Boston Rangers
Bongo Stars United wakiwa Boston

Ule mpambano wa soka kati ya Stars united na Boston Ranger uliokua ukisuburiwa kwa hamu na wakazi wa Massachusetts ulijikuta ukichezeshwa kwa dakika 70 badala 90 kutokana na timu mwenyeji kuchelewa kufika uwanjani huku uwanja ukiwa umelipiwa kuanzia 4pm mpaka 6pm.


mechi ilikua kali na ya kusisimua hasa kipindi cha pili, stars united ilianza mpira taratibu huku ikijaribu kusoma mpira wa wapinzani. katika dakika 12 kipindi cha kwanza ,Boston Rangers ilijipatia bao la kwanza,kwa krosi iliyomshinda kipa wa Stars united na kumkuta mfungaji alie ukwamisha mpira kimiani kwa urahisi.
bao hilo liliipa nguvu Boston Rangers, na kuwachanganya Stars United na kusahau kandanda safi kiwango cha TBS kwa muda takribani wote wa kipindi cha kwanza, na mtego wa kuotea ulionyesha kumsumbua mwamuzi Masoud alieruhusu magoli mengine mawili ya Boston yaliyo lalamikiwa na wachezaji wa stars united kwamba wafungaji walikua wameotea.


mpaka mapumziko Boston walikua wakiongoza kwa 3-0.

Kipindi cha pili kilichochezwa kwa dakika 25, kilianza kwa stars united kulishambulia lango la Boston kama nyuki ndipo katika dakika ya 50 Stars waliandika bao la kwanza kwa tuta, bao hilo liliasha mashambulizi golini mwa Boston huku wakichezewa nusu uwanja muda wote, na kunako dakika 65 Stars walijipatia bao la pili kwa ngonga safi zalizoanzia kwa beki wa kulia.


Huku wakiwa wanaendelea kulishambulia goli la wenyeji kama nyati aliejeruhiwa, Refa alilazimika kumaliza mpira kabla ya muda wake kutokana na timu nyingine kuwepo nje kusubiri kuanza kwa mechi yao iliotakiwa kuanza 6pm.

Bongo Stars United na Boston Rangers zilikubaliana kuwepo kwa mechi nyingine ya marudiano itakayoamua mshindi kwa dakika 90

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. BOSTON MUMEFANYA SANAA, UBAZAZI NA WATU WENU WANAJIITA MASAMJO. MECHI IMECHEZESHWA NA MAREFA WAWILI, WOTE KUTOKA BOSTON.REFA WA KIPNDI CHA KWANZA KABOLONGA, WA KIPINDI CHAPILI ANABISHANA NA MSHIKA KIBENDELA WAKE! HAPO HAPO STARS UNITED WANAKUJA KAMA NYUKI MNAMWAMBIA REFA AMALIZE MPIRA HALI MLISEMA UWANJA MMECHUKUA HADI 6pm LAKINI TUNAWEZA KUCHEZA HADI 6:15 TO 6;30pm. NOT FAIR BOSTON.HARAFU REFA KAMALIZA MPIRA 4mn. before 6pm. BOSTON AIBU, WATU WAMESAFIRI MASAA NANE HARAFU MNAFANYA UHUNI, MNACHELEWA. THAT'S NOT COOL.

    STARS UNITED (SOCCER KIWANGO CHA TBS) WAMEAHIDI KURUDI MWEZI UJAO.
    HAWATAKI MAMBO YA KIHUNI.

    ReplyDelete
  2. MICHUZI, VIPI HABARI ZA SIMBA DAY MBONA HATUZIONI?

    KAMA WEWE MZALENDO NA BLOG YAKO YA WANAJAMII TOA HABRI ZA SIMBA DAY< USIWE NA UPENDELEO>

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...