Baraka akiwa na kocha bahati ktk uwanja wa Zanaki, Dar
Baraka akiwa na kocha bahati ktk uwanja wa IST masaki, Dar
Baraka alipokutana na Hasheem milimani city conference center jijini Dar.
Baraka akiwa na mtangazaji wa kipindi cah tv 5 connect Bhoke, Hasheem coach bahati na mdau Gwamaka pale milimani city, Dar.
Baraka akiwa na vijana wacheza kikapu pale milimani city.

Mkuu kwanza pole na kazi pia hongera kwa kuendelea kuielimisha jamii kupitia blog yetu hii ya jamii ambayo imekuwa kama gazeti letu la dunia.

Napenda kumtambulisha kijana huyu Baraka Elias Mashauri ambaye ni mrefu kumpita Hasheem Thabeet kidogo na ni mcheza baskteball mzuri tu.
Kutoka na shughuli zangu za u-kocha wa mpira wa kikapu nilitambulishwa na kukutana Baraka miaka miwili iliyopita. Tangia hapo tumekuwa na mahusiano kimchezo yaani kocha mchezaji na kimaisha pia.

Katika kipindi hicho chote tumekuwa tukijitahidi kwa hali mali ili kijana huyu aweze kucheza mpira wa kikapu kama sio hapa Tanzania basi kwingineko Duniani. Kama unavyojua katika kila jambo lazima kuna milima na mabonde na leo nimeona ni bora kuujulisha umma wa Tanzania na wadau kuwa huyu kijana anaweza kufanikiwa iwapo jitihada za kweli zitafanywa.

Baraka amekuwa katika presha kubwa toka kwa jamii au wale tunaomfahamu na wakati mwingine kusahau kuwa Baraka pamoja na urefu alionao (na bado anarefuka !!!! ) anayo mahitaji yake kama binadamu (mentally and physically) ambayo kwa urefu wake ft 7. 4. (Hasheem ni ft 7.3) na kiatu chake ni size 19.!! inamuwia vigumu sana kuishi kama sie akina 5…. ft tunavooishi hapa mjini.

Baraka ana nia na ndoto ya kumfikia Hasheem na ilikuwa ni furaha sana kwake alipofanikiwa kukutana na Hasheem wiki iliyopita. Kwa utaalamu nilionao kama kocha ( nina diploma katika fani ya ‘exercise and physiology’ ) naamini Baraka anahitaji uchunguzi wa kina wa afya ukizingatia kuwa jamaa bado anaendelea kurefuka.

Kwa maelezo zaidi mdau yeyote anaweza kuwasiliana nami kwa email hii bahatimgunda@yahoo.com

Wito wangu kwa wadau ni kujitokeza kumsaidia
jamaa ili tuwe na mbongo mwingine matawi ya juu.

Mdau Bahati Mgunda

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 51 mpaka sasa

  1. wabongo kwa kuiga bana, urefu sio kucheza kikapu.....

    ReplyDelete
  2. Wabongo bwana! Urefu sio issue, anaweza kucheza basket ball?? Anaweza kujituma? Na jamaa naye siajabu kaona Hashim kafanikiwa na yeye anataka kulazimisha, sio kihivyo jamani!

    ReplyDelete
  3. TUPE NA UMRI WAKE, MAANA NAMWONA KAMA MZEE VILE?

    ReplyDelete
  4. inawezekana akawa na kipaji cha kucheza ila kwa kukosa mazingira ya kukifanyia kazi ndiyo maana hadisasa mafanikio yake hayajaonekana sana kimchezo,hivyo basi watu msimlaumu na kumponda eti anaiga,kila jambo lazima uanzie mahali fulani.kwasababu there only two ways of learning things,one is through reading and the other is by associating with smart people in that field.
    kuhusu uchunguzi wa afya ni muhimu sana!!japo sijui umri wake ni miaka mingapi ili kujua kama inawezekana bado anaendelea kuongezeka au lah!
    urefu wake wa futi 7.4 bado ni mdogo ukilinganisha na wa ROBERT PERSHING aliyezaliwa Alton illinois USA tarehe 22/feb/1918 na alipo pimwa tarehe 15/july/1940 alikuwa na urefu wa futi 8 na inchi 11=mita 2 na sentimita 72. na uzito wa 222.71 kg. aliweza kuvaa kiatu chenye urefu wa 47cm, NA wakati alipokuwa na umri wa miaka 9 tu aliweza kumbeba baba yake ambaye yeye alikuwa na urefu wa mita 1.8 na uzito wa 77kg.

    mdau***********

    ReplyDelete
  5. Thanks kwa info.
    Kwanza ungesema age yake ili tulikuwa na uzoefi na pro basketball tukwambie kama anaweza kucheza NBA au laaa.

