Siku ya leo imekuwa ni siku ya furaha kubwa kwangu kama shabiki wa miziki ya nyumbani nilipoona CD ya mwanamuziki wetu wa Kibongo Jhiko Manyika (JhikoMan, pichani) ikiuzwa kwenye duka linaloheshimika sana huku Scandinavia (Stockman).
Bila shaka kwa wanaolifahamu duka hilo, huwezi kuingiza bidhaa yoyote ambayo haijakidhi viwango vya kimataifa, na kwa kuona CD ya ndugu yetu na mbongo mwenzetu ndani ya Stockman, bila shaka muziki wetu na wasanii wetu wameanza kukubalika na wanahitaji pongezi.
Hongera sana Jhiko kwa kutuwakilisha.
Mdau (Helsinki-Finland)
Mdau (Helsinki-Finland)
mbona wivu hiyo "ZANZIBARA" hujaiona hapo?! mbona huifagilii?
ReplyDeleteHongera sana Jhikoman,kwa duka kama hilo kama kiwango cha muziki wake ni cha chini kamwe wasingeuza c-d zake.Hii ni uthibitisho tosha muziki wa Jhikoman huko juu sana.
ReplyDeleteMdau ndoto ya mchana Sweden.
Ishu sio kuwa kwenye market, ishu ni kununuliwa hizo cd, wewe mfagiliaji umenunua moja, au unafagilia tu?. Na hapo stockman kwenye sekshen ya world music kuna cd kibao za wasanii wa kibongo sio jhiko peke yake.
ReplyDeleteWee anony acha ushamba na roho mbaya. Kama kuna kazi za wasanii wengine, mbona hujapiga picha na kuiweka humu?
ReplyDeleteKatika capitalism huwezi kuweka bidhaa isiyonunuliwa kwenye duka, ukiona kazi ya msanii imo kwenye duka lenye jina kama hilo, basi ujue kiwango chake kinakubalika.
Hongera sana Jhiko. Cha kushangaza mbona wanamuziki wanaoshinda kwenye front pages zetu hawaonekani hivyo ughaibuni?
ReplyDeleteKwani Zanzibara msaniii? JhikoMam msanii na ndio lengo la mdau kumfagilia.
ReplyDeleteHakiwezi kuwa kwenye duka kama Stockhman kama kazi ingekuwa ina kiwango cha chini.Wewe unayesema kuna kazi kibao za wasanii wa kibongo,ni nani hao,wataje.Jhikoman anaperform mara kwa mara kwenye matamasha makubwa huku Ulaya,na sio anakuja kuwapigia tu jumuiya ya WaTanzania kama wasanii wengi wanavyofanya.Ana washabiki wengi huku/audience ya mataifa mengi tu.
ReplyDeleteApewe pongezi zake zinazostahili kwa kufikia kiwango hicho.
Huu ni mfano kama marehemu Hukwe Zawose wakati dunia inamtambua kwa muziki wake daima amepewa heshima yake na mchango wake umetambuliwa kidogo sana.Lini wabongo tutawapenda na kuwapongeza wasanii wetu?
Michu,
ReplyDeletetafwadhalii Shekhe tuondolee huu mzizi wa fitna kwa kutuwekea angalau 'clip' ya video moja ya Jhikoman hapa ndani ya bulogu ya jamii, maana kwa Kanumba ushaondoa fitna bin fitina.
amasivyo mzizi huu wa fitna utakua na kuwa 'liji-Mbuyu'.
Mdau
Swalihina
salamu mkuu nimefurahi kuona jina la nchi yangu na sio mkoa ZANZIBAR.
ReplyDeleteAnony hapo juu tafuta mawani, kwani maandishi ya CD hiyo yameandikwa Zanzibara ambayo sina hakika inamaanisha Zanzibar. Kama ilivyo tofauti kubwa kati ya Dar-es-salaam (Tanzania) na Dar-us-salaam (Brunei).
ReplyDelete