasa uambieni mlichukua hatua gani kwa cases zilizokuwa reported tayari. swala hapa sio kutuimbia nyimbo za CCTV suala ni je mnaboreshaje huduma zenu nyie?? hivi nikiibiwa harafu nianze kureport na kuwasubiri mchunguze kamera zenu hamuoni ni kunipotezea muda?? tunaomba wale wafanyakazi wote walioko kitengo cha kushusha na kupakia mizigo muwafukuze kazi hawafai ili watakaokuja wajifunze!!!

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 25, 2009

    Unajua watanzania siku zote ni waongo na uadilifu umetupitia mbali sana! Katika viwanja vya ndege nilivyobahatika kupitia Uwanja wa Mwalimu Nyerere Dar ni wizi mtupu!! Hizo CCTV Camera zake anazosema siyo realistic, nimeshakagua sana pale na yaonekana ni njama za makusudi!! Huo wizi umetokea 2007 kwa mujibu wa mdau, kwa CCTV zenu feki za pale unaweza kurevise mkanda hadi 2007? Si kudanganyana tu huko? Halafu pia wafanyakazi wa uwanaj wa ndege hawajui kabisa mambo ya "Customer Care", baada ya wizi kutokea ishu iliripotiwa lakini lawama zikageuzwa kwa mlalamikaji kuwa kwa nini hajafunga begi!! Suala ilikuwa si kuuliza kwa nini begi halijafungwa kwa kufuli, ilikuwa inakuwaje mfanyakazi wa airport afungue begi la abiria?? Kwa kweli tunaomba wahusika walishughulikie hili!!

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 25, 2009

    Sina uhakika kama hizo CCTV camera zipo kwenye sehemu ya kuwekea mizigo ya ndege ambako huko ndiyo kiini cha matatizo.
    Wahusika wote pale uwanjani wanaelewa kuwa wizi wa mara kwa mara hufanyika katika sehemu ya kuhifadhi mizigo ndani ya ndege yaani mahali hata CCTV na wasimamizi hawafiki.
    Hili eneo likiweza kudhibitiwa basi wizi utapungua kwa asilimia kubwa sana.

    ReplyDelete
  28. Changa la macho,hakuna lolote la maana hapo. Huo upumbavu wa uwanja wa ndege haukuanza jana wala leo! njaa+tamaa=Bongo

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 25, 2009

    MIMI NAWAUNGA MKONO WADAU WENGI WALIO TOA MAONI YAO, HILI TATIZO HALIJAANZA LEO. MUHIMU NIKUWA NA WAFANYAKAZI "WAAMINIFU". MIMI MKASA WA HAPO AIRPORT YA UWANJA WA NDEGE DAR USHAWAHI TUNITOKEA MIAKA YA TISINI. NILIKUWA NA BEGI LANGU NILILI WEKA KUFULI KWA SABABU LILIKUWA NA VITU VYA THAMANI. NILIPOLIPOKEA BEGI TAYARI KWA KUELEKEA NJE NIKAONA LIMENYOFOLEWA UPANDE. NIKAWAELEZA WAFANYAKAZI, JIBU NILILOPATA NI "UMETULETEA ZAWADI GANI...?" WALINIULIZA. WAKASEMA MILAZIMA NIFUNGUE BEGI ILI KUONA KILICHO KUA NDANI. KWA MOYO MMOJA NILIFUNGUA. CHA KUSHANGAZA WALIKUA WANA TAKA NIWAPE BAADHI YA VITU VILIVYO KUWA NDANI YA BEGI. ILIBIDI NIFANYE HIVYO KWA SABABU TULIANZA
    KUSUMBUANA KWA MUDA. HUU NI UWANJA WETU WAGENI AMBAO WANAKUJA KATIKA NCHI YETU WENGI HUPITIA HAPO NA SIFA WANAYO IPELEKA NJE NI MBAYA...

    ReplyDelete
  30. AnonymousJuly 26, 2009

    JAMANI HII IMEKAA VIPI TENA KUIBIANA VICAMERA KILA KUKICHA WAKATI MNATUAMBIA BONGO TAMBARARE??

    ZINAWAFIKISHA WAPI SASA HIVYO VITU MNAVYOIBA??