    Pili, lazima tujue jee ni muda gani amecha hicho kikapu cha mchangani?

    Kingine jee mmeshafanya PHYSICAL Test? Mkaangalia jee Bones structure zake zimekaa vipi? NBA hutumbukii kama unaingia magomeni. Hasheem Mwenyewe kazi anayo... but am optmistic concern him.

    Tupe full hint then tunaojua mchezo tutakualifu
    Mdau wa Kwa Bush

    ReplyDelete
  6. Ana Umri gani? hili ndio swala la msingi kwa hatua ya mwanzo kabisa!

    ReplyDelete
  7. Acheni kutoa komenti zenye mlengo wa kushoto ndugu zangu,huyu mtu anahitaji support,Barak kama alivyo mwanadamu yoyote mwenye kipawa na nia ya kutimiza kipawa chake ana haki ya kufanya afanyavyo katika jitihada za kufanikisha ndoto yake .Hashhem kwake ni role modal na sizani kama Hasheem anafikiri katika mlengo wa kushoto juu ya hili.Hashheem ameweka bayana nia yake ya kusaidia kukua kwa fani hii nchini.
    Hivyo acheni kutoa komenti zissizo za kujenga.

    Bwana Barak mbona hujatuambia umri wako ingawa kwa mwonekano wako katika picha naweza kisia umri wako haujafika miaka 30.so kama vivyo ndivyo u stand gud chance to realize ur dream kaka.


    All the best Barack.

    ReplyDelete
  8. personality pia inamata sio tu kuwa kama liroboti la kucheza basketi pia sidhani kama yuko flexible,urefu wake ni too much which can be also disadvantage.simkatishi tamaa ila asijiwekee tayari sana kuwa nyota wa basketi ball marekani

    ReplyDelete
  9. hakatishwi tamaa wala nini huyo jamaa kwa kumtia machoni tu umri ushaenda sannaa urefu sio ishu vitu vingingine vinaendana na bahati unaweza ukawa mrefu kama nguzo ya umeme na usichukuliwe ng'oo hata mseme kamzidi hasheem urefu nba wanamjua hasheem tu hata mlete wale ngongoti ndo kbsaaaa

    ReplyDelete
  10. Nakushauri kaka,jiunganishe au mpeleke ubalozi wa MAREKANI pale karibu na Zantel ofisi....kisha onana na uongozi wa pale ukiwa na jamaa pamoja na vyeti vyake vya kuzaliwa.Usikose.
    Mdau
    MBIJE,ANDENDEKISYE(0718-56 33 11)

    ReplyDelete
  11. Jamani anahitaji msaada sio lazima NBA!!!!!!! Kitu gani hakieleweki hapo!!!!!!?????

    ReplyDelete
  12. Huyu atakuwa ndugu yake Obama, mbona majina yao yanafanana? Kila la heri bro, Hasheem has lead the way and others ....

    ReplyDelete
  13. we mdau wa juu hapo umefulia......msaidie ww sasa,.....

    ReplyDelete
  14. mtoa maoni 01:42:00 acha kujichanganya " all the best Barack" huna hata haya??? unataka kumdanganya mwenzio?

    Hata kama comments zetu zote zitakuwa nzuri haziwezi kumsaidia hata chembe kama umri umeshapita.

    Umri wa Baraka ni mihimu sana kwetu

    Mdau

    ReplyDelete
  15. Jamaa kweli kaenda juu, ila nina wasiwasi na afya yake maana anaonekana kama vile anatumia sana machozi ya simba au supu ya mawe.

    ReplyDelete
  16. Huyu jamaa anaitwa baraka na sio barack...acheni kulazimisha mambo...pili huyu jamaa anaonekana mzee au inawezekana kuwa akipata mlo kamili anaweza akabadilika. kila la heri kijana.

    ReplyDelete
  17. ngoja tuweke maswala katika hali ya utimilifu:

    suala sio urefu peke yake.
    kipaji, afya,elimu nkvina matter.

    na kikubwa zaidi moyo wa kujishughulisha.
    Huwezi sema jamaa mimi nina kichwa kama Prof wa mlima naomba nisaidiwe niwe Prof.

