Michu naomba kwa heshima na taadhima usiniweke kapuni bali niruhusu nijubu hoja ya haja ya mdau wa Globu ya Jamii kama ifuatavyo:
Ni jambo la kushangaza na pia la kutia wasiwasi kwamba mpaka kufika hapatulipo leo bado pimajoto zetu hazijatambua hasa nini kiini cha kupanda kwajoto la mwili kisiasa hapa kwetu Tanzania.
Nipo tayari sana kukosolewa lakini hakika ni kwamba matatizo yetu Tanzania si vyama vya siasa na hata wale ambao wapo kwenye madaraka ama nyadhifa za juu kabisa katika majukwaa ya siasa ndani ya vyama hivyo.
Tutakuwa tunafanya siyo busara na siyo haki kuzidi pelekea lawama vyama vya siasa na hata uongozi wake kumbe wapika ubuyu wengine kabisa wapo pembeni kuwaachia wenye meno watafune.
Sipendi kugeuza baraza hili kuwa mahala pa malumbano marefu ya kujadili neno baada ya neno baada ya msitari wa kila anayechangia hoja humu. Hivyo sintofuata msitari huo japo kwa kunena wazi kwamba tatizo letu Tanzaniani ‘ujuaji uchwala’ ambao huzaa lafudhi mbiu kama vile ‘Fisadi’ na nyingine nyingi tuu.
Hapa panatakiwa uzalendo wajameni, hapa panatakiwa uamsho haswa wa hamasa ya kusema kwamba mimi ni mtanzania na nipo hapa kuinusuru Tanzania na watanzania wote, kwamba hapo walipo watanzania wanajivuna na kusema kwamba“nchini kwetu tuna hili na lile la maendeleo igeni toka kwetu”.
Mataifa mengi yametujua sisi kwa mambo haya ya ulaghai usiyo na utajiri, mfano kale ka 10% kametushishia kabisa hadhi mpaka wengine wakafika kusema kwamba unakwenda Tanzania masikini baada ya muda si mrefu weye ni tajiri kushinda hata serikali yenyewe!! (Sasa hapa hili ni la wanasiasa ana vyama vyao vya siasa!!!?? ).
Mimi niliupokea ujio wa JK kwa matumaini makubwa na mpaka leo hii ninayo matumaini hayo ikiwa tu JK atafumbua macho na kuangalia mbali kidogo nje ya baraza lake la mawaziri ambalo linahujumiwa kila siku na kuonekana kana kwamba yeye mwenyewe JK anaendekeza mambo fulani fulani ambayo yanatokanana mawaziri wake, ambayo kwa kweli siyo hata wao.
Ninathubutu kusema kwamba JK anatakiwa sasa kuangalia watendaji. Kuanzia makatibu wakuu wa wizara na wakurugenzi wa kurugenzi zote muhimu, maana hawa KWA TAARIFA YENU ndiyo waharabifu, hawa ndiyo mafisadi haswaa… hawa ndiyo wanajua ndani nje ya kila kitu ndani ya wizara, hawa ndiyo wana taarifa zote zinazohusu maendeleo ya kila sekta ndani ya wizara zao, hawa ndiyo wanaopindisha mambo mengi kwa ajili ya anasa zao ama zakumkomoa aliye juu yake ama hata jirani yake ili yeye tu apate nafuu na familia yake.
Hawa ndiyo wanaowarubuni mawaziri kuingia mikataba ya giza, hawa ndiyo watayarishaji wa 10% hata kama wao watapata shillingi ya kununulia kitumbua lakini kubwa katambulika kwenye kutia sahihi ya 10%, hawa hawasemwi hata kidogo kwa woga kwamba ukiwasema watafanya hujuma kubwa zaidi maana wapo jikoni na ni rahisi wao kutia sumu kwenye mchuzi.
Hawa ndiyo wanatupeleka hapa tulipo na baadaye tunabakia kutiana vidole sisi wengine na wao kukaa pembeni kama vile hawapo, hawa ndiyo wanatuamulia leo tule nini kama Taifa na ni shughuli gani ama mradi gani ufanikiwe.
HAWANDIYO CHIMBUKO LA
MADHAMBI YOTE NCHINI KWETU!!!!
Nimelipasua JIPU..
pwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!
Mdau dRU


Hujajibu hoja,Wewe hauna muono wa mbele.Unafikiria kitumbua kinacholiwa siku moja na kesho yake unatafuta kingine.
