obote kwa mchakato wa ist afrika mashariki
Wadau tunajiandaaje na Soko Huria la Afrika Mashariki? Ifuatayo ni sehemu ya hotuba aliyoitoa JK kwenye HAFLAYA UTOAJI TUZO KWA WAZALISHAJI BORA WA VIWANDANIWA MWAKA 2009 TAREHE 06 AGOSTI, 2009 MÖVENPICK ROYAL PALM HOTEL, DAR.
Ndugu Wanashirikisho;Kuanzia Januari 1, 2010, Umoja wa Forodha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utatekelezwa kwa ukamilifu. Kuanzia siku hiyo, bidhaa za Kenya ambazo, kwa miaka 5 mfululizo, zilikuwa zinauzwa katika nchi yetu na Uganda kwa kulipiwa ushuru, zitakuwa nazo hazilipiwi ushuru. Aidha, kama mazungumzo yatakamilika kama tunavyotarajia, wakati huo Soko la Pamoja la Afrika Mashariki litakuwa linaanza.
Ni wakati wa mabadiliko makubwa kwa mfumo wa biashara hapa kwetu hivyo ni vyema tujiandae vizuri kuyapokea na kuyatumia kwa manufaa yetu. Hivyo nawaomba mkae chini, muitafakari na mpange mikakati na mbinu za kuishi na kunufaika katika mazingira, hayo mapya.
Kubwa zaidi ninalowaomba mimi ni ninyi kujipanga vizuri kuzalisha bidhaa kwa gharama ndogo lakini zenye ubora wa hali ya juu. Yapo ya Serikali katika kuwasaidia kufanya hivyo ambayo napenda kuwaahidi kuwa tutafanya kila tuwezalo kutoa mchango wetu stahiki. Lakini, kwa yale mengi mbayo ni yenu, na ni mambo ambayo yapo kwenye uwezo wenu kufanya nawaomba mfanye bila ajizi.
Napenda kuwatahadharisha kuwa, epukeni tabia ya kutojiamini, woga na kujidharau wenyewe kuwa hamuwezi. Tabia hii ndiyo adui yetu mkubwa kuliko wote hapa Tanzania. Pale mwanzoni tulipoanza mchakato wa kuunda Jumuiya ya Afrika Mashariki hofu kubwa ilikuwa Tanzania kugeuka kuwa soko. Baadhi ya watu waliiamini dhana hiyo kiasi cha kutufanya baadhi yetu tuliokuwa tunaongoza harakati za kuunda Jumuiya tuonekane wasaliti. Lakini ukweli sasa unawasuta.
Leo hii biashara kati ya Tanzania na Kenya imekua sana, tena sasa sisi tunauza zaidi Kenya kuliko Kenya inavyouza Tanzania. Kwa mujibu wa takwimu za Benki Kuu ya Tanzania, mwaka 2008 Tanzania iliuza Kenya bidhaa zenye thamani ya shilingi milioni 277,820, wakati Kenya iliuza Tanzania bidhaa zenye thamani ya shilingi milioni 233,967. Zamani hali haikuwa hivi. Biashara ilikuwa ndogo na Tanzania tulikuwa tunanunua zaidi kutoka Kenya kuliko tunavyouza.
Haya yote yametokana na kufunguliwa kwa milango kulikotokana na Umoja wa Forodha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Naamini hata Soko la Pamoja likija tutaendelea kunufaika, bora tu tupange mikakati yetu vizuri na tuhakikishe kuwa tunaitekeleza. Naamini tutaweza. Kama tumefikia hapa bila ya shaka tunaweza kufanya vizuri zaidi.
Tutakuwa tumefanya makosa makubwa kama tutakurupuka tu na kusaini mikataba ya soko la pamoja bila ya kuzingatia masilahi yetu,kwa tabia zetu hizi za kudanganyika kwa jina la umoja kila siku tukauwa tunalia kilio cha mbwa pua juu!
ReplyDeleteKwanza itabidi lazima tujitayarishe kwa kuweka mikakati ambayo italinda masilahi ya watanzania na kizazi kijacho.
