Mbunge wa Msalala ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mali Asili na Utalii bwana Ezekiel Maige akimvisha beji ya bendera ya Tanzania Bwana Don Strickland kama ishara ya upendo wa wafanyakazi katika idara aliyokuwa anaongoza na kutoa mafunzo katika mgodi wa Bulyanhulu katika sherehe maalumu hapo jana.
Waheshimiwa Mh.Prof Juma Kapuya,Mh.Jenista Mhagama wakiwasili Bulyanhulu kutokea Dodoma kwa charter maalum
Mgeni rasmi Mh.Prof Juma Kapuya pamoja na Mh.Jenista Mhagama wakikaribishwa na mkurugenzi wa Barrick Tanzania Bw.Deo Mwanyika (mwenye miwani) kwenye mgodi wa Bulyanhulu.


Naibu waziri wa utalii Mh.Maige akimkabidhi Bw.Don Srtickland zawadi ya kikombe chenye ramani ya Tanzania na kumsihi kua Balozi wa taifa hili popote aendapo-Bw.Don amemaliza muda wake mgodini na anajivuni a mafanikio makubwa ikiwemo kuendeleza wazawa kielimu na kuwapa nafasi nyeti

Mr.Don Strickland-Mzungu aliepokea tuzo kwa kuendeleza wazawa kwenye kitengo chake.watanzania zaidi ya 20 kwenye kitengo cha usafishaji dhahabu wameshachukua nafasi zilizokua zimekamatwa na wazungu miaka 2 iliyopita.Nafasi hizo ni nyeti sana migodini na huyu bwana amehakikisha kwa sasa hizo nafasi wamekamata wamatumbi


Sarah Thompson Meneja wa kitengo cha Ugamvi akipokea tuzo kwa kuendeleza watanzania 15 kwenye kitengo chake na kuwapa nafasi za juu kama Superitendent na Foreman.Wadau hizi ni nafasi nyeti sana mgodini na miaka michache iliyopita hakuna mtanzania aliwahi kupewa hio nafasi ila kwa sasa wabongo 15 wamezipata,si jambo dogo

Mr.Don Strickland-Mzungu aliepokea tuzo kwa kuendeleza wazawa kwenye kitengo chake.watanzania zaidi ya 20 kwenye kitengo cha usafishaji dhahabu wameshachukua nafasi zilizokua zimekamatwa na wazungu miaka 2 iliyopita.Nafasi hizo ni nyeti sana migodini na huyu bwana amehakikisha kwa sasa hizo nafasi wamekamata waswahili.

risala ya wafanyakazi

Arthur Mgongo-Mmoja wa watanzania waliosomeshwa na Mgodi na sasa anashika nafasi ambayo hata wazungu wenyewe wanaimezea mate. (Process Plant Superitent) Mambo ya kusafisha dhahabu

Fikiri Charles-Mtanzania mwingine ambae amepelekwa Australia kusoma na kurudi kua FOREMAN.


Picha na Habari
na
MediaWorks International

MGODI wa dhahabu wa Bulyanhulu (Bulyanhulu Gold Mine Limited-BGML) ulioko wilayani Kahama, Shinyanga umezindua mpango kabambe wa kuwawezesha wazalendo kuchukua nafasi za kazi zinazoshikiliwa na wataalam wa kigeni kwa kupatiwa mafunzo na uzoefu ndani na nje ya nchi.

Akizundua mpango huo mgodini hapo jana, Waziri wa Kazi Prof. Juma Kapuya alisema amefurahishwa sana na utaratibu huo na kuzitaka taasisi zinazosimamia masuala ya ajira kuangalia na maeneo mengine mengi hapa nchini kama wanaweza kuuiga ili kujenga uwezo kwa wazalendo na kupuguza utegemezi wa wataalamu wa kigeni bila kuathiri ufanisi wa kazi.

