Kwako kaka Issa,
Sema mkubwa habari za leo, pole na Swaumu kaka nimekutumia email hii uniweke hewani kwa wadau na mimi nimeingia kwenye libenekekaka.
watu wakitembelea humu watapata kujua mambo mbali mbali kuhusu mimi na RJ Company Tanzania kwa ujumla na masalwa ya moviesindustrie.ukiwa kama kiongozi kaka nachukua fursa hii kukuomba uitangaze kaka. www.raythemostgreat.blogspot.com
Wako Mtiifu.
Vincent Kigosi
(Ray the most great)
-------------------------------------------------------------
Globu ya Jamii inatoa pongezi za dhati kwako Ray kwa kuanzisha libeneke hili ambalo ni mfano wa kuigwa.
Aidha, ingependeza zaidi wengine wa fani zingine wakafuatia ili tupate radha tofauti za libeneke na sio kila mdau analeta libeneke la habari badala ya fani aliyoizoea ama anayoifahamu.
Ray umefanya la maana kujiunga katika libeneke kwani sasa tuna uhakika wa kupata mambo ya filamu kwa mtu aliye ndani ya fani.
Nategemea wacheza mpira, wanariadha, wanamuziki, waalimu (au walimu??), wana habari, madaktari n.k. wataanzisha libeneke ili tuwe na uwanda mkubwa wa kujidai maana kuna pengo kubwa katika nyanja hizo na nyinginezo.
-Michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. jamani mbona hiki kiingereza kinatia aibu? the "most great?" seriously? hivi hakuna mtu hata wa form six anayefanya kazi kwenye hizi studio zetu??

    ReplyDelete
  2. michu umegeuzwa mgongo sasa kila anayetaka tuione globu yake anapandia mgongoni kwako. jamani ee katangazieni kwenye magazeti. sasa badala ya habari tunakalia kuletewa matangazo ya blogu mpya tu. sa hivi ishakuwa fasheni kila msanii anataka kuwa na blogu na kila msanii lazima apitie hapa michuzi kutangaza. bahati ya mtu msilalie milango wazi jamani aaaargh. kila mtu na kismeti chake mnadhani kufungua blogu ndo kupiga bao ka la michuzi!!! iga ufe!!! haya na nyie nendeni voda mkaombe ufadhili. kuigaiga tu.
    haya yule naye lady jd anatutangazia humu eti tuingie kwenye blog yake tukaone picha za afrika kusini, kila picha aliyopiga kaiweka kwenye blogu kama si ushamba nini??

    ReplyDelete
  3. Ray hongera lakini hapo umekosea kidogo, "the most great" si kiingereza sahihi, "the greatest" ndio ungekuwa umepatia....yaani movie zote hizo kumbe kiingereza is not rechabo...teh teh teh

    ReplyDelete
  4. It suppose to be "the most greatest" and not the most great...wabongo bure kabisa, na movie zenu mnaongea sana bure kabisa, ni ujinga wenu wenyewe.

    kibaki wa kenya

    ReplyDelete
  5. nikiangalia tulipotoka enzi za kina yombayomba na vurugu zake za dar au rashid kawawa a.k.a simba wa vita/muogo mchungu naona tunajitahidi. ila swali langu kwa yoyote litakalomgusa 'kwa nini mnazi-title filamu zenu kwa kiingereza?'

    ReplyDelete
  6. the most great? how about the greatest? huo ung'eng'e jamani - mie hoi

    ReplyDelete
  7. wewe KIBAKI,the most greatest ndio nini?Wewe na huyo ray wote mmekimbia umande

    ReplyDelete
  8. Ngoja ni waambieni siri ya kujitangaza mwenyewe. Sio mngoje kumtumia michuzi huku matangazo ya mitandao kila siku

    Njia rahisi ni kutembelea blog nyingi za bongo halafu uwe unatoa comment zilizoenda shule na usitumie anonymous achia jina la blog yako ...before you know utapata hit kibao....Mimi blog yangu ilijitangaza kwa njia hiyo na repeated reader kibao.

    Kama blog yako ni ya mambo ya maana watu wataingia na kesho watarudi tena for more lakini kama ni ujinga tu, kutangaza leo huku utaona hits kibao lakini watu hawatarudi tena.

    Hivyo kwa watu wanaotaka kujitangaza usitumie anonymous unapotoa comments.

    Mdau wa Kaniitieni

    ReplyDelete
  9. Tukikosoa mnatuita waosha vinywa,potelea mbali na iwe hivyo tu, mimi sijui kuact wala sina kipaji cha usanii wowote kwa hiyo siwezi kumuonea wivu Ray, nasema hivyo makusudi maana ni aibu tupu hiyo blog yake, nia yake ni njema lakini mtu kama lugha ya watu huiwezi si utumie tu kiswahili chako utaeleweka? sasa mtu anaenda kuandika eti Ray the most great manake nini kiingereza sahihi kingekuwa "Ray the most greatest" au badilisha kabisa andika "Ray the great", halafu eti msanii mzima anaandika neno Entertainment eti Enterntiment, especially anaandika expecial na msiniambie ni spelling error hakuna kitu kama hicho, jamani chekini hata spelling ni za bure kwenye mtandao! Halafu hiyo title ya Ray sijui the great una ugreat gani Ray, wewe kama kijana unamchango gani kwa vijana wenzenu? unasema the great kwa kitu gani haswa, kazi kuzungukana tu wasanii nyie wala hamuogopi ukimwi. Anzeni kujifunza toka kwa wenzenu Bollywood na Hollywood hata South Africa kuwa wanafanyaje kazi ili achaneni na hayo mapopo hawajui kitu ili mfike mbali, pia acheni kujipa matitle makubwa yasiyo na kichwa wala mkia, kina Tom cruse, John Travolta, Morgan Freeman, Denzel Washington hawajajiita the greatest hata siku moja na kazi zao ni za standard ya hali ya juu sembuse nyie, acheni hizo bwana. Lugha nzito halafu mnataka majina makubwa si muanze tu kidogo kidogo.
    -Mdau Mnoko.