(B) Wenzetu wakenya wameshajiandaa kisawa sawa,tena mpaka hivi tunavyojadili suala hili wakenya wametuzidi kete,wameruhusu na kutoa nafasi kwa raia wao wote wanaishi nje ya kenya kuchangia kukua kwa uchumi wa kenya katika kila hali na mali,wameruhusu Raia wao wawe na Uraia wa nchi mbili (DUAL CITIZENSHIP or Nationality) kwa maslahi na malengo ya kuinua uchumi wa Kenya.
Sisi ata vitambulishi vya kitaifa hatuna,hilo swala la kuwaruhusu watanzania wenzetu walio nje ya nchi kuchangia kukua kwa uchumi,ndio kabisa hatutaki kulisikia kila kitu ni mizengwe.
sasa leo tukubali kujiunga na soko la pamoja????Jamani mbona mambo ya ndani bado atujayaweka sawa?
MIMI SIPO HAPO! wanaojua kusukutua na wasomi nawachia baraza hilo
wewe mdau wa 6:07:00 acha kujenga watu hofu isiyokuwa na maana yeyote,number dont lie kumbuka,JK kishakupa statistics kwa sasa TZ inauza Kenya kuliko kununua na sasa sijui shida yako nini,yaani unafikiri maendeleo ni kufunga mipaka na kuzuia biashara kati ya mataifa,cha ajabu unalalamika kuhusu jirani zako huku Wachina wanauza karibu kila kitu Tanzania na isingekuwa wao leo vitu vingekuwa ghali sana na biashara nyingi zisingekuwepo,Biashara kati ya mataifa ni muhimu sana na walichofanya kina Kikwete kitaleta ushindani mzuri sana na kupunguza kodi kutapunguza gharama kwa mwananchi...acheni kuishi miaka ya 1947,acheni watu wafanye biashara kirahisi,nasema tena big up EA!
ReplyDeleteChemsaha Bongo kabla hujaingia kwenye shirikisho la Isti Afrika:
ReplyDeleteThe fact that we have been forgiven our debts does not mean that our president has to use the donkey as a means of travel. Does this also mean we can't buy clothes and therefore walk naked? [?1]
For President Mkapa to use that jet to go to Addis Ababa to the African Commission meeting... to tell Mr Blair, 'Please give us more money so that we can fight poverty in Tanzania,' it's a real shame [?2]
It pains to see that some investors are importing raw commodities, although just on their door steps, similar produces are left to decay [?3]
When you export unprocessed goods, in simple words, you are exporting jobs, taxes, and other key economic opportunities... it is high time we stopped this outdated trade system [?4]
The idea of African brotherhood is often just a cover-up for laziness. We must see what is achievable in our circumstances and evaluate all decisions. In terms of regional economic integration, sentimentality is not enough. We really have to be frank and honest [?***5]
There is a thought that poverty is a public policy failure; poverty is man-made by action and non-action: poverty can be eliminated [?**6]
The slogan that agriculture is the backbone of the nation still remains in theory and not in practice[?***7]
Kiswahili kimetugharimu sana, na bado kinatugharimu sana. Kiswahili ni moja ya changamoto kubwa sana zitakazoleta mafuriko ya kuporwa ajira na kudidimiza elimu na utambulikaji wa elimu yetu hapa nchini.
Mathalani, sisi tunafundishwa miaka saba kwa Kiswahili (shuleni tunanyimwa kuongea lugha za makabila na kusisitizwa Kwaswahili) halafu tunarudi shule za upili ambako tunafunzwa kwa Kiingereza [na tunapigwa marufuku kuongea Kiswahili, na tunasisitiziwa Kiingereza).
Shule za Upili tunasoma miaka sita (kidato cha I-VI) ndipo tunajiunga na Chuo... wakati huo huo, wenzetu wa Kenya wanasoma miaka minne tu shule za upili, wanaendelea na vyuo. Ieleweke pia kuwa watanzania wanawakimbizia watoto kusoma Kenya na Uganda kwa idadi kubwa kuliko kinyume chake i.e wakenya na waganda kusoma kwetu.
