Rais wa Kenya Mh. Mwai Kibaki (kulia) akiwa na Waziri Mkuun Mizengo Pinda naWaziri wa Ushirikiano wa Afrika wa Mashariki, Dr. Diodorous Kamala kabla ya mazungumzo yao jijini Nairobi leo.Mheshimiwa Pinda yuko Kenya kwa ziara ya kikazi ya siku mbili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. wewe ni buure kabisa lol

    ReplyDelete
  2. Mheshimiwa Kamala wewe ni Waziri miaka minne sasa unashindwa hata kununua shati zuri litakaloweza kuibeba tai yako. Sasa angalia hiyo tai haikai vizuri shingoni kwa sababu shati linabana. Wewe ni Waziri bwana be smart please. Humwoni Rais wako alivyo smart na anavyopendeza.Sasa angalia hiyo picha Waziri Mkuu na Rais Kibaki wamependeza ila wewe.

    ReplyDelete
  3. Jadilini mambo ya msingi kwamba hapo Wakenya wanatulengesha ili watuibie na kutuvurugia amani, basi hakuna la zaidi.

    Suti, shati na tai si vitu vya kujadili kama hujui uvaaji na mitindo yake. Suti ya Mwai ni English suit na amefunga tai English style na shati lake ni conservative style. PM wetu hivyo hivyo ila suti ni American style. Kamala suti yake ni Italian, suit amefunga mtindo unaofanana na American style na hilo shati ni mtindo wa kisasa wenye kola iliyotawanyika. Tatizo ni kwamba alitakiwa kufunga fundo la Kiingereza (Ulaya style) lakini kwenye tai pana zaidi ya hiyo. Click hiyo picha utaona shati siyo dogo, ila kola imeacha nafasi kwa kuwa ilitengenezwa kwa ajili ya tai pana za kisasa ambazo siyo conservative.

    Wasalaam, usirukie kutoa maoni bila kujua unachosema.

    ReplyDelete
  4. Akiwa masomoni Makerere College, Mwai Kibaki (Kenya) na Abu Mayanja (Uganda) walikuwa wakiongoza darasani kwa akili!

    ReplyDelete
  5. Nani Handsome kuliko wote hapo juu?? Of course Pinda Kwa kwa kwaa.

    ReplyDelete
  6. Mjomba mmoja hapo anasema tusijadili nguo halafu anatoa somo refu la mifundo ya tai za aina suti. Sijui Shayo huyo?

    ReplyDelete
  7. Dr??? alisoma wapi na kupewa na nani? isijekuwa ni sawa na waganga wa jadi wanaoitwa Prof!!!!

    ReplyDelete
  8. Wewe Anon wa 09:58 hueleweki wewe. Nilitegemea uliponiambia nijadili mambo ya msingi wewe ndiye ungeleta majadala wa hayo mambo ya msingi. Matokeo yake na wewe umezungumzia habari ya nguo. Kwa hiyo??!!! Waziri is dressed improperly. Huo ndiyo msimamo wangu. English no English/American no American. He is a poor dresser. Sorry but he should improve his wardrobe. Hakuna ufisadi kuwa smart Bwana.

    ReplyDelete
  9. Duh! kumbe Pinda akienda kenya ndo anakuwa hendisamu wao!

    ReplyDelete
  10. Nilisoma na Mnaijeria mmoja aliyekuwa bonge la exhibitionist/impressionist. Kila siku alikuwa akija darasani anavaa suti na tai, anabeba mwamvuli na lather briefcase, halafu alikuwna zile leso za pembe tatu, anavaa long woolen coat na lather shoes zilizong'arishwa vizuri sana. Alikuwa anajaribu sana kuficha lafuhi yake ya KiYoruba kwa kuigiza lafudhi ya upper class stiff upperlips.

    Halafu alikuwa anajua sana jinsi ya kuwakilisha hoja zake darasani. Kama somo limempita kando alikuwa anasema "..I agree with all the motions presented.." Kama somo alikuwa nalijua basi ataanza kuporomosha hoja na kupinga hoja za wengine hata maprofesa mpaka mwisho wa darasa au kozi.

    Tulikuwa na Profesa mmoja mzee sana sana alikuwa anafundisha kwa mkataba maalumu. Siku moja yule profesa sijui alikuwa kaamka vibaya au vipi? Alipokuwa nafundisha yule Mnaijeria akawaanamuingilia ingilia. Yule profesa akamskiliza huku akitikisa kichwa kwamba anakubaliana naye. Manijeria kuona vile akaanza kutoa na mareference ya vitabu vingine alivyowahi kusoma. Alipomaliza yule profesa akamwambia "..Your arguements are as colourful as your outfits but not harmonious at all.. What you said at first was as beautiful as your French coat, on a wrong tied windsor knot on American shirt, in a peculiar English accent..Nothing personal it is just a note to take care of" Profesa akaendelea kutuelewesha wapi Mnaijeria alipokosea hoja zake na kuelezea juu ya vitabu alivyokuwa anatolea reference.