    HAKIKA VINAWAFEDHEHESHA MILELE POLENI SANA KAMA MNANJAA SIMUOMBE TU ETI BONGO TAMBARARE TAMBARARE MNAIJUWA LAKINI??

    ReplyDelete
  31. AnonymousJuly 26, 2009

    jamani kwani airport hamuwezi wachoma moto hao vibaka au mnaogopa tai zao?

    ReplyDelete
  32. AnonymousJuly 26, 2009

    Mkuu hapo (EAPOTI ya Uwanja wa Ndege dar)Hulizwa watu kwa makusudi?

    ReplyDelete
  33. AnonymousJuly 26, 2009

    Angalieni mfano huo:

    Wizi wa mali ya mtoto wa JK: watuhumiwa watajwa

    2006-08-05 14:39:03
    Na Mwandishi Wetu, Airport


    Watu wanne waliohusishwa na wizi wa mali ya mtoto wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, uliotokea hivi karibuni pale kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Jijini Dar es Salaam wametajwa.

    Kwa mujibu wa chanzo chetu, awali washukiwa walikuwa saba lakini watatu wakaachiwa huru baada ya kuonekana hawahusiki na tukio hilo.

    Kwa mujibu wa chanzo hicho waliobaki kwenye tuhuma hizo wako wanne.
    Watuhumiwa hao wametajwa kuwa ni Shaaban Jako, George Emmanuel, Rajab Ali Mohamed na mmoja aliyetajwa kwa jina moja la Raphael.

    Tukio hilo la aibu lilitokea usiku wa kuamkia Agosti Mosi mwaka huu saa 2:50 pale uwanja wa ndege.

    Ilielezwa kuwa kijana huyo wa Rais alikuwa akitokea nchini Uingereza kupitia Dubai.
    Kijana huyo ajulikanaye kwa jina la Miraji Jakaya Kikwete, inasemekana alibaini kuwa amekwapuliwa mali zake baada ya kufungua mzigo wake na kukuta baadhi ya vitu vimeyeyuka.

    Kwa mujibu wa chanzo chetu, vitu vilivyokwapuliwa ni pamoja na simu ya bei mbaya aina ya Blackbell aliyokuwa amemnunulia baba yake, Rais Jakaya Kikwete kama zawadi.

    Habari zaidi zinasema, pia majizi hayo yasiyo na haya yalikwapua viatu vyake vilivyokuwa kwenye mzigo huo.
    Ilidaiwa kuwa Miraji alitua Jijini Dar es Salaam kwa ndege ya Emirates iliyokuwa ikitoea Dubai.

    Taarifa zaidi zinadai kuwa kijana huyo baada ya kubaini ameibiwa alisikika akilalamika lakini akaondoka kwa hasira bila kutoa taarifa polisi.

    ’’Yeye alipofika pale VIP alilalamika kwamba baadhi ya vitu vyake vimeibiwa na akataja mali zilizoibwa...hata hivyo hakwenda kuripoti kwa Airline inayohusika,’’ kimesema chanzo hicho.

    Hata hivyo, imeelezwa kuwa maafisa usalama waliokuwepo pale, walikwenda kutoa taarifa kituo cha polisi kilichopo uwanjani hapo na kesi hiyo ikafunguliwa RB namba 5681/2006.

    SOURCE: Alasiri

    ReplyDelete
  34. AnonymousJuly 26, 2009

    Wewe nawe ndio wale waleee. Mara zote Mnapoziangalia hizo kamera hamuoni yanayofanyika? Leo hii mtafanya miujiza gani muweze kuwaona hao wezi?

    ReplyDelete
  35. AnonymousJuly 26, 2009

    acheni ubabaishaji kama kweli hizo CCTV zenu zinafanya kazi tuelezeni mmeshanasa watu wangapi na wamechukuliwa hatua gani, mimi kibaruani kwangu kuna kamera na watu hawasubiri udokozi utokee ndio waangalie kamera, wanaangalia kila saa na ukionekana umebugia kisicho chako unaitwa na kufukuzwa hapo hapo, hakuna cha kuwapa watu website ya malalamiko kwani nani hajui kuwa kuna wizi?