    Ndugu yangu utasaidiwa na yatakushinda.

    kwanza jisaidie mwenyewe na wengine watakusaidia.
    ni mtazamo wa mlango wa kushoto tu.

    ReplyDelete
  18. Wadau wanaosema jamaa anaiga hawana hoja nzuri. Kuiga ni moja wapo ya mbinu za kupata mafanikio. Na hii inatumika katika kila kitu au fani. Kwani kitu kizuri kikionekana mahali fulani kila mtu huwa anataka kuwa nacho, hivyo kama Baraka ameona kuwa Hashim ni mtu mrefu halafu anafanikiwa kwenye game kwa nini na yeye asifanikiwe wakati naye anajiona ana kipaji cha kucheze kikapu?

    Kuiga sio kitu kibaya hata kidogo. Hivi karibuni kulikuwa na mashindano ya dunia ya riadha kule Berlin Ujerumani na mtu ambaye alitia fora sana ni Usain Bolt wa Jamaica,jamaa ni mrefu lakini anakimbia kwa speed vile vile.

    Kutokana na jamaa kushinda na kufunjilia mbali world records (100m na 200m)mtalaam moja wa mambo ya riadha amesema kuwa mrefu ni moja ya vigezo ambavyo vinamwezesha Usain kuwashinda wanariadha wengine wa mbio fupi kwani ingawa yeye na wanariadha wengine wa mbio fupi waliokuwa kwenye fainali ya mita 100 na 200 wana karibu ratio sawa ya kuchanganya miguu(frequencies ya kupiga hatua), Usain yeye anapiga hatua ndefu zaidi. Kitu ambacho mtaalam amesema wanariadha wengine ambao ni wafupi (wenye hatua fupi)hawataweza kumshinda Usain labla waongeze frequencies zaidi kitu ambacho sio rahisi kwani Usain naye anaweze kuongeza zake pia. Urefu wa hatua hataweze kuongeza kwani wao tayari wameshakuwa watu wazima na ni wafupi kulinganisha na Usain Bolt

    Kutokana na hilo basi mtalaam amesema kuwa miaka ijao si ajabu watu wakaona mbio fupi zinafanywa na wanariadha warefu ambao wana uwezo wa piga hatua ndefu na kuchanganya miguu haraka zaidi kwa wakati mmoja.

    Sasa hii ni kuiga kitu ambacho kinaweza kubadilisha kabisa mtazamo wa mbio fupi hasa America ambako kuna watu warefu wengi tu ila wamekuwa hawapewi kipaumbele kwenye mbio fupi. Hawa huwa anacheza basket zaidi. Sasa USA wanaweza kuanza kuwatafuta vijana ambao ni warefu na kuanza kuwatrain kuwa wanariadha wa mbio fupi.

    Kutokana na hili basi nasema kwamba bwana Baraka kama anajiona kweli ana kipaji cha kucheza basket basi afuate nyao. Na zaidi USA kuna wachina wanacheza basket, na wao ni warefu lakini muhimu zaidi wana talents za kucheze basket na interest ya game.

    Kwa hiyo bwana Baraka, kama umri wako unaruhusu, mrefu tumeona unao, una interest ya game, unajituma kwenye mazoezi, una talents za game, na una afya njema basi utafanikiwa tu. Kaza tu buti.

    ReplyDelete
  19. Duuh!Watanzania kwa kuwakatisha wenzao tamaa,mpaka inasikitisha. Baraka usikate tamaa, wewe weka nia yako palepale,utafanikiwa tuu. Hashhem alisaidiwa na Mkenya kuweza kwenda Marekani na kutimiza ndoto yake,sio Mtanzania. Kwahiyo usikate tamaa, hata mimi ningekuwa nauwezo ningekusaidia, najua ukifanikiwa na mimi nitafarijika. "Penye nia pana njia,usikate tamaa."

    ReplyDelete
  20. Hongera Bro Baraka.Nothing is impossible in this world and sky is the limit.Hivyo kaza buti!kutegemeana na umri wako,njia nyingine unayoweza kutumia ni kutafuta shule hasa kama suala ni kuchezea nje ya nchi(mfano USA) na katika wasifu wako weka hayo masuala ya michezo. Ninaamini huo unawezakuwa mwanzo mzuri.

    ReplyDelete
  21. Umri wangu ni miaka 16, Naomba msaada wenu ndugu zangu, maoni yenu yote ni changamoto kwangu, hivyo nawashukuru nyote, kwa kuguswa kwenu kwa namna moja au nyingine.