Chini ya mpango huo wa Bulyanhulu, mgodi umejiwekea malengo ya kupunguza wataalamu wa kigeni kwa awamu kutoka 184 waliopo sasa na kufikia 17 ifikapo 2015. Na ili kutekeleza lengo hilo kampuni inalazimika kutumia dola 4.5m kila mwaka kwa mafunzo ya ndani na nje ikiwemo na kuwapeleka wanaoteuliwa kufanya kazi maeneo mengine katika nchi mbalimbali duniani.

Mpaka sasa ni jumla ya wafanyakazi kuanzia 2005, jumla ya wafanyakazi 150 wameshakwenda kusoma na kufanyakazi kwa mafunzo katika nchi za Afrika ya Kusini, Australia, USA, Canada, Ujerumani, Papua New Guinea,Swaziland na Kenya.
Waziri Kapuya ambaye aliambatana na Naibu Waziri wa Mali Asili na utalii ambaye pia mbunge wa Msalala ambako ndipo ilipo BGML Mh. Ezekiel Maige, aliwataka wafanyakazi wote watakaoachiwa nyadhifa na wataalamu wa kigeni kuwa wawe mfano kwa wengine na pia waadhihirishie wawekezaji kuwa fedha zao zinazotumika katika kuwafunza hazipotei bure kwa kufanya kazi kwa bidii na uadilifu mkubwa.
Alibainisha kuwa moja ya sababu kubwa za makampuni ya nje kutowaaamini wazawa wengi ni kutokuwa waadilifu na utendaji hafifu wa kazi.

Pia aliwaasa wafanyakazi wengine wazalendo kuwapa ushirikiano wananchi wenzao wanaokabidhiwa madaraka kwa kufanya kazi vizuri na kuacha uvivu kwa kuona tuu anaongozwa na Mtanzania mwenzake badala ya mtaalamu wa kigeni. Aliowaonya kuacha kasumba hiyo iliyopitwa na wakati.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 26, 2009

    Hii inafurahisha sana, na wakati huo huo inakamua machozi ya uchungu kidogo. Hivi miaka yote hii tulikuwa wapi jamani?
    Na ujulie kuwa hii ni dhahabu tu, je Tanzanite vipi? almasi vipi? na zinginezo nyingi.

    Na tujue ya kuwa dhahabu ichimbwapo, ikitoka imetoka haioti wala hatuwezi kupanda nyingine

    inabidi kuamka kile secta.

    ni hayo tu

    P.E.D

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 26, 2009

    Teheee heee heee. Huu ni utani au matusi? Kama tunaweza kuwa na Rais Mmatumbi tuna sababu gani kusherehekea kwamba toka mwaka 2002 Mkapa alipoenda kufungua rasmi mgodi huo mpaka 2009 hatimaye wamefanikiwa kuwapa Wamatumbi nafasi za Unyapara na Urakibu. Warakibu Waandamizi wa Polisi (SSP) wote nchini ni Watanzania. Mtoto aliyezaliwa siku mgodi ulipoanza kuzalisha dhahabu anapata elimu ya msingi sasa hivi!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 26, 2009

    Inashangaza kuona watanzania wanajisifia kuwa na nafasi za juu makazini ndani ya nchi yao, mimi nilitegemea vitu kama hivyo vitokee huku ughaibuni. Imefikia time ya watanzania kutambua kwamba hizo nafasi kama mtu ana qualification zake is your right and not privilege inashangaza mtu hata kuwa na passport ya nchi yake anaona ni bonge la bahati wakati ni haki yako kama mtanzania.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 26, 2009

    Hongera sana mzee Fikiri Charles
    -Former Classmate Mzumbe Sec Class of 94'

    ReplyDelete
  5. Mheshimiwa Balozi na Mkuu wa Wilaya

    Nawapongeza waTanzania waliochukua hizo nafasi. Naamini ni ushahidi wa uwezo na umakini wao kiutaalam na kiutendaji. Nawapongeza kwa hilo.

    Hao wenzetu ni hazina, kwani huko mbele ya safari, tutakapokuwa tunamiliki urithi wa madini yetu, hao watakuwa makada wetu.

