Wanasiasa 40 walipata ajali mbaya porini, mkulima mmoja alipoona hivyo alichimba shimo na kuwazika wote kwa pamoja. Baadaye polisi walikuja na kumhoji kuhusiana na ajali pamoja na maiti na mahojiano yalikuwa hivi:-
Polisi :- Uliona ajali jinsi ilivyotokea?
Mkulima :- Hapana, nilikuta imeshatokea na maiti zimezagaa..
Polisi :- Zipo wapi maiti?
Mkulima :- Nimezizika
Polisi :- Una uhakika wote walikua wamekufa?
Mkulima :- Kuna wengine walikuwa wanalalamika kwamba hawajafa lakini si unajua wanasiasa walivyo waongo, mi nikajua tu wanadanganya nikawazika wote..
natamani ingekuwa kweli maana hawa watu hutudanganya hadi tukakubali uongo wao + kuiba kura basi wanaendelea kuongoza huku kukiwa na maendeleo hafifu sana hasa hiki chama cha (MCC)wanaiba sana kura hawa. 2010 tunataka uchaguzi wa haki!
ReplyDeleteHata mimi naikumbuka hiyo ajali ambayo iliwasibu hao viongozi wa CCM kule kwenye pori nene maeneo ya Shinyanga. Poleni wafiwa wote na polisi uchwara.
ReplyDeletenimecheka sanaaaa wakati nasoma kweli wanasiasa wanakazi kwa wananchi wao
ReplyDeleteWengine wanasema, "change is coming"; wengine :"yes we can" na wengine "nguvu mpya, ari mpya" LAkini matokeo yake, ile nyumba NYEUPE aliyoisema mwalimu inamchanganya mtu! Akiamka asubuhi anafanya lile mama alilomwambia usiku! Asalam aleikum! Nimeomba kutoa hoja tu.
ReplyDeleteTeheeee teheeee tihiiii tihiiiii...nimecheka sanaaaa... Huyu mkulima safi sana.... waraka tosha kwa wapiga kura 2010
ReplyDeleteUtani wa kizamani saana
ReplyDeleteMkulima alikuwa sahihi sana ukizingatia wakulima wamesahaulika sana wanaishia kupewa ahadi hewa za uongo wakati wa kampeni za uchuzi na uchaguzi ukishapita viongozi hulala mbele kwa kasi!!
ReplyDeleteUTAFITI ULIOFANYWA KWA MIEZI MIWILI NCHINI CHINA UMEONYESHA MAKAHABA WANAAMINIWA ZAIDI KULIKO WANASIASA NA VIONGOZI WA SERIKALINI, KATIKA UTAFIFI HUO MAKAHABA WAMEKUWA NAMBA TATU WAKITANGULIWA NA WANADINI (1), NA WAKULIMA(2)!!
WANASIASA HAWAAMINIKI KABISA KATIKA JAMII YA WATU HADI KIASI CHA KUSHINDWAA NA MAKAHABA?? LOL!!
wewe unayesama utani wa kizamani na wewe leta wako tuuone hacha kupinga kila kitu wewe vipi weka mbadala tuone ili kutubali.ni hayo kaka
ReplyDeleteWALITAKIWA WAFUKIWE WOTE MPAKA WAFE. mchuzi mdogo wangu, natuma kwako
ReplyDelete