kila kona na kila kukicha majumba ya enzi za mwalimu yote yanakula nyundo jijini dar na kuacha nafasi ya vikwangua anga vipya. hapa ni mitaa ya kati. mdau unaweza kujua ni wapi?
u

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. hapo ni kona ya haidery plaza maeneo ya posta mpya nyuma yako kuna sheli ya oryx

    ReplyDelete
  2. hapo ni mbagala mtu wangu!!!... mabomu hayoo na wala siyo nyundo..

    ReplyDelete
  3. ni kweli vikwangua anga kila leo vinaota lakini ni kichekesho cha mtu kuvaa suti mguuni ametinga kandambili vikwanguwa anga bila barabara nzuri hivi ni chakuvunia kweli?
    MZEE WA RINKEBY

    ReplyDelete
  4. uncle nanihii hapa ni pembeni ya Samora house Samora avenue. ghorofa ambalo halikuwa na nondo kwenye nguzo zake.
    G.M

    ReplyDelete
  5. inafurahisha kuona jiji linazidi kupendeza. Ila ingekuwa vyema pia iwapo baadhi ya majengo ya zamani yangehifadhiwa kama vivutio vya kihistoria na kumbukumbu ya tulikutoka. Hasa yale majengo ambamo ndani yake matukio mbalimbali ya kihistoria yalipata kutokea.

    Hii pia ingesaidia wawekezaji kupanua mji kwa kwenda nje, sio kuwek kila kitu katikati ya jiji

    ReplyDelete
  6. hapo ni mnazimmoja lakini cha kushangaza huo mnazi wenyewe sijui uko wapi.

    ReplyDelete
  7. Balozi wa nanihii hapo ni mtaa wa Samora karibu na ofisi za reli. Tena nimepita hapo sio muda mrefu wafanya kazi wa reli wamegoma.

    Man of Style

    ReplyDelete
  8. khah! hapa shingofeni usibisheee!

    ReplyDelete
  9. wanajenga vitu vipya pamoja na parking za magari au inakuwa hadithi zilezile jengo la gorofa 15 parking space ya magari 5?

    ReplyDelete
  10. Hii ndio maana halisi ya "UMASIKINI WA FIKRA"
    Nini sasa maana ya Dar es salaam bila Salamanda??!! Hatujui maana ya historia, wala ya sanaa kwa maneno mengine hatujui tulikotoka wala tuliko na hivyo kabisaa hatujui tunataka kwenda wapi!
    Inasikitisha sana. yaani tuna jiji lililozika mipango miji, bustani za kupumzikia zilizopigwa kofuli.
    Ebu jiulize London inapata wageni wengi kuliko New York na Sydney kwa pamoja.....hao watu hawaendi kuangalia uzuri wa majengo wanapenda kuona historia ya mji.
    Majengo mapya kila mtu anaweza kujenga Duniani lakini ya Historia ni nyeti na pekee kwa mahali fulani sasa sisi ......eeh "MASIKINI WA FIKRA SI MALI"
    Mzawa!1

    ReplyDelete
  11. hapo ni juction ya algeria road na samora avenue..kona ya kutoka samora avenue kwenda station bus stand..

    ReplyDelete
  12. Hapo ni samora Avenue na Algeria Street, opposite TRA Samora ambapo mpiga picha ametokea Steak Inn au Kituo cha basi Stesehini, Bustani ya Vodacom

    ReplyDelete
  13. Ni samora na Aggrey street sio Algeria street (usijepotosha wadau) ila uko sawa inatazamana na ofisi ya TRA.
    Ila swali ni je, kuna sababu ya kuvunja haya majengo ili wajenge vikwangua anga? kwani viwanja vimeisha? kwanini wasianzishe miji mipya nje ya mji? na huu wakauacha kama mji mkongwe au mji wa zamani wa kihistoria tupate kuwaleta watoto wetu miaka hiyo kuja kutembea? Mbona nchi za wenzetu wanaanzisha miji mipya badala ya kuvunja miji ya zamani. Kwani kigezo cha majengo haya lazima yajengwe posta ni nini? hiyo ndio sababu ya kuongeza foleni mjini kwani huduma zote zilikuwa zinapatikana mjini. Hawaoni mifano mizuri kama Mlimani city ilivosaidia kusogeza huduma nje ya mji hivyo hulazimiki kuja mijini kwa mahitaji? Naomba kuwakilisha!

