Ummy akiwa na Rosemary Zahoro aliyekuwa wa
tatu (shoto) na Zakia Ramadhani aliyeibuka wa pili.


Ummy Mdolwa (22) mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam UDSM, ameibuka mshindi wa Miss Utalii Vyuo Vikuu Kanda ya Mashariki 2009 baada ya kuwabwaga wanavyuo wenzake katika onyesho lililofanyika katika ukumbi wa Rainbow uliopo mbezi Beach, Dar usiku wa kuamkia leo.


Katika shindano hilo nafasi ya pili ilikwenda pia kwa kwa mshiriki kutoka katika chuo cha UDSM,Zakia Ramadhan(21) huku nafasi ya tatu ikitwaliwa na mshiriki kutoka katika chuo cha IFM, Rosemary Zahoro(22), huku nafasi ya nne ikichukuliwa na mshiriki kutoka katika chuo cha CBE, Mary Guma(21) na nafasi ya tano ilikwenda kwa Fariji Mansosa (22)wa Chuo cha UDSM.


Jumla ya washiriki 8 walipanda katika jukwaa moja kutoka vyuo mbalimbali vya Tanzania, ambapo washiriki wengine ni Beatrice Shayo(23) kutoka katika Chuo cha Tsj, na Angela Consitatine (21)kutoka katika Chuo cha UDSM, Grace Lucas (22 )kutoka katika chuo cha IFM, na Faraji Mansosa(22) kutoka katika chuo cha UDSM.




Mashindano ya Miss Utalii Vyuo Vikuu kanda ya mashariki 2009, yalilenga kumtafuta mrembo halisi wa Kitanzania kutoka Vyuo Vikuu Mbalimbali Nchini Tanzania kwa mwaka huu wa 2009.




Shindano hilo liliandaliwa na Victoria Leonard (Miss Utalii Vyuo Vikuu Kanda ya Mashariki 2008) ambapo hapo awali jumla ya Warembo 12 walitarajiwa kupanda jukwaani kuwania Taji la Umalkia wa Vyuo Vikuu Kanda ya Mashariki.




Warembo waliochuana vikali jukwaani kuwania taji hilo ni pamoja na Angel Constantine, Fariji Msosa, Beatrice Shayo, Grace Lucas, Mary Guma, Rosemery Zahoro, Ummy Mdolwa, na Zakia Ramadhani.mshindi wa Kwanza alizawadiwa mfano wa Hund yenye thamani ya Tsh za 1,500,000/= ikiwa ni pamoja na kusomeshwa kozi ya Komputer katika chuo cha Zoom POLYTECHNIQUE, sambamba na kupatiwa vipodozi asilia kutoka duka la Moringa Enterprices.




Mshindi wa pili alipata zawadi yenye thamani ya Tsh ,milioni moja 1,000,000/= na vipodozi asilia kutoka Moringa. Zawadi ya mshindi wa tatu ni Tsh 800,000 na vipodozi kutoka Moringa. Zawadi kwa mshindi wa nne na tano walipata zawadi zenye thamani ya tsh 500,000/= kila mmoja na vipodozi asilia kutoka Moringa.




Washiriki wengine walipewa kifuta jasho cha shilingi laki mbili 200,000/= kila mmoja.Naye Rais wa mashindano ya Miss Utalii Tanzania Gidion Chipungahelo mara baada ya Onyesho hilo alisema kuwa, waandaaji wa Miss Utalii Vyuo Vikuu kanda ya mashariki wamepewa motisha ya kupeleka warembo watano na Yule wa kipaji katika Fainal za Miss Utalii Tanzania kutokana na kuwa wa kwanza kufanya Onesho hilo.




Onyesho hilo la Miss Utalii Vyuo Vikuu kanda ya Mashariki kwa mwaka 2009 lilidhaminiwa na Rambow Social Club, Tigo , Image Media, MM Sign Marker, Zoom Polytechnique College, Moringa Enterprises, Auckland Tours &Safari, Savior Tanzania Limited, X-mation, River Side Bar, na Panasonic.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. siongelei bifu wala u-hater binti aloshinda ana sura nzito lol?!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...