    ReplyDelete
  22. JAMANI EEH UMRI SIO INSHU. UMRI SI UNABADILISHWA TU!!! KWANI WANGAPI UMRI WAO ULIOANDIKWA KWENYE DOCUMENTS SIO UMRI WAO SAHIHI??? ILA AWE ENERGETIC NA MWENYE NIA HASWA NA ASIWE MLEVI NA MWENYE KUPENDA NGONO!!! NWANKO KANU KWA SASA ANA MIAKA 40 KAFUA UMRI INASEMA ANA MIAKA 33, NA SI HUYO BADO ANACHEZA!!! MICHAEL ESSIEN ANA MIAKA 32 NA DOCUMENTS ZINAONYESHA ANA 26 NA SI HUYO ANACHEZA TENA BADO ANADAI. KWANI NYIE MNADHANI HASHEEM ANA MIAKA 22 KWELI MNAYOAMBIWA?? HAYA KAENI HIVYOHIVYO. HAPA SUALA NI KWAMBA HUYU BARAKA KAMA KWELI GEMMU ANALIWEZA NA SI MBABAISHAJI ILI MRADI KAJIONA MREFU BASI AJITAHIDI ACHEZE HIZO ZA TANZANIA KAMA PAZI, VIJANA NK NA ATAONEKANA TU. MBONA HASHIMU ALIENDA KUONEKANA MOMBASA!! BARAKA WE CHEZA IPO SIKU UKIWA MZURI UWANJANI WATU WATAKUCHUKUA WAKAFANYE BIASHARA MAREKANI KAMA WALIVYOFANYA KWA HASHEEM

    ReplyDelete
  23. Ndugu zangu watanzania hatusomi!!!Amesema ni mchezaji mzuri wa Basketbal...sasa mtu anania ya kucheza Basketbal unamwambia akafanye shughuli nyingine na urefu wake wapi na wapi?Na ameeeleza ana imani anhitaji kufanyiwa physical check up...Kama una nia ya kusaidia .saidia tafadhali kama huna si unyamaze tu.Maana mchango wako negative hauleti mafanikio yoyote.Labda umri kweli hakusema...

    QUOTE:Napenda kumtambulisha kijana huyu Baraka Elias Mashauri ambaye ni mrefu kumpita Hasheem Thabeet kidogo na ni mcheza baskteball mzuri tu.
    Kutoka na shughuli zangu za u-kocha wa mpira wa kikapu nilitambulishwa na kukutana Baraka miaka miwili iliyopita.


    Baraka amekuwa katika presha kubwa toka kwa jamii au wale tunaomfahamu na wakati mwingine kusahau kuwa Baraka pamoja na urefu alionao (na bado anarefuka !!!! ) anayo mahitaji yake kama binadamu (mentally and physically) ambayo kwa urefu wake ft 7. 4. (Hasheem ni ft 7.3) na kiatu chake ni size 19.!! inamuwia vigumu sana kuishi kama sie akina 5…. ft tunavooishi hapa mjini.


    QUOTE: Kwa utaalamu nilionao kama kocha ( nina diploma katika fani ya ‘exercise and physiology’ ) naamini Baraka anahitaji uchunguzi wa kina wa afya ukizingatia kuwa jamaa bado anaendelea kurefuka.

    ReplyDelete
  24. SWALA LA UMRI: TUTATENGENEZA CHETI, KAMA ANAMIAKA 30 CHETI KITASEMA 15. TUNAPUNGUZA HALF KAMA WALIVYO FANYA WAKINA KANU NA TARIBO WEST.

    NAWASIWASI NA ELIMU YAKE, ITAKUWA NGUMU KUFANIKIWA KAMA HUNA ELIMU, HATA YA FORM FOUR. ILIUFANIKIWE ESPECIALLY NBA INABIDI UPITIE COLLEGE NA UWE NA 'C' AVERAGE THEN NBA.

    ReplyDelete
  25. Baadhi ya watu kwenye blog hii walikuwa wanamkatisha tamaa Hasheem. Leo tena wanaanza kumkatisha tamaa Baraka. Sio vizuri jamaani, kinachotakiwa jamaa apewe moyo. Jamani watanzania mbon tunapenda kukatishan tamaa hivyo?