    ReplyDelete
  36. AnonymousJuly 26, 2009

    Daah hiyo mwake ila tu kama kuna kamsaada mnaweza tu saidia hapo kwa watani wa jadi(Nairobi-Kenya)tupate pa kulalamikia pia, yaani ni noma yaani mpaka tunabadilisha njia hata ukifunga mzigo wanachomoa wee achaa tu, kaka michu hebu tusaidie nako huko

    ReplyDelete
  37. AnonymousJuly 26, 2009

    daah kweli imetulia hiyo. sasa kaka Michu tusaidie pia kwa watani wa jadi (Nairobi-Kenya ) maana pale ndio kiboko mpaka tumebadili njia hawa

    ReplyDelete
  38. CHANA LIVE.July 26, 2009

    PIGA UA GALAGAZA, mimi nitajiharishia huyoi mkurugenzi wa airport akiwasaidia ,ikwani Wizi umeanza leo ,na kwani wezi hawajulikani,si wanawafuga wenyewe...wanaiba hadi vyombo vya kwenye ndege,wafanyakazi wa uwanjani wananunua,na ukitaka uhondo wa ngoma ingia ucheze, nenda katembeleee sehemu inayoitwa Karakata opposite na airport, huko kuna wafanyakazi wa airport wanaishi wamepanga huko,nenda utakuta hadi blanket ni la british airways, glass ni za emirates,sahani za South african airways,yaani kila kitu ni ndege ndege tu , kweli mtu hali polisi ,utakula kazini kwako ,ila sasa ni tooo much, sasa kama vya ndege vinaibiwa kila leo ,na CCTV zipo,sasa hiyo mizigo ya abiria je???? majiko ya mchina na vibatari vya watu wa karakata wanatumia mafuta ya ndege,hawajui mafuta ya taa, na wahusika wapo na wanajulikana,na wenzetu walinda nchi nao ndio waongoza msafara....\

    Airport UOZO mwingi jamani, cha msingi ni kuweka mabango makubwa ya kuwakumbusha abiria kuwa Vitu kama CAMERA, SIMU, LAPTOP , MP3,HELA KWENYE VIBAHASHA,Msiweke kuna wafanyakazi wameenda kwa Waganga kujiwekea dawa wakiona bagi la hela tu nywele zinasisimka,upoo hapo ,SI VYA KUWEKA kwenye luggage, wachukue kwenye hand luggage ,kwani havina uzito wa kuwashinda jamani,.....Naongea kwa experience na niko karibu sana na maeneo haya ,na sipendi tabia hiii,ama wakitaka tuwataje kwa majina tuko tayari ,kwanza Swisspert Loader ,wasiajiriwe Permanent ,wawekwe Temporary miezi 3 ,wanatolewa wawe Vibarua ndio itasaidia sana, mazoea nayo huwa yanatabu.....TEMU una kazi sana na Vijana wako ,WIZI MTUPU.

    Mdau, Chana Live,Airport.

    ReplyDelete
  39. AnonymousJuly 26, 2009

    Sasa ukimwona mwizi kwenye CCTV baada ya wiki au zaidi, na vitu vyangu keshauza hata ukimfukuza kazi itanisaidia nini?
    Kwa nini msiwe na utaratibu wa ku-monitor CCTV zenu kila saa ili kubaini wizi mara unapotokea? Nafikiri mna-monitor ila mnapoona mwizi mnamfuata awape kitu kidogo.

    ReplyDelete
  40. AnonymousJuly 26, 2009

    We anony wa kwanza 01:07.
    acha ujinga wako, we unaweza kumjua mtu muaminifuuuuuu. acha hizo. kamera ni zitasaidia sana 2 kinamna nyingine. lakini swala la kutafuta waaminifu ni mpaka tufe wote ndo anaweza kupatikana muaminifu!!!!! pande zote kamera ndo suluhisho la mwisho

    ReplyDelete
  41. AnonymousJuly 26, 2009

    tunashukuru kwamsaada ulio tupa ila bado hawa wa posta wanakera ile mbaya tupe msaada pia.tumetuma begi la kuweka cd na memory stick tuliemtumia anasema ameambiwa havifika lakini sisi tumekwenda posta fingland tumeambiwatumeambiwa vimefika vina wiki mbili.kaenda office zote kaambiwa havijafika.inakera sana.na sasa tunaidai posta ya huku maana tumevinunua bei mbaya.