Kiswahili cha hasara kuliko faida (achilia mbali umoja wa kitaifa ambao HAUTAKUFA KWA KUFUNDISHA SHULE ZA MSINGI KWA KIINGEREZA) cha nini? Kuna haja gani ya kukumbatia utamaduni kwa gharama za KIUCHUMI, KISIASA, KUJAMII (IKIWEMO KIUTAMADUNI)... kwa kupewa sifa tu kuwa tunaongea tofauti?
Afrika ya Kusini ina lugha 11 zinazotambulika [kikiwemo kiingereza]. Inaheshimika duniani kwa kutangaza utamaduni wao. Je, tanzania tunataka kuitangazia nini dunia juu ya Kiswahili kwa Kiswahili?
Shirikisho laja, sawa. Je, ajira zitakuwa na uwiano hasa tukizingatia lugha? Ni hivi majuzi tu WANASHERIA WETU "wamegongewa kengele ya hatari" kwamba LUGHA NI TATIZO .... kiasi kwamba shirikisho likiwadia, jameni, wamekwisha! Na hata sasa 'hawathubutu' kuongoza mambo kwa kimombo, hivyo NOT COMPETENT BECAUSE OF OUR SWAHILI.
Tuendelee kukikumbatia kiswahili kwenye kufundishia shule za msingi hadi lini? Mfumo wa Elimu ubadilike, lugha ya Kiingereza itiliwe mkazo, wakati pia WANETU WAKIENDELEA KUSOMA SOMO LA KISWAHILI [?*******7]
umasikini tulionao unatutosha jamani kwani hilo soko huria ndo litatumaliza sioni haja ya sisi kufanya mambo hayo tutakua tunarudia makosa wala sio kusahihisha makosa.
ReplyDeleteASANTE SANA MICHUZI KWA PICHA YA MAKUMBUSHO KAMA HII. MBONA PICHA ZAKO SIKU HIZI HUWEZI KUZIFANYA KUBWA KAMA ZA BLOGS NYINGINE.
ReplyDeletehii anony ha hapa yuu, mon Aug 31, 06:07:00 PM ni mnyonge ya kiakili, na ni moga ya kuogopa ile bitu ya kenya. kama wewe naishi inje ya sisi bitu ba tz hatutaga kaa ikubali hii dual nationality. hii kitu imefanya kenya na zimbabwe iwe inchi ya utumwa.
ReplyDeleteHao "wazee wetu" labda kwa wengine, mi simo. Obote aliua watu kuliko Idd Amin baada ya Amin kuondolewa, Arap Moi alijimilikisha biashara zote Kenya, na alikuwa kidikteta kikubwa kile kibabu.
ReplyDeletesevedo
ReplyDeleteyou are right from 1-7, but i would like to differ from you on the use of english v/s swahili!!english cannot and will never become a household language for any African nation even if we start as early as in primary schools unless we transform our culture too..so i would suggest we teach in swahili all along our academic set up and keep english as one of the lesson.all over the world countries have excelled economically by using their own languages coz is easier to innovate if you think about selling your own products,we need only few people at the marketing level to acquire some other languages like english,chinese etc otherwise we do'nt need any english at the production level!
wabongo hatuwezi kwani sisi ni watu wa longo longo kazi hatujui kabisa
ReplyDeletetumeshupalia udini kuliko kazi ok bro
HUYO MCHANGIAJI WA 09:05 ANAEJIITA SEVEDO.INAONESHA NI JINSI GANI ULIVYOKUA BOGUS YENI KAMA ULIENDA SHULE ELIMU YAKO HAIJAKUSAIDIA KUELIMIKA YANI HAUJAELIMIKA.
ReplyDeleteWATU WANADISCOUS ISSUE MUHIMU ZA MAANA WEWE UNAANZA KUELEZEA AIBU ZAKO ZA UMASKINI WA KIMAWAZO YANI UTUMWA WA KIFIKRA.
