Hapa Mwenyekiti wa Wazee wa Arusha
Danford Mpumilwa (kushoto) akiwa katika picha langoni mwa Bunge na Mzee
Kasoli, Mwanahabari Said Mkumbo wa TBC na Mzee Mike Taylor

Mr. Nanihii!
Vijana wa enzi za Mwalimu wa A-Taun, (Arusha Wazee Sports Club), hivi majuzi walitinga jijini Dodoma ambako walikuwa wageni was timu ya mpira ya Bunge.
Pamoja na Spika wa Bunge Mhe. Sitta kumwaga mkwara kuwa jioni yake wangeonekana wanyonge na wamenuna kwa kufungwa kwani timu ya Mhe. Ngeleja, Waziri wa Nishati, haijawahi kufungwa, Wazee, timu inayojumuisha wote wale waliofulia umri waishio Arusha kutoka nchi mablimbali waliwachakaza Wah. hao magoli 2 - 0.

Wah. wabunge mameapa kuja A-taun kulipiza kisasi. Hata hivyo Vijana wa enzi za Mwalimu wanaendelea na libeneke la tizi kwani mwezi ujao Agosti tarehe 7 wanawakaribisha Baraza la Wawakilishi toka Zenji.
Wah. Wawakilishi wanakuja A-taun kutembelea kujonea mandhari pamoja na kukichapa na Vijana wa Enzi za Mwalimu wa A-Town. Kundi hilo la Wawakilishi kama 50 hivi wameapa kuwanyamazisha Vijana wa enzi za mwalimu wa A-taun.
Kwa kujiamini kabisa Wah. hao wa Zenji wamesema wao sio wa Dodoma Ati!
Haya na tusubiri.....
Wenye uzi wa Real Madrid ndio Vijana wa Enzi za Mwalimu wa A-taun
wakiwaloga Wah. Wabunge kabla ya mchezo wao hapo Dodoma.


Meza kuu wakifuatilia kwa makini mtanange huo. Toka shoto ni Mzee Chief Mirambo, Mhe. Rashid Hamad (MB), Mwenyekiti wa Vijana wa Enzi za Mwalimu, Danford Mpumilwa pamoja na mwenyeji wao Diwani Mwanyenza

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 11, 2009

    He he heeee kweli tunakula chumvi!!Bro Mithupu hebu msalimie sana "Mzee Malfyale" Danford Mpumilwa.Toka amehama Dsm sasa ni miongo mingi!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...