    ReplyDelete
  42. AnonymousJuly 26, 2009

    Hehehhehe! FISADI INTERNATIONAL AIRPORT. GUD NAME

    ReplyDelete
  43. AnonymousJuly 26, 2009

    nadhani ni sahihi kwa huyo mkurugenzi kujilipua (kuachia ngazi) vinginevyo alipuliwe. hakuna chochote anachofanya. kusema ukweli hawajibiki.

    kama kuna cctv je si kuna watu wanamonita hizo cctv. kama hakuna basi hazitakiwi kuwepo vinginevyo tulitakiwa kusikia wangapi waliwahi kukamatwa bila hata kuwa wamepata malalamiko. suala la pili ni kwamba hili suala la wizi limeanza kitambo. sijui kachukua hatua gani mpaka sasa.

    kama aliweza kukamata wezi wa mali ya mtoto wa mh. raisi alitakiwa kutoachia hapo. naungana na wengine kwamba awajibike vinginevyo apafanyie marekebisho ya nguvu sana.

    sikubaliani na wengine kama us blogger kwamba hiyo information email inaweza kusaidia lolote. hizo allegations ni za siku nyingi sasa hiyo saver yake ina uwezo gani wa kutunza kumbukumbu. alichofanya hapo ni usanii. ukienda utaambiwa hiyo disc ya siku hiyo ilimwagikiwa na pombe.

    tuanakiwa kuwa serious na kazi zotu. tuache ubabaishaji.

    ReplyDelete
  44. AnonymousJuly 26, 2009

    UJUMBE KWA RAIS KIKWETE:

    MHESHIMIWA RAIS, HAWA WATU WA AIRPOT, POSTA NA BANDARI WANAKUTIA SANA AIBU, NI WEZI, WANANYOFOA VIFAA VYA WATALII WANAOLUTLETEA MAPATO, WANAPORUDI MAKWAO WANASIMULIA YANAYOWAPATA TANZANIA NA MATOKEO YAKE HATA NDUGU NA MARAFIKI ZAO HAWATAKI KUIKANYAGA TANZANIA

    WATU WANAFIKI KAMA HAWA VIONGOZI WA UWANJA WA NDEGE WA DAR ES SALAAM WATIMULIWE. HAKUNA CHA CCTV WALA NINI. HII NI KARNE YA UTANDAWAZI NA KARNE YA "MKONGO" NA MHESHIMIWA RAIS ULIVYOSEMA, MAENDELEO YAMEFIKA. WATIMUE HAWA WOTE, KUANZIA WAKURUGENZI WANAOLETEWA HESABU ZAO, NA HATA DAY WORKER WOTE. CHUKUA VIJANA CHUO KIKUU WAENDESHE HIZI IDARA. TUMECHOKA NA UFISADI WA KIJINGA WA HAWA WAJINGA.

    DR. KAWAMBWA NA WAZIRI WA USAFIRISHAJI, MUMSAIDIENI RAIS, KWA MAANA HAWA NAMAFIKI WA EAPOTI WANATUTIA AIBU. UKIFIKA MTANZANIA EAPOTI, WANATUSUMBULIA VITU VYA KIJINGA, HATA MIZIGO YAKO WANATAKA KUCHEKI, WAPI NA WAPI, VINGINEVYO TUTAANZA KUTUMIA NAIROBI NA MOMBASA ILI KUEPUKA HIZI KERO ZA KIJINGA ZA DAR JKIA

    ASANTE SANA KUNISIKILIZA RAIS JK
    MDAU
    ZAUSI AFRIKA
    BAMBI MKUMBO.

    ReplyDelete
  45. AnonymousJuly 26, 2009

    Kaka Misupu hivi kweli unaamini CCTV za kibongo zitaonyesha nini kama kule kwenyewe kwa waheshimiwa kama sikusea kuna mheshimiwa mmoja alikutwa akiwanga lakini hizo CCTV walipoziangalia hata sura yake walishindwa kuitambua.
    Bongo usani kibao na kujikosaha kwingi ila misupu nakushukuru sana kwani platform hii naona waheshimiwa wanaisoma na malalamiko ya wanyonge yanafika
    BIG UP MISUPU

    ReplyDelete
  46. AnonymousJuly 26, 2009

    Watanzania kweli tuna matatizo,
    Mtu unalalamika mtandaoni kuwa umeibiwa, unaambiwa jinsi ya kuweza kufuatilia malalamiko yako unaanza kumshutumu, kumkejelei na hata kumtukana aliyekuambia.