    Papo hapo suala la Barrick linahitaji kufuatiliwa, sambamba na suala zima sera ya uwekezaj nchini mwetu. Je, serikali ya Tanzania inaielewa kampuni ya Barrick na kampuni zingine zinazoingia nchini au inafanya mchezo?

    Wadau wanaotaka kujipanua upeo angalau kiasi fulani kuhusu hii kampuni ya Barrick wajaribu kupita pita hapa: http://protestbarrick.net/

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 26, 2009

    changa la macho

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 26, 2009

    Michuzi nani ameandaa hii Award? Ni serikali au ni Barrick wenyewe? Inawezekana Barick wanajiandalia award na kuiambia serikali iwape? Je Nituzo ya serikali kwa makampuni binafsi? ilishawahi kulewa kwa makampuni mengine? Tafadhali nielimiesheni.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 26, 2009

    Vyeo sawa wamepeta, je misharaha na masurufu mengine vipi? Kama vyeo hivyo walikuwa wanashikilia wazungu zamani ni lazima walikuwa wanachukua mshiko wa kutosha tu. Je wamatumbi mshiko wao vipi? Wasije tu wakadanganywa kwa vyeo wakati mshiko hakuna. Wajanja wanasema "KAZI BABU MSHAHARA KIJANA" Je wamatumbi hapo Bulyanhulu vipi msemo huu?

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 26, 2009

    "hata wazungu wenyewe wanamezea maate" unapaswa kufikiri maana ya sentence zako misupu....unamanisha wazungu ndo kipimo cha ubora au? haina shaka....ukikua utaelewa.....

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 27, 2009

    If your thinking is a refletion of many Tanzanians, we have a very long way to go just to free our mind. Foreman? How about strategists? Anyway may be is not majority thinking.

    Mdau

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 27, 2009

    Eti ni ishara ya upendo, mmmmh!Zaidi ya watanzania 20 wameshasomeshwa je wangapi wameadhirika? Pesa bwana kweli ina maajabu yake. Angalia wazee wetu wanavyojikomba nawe eti wazungu wanatamani hizo post?

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 27, 2009

    Barrick is the reason George Bush alikaa Bongo siku 4 katika ziara yake ya Afrika ya siku 6! Jiulize hapo. Sisi si tulipata vyandalua bwana! I just hope Obama naye hataingia dili!

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 27, 2009

    Changa la macho babu! Siye tulioko mgodini hapa tunajua kinachoendelea tu..huu ufomeni hauhitaji shule ila tu uzoefu..sasa bwana mkubwa hawa wenyewe wanaopewa huu ufomeni wako wa aina mbili
    1. Waliokuja na taaluma zao toka vyuoni wakiwa smart sana lakini wakawa wanaongozwa na ma.mbumbu wa kizungu, kwa hiyo wakati mwingine promption hizi zinaambatana na YEEES SSSIR kibao! Hapa mshahara hadithi wanetu msidaganywe na mambo hayo!
    2. Wako hawa wengine ambao wao hata skuli hakuna mf FIKIRI yeye ni form 4 tu lakini alionekana mchapakazi mzuri tu kwenye idara kwa vigezo ambavyo havijulikani, sasa huyu anawasimamia ht wenye dips na digriiz wengi ambao amekuwa bize kuwafrustrate hadi wanaacha kazi ili wasimchallenge..

