mdau mwenye data tunaomba msaada kwenye tuta hili. tujuvye nini asili ya neno 'ndafu'

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 32 mpaka sasa

  1. Mwulize Mkenda wa tazara au mwika, sinza

    Sijui asili yake, lakini mzee umenikumbusha mbali sana yaani. Unanikumbusha kule Tazara kwa Mkenda! Mkenda tupe jibu kwa sababu ulichinja wengi sana wewe

    ReplyDelete
  2. hilo ni lijicake special kwa wachaga , kwa mara ya kwanza mzungu aliona akasema this is wonderful! toka siku hiyo wachaga wakaita ndafu.

    ReplyDelete
  3. Kichaga ni chakula cha heshima ambacho wazazi wanampa mtoto wao anaenda safari ikiwa na maana safari ya maisha mapya ya ndoa ambayo ni matamu kama hiyo ndafu lakini wakati mwingine ni magumu kama unavyoitafuna sio rahisi kama keki.

    ReplyDelete
  4. Tunaomba wachagga watupe jibu maana ni chakula kilichobuniwa nao

    ReplyDelete
  5. Mmmmh!! msosi wa heshima

    ReplyDelete
  6. NDAFU ASILIA YAKE NI UCHAGANI WAKIMAANISHA NYAMA YA KUOKA.

    ReplyDelete
  7. Hii ndiyo keki asilia,katika mila za kichaga na Tanzania kama inanyokubalika na wengi katika sherehe mbali mbali hasa harusi.

    ReplyDelete
  8. Uliza wachaga maana , sema hapa mate yananitoka nikikumbuk autamu wa hiyo nyama ugaibuni hatuyapati hayo LOL!

    ReplyDelete
  9. Maswali mengine jamani!!yaani kuna mtu hajui nini neno ndafu???au mnapenda tuu kuweka picha kwenye blog ya jamii...
    mdau norway

    ReplyDelete
  10. Jamani kwa wale msiojua..neno ndafu linaokana na neno la kiingereza "wonderful" kwani hapo zamani za kale waingereza walipoenda Moshi/Kilimanjaro walikaribishwa nyama ya mbuzi iliyochomwa kwa mtindo ule sasa baada ya kuonja wakapata utamu nakuanza kushangaa.."ooh it's wonderful!!!" pamoja na maneno mengine ya kusifia msosi basi Wachaga wa enzi hizo wakanasa neno "Ndafu" Aithee ndafu!!! basi ndo tangu hapo ikawa ndafuu ...ndafuu...

    ReplyDelete
  11. Asili ya neno ndafu ni kwamba kuna mzungu alikwenda uchagani akiwa na rafiki yake mmoja wa kichaga. Alikaribishwa kama asili ya WATZ kukaribisha kila mwenye ngozi nyeupe kwa uzuri. Wakati wanakula hiyo mbuzi ya kubanika Baba wa huyo kijana wa kichaga akamuuliza mtoto wake Masawe vipi mgeni anasemaje kuhusu hiyo mbusi? Mzungu akamuuliza mwenyeji wake mzee anasemaje? Masawe akamwambia nini mzee anauliza basi mzungu akasema oohhh is wonderful. Baba Masawe akasema eti amesema ndafu??? Basi, since then ikaendelea kuitwa ndafu na wazee wa kichaga

    ReplyDelete
  12. AAAAAGH!!! wajameni haya ni mambo ghani tena munayafanyaga tena wachaga???. Sasa mbona huyu Mbuli mmechoma na kichwa chake tena kinaonekana bado kibichi kabisa na jani mdomoni?? eeeeegh bhagosha hiiiii he maake a'genaya lolo??? sasa huyu kama len'twe litaleho mh samahani namaanisha kama likichwa bado lipo si munakulaga na mamininga mh samahani namaanisha munakulaga na ma-damu yakiwemo ndani yake bhagosha!! hebu njooni Ng'wanza tuwaonyashe jinsi ya kuchoma bhajameni, huku tunachomaga haya ma-sato na ma-sangara achilia mbali ma mbuli!!

    ReplyDelete
  13. imetokana na nene ENDAHU likimaanisha mbuzi dume.ambaye maranyingi alitumika ktk sherehe kama kitoweo cha heshima na siyo mbuzi jike aka EHABIRI.