    Si ajabu kuwa wengi ambao wangeweza kutoa msaada wao kusuluhisha ama hata kukomesha tatizo hili wanaamua kujinyamazia kimya kuacha ninyi wajuaji sana kuendelea kulalama na kushutumu tu

    Sasa kama haujafuatilia eti tayari vitu vimeshapotea ni vipi suala hilo likakomeshwa kama kila mtu atafanya kuacha kufuatilia.

    Kama wewe unaona eti huna muda wa kufuatilia masuala haya ujuwe kuwa hicho ndio chanzo kikuu cha matatizo kama haya kukubuhu kwani waaofanya haya wanajua kuwa mwisho wa siku utaachana nao bila ya kufuatilia na kuhakikisha hatua zinachukuliwa hata kama itachukua miezi au miaka.

    Wakati tunalalama kuwa watu hawatekelezi wajibu wao nasi pia tunapaswa kutambua kuwa kama raia ama waathirika wa matukio ya wizi na uzembe wa aina hizi tuna wajibu wa kufuatilia hadi kupata muafaka ili sio tu haki itendeke lakini pia wengine wataogopa kufanya uhuni wa aina hii.

    Watanzania tuna tatizo kubwa la kukwepa majukumu yetu kwa kutupia lawama wengine hata kama ni kweli wanapswa kulaumiwa. Lakini jee baada ya kulalama na kufikisha malalamiko yako katika njia zisizo rasmi kaka hapa bloguni na kudharau kufuatilia mahala muafaka unadhani ni nani atachukua jukumu la kupambana kwa ajili yako.

    Tuache kupenda ku-outsource majukumu yetu halafu tukategemea mavuno tofauti na jamii zembe isiyo na uaminifu kama tuliyonayo sasa.

    Kama umeibiwa, umeonewa ama umefanyiwa uhuni wowote ule hakikisha unafuatilia hatua/ngazi zote husika hadi unapata muafaka ili hata kama hujapata vitu vyako lakini unatengeneza mazingira ya kuhakikisha kuwa tendo kama hilo halitokei tena ama kwako, kwa ndugu yako, mwanao, rafiki mama hata adui yako.

    Ukiona muda wako una thamani sana kufuatilia masuala haya basi uwe tayari kukumbana na masuala haya milele amina...

    Na wengine wanajidai hapa kuthamini uaminifu na utekelezaji wa majukumu yao wakati ndio wezi, mafisadi, waongo, wavivu, watoro wa majukumu yao kuanzia katika familia, maofisini hadi huko kwenye nchi za watu ambao wanaona kuwa ndio mfano bora wa kulinganisha na matatizo yetu hapa nchini....

    Nchi inaoza kwa kuwa wananchi tumevunda....

    ReplyDelete
  47. AnonymousJuly 26, 2009

    Hii kidogo inatia moyo..........tutafika tu!

    Mkulima Kijijini Gezaulole.

    ReplyDelete
  48. AnonymousJuly 26, 2009

    Ninamuunga mkono mdau wa Sunday July 26 03:47. Kweli wote tuna hasira na tumeshaibiwa kwa namna moja au nyingine. Tunatakiwa kushukuru hata malalamiko yamefika kwenye ngazi husika kwani Anko Issa angeweza kuyaacha hapa hapa blogunina siyafanyie kazi. Sasa tunaombwa kutoa ushirikiano tunaendelea kuto malalamiko badala ya kuchukua hatua. Kusema kweli hatutafika popote. Tujaribu kutoa ushirikiano kisha ukiwa hauzai matunda ndiyo turudi tena hapa barazani tuendelee kulalamika.
    Vilevile tukiwa kama Watanzania halisi haitatattua tatizo kuhama Airport na bandari za nchi yetu bila kuhakikisha matatizo yanarekebishwa. Huko ni kuahirisha tatizo tu. Sasa sijui na huduma ya posta tuhamie Kenya au Uganda?

    ReplyDelete
  49. AnonymousJuly 26, 2009

    It is seen vividly from most comments complaints that there are are contol and security problems at the airport.

    It is true as well that the administrator(mr Mbamba)wants to find altenative solutions that are likely to solve these issues.

