MSHITAKIWA Bosco Kimela ambaye alikuwa ni ofisa wa Benki Kuu (BoT), anayekabiliwa na kesi ya wizi wa fedha za Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), amepandishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, akikabiliwa na tuhuma za kuhujumu uchumi.
Kimela alipandishwa kizimbani jana pamoja na waliokuwa maofisa wengine wa BoT, ambao ni Simon Jengo, Kisima Mkango na Ally Bakari, ambapo walisomewa mashitaka matatu ya kuhujumu uchumi.
Aidha katika kesi hii, Kimela na wenzake wanakabiliwa na tuhuma za kughushi na kuhujumu uchumi kulikoisababishia Serikali kupata hasala ya zaidi ya Sh Bilioni 104.1.
Washitakiwa hao, walirudishwa rumande kutokna na kesi hiyo, kutoruhusu wao kupata dhamana kwa mujibu wa sheria.waliondoka mahakamani wakiwa wamesimama katika kalandinga, baada ya kukosa siti katika gari hilo la mahabusu.
Kimela alikuwa ni Kaimu mwanasheria katika BoT, wakati Jengo alikuwa Director of banking, Mkango Deputy director currency of BoT na Bakari alikuwa Director of banking.
Aidha katika kesi hii, Kimela na wenzake wanakabiliwa na tuhuma za kughushi na kuhujumu uchumi kulikoisababishia Serikali kupata hasala ya zaidi ya Sh Bilioni 104.1.
Washitakiwa hao, walirudishwa rumande kutokna na kesi hiyo, kutoruhusu wao kupata dhamana kwa mujibu wa sheria.waliondoka mahakamani wakiwa wamesimama katika kalandinga, baada ya kukosa siti katika gari hilo la mahabusu.
Kimela alikuwa ni Kaimu mwanasheria katika BoT, wakati Jengo alikuwa Director of banking, Mkango Deputy director currency of BoT na Bakari alikuwa Director of banking.
BoT inaandamwa sana. Ina maana hakuna taasisi nyingine huko TZ?
ReplyDeleteWhat do you mean "...hakuna taasisi nyingine huko TZ?". BoT (Bank of Tanzania) is the supreme financial sector in the country, whereby all other such sectors have to go thru. it for their financial needs. BoT is the Bankers' Bank, its the Government's Bank and its the Advisor to the Gavernment.
ReplyDeleteTATIZO NI KWAMBA MASIKINI NCHI YETU INAENDESHWA KWA REMOTE CONTROL NA AUTO PILOT TENA NADHANI YA MWAKA '48. KUNA BODI YA WAKURUGENZI NA IDARA YA UDHIBITI WA NDANI YA BOT MBONA WAO HATUWASIKII WAMESHITAKIWA NA NDIO WALITAKIWA KUJIRIDHISHA NA UFANISI WA SHUGHULI ZOTE ZA BENKI HIYO.
ReplyDeleteTatizo haooo wakurugenzi na idara ya udhibitii wa ndani ya BOT ni watu ambaooo waliwekwa kwa migongo ya wakubwa wakiwa na uwezooo mdogooo wa kielimu katika iyoo secta ,Mimi ninaona muheshimu raisii na wizara zake apitiee upya jinsi haooo wafanyakazi wa BOT walivyoajiliwa kutokana na professional zaooo,Kwa kutengeneza internal rectruitment structure mpya ya sehemu nyetii kama hiyoo ya serikali bila hivyoo watanzania na hizoo ahadii za maisha bora tutazisikia masikioni tuumpaka miaka kumi ya utawala inaisha ya JK
ReplyDeleteBora Mzee wangu alistaafu, manake angekuwa ndani sasa hivi
ReplyDeleteKwa kifupi hakuna ambapo ufisadi haufanyiki katika nchi yetu, hata karani anafanya ufisadi katika meza yake, ni tabia iliyoota mizizi nchini kwetu hivyo kushikwa kwa hawa ni bahati yao mbaya tu, tupo weeeeeeeeeeengi.
ReplyDeleteHUYO JAMAA ANAESEMA BoT INAANDAMWA AMELOGWA HUYO SIE TUNAMJUA WALIIBA MAPAZIA MSIKITINI WAKASOMEWA KUULWA ULWAUU 3 NA ALABADILBAYANA 1 MWACHENI AROPOKWE TU
ReplyDeleteNAJUA TRA HUKO MATUMBO MOTO SASA, NEXT JNIA-JULIUS NYERERE INTERNATIONAL AIRPORT, KAMA UNAJIJUA NI KIBAKA ANZA MAPEMA KUACHIA NGAZI.
ReplyDeleteDa,, na huyo bwana Jengo yumo muhuu.... mwimbaji mzuri wa nyimbo za dini hapo Azania Front, mungu amsaidie kwa hilo
ReplyDeleteMdau,, Malaysia
hii mijitu ya namna hii ndo inasababisha maisha yanakuwa magumu kupita kiasi..watoto wetu wanasoma katika mazingira magumu ya kukaa chini yenyewe yanafanya uzembe wa kuliingizia taifa hasara za kipuuzi...wacha sheria ichukue mkondo wake...lisipokufika leo kesho litakufika madhambi mengine unayoyafanya duniani malipo ni hapa hapa duniani...mtajuuuuuuta kufanya kazi na awmu ya nne.....
ReplyDeleteVYEO JAMANI DHAMANI. MSITUMIE NAFASI KUIBIA NCHI. KUWENE NA UCHUNGU NA NCHI YENU. UNAIBIA SERIKALI UNAENDE KUJENGE, KUNUNUA MAGARI, KUHONGA WANAWAKE AU WANAUME.
ReplyDeleteMWISHO WA SIKU NA UTU UZIMA WOTE HUO AIBU TUPU NA KUANGAIKA.
TUISHI MAISHA YANAYOENDANA NA KIPITO HALALI WATANZANIA WENZANGU.
SHERIA NAOMBA ICHUKUWE MKONDO WAKE
JAMANI HUKO BOT WAKIANZA KUFUNUAFUNUA HABAKI MTU MAANA WAFANYAKAZI WAO WALIFANYA KUFURU NA HELA ZA UMMA. WANAMILIKI MAHEKALU, MAKAMPUNI NA MAGARI YA KIFAHARI BALAA, USEMI WA MAISHA BORA KWA KILA MFANYAKAZI WA BOT WALISHAUTIMIZA!!EEH MOLA UWAANGAZE MAFISADI WOTEEEE
ReplyDeleteHawa ni vidagaa tu vya ufisadi, msidanganyike na lolote. Mapapa na manyangumi hayaguswi kabisaaaa. After all baada ya kesi kuendeshwa kwa miaka kadhaa watashinda. Hii ndiyo bongo zaidi ya uijuavyo. Watanzania bado tupo ktk enzi ya ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI.
ReplyDelete