NYINYI NDIO MNATURUDISHA NYUMA HATUA MIA NYUMA,HAO WAKENYA MNAOWADISCOUS WANAJIVUNIA KISWAHILI WANAJITAMBA NA KUJITANGAZA KWAO NDIO MOTHERLAND OF SWAHILI LANGUAGE!!WANAPATA WATALII KIBAO KWA KUPITIA KISWAHILI!!HII LEO UKIFUNGUA CHANEL KALIBIA ZOTE ZA TV ZA ULAYA UNAONA WAZUNGU WOTE WANAJUA KENYA NDIO WANAOZUNGUMZA KISWAHILI NA WANAJUA HUKO NDIKO KILIPOZALIWA.
ANGALIA PROJECT ZOTE KUBWA ZA KISWAHILI ZOTE ZIPO KENYA MFANO ZA KUINGIZA KISWAHILI KWENYE COMPUTER,SIMU N.K ZOTE ZIPO KENYA NA ULAYA NA HII KUTOKANA NA USHAMBA WETU WA KUJIDHARAU.
IMAGINE PROFESA ALIYETOA WAZO LA KISWAHILI KIINGIZWE KWENYE COMPUTER ANAASILI YA MALI ILA ANAURAIA WA MAREKANI.
HAO WASOUTH AFRICA KWATAARIFA YAKO HUKO KUFUNDISHWA KWA KILA KABILA LUGHA YAKE NI PROJECT MAALUMU YA KUWAFANYA WASIWE NA UMOJA YANI WASIUNGANE.
ANGALIA NCHI ZA KIAFRICA ZIMEANZA KUPITISHA KISWAHILI KUWA LUGHA YA TAIFA MFANO UGANDA NA NYENGINE KAMA RWANDA,BURUNDI,ZIPO NJIANI NCHI KAMA CONGO RAISI WAO ANATUMIA KISWAHILI KWENYE SPEECH ZAKE.
ANGALIA RAISI ALIYEPELEKA WAZO KISWAHILI KIINGIE KTK A.U NI RAISI WA MSUMBIJI NA SIO WA TANZANIA KWA KUWA SISI TUMELALA.
TUACHE USHAMBA WA KIMAWAZO,HATA SIKU MOJA HUTOMSIKIA MZUNGU ANAJIVUNIA UKABILA BALI ANAJIVUNIA UTAIFA ILA WAKIJA HUKU KWETU WANATUPAKA MAFUTA KWA MGONGO WA CHUPA,WAAFRICA MNAMAKABILA NA CULTURE ZENU ZA KIKABILA NZURI SIO CULTURE ZA MTANZANIA ILI TUSIJETUKAWA NA UNITE TUKAPENDANA.
SASA HIZI LUGHA ZETU ZA KIKABILA HAZITUUNGANISHI ILA ZINATUBOMOA UMOJA WETU WA KITAIFA.
TUJIFUNZE LUGHA ZA WATU LKN TUJIVUNIE TULICHONACHO TUACHE USHAMBA NA UMASKINI WA KIFIKRA(SLAVE MENTALITE)
BADO TUNAFANYIA KAZI MAANDALIZI, KWA SASA TUNAKUSANYA MALALAMIKO DHIDI YA WAKENYA KISHA TUTAANGALIA NI MAANDALIZI GANI TUYAFANYE, LAKINI TUKO TAYARI KUKABILIANA NA SOKO HILO LA PAMOJA.
ReplyDeleteMTOA MAADA YA SOKO HURIA ist africa
ReplyDeleteUMEDANGANYA KUWA TZ TUNAUZA BIDHAA KENYA ZAIDI YA KENYA WANAVYOUZA KWETU.NDIOINAVYOONEKANA KWA WAJINGA WENGI UKIWEMO WEWE.
UKWELI NI KWAMBA.
BIDHAA TUNAZOUZA KENYA NYINGI NI KUTOKA VIWANDA VYA WAKENYA VILIVYOKO TZ.
KENYA NI MWEKEZAJI NAMBA MBILI NCHINI TZ,
WAKWANZA NI UK
WAPILI NI KENYA
TATU NI INDIA AU SOUTH AFRICA,
HUO NDIO UKWELI.