    I would like to stress the following and recommend from my perspective what is to to take place.

    The whole security control adminstration to be changed or outsoursed from a foreign company after a fixed short period,to ensure competence of services provision.

    There should be a proper personell recruitment taking into account awareness,attitude and action towards risks such as that if theft.

    There should be segregation of tasks among employees to avoid collusion and partiners in crime.

    The employees and directors should be remunerated adequately to motivate and committ their duties to serving customers approprietely.incentivising of labour force to abide with standards and produce best results as expected.

    The whole system should be monitored by an independent person with objective personality toward the control mechanisms.example,a person monitoring CCTV should be certified and have regular training. let say(mzungu).....Kiingereza'

    Moreover,appropriate steps in connection to any breach of controls should be taken immediately with objective evidence at hand to testify in courts.eg caught red handed stilling by CCTV,swipe cards access to show thief present in the area at the time etc

    The whole culture of an organisation should be that of satisfying customers needs by embeding detailed risk procedures in their management systems.

    I could discuss moral reasoning issues(trustfulness,fairness,integrit and many more) that are fundamental to describe fiduciary relationships to safeguard people assets.But it will not serve purpose on this issue since it is long way for Tanzania to change.

    Therefore,from the above,stringent controls should not be prone to be overiden and make peoples items susceptible to theft.

    There is a lot write with regard to these issues and how modern procedures could help minimise or obliterate thievish culture at the airport and in most public service organisation.


    Mdau(John) UK

    ReplyDelete
  50. AnonymousJuly 26, 2009

    USHAURI KWA RAIS WA URT:

    Ninajua kuwa kuisafisha system iliyojaa "Vultures wa mali za watu na Uma" ni ngumu sana. Kwani huu ni mtandao ambao umeonekana wa kawaida, yaani kuanzia polisi, usalama wa taifa na mpaka mawaziri na wanyikulu wote ni watu wenye tamaa.

    Hii tabia ni ngumu sana kuishinda kwa njia za kawaida na hata TAKUKURU wameonekana pia si lolote si chochote. Watu wanaogopa kuchukua hatua kwa kuogopa kulipiziwa visasi, kama kuuwawa na wengine pia wenye imani ndogo wanaogopa kurogwa, kushushwa mishipa na kutiwa vichaa n.k.

    Ili kukabiliana na hili, Mheshimiwa rais nakushauri kwa siri kubwa tena hata bila kuwashirikisha UWT na baadhi ya wasaidizi wako, unda "KIKOSI KAZI CHA RAIS- KIITE NGE WEUSI". Kikosi hiki kisiwe na ofisi popote bali ofisini kwako, waajiriwa wasijulikane, walipwe vizuri sana, Ikibidi hata kukuzidi wewe na walishwe kiapo cha utii na uaminifu kwako. Kazi ya hawa iwe ni ku- identify watu waaminifu wasomi wanaoishi nje ya nchi na hasa Europe na Marekani ili waje kubadili system na kuondokana na wachumia tumbo wengi waliopo bongo.

    Nimetaja watu wa nje kwa sababu ya exposure na kuwa na experience jinsi wenzetu wanavyofanya mambo yao. Hii itabadilisha utamaduni wa kupeana kwazi kwa kujuana na kiitikadi badala ya uaminifu.

    Tukishapata watu hawa ambao watakuwa ni wafuata sheria na haki anza kustaafisha wabongo wote mmoja baada ya mwingine katika sehemu zinazolalamikiwa na jamii. Hii itajenga uaminifu mheshimiwa. Kwa nini Kenya wanaweza sisi bado tuna suasua tu. Juzi nilikuwa naongea na rafiki yangu mmoja alikuwa Kenya holiday nikamuuliza kama anaifahamu Tanzania akasema aliifahamu kupitia Kenya kwa kuonesha mlima Kilimanjaro ila aliambiwa kuwa usalama wetu ni mbovu sana hasa wizi kwenye mahotel na viwanja vya ndege. Iliniuma sana.

    Hivi tukiamua kuajiri graduates waaminifu ambao ni wengi sana mitaani kwa sasa na kuwalipa vizuri sehemu kama hizi za check up, polisi n.k si tutakuwa tumepiga hatua sana?.

