Kaka habari za kazi,
Mimi ni swali moja naomba msaada watu wanipe ushauri wenu tafadhali sana.
Ni hivi, mie bwana nina mwanaume ambaye nampenda sana, nahisi na yeye ananipenda pia, lakini nimengundua kuwa alikuwa ameoa lakini yeye alikuwa hajawai kuniambia chochote kuhusu kuoa, ila nimengundua mwenyewe.
Sasa swali ni je, nimuache au niendelee naye? lakini kwa sasa najua hawapo pamoja tena.. ila kinachoniuma ni kwamba mbona alinificha siku zote mpaka mimi mwenyewe ndio nimengundua.
Asante sana-
Naomba ushauri wenu wadau
Mary
Mleta maoni ni mwanamume, sasa hapo itashindikana kwa baadhi yetu kutowa ushauri nini afanye lakini asante kwa kuleta maoni yako naimani wapo wenye fani hiyo wataweza kukujibu
ReplyDeleteBy :Abubakar bin sadiQ
Wewe kama hili swali kama lilikuwa muhimu sana kwako mbona hukumuuliza?
ReplyDeleteKama ungemuuliza na akakwambia kuwa hajaoa, halafu uje kugundua kuwa ameoa hapo ndio issue.
Hebu acha kizabinazabina na utulie. Labda mwenzako alikuwa hataki kuongelea past, anaangalia mambo ya future wewe unaanza zako za kuleta
Kama ulivyosema hapo awali kabisa kuwa wewe ni BWANA na una mwanaume, katika misingi ya utamaduni wetu na dini zetu, mwanaume haruhusiwi kuwa na mume, sasa cha msingi achana naye na umrudie mola wako.
ReplyDeleteEndelea naye kwani alikuwa na nia nzuri kwa sababu asingeweza kukwambia kwani huenda hukumwonyesha kuwa wewe ni wa kudumu.
ReplyDeleteAcha ushamba dada kwani unga wenyewe robo alafu ni saa sita mchana shauri yako. leta mchezo ukutane na mwenye wake wawili na vimada kama nyinyi 9
ReplyDeleteIna maana ktk matatizo yako yooooote hili ndio umeliona kubwa?na je umekosa kero yako kwa wanajamii wakaitatua ukaiona hii ndio kero kubwa kabisa kuliko zote na wadau wakupe atensheni kwa kushea kero yako hii pamoja na wewe?ukitukaniwa mzazi wako kwa bahati mbaya je utaona umeonewa???MWISHO:ASANTE HII SIO BLOGUMAPENZI
ReplyDeletekwanza inabidi upate kuelewe wameachana kwanini na kwa sababu gani? pili uelewe je ni kwa nini hakukueleza anaye mke kwa mara ya kwanza, tatu je anakimada tena mwingine za wewe?
ReplyDeletenne je anampango gani wa ziada na wewe zaidi ya mhhhh!!!....?
Tano click mawazoni kwako uwe na uchaguzi wa kusuka au kunyoa.
"Mali ya wizi ni matamu sana; mkate unaoliwa kwa siri ni mzuri sana." Lakini mjinga au mpotevu hajui kwamba humo mna wafu, wageni wa mwanamke/mme huyo wamo chini Kuzimu.
ReplyDeletewe binti fulani wa fulani, usisahau kwamba penye maneno mengi hapakosekani makosa, lakini anyeuzuia ulimu wake ana busara.
walengaulenge husema, "It takes two to tango, and you are not as innocent as you would like the public to believe."
re: mdau 'anonymous 12:34:00 am' alivyosema "...huenda hukumwanyeshe kuwa wewe ni wa kudumu" and that is why he saw no need for full disclosure because you may have seemed to a "passing cloud" in his life.
KAMA NI MUISLAMU OMBA UKE WEZA, KAMA NI MKRISTU UNAWEZA KUWA NYUMBA NDOGO UKIPENDA. KAMA UNTAKA KUOLEWA TAFUTA MWINGINE. KAMA UNATAKA AMTALIKI MKEWE ONGEA NAYE.
ReplyDeleteHukuuliza bibi we naye hakutaka kukuogopesha mapema mana kama mwanadamu anajua si rahisi watu kuelewa mambo ya talaka na nini.Kama ni mwaminifu kwako na kakupa sababu nzuri za kuto kwambia mapema muelewane mjue yanakalia vepe.Ila kama kigugumizi na we roho yako yasita haina amani nini kujikondesha.Kwa ufahamu wangu wewe kuuliuza hapa nafsi yako inakataa kabisa kuendelea naye ila unawaza nitakuwa single ngoja tu nijiendeleze.Mie huwa nafanya hivi nikiona najiuliza watu kutaka ushauri juu ya mtu nampenda sababu binafsi cna hakika, nasema hakuna haja kuendelea mana sina amani moyoni na sina hakika.Deep down najua swala ya yeye kuoa unapingana nalo so mkasi huooooooo,kusuka au kunyoa bibie wote urembo tu.
