Kaka Michuzi,
Jana (Jumapili) vikundi vitatu vya mazoezi ya viungo vya KITAMBINOMA, MAZIZIZINI BEACH EXCERCISE GROUP NA KATA PRESHA vilishirikiana kufanya mazoezi ya pamoja ya viungo katika kijiji cha Kizimkazi ( a.k.a kijiji cha Pomboo, Dolphin), kama kilomita 50 kusini mwa Zbar town.
Lengo kuu ilikuwa ni kuwahamasisha wanachi wa vijijini kufanya mazoezi kwa ajili ya afya zao. Uhamasishaji kama huo ulifanyika Nungwi (kilomita 55 kaskazini mwa Zbar town) na wananchi wameshaanzisha kikundi chao huko. Mipango pia iko mbioni kwenda Chwaka na Maeneo mengine ya vijijini.
Kuna zaidi ya vikundi 15 vya mazoezi mjini znz hasa katika funkwe za Ngazimia na KizingoPicha hizi zinaonyesha jinsi mazoezi yalivyokuwa jana. Napenda kuwasilisha,
Mdau Zenjibar
Well done Michu, zoezi lilikuwa bomba sana, tulie enjoy mno, na wanachi walijitokeza kwa wingi kutusikiliza
ReplyDelete