    ReplyDelete
  14. The legend has it,;A group of tourists hired a few local chaggas as tour guides as they were climbing Mt Kilimanjaro (date unknown). One of the nights, the porters baked a goat. Upon testing it, the tourists were amazed by how soft and well cooked the Goat was, and off course, baked on open fire hanging from erected tree y-shaped branches. They asked the chaggas who prep the fiesta of the name of the dish: There was, unfortunately language barrier. Never the less, the wazungu's started praising the fiesta "this is WONDERFUL" over and over. The local chagga figured out the wazungus must have JUST named the fiesta "Ndafu" (am sure influenced by, if anything, rhyming of the words). Word passed around, and the chagga boys figured they can make some money by making "Ndafu" special occasion dish.....as I said earlier, the legend has it. Kaka Yenu

    ReplyDelete
  15. Hildebrand ShayoAugust 05, 2009

    Mimi sintapenda kuingia malumbano ya nini maana ya Ndafu, ila kwa wadau wanaotaka kuelewa asili ya ndafu na jina limetokawapi kitafuteni kakijitabu kinaitwa "maisha ya Mchagga duniani na Ahera" au soma kitabu kinachoitwa People of Kilimanjaro kilichoandikwa na Charles Dunda (sina uhakika na hli jina la pili) kwani nilivisoma zamani kidogo katika kutaka kuwaelewa wachagga!

    Kitabu kimoja kimeandikwa na Marealle ambaye ni mchagga na kingine British.

    Kwa wale ambao wanahitaji copy wasiliana na mimi, nitawatumieni micro copy ya vitabu hivyo kwani havichapishwi tena!

    ReplyDelete
  16. Tarehe Wed Aug 05, 10:52:00 PM, Mtoa Maoni: Hildebrand Shayo

    Shayo ati babangu tutakupataje aisee? Haki ya Mungu wewe Shayo umeondoka na vile vitabu vyangu. Naona ni wewe kabisaa ulivichukua. Mimi nikifumba na kufumbua haya macho na mashavu nkute ftabu fyangu fimerudi, la sivyo nitakuchoma na huu mkuki, ukikatika babayako alipe, ikiingia kwa kifua haki lee, usafishe hiyo kisusio. Michu mdogo wangu naomba kuwasilisha kwa mchagga (mtani wangu)

    ReplyDelete
  17. Hakika wawili tu ndio wako sahihi .asili ya neno ndafu ni wonderfull- source watalii walikuja kupanda mt.Kilimanjaro.

    ReplyDelete
  18. Anony wa Wed 05 Aug,09, 14.00 umenichekesha sana. Mi natokea Mwanza na ni msukuma, so huo utani wako umenichekesha sana. Asante kwa kunifurahisha.

    ReplyDelete
  19. Mimi ni mchaga asilia namuunga mkono huyo anon aliyesema Kuhusu Mzungu: Enzi hizo za ukoloni mzungu alinja akasema this is wonderful! Kutokana na upeo wa zamani wa kutojua kiingereza tukasikia Ndafu, tulielewa mzungu kaiita hivyo basi toka siku hiyo wachaga tukaita ndafu.

    ReplyDelete
  20. Hivi wewe uliosema limetokana na ENDAHU ikimaanisha na mbuzi dume unaakili timamu kweli??? Umefikiri kabisaaa!! Hebu kama hujui historia za kichaga nyamaza. Na BEBERU aitwe vipi ikiwa ENDAHU ni mbuzi dume?? Mbuzi dume ni Beberu.

    ReplyDelete
  21. Aliyesema EHABIRI na ENDAHU anachekesha tuu wala hajui kichaga pengine wala sio mchaga. Watamcheka watuu

    ReplyDelete
  22. JE MNAELEWA MAANA YA HILO JANI kwa kichaga linaitwa ISALE??? Toeni maoni yenu mkikosa halafu nitatoa jibu baadae

    ReplyDelete
  23. hildebrand shayoAugust 06, 2009

    hi

    kwa wale wanaotaka copy ya vitabu vya wachagga hasa hicho kinachozungumzia ndafu na mambo mengineyo kama ni kwa namna gani ya kumchukua mtu msukule, namna gani ya familia kupata mtoto/watoto wenye akili, dawa za kiasilia na mambo mengi tu ambayo kwa mtizamo wangu ni muhimu lakini historia inapotea, vinapatikana National Achieves, kew richmond surrey, UK. la sivyo wasiliana na mimi kwa kutumia shayohill@yahoo.co.uk

    ReplyDelete
  24. haaaa,wajameni wachaga oyeeee,sisi bwana ndafu inatumika kama ishara ya furaha na kutakiana heri,wengine wanaiga tu ....,huwezi kuchoma ndafu kwenye msiba .miss mushi

    ReplyDelete
  25. Hata mimi nilishasikia tafsiri/historia kama hiyo kuhusu waingereza na hilo neno ndafu,lakini hiyo ya "endahu" na "ehabiri" ni mpya kwa wengi,japo ndafu sharti awe beberu! labda aliyesema atufafanulie zaidi pengine kuna ukweli pia.