    ReplyDelete
  14. Nakubaliana na Anonymous wa 06,04:10:00. Vizazi vijavyo havitaelewa ni namna gani mababu na wazazi wao walivyoishi kama hatuelewi maana ya historia yetu.

    Ndiyo maendeleo tunayahitaji, lakini kwanini tufunje majengo ambayo ni historia ya mji wa Dar yanatuelimisha tulikotoka?

    Dar es Salaamu bado ni kubwa ki maeneo, ingekuwa vizuri serikali kutafuta sehemu nyingine kama Kigamboni na kujenga mji mpya, na kukarabati majengo ya katikati ya mji kwa ajili ya historia yetu. Isitoshe siyo rahisi kwa wadau wengine walivyodokeza kujenga majengo makubwa katikati ya mji bila sehemu ya kupack magari au kupanua barabara pia hata kuwa na green areas (bustani), mahali watu wanapoweza kupumzika. Hii ni vurugu tupu.

    ReplyDelete
  15. Hapo mimi sipajui ni wapi!!!

    ReplyDelete
  16. Yote TISA, kumi: maji, barabara na infrastracture zingine kwanza! Hata tungejenga mpaka mbinguni lakini kama huna barabara ya kwenda huko "nyumbani ni nyumbani" - au huna maji, basi utakimbilia ughaibuni kila siku!! Tufukuzie na tujadili hizi infrastracture kwanza (urban planning zetu ziwe namna gani kwa kipindi kifupi, cha kati na cha muda mrefu). Michu mdogo wangu naomba kutoa hoja.

    ReplyDelete
  17. Hapa ni Mwanza, Pamba Road, Jirani kabisa na kwa Tanganyika Bus.kushoto kwake kukiwa na Pamba Post Office.

    ReplyDelete
  18. Naungana na wale wote wanaoona ushangiliaji wa 'eti vikwangua anga' kuwa ni upuuzi. Ndiyo, ni upuuzi mtupu. Huo ni ushamba! Naïve!

    Sababu nyingi za kukemea upuuzi huo zimeelezwa. Bongo ina sehemu ya kutosha tu ya kuanzisha mipya ikiwa ini sehemu ya upanuzi wa hilo tulaloliita 'jiji'. Kaskazeini, Magharibi, na kusini ya mji wa sasa. Hata kama kuna 'va' yaani vikwangua anga, kwanza ni vya kuhesabu (hapana, sio kwamba naikandia Bongo yest, bali ni ukweli). Pili, ni nani anapenda viraka viraka? Yaani jengo 'oldi', jengo'va', and vaiiss veesa! Haipendezeshi, ni vyema kuacha sehemu flani ikawa na majengo makongwe, na nyingine ikawa na mapya 'va'. Hili litavutia utalii, achilia mbali historia kwa wanetu.

    Halafu linakuja swala la usafiri. Wadau weshalisema hilo. Kuna main roads tatu ziingiazo mjini - Kilwa Road, Nyerere Road, Morogoro Road, na Ali Hassan Mwinyi Road. Zote zinaingiza magari kati ya mji, halafu hapo jaza mwenyewe kinachotkea. Mkazi wa Tegeta lazima mtu uamke saa 9 alfajiri kama unataka kuwahi shughuli yako saa 2 asubuhi. Na hapo utapigwa jasho huku ukikodolea 'va', sijui utafurahia kuviona au utavilaani! Kudaaadeekk!

    Japokuwa mmiliki wa kiwanja au jengo ana uhuru wa kufanya atakavyo ikiwa ni pamoja na kuuza au kujenga vile atakavyo, bado naamini kuwa serikali inahusika na hali tunayoishuhudia hivi sasa. Wanalala tu, kwa kuwa hawajui kwa sababu gani wapo katika nafasi hiyo, zaidi ya kujua kuwa ni ushikaji ndio umewaweka hapo na s vinginevyo. Serikali makini ina uwezo wa kuamuru wajenzi wajenge majengo ya aina fulani mahali fulani. Nilibahatika kwenda katika jiji la Casablanca huko Morocco, nilisemalo lazweza kudhihirika huko. Casablanca ni jina litokanalo na maneno mawili ya kihispania - Casa na Blanca yakiwa na maana ya Nyumba Nyeupe (au white house kwa lugha ya kwini). Serikali iliweka utaratibu na kusimamia nyumba zote katika jiji hilo ziwe na rangi nyeupe. Hilo linafuatwa mpaka hii leo.