    ReplyDelete
  26. Wadau wengine sijui wakoje. Usenene mtindo mmoja. Mmeshaambiwa Baraka anacheza mpira wa kikapu. Ana malengo ya kupiga hatua moja mbele na kucheza kwenye ligi kubwa zaidi. Ligi kubwa zaidi sio NBA peke yake. Hata ligi za Ulaya nazo ziko juu kuliko bongo. Mmeona amejaribu kupata uzoefu kutoka kwa mwenzie aliyeweza kupiga hatua hiyo mnataka kumrudisha nyuma.
    Msaada alioombewa ni wa kiafya zaidi, kuangaliwa kama anakabiliwa na tatizo lolote linalomfanya azidi kurefuka. Japo sio daktari nakumbuka mwalimu wa elimu viumbe alipata kunifunza kwamba kuna gland ambayo inaongoza kukua ikiwa inafanya kazi kupita kiasi inaweza kusababisha mtu arefuke kupita ilivyozoeleka kuwa kawaida. Piteni Muhimbili hapo wanaweza kuchukua vipimoj kutambua tatizo ni nini na kutoa ushauri mzuri zaidi.
    Baraka endelea na juhudi zako katika mpira wa kikapu. Hawa hawa wanaokulaani leo kesho ukifanikisha malengo yako wataanza kujitia walikuombea mema.

    ReplyDelete
  27. Nakuunga mkono mwana blog wa hapo juu 06:03:00pm. kwa comment yako uliyoitoa, Sishangai sana kwa negative comment za baadhi ya wabongo kwani wengi ndivyo walivyo. baada ya tupeane moyo na fikra zaidi zakimaendeleo ndio kwanza wanakupiga mawe, tutaishia kusifia vya watu, unafki na upambe.

    ReplyDelete
  28. TAFUTA CHUO MAREKANI HALAFU UANZE KUCHEZEA TIMU YA CHUO NA IKIWA BOMBA UNKUWA NBA.

    WATU ACHENI UHASI.

    ReplyDelete
  29. Sio Wote Watakao weza Kucheza kikapu, Nyie Mna-KREMU!?, Kwani Hasheem Ndio Mtu wa kwanza kuwa mrefu!?, Kuna vipande vya Miti Kibao Mitaa ya wenzetu na havijishughulishi na Kikapu, tafuta Nyenzo Nyingine.

    Kwanza naona Flaws Kibao, Umri, Miguu yake bado nyoro, halafu design Kikapu ni cha ukubwani!...

    Ujio wangu tuu,
    B.

    ReplyDelete
  30. ningependa kutoa ushauri wa kiafya, watu wenye urefu kama wa Baraka na kupita (especially kama bado wanazidi kukua) wanaweza wakawa na condition inayoitwa pituitary gigantism.
    Hii condition inasababishwa na tumour itayoota kwenye pituitary gland ambapo growth hormone ndipo inapotengenezwa, as we all know kwmba tumour inasababisha overexpression au overproduction ya hii growth hormone na matokea ya overproduction of the growth hormone ni overgrowth of all organs in the body ikiwa urefu ni mmoja wapo.
    kwahiyo ushauri wangu ni kwamba, jaribu kufanya simple test kama kucheki growth hormone levels kwanza. Ukikuta ziko katika kiwango cha juu kuliko kawaida then doctors can go on and check if there is any tumour in you pituitary gland.
    The brain scan should be able to tell, kwasababu normal size ya pituitary gland ni size ya blueberry, ikizidi hapo then ni sign ya tumour.
    Matibabu yake ni simple surgery pamoja na drug therapy za ku-stabilize hormone levels.

    Kila la heri
    dada wa Coventry

    ReplyDelete
  31. It's not about height peke yake maana naoma michuzi mpake heading yako umeandika kwamba eti ni mrefu kuliko Hasheem ....so???? urefu si hoja but flexibility as well maana mtu akishakua too tall hata kukimbia itakua tabu.hivi watu mnaanganlia nda au mnatania...mtu anatakiwa atoke baru back and forth and isitoshe the guy looks way older than hasheem...
    but nways gud luck to him

    ReplyDelete
  32. Kwa maelezo ya kocha inaelekea huyu kijana anaweka kuwa na matatizo ya Thyroid Gland ambazo hudhibiti ukuaji wa mtu. Hizi tezi zake zinaendelea kumkuza na inabidi apate uchunguzi wa kina amasivyo anaweza kuathirika kiafya.