UWEKEZAJI WETU NJE NI MDOGO SANA UKULINGANISHA NA KENYA.
SISI TUTAISHIA KUFANYA KAZI KWA MAKAMPUNI YA WAHINDI NA WAKENYA TUKIJIDANGANYA KUWA NI VIWANDA AU MAKAMPUNI VYETU.
KALAGABAHO
BONGO TAMBARRRRRRRRRRRRRRRAAAAAAAARRRRRRREEEEEEEEE.
TEHE TEHE TEHE
NDUGU YANGU ALIYETOA HOJA YA KUKIPONDA KISWAHILI INAONESHA NI JINSI GANI ALIVYOKUA NA MAWAZO FINYU!!
ReplyDeleteKISWAHILI SIO FACTOR INAYOTURUDISHA NYUMA ANGALIA KUNA NCHI NYINGI ZENYEWE ZIPO KTK COMMUNIT LKN RAIA WAKE HAWAJUI LUGHA NYENGINE MFANO WAFARANSA WALIOWENGI HAWAJUI KINGEREZA MPAKA RAIS WAO ANATOA SPEECH KWA KIFARANSA,NCHI KAMA UHOLANZI,POLAND,CHINA N.K
MBONA LUGHA ZAO HAZIKUWAAFECT KTK KUTAFUTA AJIRA?
POINT NI KWAMBA HATUPO COMPITANT KTK KAZI YANI HATUNA UJUZI NA SIO ISSUE YA LUGHA.
PIA MKUMBUKE KISWAHILI NDICHO KILICHOKUFANYA UKASTAARABIKA NA KUKUNGANISHA NA WATU WENGINE.
WEWE UNATAKA TUUNGANE NA WATU WENGINE KWENYE EAST AFRICA COMMUNITY LKN UNATAKA NDANI TUSIUNGANIKE KWA KUPENDA UKABILA,SASA KAMA NDANI NYINYI WENYEWE HAMNA UMOJA UNADHANI UNAWEZA KUSHINDANA NA MTU MWENGINE MWENYE UMOJA?
PUMBA ZENU ZA UKABILA USITULETEE WATANZANIA,PELEKA KWENU HUKO AMBAKO HAKUNA USTAARABU
Wevkipunga wa 3:11 unaonekana hata shule hujaenda na unafikiri lazima viwanda viwe vya mtanzania ndio vitajenga uchumi wetu,kama mkenya kafungua kiwanda TZ na anatoa ajira ndani ya TZ na kulipa kodi zote tatizo ni nini?lazima ujue dunia ya leo hata Us viwanda sio lazima viwe vya wazawa na ujue investment nyingi Us ni za watu wa nje,watu wanataka kodi tuu na ajira kwa watu wao,wewe kaa na ukipunga wako wa kufikiri maendeleo lazima yawe ya viwanda vya watanzania...jiulize kwanini kila siku JK anazunguka kuomba wawekezaji waje TZ,sina hata muda wa kukuelewesha kipunga kama wewe naona ni kupoteza muda tuu,lakini uzuri mawazo yako hayana nafasi dunia ya leo!
ReplyDeleteJE MAMLAKA ZETU ZA USIMAMIZI ZINAZEMBEA UAJIRI WA WATAALAMU WA KIGENI?
ReplyDelete(AMA LIBENEKE LA WATANI WA JADI KWA MLANGO WA NYUMA!)
Ni jambo la kisikitisha na kutatanisha kuona jinsi wataalamu wengi wa nje walivyoajiriwa kiujanja-ujanja na kwa visingizio (vingine vya kitoto) kwenye fani, makampuni na mashirika mbalimbali. Nafasi nyingi kati ya hizo zingeweza kabisa kuchukuliwa na wazawa wenye uwezo na vipaji chekwa.
Kwa uelewa wangu, kote duniani, ni juu ya mamlaka za taifa za udhibiti kusimamia na kuhimiza kampuni na mashirika kutengeza na kusimamisha sera na vigezo mahususi kwa ajili ya malengo ya ndani yanayoendana pia na malengo makuu ndani ya nchi husika.
