kaka Issa wa Michuzi ,
Hapa ni Algiers kwenye PANAF ambapo wabongo waliwakilisha kiswasawa kwenye libeneke la matembezi ya ngoma za kitamaduni. Wanafunzi wakibongo wanaoishi hapa walishindwa kuvumilia na hatimaye walijitosa na kujumuika kwenye jaramba hilo kuanzia mwanzo hadi mwisho. Ila jamani hao madansa hawakuweza kununuliwa angalau raba zinazofanana?
sidhani kuwa hivi viatu vyao vya yeboyebo ni idea nzuri katika matembezi ya kucheza na sarakasi hivi. Ila wadau mkae mkijua kwamba Bongo iliwakilishwa haswa! Cheki bendera yetu inavyopepea na kwa jinsi wadau hawa walivyochakarika ilikuwa kama kwamba walijitayarisha, kumbe ilikuwa ni mambo ya papo kwa hapo, kudhihirisha kwamba wabongo huku ughaibuni wana usongo ile mbaya na nchi yao na hawakubali kupitwa.

Na mdau J.C

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 06, 2009

    SAFI SANA HATA MIMI NILIPOIYONA BENDERA NA WANA WA BONGO YETU KWENYE TV NILIFURAHI SANA

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 06, 2009

    Hongereni sana kwa kufanikisha siku hiyo, ukweli ni kwamba Viatu vimechafua Mada halisia, kuna viatu kama vya kimasai, kam vya ngozi hasilia vilivyo rembwa kwa shanga AU (katambuga - inayotengenezwa na mabaki ya tairi) ingetoa uhalisia zaidi (yeboyebo ya mchina kazi kwelikweli) HONGERENI SANA

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 06, 2009

    Na hivyo viatu ndio uniform, hiyo yeboyebo.Angalau si wangechagua viatu japo vya asili vile vinavyoshonwa shonwa mitaani na wataluma, kuliko hiyo miplastik ya yeboyebo

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 06, 2009

    jamani geography yangu si nzuri sana hii nchi iko wapi tena ??

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 06, 2009

    mwafrika bwana bila ya ngoma hajafanya jambo!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 06, 2009

    safi!safi sana! hongereni sana umewakilisha nyinyi ni mfano hai wa kuigwa na wengine wanaoishi ughaibuni.
    Wabongo msiogope kuijitoa uwanjani katika Fest kama hizo huko ughaibuni.Acheni kila wakati kung'ang'ania kuvaa tai na kufuga vitambi aka matumbo

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 07, 2009

    anonym wa saa 6:14 hiyo nchi iko north of africa!jirani na tunisia na morocco! kama na hapo hujui basi nenda shule tena!sio siri watz wanacheza si mchezo ila ndio hivo mavazi na viatu hivo... hataaa! tunaomba picha zaidi maana festival hii inapendezaa!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 07, 2009

    algeria kwa kiswaili

    yeboyebo tena???

    ngrrrrrrrrrrrrrrrr

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...