    ReplyDelete
  33. Michuzi pole na shughuli za kila siku ndugu yangu. Ee bwana fanya juu chini huyu jamaa asaidiwe hilo tatizo lake la urefu maana kama bado anazidi kurefuka basi soon atakuwa mtu wa kitandani, nimeyaona hayo mengi tu kupitia vipindi mbalimbali vya television hapa UK.Mtafutieni jama dogo connection hatibiwe haraka sana nje ya nchi kama michango mi nitakuwa mmojawapo katika kuchangia. Mfungo mwema.

    ReplyDelete
  34. Kuna kitu ambacho Bahati umenena nakuunga mkono"....anahitaji msaada mentally and Physically..." very true, nilikutana nae 7 7 mwaka huu katika banda la Vodacom, kweli kabisa anahitaji msaada mkubwa zaidi kisaikolojia..

    ReplyDelete
  35. Jamani star si lazima awe mmoja, ndio maana huwa hatuendelei inatakiwa kupeana support watu wengi waendelee katika vipaji vyao sasa watu wengine hapa wanataka abaki huyohuyo aliepo tu. Hio kwani itasaidia nini? (Maana nimesoma mdau mmoja hapo juu anasema eti ameiga sasa hapo huyo Baraka alichoiga ni kitu gani?)

    ReplyDelete
  36. The era of Hashimlization has come ....every body please become hashim...is this a reality???? jamani kila shetani na mbuyu wake na bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi nani kasema kila mtu mrefu ni shoto kulia usawa wa basketball ebo nyie vipi?? anyway biashara ya kuku ilianza kila mtu aliuza na mimi nataka kuwa hashimu jamaniiiiiiii....hivi kwa nini sisi sio wabunifu wa mambo mengine? kwa nini asiwe model?

    ReplyDelete
  37. nshimimana aka DumisaneSeptember 01, 2009

    KWELI SIKUJUA KAMA ITAKUWA HIVI!?

    = = =
    Buffalo, (Kwa Kina Hashimu?)
    New York

    ReplyDelete
  38. Kukatishana tamaa ni tatizo la kitaifa kwa Tanzania sishangai,na kweli wabongo hatupendani sijui kwanini hatujifunzi kwa yaliyomkuta Musa Hassan Mgosi na Ezechwuku aliyemwekea kauzibe akimpigia debe Mnigeria mwenzake. Kumbukeni kuhusu Yao Ming historia yake, achilia mbali Hashimu Thabiti kabla hajawa Hasheem Thabeet.Yao alikua drafted to NBA mwaka 2002 akiwa na miaka 22. Hashimu kabisa alikua hajui kikapu na wala hakudhani kama ana kipaji cha mchezo huo hadi pale alipoanza kusoma makongo na kutembelea mazoezi ya Outsiders ndipo jamaa wakamshawishi kupiga kikapu na alianza kujifunza akiwa na umri wa miaka 15! umri ambao Theo Walcot anapiga soka Southamton,Rooney yupo Everton,Messi yupo Barcelona! . Nachotaka kusema huyu jamaa ana atributes za wacheza kikapu na pia ana nia na anacheza kikapu isipokua hajapata kuonekana ama kutangazwa vya kutosha( just like ukiwa na ball control, footwork nzuri, frexible, na mbio kiasi na physic nzuri unaweza kuwa footballer ). Kwa waliokua wakifuatilia Basket ball kitambo kile pale Indoor hawawezi kutomkumbuka Dulla jinsi alivyokua na kipaji cha ajabu kwenye kikapu, namna alivyokua na shots za kweli lkini hakuweza kufanikiwa au hata kugusa hapa alipogusa Hashim kwa sababu alikosa ile spotlight ya kutosha. Hashim kama si ile zali aliyopata kuonekana kule Nairobi pengine asingefika alipo sasa. hivyo ni kutokana exposure ya aliyopata na bila ubishi waliomshawishi na waliovutiwa na Hashim kucheza kikapu ni kwa kuona urefu wake na hivyo kumpa hamasa kwamba kutokana na urefu huu jamaa piga kikapu. Hivyo basi tunapenda kama wapenda maendeleo uigaji wa namna hii kwani jamaa kama akifanikiwa nae kuwa drafted na kuingia NBA ni kitu kizuri hata kwa uchumi wetu, kwani wakiwa wawili katika kipindi chao cha uchezaji wanaweza kuongeza hata watanzania wengine 10 kwenye profesional basket ball sehemu nyingine duniani na kuiletea nchi mafanikio.
    Si mnaona mafanikio aliyopata Filbert Bayi leo hii watoto wenu wanasoma kwenye shule zake wanapata elimu nzuri hamuoni kwamba mafanikio ya uanamichezo wake yana impact hadi kwenye uchumi wa nchi?
    Big up Bahati kwa support yako kwa watanzania wenzako!
    jojigeorige@yahoo.com