    Kwa mfano huo hapo juu, kwa nini serikali yetu isifanye kitu kama hicho? Iwapo mtu au kampuni itataka kuporomosha jengo refu, ambalo ni dhahiri litaongeza uwingi wa wafanyakazi katikati ya jiji, kwa nini wasizuie ujenzi huo na kuelekeza kikajengwe sehemu za nje ya jiji?

    Hivi majengo marefu na mazuri yaliyojengwa miaka kumi iliyopita yangekuwa nje ya jiji hii misururu ya magari ingekuwepo mabarabarani? Yengeweza hata kuchomekwa kule Bagamoyo, biashara zingefuata hukohuko, wallah nasema. Lakini sina maana wakaanze kubomoa zile Kaole, Livingstone, na nini sijui, ... haattaa!!! Manake hawa wakisikia kila mmoja atataka awe futi mbili kutoka ufukweni!

    Kama mdau mwingine alivyosema, uwiano wa majengo unatakiwa kwenda sambamba na ujenzi, upanuzi au uboreshaji wa barabara. Lakini kimeo cha msongamano wa manyumba uliopo unawezesha hilo kufanyika? Nina mashaka na hilo.

    Eti 'vikwangua anga', hivi uzembe wa kufikiri utaendelea mpaka lini Bongo? ... napata ghadhabu, ngoja niingie mitini ...

    ReplyDelete
  19. kwendeni huko ati vizazi vijavyo watafaidika na nini kwani wewe umefaidika na nini na hayo magofu? mengi yao yanaficha vibaka tuuu yess bomoa bomoa weka jiji smart hadi tufanane na huko majuu mlikobana sasa hivi jiji lina shida na parking za magari wakibomoa hayo magofu unayoyatetea huwa wanajenga na parkiing za undrgroungd dont worry vizazi vijavyo watafaidika tu wataenda zanzibar mbuga za animals au wakapande mlima kili ni vivutio tosha sababu hata wewe mwenyewe hufikirii kupanda ukome kuandika ushuzi humu ndani

    ReplyDelete
  20. Miji ya wastaarabu kuna old city na new city. Old city kutunza historia na new city kuendeleza Historia. Unafikiri dunia inakoenda majengo haya ya "angani" yatakuwa mapya? kuna siku itafika yatakuwa ya zamani sana. Tutabomoa hadi lini? Tutumie busara zetu na mipango miji yetu.
    Mimi imenikera sana kubomoa.
    GJK

    ReplyDelete
  21. Anonymous Sat Aug 08, 12:06:00 PM, usihamaki kaka. Magofu yanatunufaisha kusuuza macho. Huenda huelewi hili, na wala sio kosa lako. Huenda kuwa pia shughuli zako hazibughudhiwi na hayo tunayoyasema. Hivi unategemea m'beba madafu kwa baiskeli kutoka Mbagala ataona uchungu wa wenzake wanaosota kwa magari barabarani? Hakuna.

    Tunaomba Bongo ifanane na majuu, na hilo ndilo lisemwalo. Hayo tunayoyasema ndiyo tunayoyaona majuu. Kama majengo ya hovyo hovyo huficha vibaka, basi wabongo woootee ni vibaka, ndiyo pamoja na wewe isipokuwa mimi tu. Kama unafurahia kuona majengo mapya na marefu, kwa nini usitoe nafasi kwa wanaopenda magofu nao wafurahi?
    Kumbuka historia haifanyizwi, bali hutokea tu na ni lazima itunzwe.

    Asiyethamini historia hathamini ustaarabu, kwani historia hutueleza tutokako, tulipo, na kutuongoza kule tuendako. Pata Bonge la shule hiyo we mkulima!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...