Ni juu ya mamlaka idhibati basi kupima kama vigezo na sera hizi za utawala ndani ya kamouni/mashirika chini ya mamlaka hiyo ni mwafaka kama ilivyokusudiwa.
Sasa swali: Je, kwa nini inaonekana wazi kuwa Benki kuu ya Tanzania pamoja na Wizara za Kazi na Mambo ya Ndani zimeshindwa kabisa kudhibiti mfumuko wa wataalamu wa kigeni nchini mwetu? Mamlaka udhibiti hizi zilitakiwa kuhakikisha si zaidi ya wataalamu wa kigeni watano kwa shirika/kampuni kwenye mikataba ya muda mfupi. Pia ikiwa kwamba makampuni haya yamesimamisha mpango mahususi wa kuendeleza wazawa kuchukua nafasi hizi ndani ya mikataba hiyo isiyozidi miaka miwili
Labda nitoe mifano miwili mitatu:
(inaendelea...)
(...inaendelea)
ReplyDeleteLabda nitoe mifano miwili mitatu:
Benki ya Standard Chartered in wataalamu wa kigeni takriban 10. Japo ni rahisi kusema kuwa inatia sana moyo kwa kuwa nao wameshapeleka wazawa 10 nje ili kuwaendeleza.
Benki ya Barclays ina takriban wataalamu wa kigeni 23! Ikiwa ni pamoja na mkuu wa kitengo cha ‘Rasilmali Watu’ (Uajiri). Hamna mipango yoyote madhubuti ya kendeleza na kumuachia mzawa (labda kwenye mafaili tuu kuridhisha hizo mamlaka udhibiti). Hebu tazama, hawa jamaa wanaingia kwa visa ya kibiashara ya miezi mitatu, mitatu – huku wakiongezea mara ziishapo. Mambo kama likizo wanapata kaa kawa na yote yapo katika maandishi. Ukiangalia menejimenti yao ya juu ya sasa, ni mlolongo wa ‘watani wa jadi’, halafu wabara hindi na pia hata Zimbabwe.
Niseme tuu kuwa hii ni mifano kuna benki nyingine za kigeni zenye ‘kunguni’ (kama moja ambayo nayo inatawaliwa na wataalamu wabara-hindi wengi tu!) ambazo tunaziacha kapuni kwa leo!
Zain, Zanzibar Telecom zina zaidi ya wataaalmu wageni 20, wengine vijana barobaro wa miaka 20 tuu!
(inaendelea...)
(...inaendelea)
ReplyDeleteHebu tazama hapa kwa mameneja utawala/Rasilmali Watu katika makampuni yetu leo hii:
Tigo – Head of HR [Mkenya]
Barclays – Head of HR [Mkenya]
Barclays – HR Ops Manager [Mkenya]
Na wengine:
Zantel – HR Planning Director [Mu-Irish]
Zantel – HR Admin Director [Mu-Irish]
Kenya Commercial Bank – HR Manager [Mkenya]
Ni wazi kwangu kuwa huu ni uthibitisho tosha kuwa BOT na Mamlaka Ithibati zinginewe wameshindwa kudhibiti kabisa jambo hili. Hivyo sote tunahitaji kulikemea ili nao waamke mwenye usingizi wa pono wanaokoroma hivi sasa.
Hebu thubutu kwenda Kenya ukaombe nafasi mojawapo ya hizo uone kama ‘Banki Kuu ya Kenya’ – CBK watakupa kwa namna yoyote kibali (permit) cha kazi kwayo.
Pia wana-habari wetu wajitahidi zaidi na zaidi kufanya ujasusi-habari (investigative journalism) katika masuala yote si EPA na Richmond pekee. Wanasiasa pia wawe mbele kama sauti ya jamii tuiweke nchi na maslahi yetu kwanza na mengine yoote ndo yafuatie.