    ReplyDelete
  39. kwa kumchek jamaa i agree anaweza kuwa na somesort of Hormonal disorder...kuna program niliangalia TLC ya kijana mmoja alikua na case kama ya huyo kaka na doctors wali diagonise a growth hormone disorder.it's sad badala ya kutafuta matibabu anakomalia to play in the nda. asipopata matipaptu anaweza endelea kurefuka mpaka akafa jamani me sitanii. kuna case moja ya the tallest man in the world alikufamapema coz he kept growing please watanzania acheni kuentartain nba the guy needs medical help
    ni hayo tu michuzi

    ReplyDelete
  40. HEBU ACHENI UMASKINI WENU WA KIMAWAZO!!ALIYEKWAMBIENI KUWA HASHIMU ANALESENI YA KUCHEZA KIKAPU NINANI MPAKA WATU WENGINE NAO WASICHEZE?
    HEBU ACHENI UTAHIRA NANI ALIYEWAAMBIA KUWA HUYU JAMAA AKIENDA NAEKUCHEZA KIKAPU BASI ATAKUWA AMESAFIRIA NYOTA YA MWENZIE AMA KUMBINYIA HASHIMU?
    NYINYI NDIO WENYE MAWAZO YA KITWANA UKIFUNGUA DUKA HUTAKJI NA MWENZIO NAE AFUNGUE.
    HASHIMU MWENYEWE KAJA PALE MAKONGO HAJUI HATA KUSHIKA MPIRA WA KIKAPU AKAJIFUNZA AKAJUA.
    JAMANI TUNAJIFUNZA KWA KUONA AMA KWA KUSIKIA NASIKU ZOTE TUNAJIFUNZA NA KUIGA YALIYOMAZURI

    ReplyDelete
  41. mbona Hashim anampa mkono kama vile anamuogopa? inawezekana Baraka ana ndumuka na drugs. Anyway tabia ya wabongo kukatisha watu tamaa sio nzuri

    ReplyDelete
  42. kama anendelea kukua basi tumtafutie msaada wa kiafya. Inawezekana kwenye ubongo kuna something .....

    Na kama umemchezesha mika miwili ball lakini haonekani yuko fit what is wrong?

    ReplyDelete
  43. Nimesoma kuwa Baraka ana umri wa miaka 16 na bado anakuwa.

    Maajenti wakiwasiliana na World Guiness Book anaweza kupata ulaji na umaarufu kwa kuwa binadamu mrefu kupita wote akifikisha miaka 21.

    Pia kutokana na kuanza kufatiliwa na World Record Guiness Book kuanzia sasa, ataweza kufanyiwa vipimo vya 'pitutary glands' na mifupa yake nchi za nje.

    Hivyo Mdau Bahati Mgunda tembelea webusaiti ya World Record Guiness Book kwa ajili ya kumtambulisha rasmi dogo Baraka.

    Mdau
    Chakumwenda

    ReplyDelete
  44. Bahati Mgunda/Baraka wasiliana nasi: www.guinessworldrecords.com

    Kupitia Guinessworldrecords watu wengi wamepata umaarufu hata kama sio kina Usain Bolt. Habari zinasema Baraka una umri wa miaka 16 tu na bado unakua.

    Kupitia kwetu Guinessworldrecords milango itafunguka ktk nyanja zote iwe sinema, NBA, matangazo TV n.k

    Tuma details zako na picha haraka www.guinessworldrecords.com tushuke huko Tanzania tufanye kazi yetu ya kurekodi rekodi za Dunia.

    ReplyDelete
  45. Bahati you have taken a step in the right direction.I cannot be easy for Baraka to lead a normal life hapa Bongo.His pychological needs have to be met first ajikubali,ajiamini,ajipende na ajitume kwa kaDRI AFYA YAKE ITAKAVYORUHUSU.
    Kama ni pituitary gland kama ilivyoelezewa kwa ufasaha na mdau hapo juu it can be dealt with medically.
    Mambo mengine ni kumjengea haiba na uthubutu aweze kusinga mbele.

    Kocha tuambie mkakati wako ukoje na unanini wadfau waweze kusaidia.Hasheem alisema kwenye 5 Connect "Urefu siyo hoja.Kuna warefu wengi kuliko hata mimi na wanasafisha madirisha...".
    Tupe strategy wadau wajitokeze.