    Kikosi kazi chako hi muhimu sana kurudisha discipline, nakumbuka wakati wa Nyerere walikuwa wanahojiwa na kunyang'anywa majumba ambayo waliyapata kwa ubadhirifu, leo hii mfanyakazi wa serikali mshahara wake laki tano kwa mwezi yupo kazini miaka mitatu hana biashara ila anamiliki nyumba ya milioni mia nane!, tunamwacha tu. Hivi ni vitu vinavyochochea wizi sehemu za kazi kwani mtu hawezi kuulizwa kavipataje?.

    ReplyDelete
  51. AnonymousJuly 26, 2009

    Ushauri wangu kaka Issa,wapelekee hizi comment zote. kwani inaonyesha watu wengi wameguswa na hayo matukio ya Airport. Mimi wameshawahi kuniomba,kila nikitoka tanzania hawaishi kusema niwaachie madafu.Nashukuru sijawahi kuibiwa,lakini nitakuwa makini. Vitu vyangu vya electronic hand luggage tu.

    ReplyDelete
  52. AnonymousJuly 26, 2009

    mie dar airport sipiti tene, naondoka london na ndege ya kwenda mombasa halafu nachukuwa basi kwenda bongo, better nilale njiani kuliko kuuibiwa. mwaka jana nilisafirisha magari mawili kupitia mombasa no problems, no honga honga kama bongo documents zinasainiwa na wtu kumi tofauti halfu kila mmoja anataka hongo, mombasa fresh sana please nawaomba mutumie bandari ya mombasa hata kama utatoa hongo basi ni kwa mtu mmoja tu at least! Tanzania pors and airports are rotten! i hate them like a death! God Bless TZ

    ReplyDelete
  53. AnonymousJuly 26, 2009

    JAMANI WAHUSIKA WA SWISSPORT, MDAU MIE NATUA JKNIA MWISHO WA MWEZI WA NANE...NIMESHAKAMATA NONDO ZANGU NARUDI NYUMBANI FOR GOOD. SIONI UMUHIMU WA KUWAPA FLIGHT WALA CARGO DETAILS KWAN HAMKAWII KUNYANYA MABEGI JUU KWA JUU MSEME HAYAJAFIKA!!!! NIMEPIGA BOX SANA NA NIMEUMIA KUKUSANYA $$$ KUNUNUA MAHITAJI YANGU NA ZAWADI KWA NDUGU NA MARAFIKI. NATOA TAHADHARI MAPEMAAA; OLE WA KIUMBE ATAKAECHOKONOA LUGGAGE ZANGU NA KUCHOMOA CHOCHOTE..WALLAH, UWANJA UTAKUA HAUTUTOSHI HUO, PATACHIMBIKA SI KAWAIDA. FLIGHT NTAKAYOTUMIA INA CONNECTION MOJA TU NA NI YA KUELEWEKA HAINAGA SCANDAL ZA WIZI, (SIO ETHIOPIAN) IVYO KAMA NIKIIBIWA LAZIMA ITAKUA JKNIA NA MTAJUUUUUUUUUUUUUUUTTTTTA KUNIFAHAMU!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  54. AnonymousJuly 26, 2009

    WEWE ANON 03:47 UNAONEKANA HUJATULIA KABISA AU NDIO YULE MTOTO WA KIKWETE AMBAYE VITU VYAKE VILIIBIWA NA USALAMA WATAIFA WAKAWEZESHA KUPATIKANA KWA WAHALIFU NA SIO HUYO MKURUGENZI

    WATU WOTE HUMU WANAMACHUNGU SANA KUTOKANA NA KUIBIWA VITU VYAO VYA THAMANI SANA

    HAPA JAMVINI TUNAPASHANA ILI KUPUNGUZA HUO UDHALIMU WANAOFANYA
    KITU NI WAJIBU WAKE KWANINI WATU WANAIBIWA NA SIO KUMWAMBIA TUMEIBIWA
    YAANI NI AIBU TUPU

    ReplyDelete
  55. AnonymousJuly 27, 2009

    Ulaji huoooooooooooooooo! Mie mtalaamu wa CCTV ngoja nikaombe kazi huko JKN eapoti nikimwona mwizi tu lazima anikatie la sivyo naita Waandishi wa habari wote waje washuhudie. Na kwa hali ilivyo nipeni mwaka tu mambo yangu yatakua ppooaa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...