Mkuu wa udhamini na Mawasiliano wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania George Rwehumbiza(kushoto)akimkabidhi Cameron Mckee kombe baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika mashindano ya mashua ya Vodacom Laser open,yaliyofanyika katika fukwe za bahari ya Hindi jijini Dar wikiendi hii.
Meneja mtendaji wa Teknologia mpya wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Dylan Lennox (kushoto) akimkabidhi mshindi wa kwanza kwa watoto Peter Van kikombe baada ya kuibuka mshindi wa kwanza kwa watoto katika mashindano ya mashua ya Vodacom Laser open,yaliyofanyika katika fukwe za bahari ya Hindi jijini Dar.

Mkuu wa udhamini na Mawasiliano wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania George Rwehumbiza(kushoto)akimkabidhi Don White kombe baada ya kuibuka mshindi wa pili katika mashindano ya mashua ya Vodacom Laser open,yaliyofanyika katika fukwe za bahari ya Hindi jijini Dares Salaam.(katikati)Meneja huduma na bidhaa wa Vodacom Tanzania Elihuruma Ngowi.
Meneja huduma na bidhaa wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Elihuruma Ngowi akimkabidhi Peter Van kikombe cha ushindi wa tatu katika mashindano ya mashua ya Vodacom Laser open,yaliyofanyika katika fukwe za bahari ya Hindi jijini Dares Salaam.

Baadhi ya washiriki wa mbio za mashua za Vodacom Laser open wakichuana vikali katika mashindano hayo yaliyofanyika fukwe za bahari ya Hindi jijini Dares Salaam.

Mmoja wa washiriki wa mashindano ya mashua ya Vodacom Laser open akishiriki ipasavyo katika mashindano hayo yaliyofanyika fukwe za bahari ya Hindi jijini Dar.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ebana maji ya bahari ya hindi yanaonekana mazuri kuliko bahari ya Atlantiki.Kila nikienda fukwe za Atlantic City hamu ya kuogelea inakwisha sababu mimaji inaonekana michafuuuuuuuu.Malimbukeni mtapinga.

    ReplyDelete
  2. MBONA WASHINDI WOTE WAZUNGU! WABONGO TUNAOGOPA MAJI AU VIKOMBE.

    ReplyDelete
  3. Wabongo kazi kuchonga lakini kushiriki international sports no. Angalieni wenzetu kwa mzee kibaki wao hata michezo ya barafu wamo though sisi tuna Kilimanjaro barafu juu. Tuwe wavumbuzi badala ya kulalama tutaishiaga kuishangaa nchi ndogo kama Rwanda huku sisi milioni 50 blablablaaaaaa tuu. Ndio maana tunaogopa hata EAC kwani wenzetu watafanya kweli na sisi tutaishia kunywa bia walio na centi na vijana wetu wataishia kukaa vijiweni bila kazi na elimu 24/7. Umbea na kujifanya tunajua sana kuongea kutaimaliza nchi jamani tufanye vitendo vyenye outcome ya kutupeleka mbele na kuiweka nchi yetu katika ramani na kuitangaza kwa faida ya leo na vizazi vijavyo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...