    Mdau PAZI

    ReplyDelete
  46. KIMTU MWAFRIKASeptember 01, 2009

    nilisoma kwenye blog flan barraka ana miaka 18...ukweli ni kuwa hata hashim hakuwa mzuri kwenye basket ukilinganisha na uwezo waliokuwanao kama mheshimiwa temba,juma kisoki,gilbert batungi etc,lakini kujituma na lishe bora ndio kumemfikisha hasheem hadi alipo sasa...ikitokea baraka kutokuwa na disoder yoyote kama alivyoshauri kocha wake,itakuwa ni fulsa nzuri kutimiza malengo...kuna mdau aliwahi kutoa statement nzuri sana na yenye logic"HUWEZI KUFUNDISHA UREFU BUT UNAWEZA KUFUNDISHA SKILLS"...

    ReplyDelete
  47. BONGO TAMBARRRRRRAAAAAARRRRRREEEEE
    HASHIM NA BARAKA WASICHEZE NJE WACHEZE HUKOHUKO TZ
    KALAGABAHO

    ReplyDelete
  48. kwani hicho chama cha basketball kazi yao nini? kupeleka vitambi vyao marekani baada ya watanzania kufanikiwa kwa bidii binafsi? pumbafu kabisa hizo nauli wangejengea viwanja sio kupeleka vitambi nje wakati kuna watu kama hawa ndo kazi zao kuwaendeleza wanawaangalia tu.. Very SAD... That's why i left that country and not planning to go back!
    Baraka nenda kenya serikali yao pamoja na vyama vya basketball vya huko vinaweza kukusaidia kuliko vya hapo TZ wanasubiria uitoe waje kukupongeza..wakenya wa kawaida tu kila siku wanakuja kucheza basketball hapa kwa scholarship...Your height is exceptional utapata shule right away! I hope umemaliza form four...
    pia fata ushauri alokupa Hasheem he can help you more than we all can.. Good luck!!
    AGAIN, SHAME ON TZ NA CHAMA CHAO CHA BASKETBALL CHENYE MADHUMUNI YA KULA HELA NA KUPONGEZA BIDII BINAFSI ZA WACHEZAJI SIO KUKUZA VIPAJI!!

    ReplyDelete
  49. michezo mingine hii! ndo maana mimi nimedata kwa kandanda na mbio za riadha, ambapo ni tambarare kwa kila mtu. si umbo (urefu/unene/ufupi/wembamba nk), si cheo (utajiri, tabaka, nk) vina umuhimu. watu wanafunga 'matambara' kinapigwa chandimu kona ya mtaani. angalia kijiumbo cha maradona na akiwafungisha watu tela ile ile! Michezo kama Tenisi golf na kikapu hadi mtu atumie, maana mavifaa ya kufa mtu, maviwanja hadi zege ama kapeti la ukoka na kadhalika. hayaa, eti ukiwa mrefu (kikapu, netiboli) basi unakuwa umeanza mbele. kandanda mwanangu, watu wanaufanya mpira vitu kwa mguu na kichwa hata mkono hauwezi..samahani kwa kuhama mada, wadau!

    ReplyDelete
  50. this guy has excessive growth hormone(Gigantism) There have been numerous people in the world who have the height and many of them have tried basketball but have not succeeded. Dude, some good free advice--->>DON'T QUIT YOUR DAY JOB( IF YOU HAVE ONE THAT IS)...HASHEEM is where he is supposed to be, we support him and pray for his success. Don't try to ride on his name by using your height as a connecting factor..so what if your taller?? HE IS BETTER BUILT, HAS MANY MORE YEARS OF EXPERIENCE, BATTLED THE BIG GUNS OF USA BASKETBALL...HIS RESUME WOULD TAKE YOU ATLEAST 8YEARS TO CATCH UP....stick to what you were doing before and get medical help, hormone imbalances can be fatal.

    ReplyDelete
  51. Baraka usisikilize hawa wabongo nuksi walio-stuck up na maisha yao hawajui hata wafanye nini wanabaki kukatisha tamaa wenzao ili kila mtu afeli kama wao. Hata Hasheem walikuwa wanamkataa mwanzoni kafanikiwa ndo hawana jinsi inabidi wakubali kishingo upande
    Follow your dream man, dont give up hope and try to find a way to play in any college in USA utafanikiwa! again, try to make connection with people in Kenya they might help you..and always dont be afraid to express your interest in going to America to play ball

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...