Sasa, ndugu zanguni, wazalendo wenzangu wa nchi hii, ndo kusema kazi kama ya Rasilmali watu, huduma kwa wateja, mauzo. Ni mawazo yangu na nna uhakika yana usahihi kuwa ruhusa (work permits) kwa wataalamu wageni ni pale ambapo taaluma husika ni adimu (rare profession).
(inaendelea...)
(...inaendelea)
ReplyDeletePia ni wazi maendeleo ya nchi hasa yanayoletwa na uchumi wa ndani, yanategemea sana kukua kwa kipato cha tabaka la kati (middle class). Ambalo mara nyingi hujengwa na wafanyabiashara na mameneja wa kati na wa juu. Fikiria kama nafasi hizi zimeshikwa na wabongo wanapotaka kujenga nyumba wanaajiri wabongo wengine wangapi? Je wanapoanzisha biashara zao wenyewe pia, wanatoa ajira kwa wangapi nk, nk, nk. Halafu serikali inazungumza kutengeneza ajira milioni 1 wakati mambo kama haya inayafumbia macho? Usipojali vijisenti, mashilingi pia hayatengenea!... UzenG!
wee annon wa 3.11 inaonekana huelewi maana ya lugha ,hatuzungumzii wa2 wa kuendesha mashine (production operators)hao watakuwa wengi tu tukifanya kiswahili kiwe somo la kawaida kwenye shule zetu wapo wa2 wapo hapa UK wakitokea poland indonesia n.k hawa hawana uhusiano na hoja hii,kwani wee unataka kuwa mtumwa mpaka lini?tunaposema kenya wametudizi sio kwa watwana bali mabwana wenye uwezo wa kuanzisha ajira hilo ndo tatizo letu!! lakini na kenya sio wao bali wa2 wa nje ambao wamekuwepo hapo wakati sisi tuna-embrace ujamaa na sio kwamba ujamaa ni mbaya bali tulikosa innovation capacity kwa sababu china ni wajamaa kuliko sisi na wamepeta(lakini kwa kutumia kichina!!)kuna tofauti kubwa kati ya skill na english,wakenya wameishi katika vocational training pamoja na viwanda vyao wakapata skill na sie tulipoteza muda katika
ReplyDeletepolitics ukichanganya na kuto kuwa na viwanda hatukupata skill!!!hivyo mzungu au mwaekezaji akija atataka mkenya kwenye kiwanda chake kuliko we unasema unaelewa wakati hujui.nadhani umenielewa next tym njoo taratbu..
na ni hatari kuubwa kuruhusu wakenya kuchukua position kama za HR. mana ndio zaidi wanaletana wabanane apaapa. bada ya apo anapigiwa ndogondogo aletwe na mkuu wa kifedha toka ukouko, basi mchezo kwishnehi! nsikilizie vitenda voote va ovyo-ovyo zinaenda kwenye vikampuni uchwara va watu wa kwao (watani wa jadi). Na hapo ndio muungano bado, mbona tutashaa. akili mumkichwa wabongo
ReplyDeleteLUGHA YETU YA KISWAHILI NI SAFI SANA!!NI POST CHACHE SANA KTK KAMPUNI ZINAZOITAJI LUGHA!!
ReplyDeleteMIMI NAFANYA KAZI HAPA UHOLANZI MIJITU MINGI HAIJUI LUGHA BUT WANAFANYA KAZI KAMA KAWAIDA,HEBU TUACHE MAWAZO YA KIKOLONI HAPA.
POST CHACHE SANA AMBAZO ZINAITAJI LUGHA KTK TAASISI,UKISOMA MANAGEMENT MTALIJUA HILO.
KWANZA HAO WAGENI WAKITAKA KUJA KUFANYA KAZI KWETU INABIDI WAO NDIO WAJIFUNZE KISWAHILI MAANA WATEJA WALIO WENGI YANI POPULATION KUBWA EAST AFRICA INAZUNGUMZA KISWAHILI.
NI POST CHACHE SANA ZINAZOITAJI LUGHA MFANO ZILE ZENYE DIRECT CONTACT NA WATEJA AMBAZO KWA LUGHA YA KIITAALAM TUNAZIITA FRONT OFFICE