    Kusema kweli kabla ya kasheshe la yule profesa na Mnaijeria hata baada ya kusoma kwa miaka 4 Uingereza nilikuwa sijawahi kujua mavazi ya suti na tai huwa yanapangwa kufuatana na mtiririko maalumu. Mimi nilikuwa nikienda kwenye semina, mikutano au pati navaa koti, shati, tai na viatu vyangu vya ngozi nikishajipulizia perfume naona tayari. Tena nilikuwa na suti zangu tatu na nilikuwa nazivaa katika shughuli yoyote.

    Nilipoanza kazi barua yangu ya kazi pamoja na mambo mengine ikaeleza wazi mavazi tunayotakiwa kuvaa katika shughuli mbali mbali za kiofisi. Human Resources Manager wetu kwenye orientation course alitusisitizia sana suala la personal appearance zetu kwamba ni lazima zirefrect image ya shirika. Malipo ya kwanza niliyolipwa yaliambatana na outfit allowance.

    ReplyDelete
  11. mimi naomba niwe nje ya mada kidogo,nijadili kile nilichokisoma leo ktk gazeti moja la hapo tanzania kuhusu alicho kisema mheshimiwa waziri mkuu mizengo pinda akiwa nchini kenya.
    mheshimiwa pinda amesifu sana GENETICALY MODIFIED FOOD na kusema haoni madhara yake ,ila nii propaganda tu zinazoendeshwa na vyombo vya habari kupinga GMO,akadai hajaona cha ajabu zaidi ya sayansi tu ya kawaida. well mheshimiwa yeye ni mwanasheria na ktk hilo nadhani hajambo,ila anapofika ktk viwanja vya wenyewe basi inapaswa ama aulize wataalam wamueleze nikitu gani kinaendelea.
    kwa ufupi tu sitaeleza kwa kina ni kitu gani huwa kinafanyika ktk kumodify mazao hayo,ila afahamu kwamba huwa ni kubadili tabia ya asili ya zao husika,kwa kubadili gene moja au kadhaa toka sehemu moja hadi nyingine na hivyo kuzalisha product ambayo ni mutant. na kinacho isafirisha gene hiyo kutoka mahali pakr pa asili hadi mahali kupya si kitu kingine zaidi ya virusi au plasmid ambao wanataweza kufanya hivyo. na bila kusahau kwamba virus wanaweza ku undergo mutation na kufanya kile ambacho hakikutarajiwa,ikiwa ni pamoja na kuanza kuingilia baadhi ya mifumo ya utendaji kazi wa mwili wa binadamu ambayo hiyo ni ugonjwa tayari.
    matokeo ya GMO kwa ujumla sio mazuri,tumeshuhudia magonjwa ya ajabu na mabadiliko ktk jamii nyingi hasa hizi za nchi zilizo endelea,mengi ya mambo ya ajabu ni pamoja na kuanza kuzaliwa watoto wenye matatizo ya namnatofauti kuanzia kimaumbile hadi ya kimfumo wa uzalishaji wa vichocheo (hormones)ktk mwili.
    sasa mheshimiwa pinda kwa uelewa wake anaposema hizo ni propaganda tu,ina maana kwamba siasa inaweza kutawala sayansi na kusema tu ilimradi umejisikia kusema. NDIYO MAANA HATUTAKAA TUKAENDELEA KWA MTINDO HUU.INASIKITISHA SANA!!!!maana unaganga njaa kwa uharaka,huku ukizalisha tatizo ambalo halitakuwa na tiba baadaye.
    tambueni kuwa vitu vingi hujakufanyiwa majaribio huko,kwa mashinikizo kwa kuwa tuna umasikini.lakini inapofikia hata kile tunacho kifahamu kuwa hakitufai pia tunyamaze ili vituathiri? la hasha!fanyeni ila mjue matokeo yake ni yapi!!

    mdau-masomoni ughaibuni

    ReplyDelete
  12. Hizi comments za hii thread inaonyesha watanzania hawaoni hatari iliyopo mbele yetu.

    Wakati wakenya wanatafuta namna ya kuhamishia baadhi ya raia wao Tz kupunguza mgogoro wa ardhi kwao sisi tunajadiri suti.

    Duu, na hao akina Pinda wanajadiri nini huko?

    Wengine husema sisi ni mfano wa viongozi wetu.

    Haya ni mawazo yangu.

    ReplyDelete
  13. VIONGOZI WETU KWA KUPAA HAWAJAMBO. RAISI, MAKAMU SASA WAZIRI MKUU. HAWAPENDI BONGO KWANINI.....NDO MWANAMBIA NIRUDI BONGO WAKATI KILA KIONGOZI ANATAFUTA KIOUTING

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...