Hapa ni Algiers kwenye PANAF ambapo wabongo waliwakilisha kiswasawa kwenye libeneke la matembezi ya ngoma za kitamaduni. Wanafunzi wakibongo wanaoishi hapa walishindwa kuvumilia na hatimaye walijitosa na kujumuika kwenye jaramba hilo kuanzia mwanzo hadi mwisho. Ila jamani hao madansa hawakuweza kununuliwa angalau raba zinazofanana?
sidhani kuwa hivi viatu vyao vya yeboyebo ni idea nzuri katika matembezi ya kucheza na sarakasi hivi. Ila wadau mkae mkijua kwamba Bongo iliwakilishwa haswa! Cheki bendera yetu inavyopepea na kwa jinsi wadau hawa walivyochakarika ilikuwa kama kwamba walijitayarisha, kumbe ilikuwa ni mambo ya papo kwa hapo, kudhihirisha kwamba wabongo huku ughaibuni wana usongo ile mbaya na nchi yao na hawakubali kupitwa.
Na mdau J.C
SAFI SANA HATA MIMI NILIPOIYONA BENDERA NA WANA WA BONGO YETU KWENYE TV NILIFURAHI SANA
ReplyDeleteHongereni sana kwa kufanikisha siku hiyo, ukweli ni kwamba Viatu vimechafua Mada halisia, kuna viatu kama vya kimasai, kam vya ngozi hasilia vilivyo rembwa kwa shanga AU (katambuga - inayotengenezwa na mabaki ya tairi) ingetoa uhalisia zaidi (yeboyebo ya mchina kazi kwelikweli) HONGERENI SANA
ReplyDeleteNa hivyo viatu ndio uniform, hiyo yeboyebo.Angalau si wangechagua viatu japo vya asili vile vinavyoshonwa shonwa mitaani na wataluma, kuliko hiyo miplastik ya yeboyebo
ReplyDeletejamani geography yangu si nzuri sana hii nchi iko wapi tena ??
ReplyDeletemwafrika bwana bila ya ngoma hajafanya jambo!
ReplyDeletesafi!safi sana! hongereni sana umewakilisha nyinyi ni mfano hai wa kuigwa na wengine wanaoishi ughaibuni.
ReplyDeleteWabongo msiogope kuijitoa uwanjani katika Fest kama hizo huko ughaibuni.Acheni kila wakati kung'ang'ania kuvaa tai na kufuga vitambi aka matumbo
anonym wa saa 6:14 hiyo nchi iko north of africa!jirani na tunisia na morocco! kama na hapo hujui basi nenda shule tena!sio siri watz wanacheza si mchezo ila ndio hivo mavazi na viatu hivo... hataaa! tunaomba picha zaidi maana festival hii inapendezaa!
ReplyDeletealgeria kwa kiswaili
ReplyDeleteyeboyebo tena???
ngrrrrrrrrrrrrrrrr