ReplyDeleteMaada ya mtu wa kwanza ilikuwa ni ya muone wa mbali wa kidemokrasia hapa Tanzania kwa kuzingatia demokrasia ndio chemchem ya kurekebisha serikali ili iweze angalia mahitaji muhimu ya watanzania.
This is stupid kwanza jambo ulilolisema linajulikana tangu zamani na pia hao makatibu mafisadi wanafahamika. Pili ufisadi wa Tanzania hasababishwi na makatibu huo mtizamo finyu ufisadi wa tanzania unasababishwa na tamaa za maisha ya haraka walizonazo watanzania. Mtu akishateuliwa kuwa Katibu mkuu anawekea usongo kuwa lazima awe na prado, nyumba kumi etc kisa na yeye wakati wake wa kutesa umefika. Si JK wala Sitta na wenzie wanaweza kutatua hilo tatizo ni sisi watanzania tukishaamka tukayajua matatizo yetu na tamaa zetu za kijinga then tutaweza kutatua matatizo yetu venginevyo hii ni siasa tupu na kupotezeana muda. Wacha nikale kitabu na kubeba box maana huu ni upuuzi mtupu tusidanganyane
ReplyDeleteNikweli kabisa hayo, mawaziri wengi hawana utaalamu wa hizo wizara kabisa wanasikiliza kutoka kwa Director na viongozi wengine , uwezi hamini director wa wizara anauwezo wa kumtoa waziri ... this is very serious Ushauri JK watumishi wote wa serekali wale kiapo kama cha polisi kabla ya kuingia madarakani!!
ReplyDeleteWao ndio waaribufi wana kaa miaka nenda rudikwenye wizara moja mpaka retirement au kuwe na perfomance control kila mwaka . bila ya kuwabana hakuna kitakacho fanyika watu lazima waajibike kama watumishi wa umma.
Jamani jamani kwa nini tunalumbana pasipo sababu yoyote, kwa mapendezo yangu kwa nini serikali hisiangalie kwa ndani kuhusu kiongozi yoyote au hao makatibu wakuu na wakurugenzi kama mishahara yao inakwendana na mali zoa kama kuna utata basi waitwe waeleze mali hizo wamepataje, mimi sioni kama kuna uwiano wowote kati ya thamani ya mali zao na mishahara yao, kama watu wenye madaraka watasalimisha mali zao kabla ya kupewa madaraka basi itakuwa vizuri siyo kudanganyana eti huyu mwizi huyu fisadi, kumbukeni cheo ni dhamana wakati wowote watu watataka dhamana yao hivyo wawe tayari kuuelezea umma wa watanzania hizo mali za dhiada wamepata wapi?
ReplyDeleteWow, shule ya kusomea uwaziri wa afya!!
ReplyDeleteNdio, hata JK hakusomea uraisi.
ReplyDeleteNDIO MAANA TUNALIA NA JNIA MIMI NA WAO.
ReplyDeletedah kaka inaelekea kama unaelekea upande mmoja sasa huyo jk atafanya kazi ngapi katika serikali ya tanzania !
ReplyDeletekufichua mafisadi sio JK pekee hata walio kwnye ngazi muhimu washirikiane ndio maana kuna kitu kinaitwa uzalendo je hao hawana imani na nchi yao ?
basi kama hawana imani na hata upendo kwa ndugu zao pia hawana wanazidi kuwaumiza angalia shinyanga,kilimanjaro ... wanavyo
umia
kama wamekosa vyote hivyo basi waangalie malezi kwa watoto wao yaani wananchi wawape makuzi bora
mbona hawataki kuwa kama jamii ya sisimizi wanashirikiana kwa kila kitu
nimesoma maoni yote lakini naona wote wanakwepa ukweli.
ReplyDeleteTatizo letu la kwanza kabisa ni la CCM. CCM wameshindwa hata kutimiza ahadi walizowapa wakati wa uchaguzi kuhusu rushwa. viongozi wengi wa CCM wamepatikana katika misingi ya rushwa, sasa itakuwaje leo hao hao viongozi wawe vinara wa mapambano dhidi ya ufisadi.
Wananchi tuamke tuchukue hela zao mwakani lakini tusiwape kura.
Someni waraka wa kanisa katoliki katika maandalizi ya uchaguzi 2010.
Mungu ibariki Tanzania.