    Isitoshe hii wameandaa idara wenyewe hapa mgodini wala si serikali..CHANGA LA MACHO TU BABU..hawa ni maakida, wajumbe na maliwali kama ilivyokuwa eeeenzi ziiiileeee za mkoloni..!!!!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 27, 2009

    Jamani wenzetu wanapoendelezwa hebu tufurahi na kuwapa ushirikiano.wabongo kumbukeni kua sekta ya madini ni ngeni sana hapa nchini kwetu na hatuna wataalam wa kufanya kazi kwenye technical areas za uchimbaji dhahabu.hawa waliondelezwa tuwatumie kama lulu kwani ndio watakaotupa ujuzi na utaalam huko mbeleni hawa watasha wakishaondoka.mimi binafsi nawapongeza Barrick,i think u guys have done a great thing...keep it up.cha muhimu hakikisheni mnawaongeza mishahara..na nyinyi wabongo mliopandishwa vyeo msibweteke jitahidini 2 prove these guys wrong na kuwahakikishia kua tuna uwezo mkubwa na tukipewa nafasi tunaweza...big up sana

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 27, 2009

    Hi Michuzi, To me this is an insult, it won't change anything, Those guys are going to be used as pupets, Imagine Mr. Deo Mwanyika has been there over five years as General Manager but we didn't notice his presence in the Management as We have withnessed our Gold being stolen from Mines and only received a peanut as taxes, So What is important is to change those contracts and not to promote local employees,I had been working with Investor's company for more that four years in the senior post, My experience is that They will use those high ranking local staff as Token in pool table, we buy token in order to play, but once bought we put it aside and play the game, actually token is not the part of the game in pool table, though we must buy to play the game.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 27, 2009

    Fools are the tools of wise.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 27, 2009

    Inasikitisha kuona watanzania bado tunaendelea kuwa wageni ndani ya nchi yetu.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 27, 2009

    Kuna mameneja wangapiwana first degrees na sub-ordinates wao wana 2 or more degrees? Ni uchapaji kazi tu. It doesnt matter kama mwenye degree moja akamuongoza mwenye degree 5. . Wewe ktk wizara yako huyo waziri wako hujamshinda kwa elimu? tusilinganishe degrees.
    Huyo unayemsema ana cheti cha form 4 tuu inawezekana ana experience ya migodini kuliko wewe uliyeanza kazi mwaka jana na degree yako.If so, unategemea wewe utapewa hicho cheo

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 27, 2009

    Niliishi Mwadui Ma oreman wote walikua wamatumbi. Wapewe nafasi za umeneja ndio tufurahi. Halafu je maslahi ya superitendet mmatumbi na mzungu sawa? Mzungu atapewa allowance ya malaki kila wiki mshahara analipwa kwao. Gari, wafanyakazi atalipiwa na mgodi

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 27, 2009

    Mzee wa maoni ya token umenifurahisha kwa maoni yako. Watu wananunua tokeni wacheze pool lakini wakishaitia tokeni mezani basi tena, haiwi sehemu ya mchezo wenyewe wa pool. Nawapa pongezi hawa Wamatumbi kwa uvumilivu wao wa miaka nane ya mafunzo. Walau sasa wamekuwa maforemen kama wenzao wa Mwadui walivyokuwa toka enzi na enzi.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 28, 2009

    Hakuna kitu hapo! Kama ufisadi ndo upo hapo,nliwahi kufanya kazi na kampuni moja ya private hapo inayoitwa PALEMON CONSTR.LTD ilikua ni kazi ya kujenga parkings za magari ya wazungu na walkerways kwenye ile Motel six enzi izo nkiwa na ki-FTC changu cha kutoka Arusha Tech.Hakiyanani nliyoyaona mle ndani ni magumu kuandikika kwenye hii Blog msitake nkatafutwa kuhojiwa.
    Labda swali kwa wale waliopo hadi sasa 'ivi ule udongo bado unasafirishwa kwenda USA kwa ajili ya kuchunguzwa?' Kama jibu ni ndio 'Je wanasafirisha hadi Tonnes mia ngapi sasa ivi? Maana mi nliacha ni Tonnes 700-800 per day!
    Langu la mwisho 'Je huo udongo kwanini huwa haurudishwi hapa kwetu?' Je ni sample gani ya udongo wote huo? sijui ndo changa la macho hilo?
    By Mdau Mbeki mi nipo St Joseph CoET(Brigita Campus)-DSM napiga shule nkirudi uraiani jiandaeni mafisadi wa ki-Handisi tafuteni njia.CHAO

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...