Hi Kaka Michu!!
Ni long time sijakupa updates ila leo ipo hii:
Nipo Mkoani Iringa, na moja ya maeneo ninayoyatembelea ni vijijini.
Kuna kijiji kimoja kinaitwa Mpanga Tazara, kijiji hicho awali ilikuwa unaweza kufika kwa treni tu. Hakukuwa na barabara kabisa mpaka hivi majuzi tu ilipojengwa na kupatiwa ufumbuzi. Na kwa mara ya kwanza wananchi wa kijiji hicho gari ya kwanza kuiona maishani mwao ilikuwa ni gari ya mkurugenzi. Yaani amini usiamini almost tangu uhuru! Wanakijiji wa hapo kwa ujumla ilibidi waje kuishangaa na kuigusa gari ya Mkurugenzi.Binafsi nilipatwa na butwaa, ila habari ndio hiyo.
Good day.
Mdau JM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. hii ni ajabu kweli. serikali mbili za karibuni ndio zime wastaarabisha hao watu. kama sio hizi serikali za awamu ya tatu na nne hao watu wasingeona gari maishani mwao.

    ReplyDelete
  2. WACHA HIZO!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  3. DU! hi ni kali,miaka yote toka gari ziingie tz!Hi maana yake nini? Huduma muhimu za kijamii zipo kweli huko?

    ReplyDelete
  4. Mhmmm.....mdau wa kwanza hapo umenikumbusha hali ya mpanga Tazara, inabidi nipange kwenda kupaona mahali hapo. Yaani ninakumbuka mwezi wa pili mwaka huu nilikuwa ninafanya needs assessment ya dispensaries zote za wilaya ya mufindi, mpanga Tanzara peke yake ndo nilishindwa kuifikia maana kulikuwa hakuna barabara (ndi ilikuwa inajengwa kutokea kijiji cha isipii) na treni ya tazara yenyewe ni shida tu. Yaani kule hata dawa za hospitali kuzipata ni taabu kweli. Hongera sana serikali na mkurugenzi wa wilaya husika bwana Shimwela Limbakisye.

    ReplyDelete
  5. Usishangae ndugu yangu. Ninakumbuka mwezi Juni 1984 nilifika Gaborone pale hoteli ya President kumbe ndiyo ilikuwa siku taa za barabarani za kwanza zimewekwa na zilikuwa zinafanyiwa commissioning. Huku Tz twaziita traffic lights lakini wenyewe wazungu wa south wanaziita robots. Nilikuwa nimeongozana na jamaa yangu Balozi Mpungwe. Tulishangaa kama wewe ulivyoshangaa tulipokuta mji mzima upo pale na wao wakishangaa hizo robots. Na hasa pale zilipokuwa zinazuia magari yasipite na wao ndiyo wapite. Kwa kweli ilikuwa burudani tosha. Hiyo ilikuwa mwaka 1984. Nilipoenda miaka mitano baadaye uchumi ulikuwa umeshika kasi hakuna aliyekuwa anashangaa tena.

    ReplyDelete
  6. Ndio maana nchi zingine zingine zinatushangaa mipango yetu ya maendeleo ilivyokosa vipaumbele vya maana.

    ReplyDelete
  7. Hii story haijatulia, ina maana hao wanakijiji hawakuona gari ya surveyor aliyekuja kupima barabara itapita wapi? au naye alienda na pikipiki..!!

    ReplyDelete
  8. sasa kaka unayetupa story nikuulize ina maana barabara zao zilijengwa kwa matako kama si magari makubwa.story zingine kazitolee chumbani kwenu wala hatujaizimia.maeneo mengi watanzania wameendelea kwa sasa usiwafanye wehu kiasi hicho alah! sisi tuko nje lakini tunaipenda nchi yetu!

    ReplyDelete
  9. sasa kaka unayetupa story nikuulize ina maana barabara zao zilijengwa kwa matako kama si magari makubwa.story zingine kazitolee chumbani kwenu wala hatujaizimia.maeneo mengi watanzania wameendelea kwa sasa usiwafanye wehu kiasi hicho alah! sisi tuko nje lakini tunaipenda nchi yetu!

    ReplyDelete
  10. Acha usanii wewe, hiyo barabara imetengenezwa na jembe la mkono? Kabla hujatoa fix zako, soma kwanza mwenyewe ulichoandika!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...