JK akiwa na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) Mama Sipho Moyo, wakizindua kwa pamoja ujenzi wa barabara ya Singida-Babati Minjingu. road construction. Kulia ni Waziri wa Maendeleo ya Miundimbinu Dk. Shukuru Kawambwa. Sherehe hizi zilifanyika leo kijiji cha Kititimo mkoani Singida. ADB ndio wadhamini wakuu wa mradi huo mkubwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Yaani ninavyongojea siku ambayo barabara ya kutoka Minjingu kwenda Kondoa Dodoma Iringa itakapojengwa kwa kiwango cha lami. Eh Mola tunakuomba Rabana siku hiyo ije iwe kweli!!!!

    ReplyDelete
  2. Makao Makuu ya African Development Bank mjini Tunis yalitanhaza mwaka jana kuwa itatoa kiasi cha dola za ki-Marekani million 92 (72%) (serikali ya Tanzania itagharimia 28%) kwa ajili ya kutengeneza mabarabara ya mikoa ya Dodoma na Singida ili kuuunganisha mikoa na mikoa ya kasikazini hadi Kenya.

    ReplyDelete
  3. UUi barabara ya kwenda kwetu Babati inatengenezwa,Bwana asifiwe saana! It has been too long and IT IS ABOUT TIME, JESUS!

    ReplyDelete
  4. wenye mabasi mabovu mwanza arusha na mwanza moshi kupitia singida mjiandae kuondoka haraka maana wenye macopolo wameona hii nafikiri wameshaanza kuyaandaa tayari kwa ajili ya njia hiyo

    ReplyDelete
  5. Wajenge ili iendelee kuua watu wetu? Afadhali tuendelee kuwa na mashimo ili watu waende taratibu kwa sababu tanzania hatuna speed limit au hata tunazo hatuzizingatii hizo wala alama nyingine zozote za barabarani. Michu, naomba utoe kaquiz kadogo ka kuulizia alama za barabarani, mimi niko tayari kutoa zawadi ya shs. million 200, kwa atakayepata alama 10/10 (yaani uliza alama kumi za barabarani na maana yake tu)!! Naomba kutoa hoja Michu mdogo wangu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...