    ReplyDelete
  10. asante sana mdau mnoko acha iwe mbaya ebu niambie tu hata kina rambo shwaziniga van dame ni wababe kweli kweli kwenye movie lakini hawajawahipatwa na kwi kwi ya kujiita great sijui greatest na walikuwa juu sana uspime nani hamjui rambo? sasa watu wengine na ngojera zao wanazoziita movie wanajipa majina makuuubwa kwa kipi haswa??? au kwa vile mnauza sura kwenye magazeti ya udaku basi ndo wee tayari nyie ni moto wa kuotea mbali kujipa maujiko ni ishara ya kutojiamini by the way katika hayo maigizo yenu walau kanumba yuko bora zaidi yako ni hayo tu
    miss michuzi

    ReplyDelete
  11. Kujua kiingereza sio ndio kila kitu, kuna nchi kama japan unakuta profesa hata kiingerza cha kuombea maji hamna lakini anaheshimika na kufanya mambo makubwa,so dont judge the guy by such'COMMON MISTAKES' He is better-off than most of you stinking mouths.

    ReplyDelete
  12. Wewe anony wa sept.6,2:41PM Japan ni nchi ambayo haihitaji kiingereza ili kupata maendeleo, upo hapo, imejitosheleza vya kutosha kuliko, pili sio kuwa hawajui kiingereza ni wamechagua kwa hiari yao kutojifunza hiyo lugha cause it makes no difference kwenye maisha yao, lakini Ray anahitaji kiingereza penda asipende, yuko kwenye nchi ambayo bila hiyo lugha aendako atakwama, system yetu ya elimu siku hizi ni ya kiingereza TZ kwa hiyo he has no choice, tatu anakuwa judged kwa ignorance yake ya kung'ang'ania lugha asiyoijua na sio kwa kutoijua, hana haja ya kujifunza ila kama msanii wa Tz anayetegemea ku exhale kupitia vyombo vya nje lazima ajue hiyo lugha na ni aibu kuwa hata kile tu cha kumbaru hajui, acheni hoja za mbona wachina, wajapan na wakorea hawajui kiingereza na wako mbali, kwa taarifa zenu hawaitaji hicho kiingereza they are far advanced na hata nchi kama UK na USA zinawategemea kwa mambo mengi, kwa hiyo usidanganye wabongo eti sio lazima kujua kiingereza, kwa wabongo kiingereza badoo ni muhimu kwa sasa kwa maendeleo yao period.
    -Mdau Mnoko.

    ReplyDelete
  13. Wewe mnoko mbona hata wewe hujui kiingereza wala kiswahili, mbona sisi hatupigi mayowe kama yako? Ili kuagua hilo soma uzuri ujumbe wako.

    ReplyDelete
  14. Sasa mnoko umezidisha,

    lengo la lugha ni kuwasiliana, kama umepata ujumbe yatosha. sio kuonyesha umahiri kama mtaalamu wa lugha, kama hukuelewa vizuri hapo sawa lugha imepotoshwa lakini kwa sababu ulirekebisha naamini ulimpata Ray. Vilevile lugha ya kiingereza sio njia ya kupata maendeleo kwa hiyo usihusishe maendeleo ya Japani au china na uhitaji wao wa lugha ya kiingereza. mahitaji ya lugha kwa mtanzania, mjapani, mchina n.k. ni sawa na haijalishi uko katika kiwango gani cha maendeleo. hata tukijua hii lugha maendeleo yetu bado yanaweza kuwa duni tu, kwa msanii kama Ray anaweza kufanikiwa endapo ataweza kufikisha ujumbe kwa kiingereza, kifaransa, Kiankole, kisukuma na lugha nyenginezo za Africa/Kihindi/Kiarabu ikiwemo Kiswahili. inategemea wapi ameweka mitego yake ya kujipatia mapato.

    ReplyDelete
  15. wewe anoni wa sept 7, @:52PM sasa mnoko kakosea wapi, mbona lugha inaeleweka kabisa, watu wengine bwana sijui ni ulimbukeni au ni nini!

    ReplyDelete
  16. Kwani hizo Fake Pastor aliandikiwa na nani? Ndo maana watu wengi wakitoa maoni juu ya filamu za Bongo Watu tunawaona wanonko, wana haki zote kusema hivyo. KWANINI Watu mzipe Filamu zenu majina ya kingereza? Wakati mkingali chekechea. Nenda shule kwanza pitieni kazi zenu kwa ufasaha ndo mje mwende kwa lugha za wenzetu. Kuwa wazalendo kwa Lugha zenu kama hamuwezi za wengine mnaigaiaga nini! Kababy

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...