    ReplyDelete
  26. ..............hapo hapo... tizama mdomoni mwa ndafu kuna sale! Je, neno sale asili yake wapi?

    ReplyDelete
  27. HAKUNA CHA NDAFU HAPA, HUU NI UDHALILISHAJI WA WANYAMA NA HAKI ZAO !!

    ReplyDelete
  28. HAKUNA HATA MMOJA WENU ALIYE PATIA JIBU.
    NI KWELI WAZUNGU WALIFIKA KWA WACHAGA NA KUTAFUNA MBUZI ALIYE OKWA. MMOJA WAO AKATOA COMMENTS; THIS IS WONDER OF FOOL. KWAMBA NI MAAJABU YA MJINGA. NAO WACHAGA WAKADAKIA NDAFOOL
    HEHE! tHE!!!EEEEH!

    ReplyDelete
  29. Katika kichaga hakuna neno Endahu wala Ehabiri. Wasio jua kichaga wala wasio wachaga wasichangie mambo ambayo hawajui. Hata wewe ukiwa ni mchaga lakini hujakulia uchagani na ukawa hufahamu kilugha pia usichangie kwasababu utakuwa unachangia uongo tu.

    Ngakukaba kyandu ukichangia kama hujui

    ReplyDelete
  30. Wewe uliyeuliza maana ya ndafu soma makala haya kupitia gazeti gwiji wa habari Tanzania, habarileo kwenye link hii utaona maana ya ndafu na asili yake.

    www.habarileo.co.tz/biasharaFedha/index.php?id=4528

    www.habarileo.co.tz/biasharaFedha/index.php?id=5010

    Mimi mdau.

    ReplyDelete
  31. hildebrand shayoAugust 08, 2009

    Wadau, wanaochangia hoja za hapa na pale kuhusu ndafu, na hilo jani la isale.... nawaombeni muelewe kuwa jambo usilolijua ni kama usiku wa giza. fanyeni kautafiti kidogo, ndiyo mtagundua siyo ndafu na asale tu, kuna mti unaitwa "mfifina", "Kichongu", jani linaitwa "makengera"
    nk n , vyote hivi vinaumuhimu wake unapozungumzia mila na desturi za kabila fulani. Mtagundua ni kwa nini wanawake wanapewa sehemu ya nyama inaitwa "ilongu" na baba mzazi anaewa "kidari"

    Usichangie tu kwa vile uiona ndafu kwenye harusi!

    ReplyDelete
  32. Wote tunajua ndafu ilikuwapo kabla ya mzungu kuja, kwa hiyo jambo la wao kutunga jina si la kweli, nahisi ni vichekesho vya ma MC wa bongo wamesambaza hadi ilekuwa kama ukweli.
    Pia wanajaribu kuexagerate mambo machache wanayoyajua kuhusu makabila ikiwamo wachaga. Mambo yetu mengi yanapotea. Mfano kichaga mwanamke haruhusiwi kushika kisu kumkatia mwanaume au mzazi nyama, lakini hawa jamaa wanalazimishia eti binti amlishe baba, maajabu baba wa kichaga anapokea!!
    Tamaduni zetu ikiwamo lugha zinapotea sana, mfano ni misamiati kama aliosema shayo. Vitabu alivyosema ni muhimu sana kuwa navyo, pamoja na vingine vyenye hadithi za kale na misamiati mingi tu. Nasikitika sana havipatikani siku hizi.
    Kuna watu wameanza kuwahoji wazee na kurekodi historia, naomba tuendeleze, kwani tunakoelekea bila kuwa na base tutakuwa tunaelea kwenye limbo.
    shayo naomba kopi ya vitabu hivyo, mimi ni wa marangu na hicho kitabu kimoja nimekisoma ni mahususi wa wavujo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...