ReplyDeleteAnaye omba ushauri ni mwanamke jamani,ila kaongea ile kiongezi sauti mie bwana kumaanisha mimi nina sio yeye ni jinsia ya kiume na anampenda mwanaume.Nilielewa hivyo mara ya kwanza ila kusoma kwa ufasha nikakundua mie bwana ni muhemo tu sio vile
ReplyDeleteMbona naona kama hilo ni tatizo dogo sana?kama alikuwa na mwanamke akaachana naye kwan kuna noma gan?Wenzako hawaangalii hata kama ameoa anakwenda nae sasa wewe huyo aliyeoa akaacha ndio inakua hoja?Halafu umeshasema hapo unampenda sasa hata tukikuambia uachane nae utaweza?We jaribu kususa kama wengine hawajala.Watu sasa hivi wanaangalia maisha sio mambo ya majungu.
ReplyDeleteUnampenda??Hapana wewe unamtamani. Tumia macho ya kiroho. Huyo hakufai muwache. Huo sio upendo. Nakushauri uokoke ndipo utapata macho ya kiroho na huyo Bwana utaona hafai hafai. Bwana Asifiwe.Tafuta mwanaume aliyeokoka.
ReplyDeleteMhh sina uhakika. Lakini kwanini alikudanganya? Alitaka kukufanya mke wa pili au? Je amezaa na huyo mwanamke? Na kwanini ameachana nae au amefariki???? Ulipogundua ulifanyaje, ulimwacha? Tafakari hayo then uamue.
ReplyDeleteusimuoe wala nini, mpikie nyama ale tuu
ReplyDeleteWe mshamba,kwani unaona noma hiyo?? kwani kama hujagombana naye kuishi ni nini ?kaa unajua kuishi kwa mke na mume ni upendo wa kudumu,sio yakukaa unakagua yaliyopita,,hivi wewe akikuangalia hawezi kupata habali za jinsi ulivyokua ukipigwa mchuma na watu wengine?au ulifika kwake ukiwa bado bikila?tuliza manyoya wewe,
ReplyDeletefanya uchunguzi zaidi,mtafute mke wake umuulize ,una uhakika wameeachana wewe?usicheze na waume wa watu wewe,utaokota makopo barabarani wewe,hujui wametoka wapi wewe
ReplyDeleteHivi kwa mtazmo wako unadhani kama anakupenda ndo atakueleza kila kitu? we kama uligundua hilo ungepaswa kuuliiza au kama vipi,mteme tu huyo hana maana.
ReplyDeleteMAMBO YA MUGIDEZ MUGIDEZ SIYO? NIMESHUHUDIA TUKIO LA BWANA MMOJA KUMUACHA MKE WAKE TANZANIA AKIWA MJA MZITO AKAMUOA ILI APATE VYETI VYA KUCLAIM ALLOWANCE YA FAMILIA CHUONI MWAKE. ALIPOFIKA HUKO AKAKATA MAWASILIANO NA FAMILIA YAKE KABISA. HATUMI HELA NA ANATANUA NA WAREMBO KAMA WEWE. MKEWE AMEJIFUNGUA ANAJIDAI HANA HABARI.
ReplyDeleteNAONA NI HUYO BWANA. NI MUONGO SANA. ANASURA NA HADITHI ZA KUDANGANYA SANA. BWANA INAWEZEKANA SANA AMEMUACHA MKE WAKE AKIWA MJA MZITO NA HATAKI KABISA KUMHUDUMIA WALA KUMTAMBUA MTOTO KWA SABABU YA UBAHILI.
HUYU JAMAA ANAPENDA STAREHE NA ANACHOKIFANYA NI KUPIGA SIMU KWA WATU TZ NA KUWATAMBIA VILE AMBAVYO ANALALA NA VIATU ULAYA KWA KUWA HAKUNA VUMBI. SIJUI LAKINI ASIKUTUMIE KUMKOMOA MKE WAKE WALA HANA JIPYA.
HUYU JAMAA ATAKUWA MWANAFUNZI AMBAYE HUENDA YUKO NG'AMBO ANASOMA NA HAZUNGUMZII SANA FAMILIA YAKE YAANI UKOO WAKE AKIWA NA WEWE.
DADA KAA CHONJO HUYO NI MUME WA MTU-MCHUNGUZE-TANGU LINI ALICHOUNGANISHA MUNGU BINADAMU AKATENGANISHA?
UKO MZURI KWANINI USITULIE UTAFUTWE? CHUNGUZA CHANZO CHA JAMAA KUACHANA NA MKE WAKE? KWA WATU WANAOMFAHAMU KWENYE FACEBOOK ETC. SIYO KILA KINGAACHO NI DHAHABU DADA MARY.
ushauri wangu; kama unampenda ukweli endelea naye na Mungu atakusaidia mtaoana na mtakuwa na maisha mzuri ya ndoa yenye furaha tele. Nasema hivo kwa sababu kuna watu wana historia mbaya hata zaidi ya hiyo, kuoa na kuacha kitu gani bwana? what if unasikia mtu uliye naye ana scandal za kuwa shoga? au ni victim wa HIV au aliwahi kubaka?
ReplyDelete